Umeni dissapoint, nilitegemea ungekuja na jipya!Kwanza kabisa Nyerere alichotaka yeye ni kuboresha hali ya maisha ya wananchi (tokana na Watu na Mazingira aloyakuta) na ndio maana alipotangaza Azimio la Arusha alisema wazi kwamba maadui wetu ni watatu. 1. UMASKINI, 2. UJINGA na 3. MARADHI, haya ndio maswala aloyafanyia kazi kwa muda wote wa miaka 24 ya utawala wake na hakuna mtu hata mmoja hapa anayeweza kunambia tulikuwa na ubora zaidi ktk haya wakati wa mkoloni kuliko wakati wa Nyerere japokuwa sii kwa vipimo ambavyo vijana wa leo wanataka kuvitumia. Nyerere alikuwa na vision hii kulingana na hali halisi aloikuta ama kuiona wapi tuanzie, na alipambana na vitu ambavyo vilimkwaza Mtanzania ktk kuijenga nchi kwa kutazama vitu hivyo vitatu. Sasa aje mtu hapa anambie ni shule au Hospital ngapi zilijengwa Kusini dhidi ya zilizojengwa Mikoa ya kanda ya ziwa, Nyanda za juu, Kaskazini, Mashariki na magharibi.
Siandiki lolote kuridhisha mtu maana kama Idd Amin angekuwa Mkristu na Nyerere Muislaam basi ungekuwa na sababu zote za kumshambulia na kuboresha maisha ya wananchi - Akili hiyo mimi sina!Umeni dissapoint, nilitegemea ungekuja na jipya!
Vile vita vya kagera vilimboreshea vipi mwananchi hali yake ya maisha?
Hivi vita vilikuwa ni kupigana na UMASKINI, UJINGA NA MARADHI?
Kwanini Nyerere hakuendeleza kusini kwa miaka mingi?
Kwanini sehemu nyingi zenye Waislamu wengi hazikuendelezwa kwa miaka mingi? (Hii ni tokea ukoloni)
Jadili.