Kwanini Mwalimu Nyerere aling'oa reli ya Dar-Lindi, Mtwara, Nachingwea?

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
TRAIN-NACHINGWEA_site.jpg

Hili ni jambo ambalo ukimuuliza Nyerereist yoyote hatokupa jibu

Mindhali humu kuna GREAT THINKERS naamini tutapata data tuu kwa nini the so called baba wa taifa alimua hii reli ingolewe

Nawasilisha

Swali lililokuwa likiwasumbua watu wa kusini limepatiwa jibu leo bungeni baada ya Mbunge wa viti maalumu (CUF) Mhe.Clara Diana Mwantumu kuhoji sababu za kung'olewa kwa reli ukanda wa kusini?

Jibu lililotolewa ni kwamba reli ilijengwa na wakoloni kwa lengo la kusafirisha zao la karanga kuelekea bandari ya Mtwara, baadaye ikagundulika kwamba hali ya hewa ya mikoa ya kusini isingefanikisha ustawi wa zao hili na kupelekea kampuni ya British Overseas Food production Company kusitisha uwekezaji wake.

Waziri hajataja sababu nyingine zaidi ya hiyo na kumchochea Mhe.Mwantumu kuhoji ilikuwaje ikang'olewa wakati ingesaidia shughuli nyingine kama kusafirisha watu,mizingo na sasa chuma kutoka Liganga na Mchuchuma? Waziri amesema serikali ina mpango wa kujenga reli kutoka Mtwara mpaka Mbamba Bay, pia wanakaribisha wawekezaji wenye interest Kwa kuwa kuna madini ya Nikel watapatikana.

SWALI LANGU: Serikali haikuwa na alternative zaidi ya kung'oa reli?

Nimewahi kusikia kuwa kabla ya uhuru wa Tanganyika kusini mwa Tanzania Mkoa wa Mtwara kuliwahi na Railway line iliokua inaunganisha Mtwara na Wilaya ya Nachingwea. Aiadha mara baada ya uhuru wa Tanganyika serikali ya Mwalimu ikaamua kung'oa reli hiyo na kwenda kujenga reli ya Dar/Moshi.

Kwa ufahamu wangu naamini kuwa wazungu (wakoloni) walioamua kujenga reli hiyo walikua na madhumuni yao kwa mikoa ya kusini mwa Tanganyika.

Lakini mpaka hivi sasa sijui kwa nini Wazungu waliamua kujenga Reli kusini na Kwa nini serikali ya Mwalimu iliamua kung'oa reli hiyo?........Naomba wan jf kwa yeyote ambae ana ufhamu mzuri kuhus hili basi anifahamishe na mimi niongeze ufahamu wangu.....nawakilisha.
View attachment 39504
Swali na hoja hii ni nzuri sana. Project ya karanga Nachingwea ilikuwa baada ya project kama hiyo ya Overseas Food Company (OFC). Kongwa. Naikumbuka sana kwa sababu ndio wakati nilipozaliwa na mzee wangu alikuwa Agromechanic Kongwa akahamishiwa Nachingwea.

Pamoja na project hiyo kuna ile ya kufuga (NARCO) ambayo bado ipo hata baada ya kunyofolewa nyofolewa.

Hoja ni kwamba kuna uwezekano mkubwa tulipopata uhuru, ama makabidhiano ya miundombinu na mali zingine hayakufanywa kwa umakini; ama tulikuwa wachanga mno kutokujali umuhimu wa miundombinu na mali zingine kiasi ambacho hata nyaraka na mipango mbalimbali hatuiihifadhi.

Mifano mibaya inayoniuma sana

1. Master Plan ya Dar es Salaam ikiwa na underground train iliyoextend hadi Kibaha. Holela ya sasa hivi ni uswahili Dar Plan kweli ilikuwa "Heaven of Peace" ya akili na mwili.

2. Infrastructure za kilimo Kongwa zimefukiwa ambazo zilikuwa meant kwa kilimo cha kumwagilia miaka hiyo baada ya vita.

3. Unazungumzia kung'olewa reli ya Nachingwea nawakumbusha reli ya Kongwa wakati huo Kongwa ikiwa na jina la Uingereza

4. Mashule yaliyoachwa nk

Kifupi tunaendeleza tabia ile ile ya uchanga na utoto wa kupata uhuru kwa mizaha mizaha tu. Mipango yote ya uchumi iliyofanyiwa utafiti na Wajerumani na Waingereza tumeizika tunaparamia tu kwa majibu mepesi mepesi. Suala la reli ni la kiuchumi. Unapozungumzia reli, unazungumzia infrastructure yenye kudumu si chini ya maika mia (100); kwa hiyo kuing'oa ni uamuzi unaotakiwa kufanywa kwa umakini sana.

Reli ya Mbamba Bay Mtwara ililenga kuchukua mizigo ya Malawi (makaa ya mawe). Malawi sasa hivi wanapanua ziwa nyasa angalau meli zipakie ndani ya Malawi litokee bahari ya Hindi kupitia Mozambique na kazi imeanza. Lakini tungejikita zaidi kwenye miundombinu inayochochea ukuaji wa uchumi wa ndani ili mengine yawe bonus.

SAMAHANI NAYASEMA YOTE HAYA KWA SABABU KWA KAZI YANGU YA USHAURI SEKTA YA UCHUKUZI KWENYE NCHI ZOTE HIZI LABDA NAFAHAMU MAMBO AMBAYO WATAWALA HAWAYAELEWI NA WALA HAWATAKI KUYAELEWA.

Ila kwenye fani naongozwa na "FACTS YOU DECIDE" na si majibu ya kisiasa uchwara

 
Ndugu,
Hata kama unamchukia mtu si vizuri kumzushia mambo ya uongo....Hapajawahi kuwa na reli ya Dar- Mtwara ni uwongo mkubwa...reli iliyokuwepo ni Mtwara mpaka Masasi iliyong'olewa na mkoloni kwa kutokuwa na umuhimu wa kiuchumi wakati huo....mbona Zanzibar ilikuwepo treni ya Bububu na iling'olewa pia na hulalamiki?
 
unajuwa enzi hizo vipaumbele vya reli na kuweka rami vilivuata zaidi uchumi wa eneo husika yaani nini kilichopo eneo husika ambacho kinaweza kuiletea taifa na kuingizia taifa mapato so nadhani kama ilikuwepo waling'owa kwa sababu ya kuwa eneo husika halikuwa na tija kiuchumi

mapinduziiii daimaaaaa
 
resize_image.php


Hili ni jambo ambalo ukimuuliza Nyerereist yoyote hatokupa jibu

Mindhali humu kuna GREAT THINKERS naamini tutapata data tuu kwa nini the so called baba wa taifa alimua hii reli ingolewe

Nawasilisha

Umehamisha mashambulizi kwa Nyerere sasa sio?

PATHETIC!!!!
 
Reli ya mtwara ilianza kujengwa mwaka 1947 na waingereza na nadhani ilikwenda mpaka tunduru.nadhani walikuwa na lengo flani either kuipeleka mpaka liganga ,mchuchuma au sijui wapi.waliishia Tunduru baada ya kuona mambo ya kupigania uhuru yanaanza.navyojua mimi ni kwamba hii reli iling'olewa wakati wa Nyerere kwa sababu ambazo kwa kipindi hicho zilikuwa za msingi.lakini baadae serikali ilikuja kujuta kwani ingekuja kusaidia sana kulink na mchuchuma,liganGA,NA MIKOA HIYO YENYE KUZALISHA CHAKULA KINGI
 
Reli ya mtwara ilianza kujengwa mwaka 1947 na waingereza na nadhani ilikwenda mpaka tunduru.nadhani walikuwa na lengo flani either kuipeleka mpaka liganga ,mchuchuma au sijui wapi.waliishia Tunduru baada ya kuona mambo ya kupigania uhuru yanaanza.navyojua mimi ni kwamba hii reli iling'olewa wakati wa Nyerere kwa sababu ambazo kwa kipindi hicho zilikuwa za msingi.lakini baadae serikali ilikuja kujuta kwani ingekuja kusaidia sana kulink na mchuchuma,liganGA,NA MIKOA HIYO YENYE KUZALISHA CHAKULA KINGI

Reli ilijengwa mpaka Masasi(sio Tunduru) kwa jili ya mradi wa kilimo cha Karanga ili kutengeneza Mafuta ya kula Uingereza
 
Mimi nimeishi Mtwara ni kweli reli ilikuwa toka mtwara mpaka masasi,lengo lilikuwa ni kupata access ya bandari toka masasi by that time.
 
Ili kupata jibu ni muhimu kujua ni kwa nini Nyerere au mkoloni alijenga reli hiyo. kama alijenga kwa sababu za kiuchumi tujue ni uchumi upi ulikuwepo sehemu iliyopita reli hiyo? kama uchumi huo ulikufa hakuna maana ya kuwepo reli tena ili kukidhi gharama za uendeshaji. kumbuka miaka ya mwanzo wa uhuru watanzania wachache sana waliokuwa wanasafiri kutoka sehemu moja na nyingine hivyo uendeshaji wa reli ulitegemea sana mazao ya biashara. kwa mfano, reli ya kati ilijengwa kwa ajili ya mashamba ya Pamba mikoa ya shinyanga na Mwanza, Mkonge mikoa ya Tabora, Morogoro na Tanga, Kahawa na ndizi mikoa ya Kilimanjaro na Kagera.

Reli ya Mtwara - masasi inawezekana ilikuwa na lengo la kuinganisha masasi na bandari ya mtwara sina hakika sana ni zao gani lilikuwepo masasi lakini nachelea kuhisi hivyo.

Tazara ilikuwa ni reli ya ushirikiano wa kuinganisha zambia na Bandari ya Dar es salaam na usafirishaji wa bidhaa nyingine kati ya nchi mbili za Tanzania na zambia lakini pia kukidhi haja za kibiashara kati ya Mbeya na Iringa na Morogoro. Kutoka Zambia kipaumbele kilikuwa katika usafirishaji wa shaba.

Kama ulikimbia shule (elimu dunia) haya yote hautayafahamu lakini ungeyapata katika somo la jiografia na Historia na kidogo sana katika somo la siasa au Uraia.

Mufti kasema juzi kwamba ukiwa na elimu dunia ndogo utakuwa ni mtu wa kukubali lolote hata kama unadanganywa kwa sababu ubongo wako hauna tafakari kubwa ya mambo mengine zaidi ya yale ya dini. akasisitiza kuwa ni rahisi sana kuyumba katika maamuzi kwa sababu ya kukosa elimu hii.
 
Nyerere pia alitaifisha majumba ya watu, mashule na hospitali kwa nia njema sio kwa nia ya kulikomoa kundi fulani katika jamii na kulinufaisha kundi lingine. Maamuzi haya yaliwajeruhi wakristo kwa waislamu lakini ilikuwa kwa faida ya sisi wote.

Nyerere kama binadamu alikuwa na mapungufu yake hakuwa malaika
 
Hivi kama hakuna tena uzalishaji ndio in'golewe njia? Hee ama kweli nyerere alikua ni adui mkubwa wa waislam. Aliwahi pia kusema kua kama ana uwezo angevitupa visiwa vya zanzibar ktk bahari ya hindi.
 
Huyo anayesema ilikuwepo reli kati ya dsm na Mtwara atueleze ilipitia vituo gani, na hasa mto rufiji ilivukia wapi?. Kwa vyovyote kama iliwezekana wakati huo kutandaza reli kuvuka mto rufiji isingekuwa shida pia kujenga daraja kwa ajili ya magari!
Hoja hii ilichosaidia ni kuibua ile reli ya mtwara -masasi; kama ilikuwa inakusudiwa kufuata karanga, then masasi sasa waangalie uwezekano wa kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
Kama ilikusudiwa chuma cha mchuchuma na liganga, then reli hiyo inaweza kurudishwa na chuma kinasafirishwa hadi mtwara bandarini. Hakuna haja ya kuongeza msongamano bandari ya dsm.
Uwekezaji wa mchuchuma na liganga umefikia hatua hii:
Chinese investor scoops Liganga, Mchuchuma bid


By The guardian reporter


18th January 2011





A Chinese firm has won the tender to invest in the Mchuchuma and Liganga mining projects in southern Tanzania and is expected to pump in 3bn/-.


The investor, Sichuan Hongda Corporation won the competitive tender in a bidding exercise that attracted 48 international companies.


Take-off of the investment now awaits green-light from the government through the National Development Corporation (NDC).


Teams of experts from the Chinese company and NDC are now engaged in a four-day negotiations on modalities of implementing the project.


NDC Board Chairman, Chrisant Mzindakaya said in Dar es Salaam yesterday that implementation of the projects would start after completion of the ongoing negotiations between NDC and the investor.

Shida yetu ni wanasiasa kuingilia masuala ya kitaalamu, si ajabu ukakuta Mzindakaya ndiye anaelekeza makubaliano yaweje..wakati yeye ni mwanasiasa tu!
 
Nyerere pia alitaifisha majumba ya watu, mashule na hospitali kwa nia njema sio kwa nia ya kulikomoa kundi fulani katika jamii na kulinufaisha kundi lingine. Maamuzi haya yaliwajeruhi wakristo kwa waislamu lakini ilikuwa kwa faida ya sisi wote.

Nyerere kama binadamu alikuwa na mapungufu yake hakuwa malaika

mwenye mapungufu ana hadhi ya kuwa mtakatifu?
 
Mkuu hata wewe ukifungua saluni kwenye sehemu yenye watu wenye vipara utafunga mwenyewe. Reli ya kwenda kusini ilikuwa hailipi kabisa

sasa na wewe unaona sehemu hii watu wote wana vipara, kwa nn ufunfue saluni? ina maana hukufanya feasibility study ya kutosha.
 
Hivi kama hakuna tena uzalishaji ndio in'golewe njia? Hee ama kweli nyerere alikua ni adui mkubwa wa waislam. Aliwahi pia kusema kua kama ana uwezo angevitupa visiwa vya zanzibar ktk bahari ya hindi.

Jambo hili linapelekwa kidini tena jamani? Wana JF vipi? Hivi dini ni moja tu huko Mtwara na Lindi? Sina alama ya kufyonza kwa maandishi. Akchwale nimefyonza huu mwelekeo.
 
Back
Top Bottom