Kwanini Nyerere alimtimua Sheikh Yahya Hussein?

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Kipindi cha Mwalimu Julius K. Nyerere, sheikh Yahya Hussein alitimuliwa nchini na akawa akiishi maisha ya kutangatanga nchi za Arabuni kama chokoraa.

Je ni sababu zipi zilizopelekea Mwalimu kumtoa Nduki mnajimu huyu wa Kikwete?
 
Nyerere alikuwa hataki mambo ya unajimu wa kishetani, majini na uchuro! Watu kama Sheikh Yahaya ni hatari kwa usalama wa nchi
 
Rev umenena mfano kama ile statement ya kusema kuwa atakayemvaa Kikwete kwa kinyanganyiro cha URAISI atakufa!

With that statement kwa nchi ambazo ziko seriuos ilibidi awe amepewa 24hrs kudenounce iyo stm.

Usikute JK anamtumia ndo maana kamkalia kimya bila kumjibu ingawa Kinana kamjibu kuhusu huo ulinzi wa ShEIKH
 
hakumtimua...huyu alikuwa shushushu wakati wa MWALIMU kabla ya kuhamia huku kwenye MAJOKA YA MDIMU....soma hii The Dark Side Of Nyerere's Legacy, By Ludovick. S. Mwijage | My Africa

Asante Safari for this link, it is an interesting story, it is like reading a detective story, thank you, it is long, but I realized, it repeats itself after a while. But whatever the case the early 1980s were the most difficult years for Tanzanians. The economy was behving very bad and there was desperation everywhere and Nyerere was struggling to keep the country together.

This was the time when we had the treason cases, the sabotage wars by Sokoine and threatened businesses in the country, a lot of Asians left at this time, some throwing their valuable trading goods into the ocean. IT WAS SIMPLY BAD! AND CIA was deeply involved as Nyerere kept on siding with the socialist China and Russia
 
JAMAAA Shehe Yahya Hussein baada ya kutimuliwa na Nyerere akahangaika Arabuni, kisha akaja Kenya akafanya makao yake yakudumu.

Alijikita pale Mombassa , na alikua maharufu saana, miaka ya mwanzoni mwa 1980 niliwahi kumkuta pale , akiagua watu kwa kutumia kitabu, akitoa dawa na kinga za Kishetani kama anayompatia Kikwete (mgombea Urais kwa tiketi ya CCM) .

Siku moja akalikoroga , akawatabilia watawala waKenya upuuzi, akapewa notice ya siku saaba , aondoke kule, ndio sasa akaibukia Dar tena, akarejea mtaani kwake mwembe chai, akiwa hana makeke.

Baadae akaanza tena Mbwembwe na mihangaiko yake. akijidai kuelewa mambo mengi saana ya kinajimu nyota na majini. Akawa maarufu sana, na hapa ikumbukwe alipata pesa nyingi kwa deal hizo, akaoa madada kadhaa wa kadha.

Katika miaka ya hivi karibuni umaarufu wake umeanza kupungua kwa kasi ya ajabu, watu wameanza kupuuza uwezo wa nguvu zake, anahangaika kurejesha umaarufu wake, lakini wapi jua limemchwea.
 
Hayo ya unajimu hayakumuudhi SANA Nyerere.

Sheikh Yahya Hussein alihusika na chama cha siasa cha AMNUT (All Muslin National Union of Tanganyika) licha ya kuligawa taifa la Tanganyika ki-dini na kutaka uhuru wa Tanganyika ucheleweshwe hadi hapo Waisalmu watakapoweza kuwa sambamba na (sijui, Wakristu),
Sheikh Yahya Hussein pia alituhumiwa kwa uhaini.
 
Yupo saa Zajion na alie mleta atamchukua na baada yake hatoibuka mtu kama uyo Tz in might Jesus! Amen.
 
kwa hio kumbe alimpenda na yeye ?

Hapana, Sheikh Yahaya alianza kama mkereketwa mkubwa sana wa TANU hapo kwao Ujiji; lakini alikuja furumishwa na Nyerere kwa upuuzi fulani mwishoni mwa miaka hiyo ya sabini akahamia Nairobi.

Ushushushu, alikuwa anajifanya tu kwa njia ya kujikomba kama anavyofanya sasa hivi eti ni mlinzi maalumu wa Kikwete. Ni kweli alikuwa akipeleka taarifa za kishushushu kwa jamaa wa usalama anapozipata kwa ajili ya kujipendekeza tu, hakuwa na lolote.
 
Nimesoma maoni yenu nyote muliochangia.

Huyu jamaa ni mhuni. Na kama leo jitu kama Ben Mkapa lingekuwa State asingeleta hayo mazingaombwe yake.

Kikwete anapenda masihara ndo maana anamuangalia tu.

Sasa.................Tumfanye nini huyu tapeli mkubwa???
 
Huyu jamaa aliporudi kutoka ughaibuni alikuja na balukta, chombo cha kuhifadhi kuran.
Hiki chombo kilikuwa cha kihuni kabisa, hata mwinyi akashindwa kumvumilia akaamua kumtimua na kuifutilia mbali balukta.
Huyu ndiye aliyekuwa mchochezi wa zile vurugu za mwembe chai akisaidiwa na kina sheikh ponda
 
Kipindi cha Mwalimu Julius K. Nyerere, sheikh Yahya Hussein alitimuliwa nchini na akawa akiishi maisha ya kutangatanga nchi za Arabuni kama chokoraa.

Je ni sababu zipi zilizopelekea Mwalimu kumtoa Nduki mnajimu huyu wa Kikwete?

Ni kwa maelekezo aliyokuwa amepewa na yule mganga aliyempa kile kifimbo chake? Kwani siku zote mafahari wawili hawawezi kukaa katika zizi moja.
 
Back
Top Bottom