Kwanini Nyerere aliachia madaraka mapema?

mandela anaweza kusema kaachia madaraka mapema.

Myerere kakaa miaka 23 kwenye power, huwezi kusema "kaachia madaraka mapema". Miaka 23 ni umri wa mtu aliyefikisha "age of majority" tayari.

Unachoweza kuuliza ni kwa nini aliachia madaraka bila ya kulazimika.

Jibu ni kwamba aliona kashindwa na kuendelea kungeharibu legacy yake kama "philosopher king" akajua principle ya quit while you can, before the masses causescu you brutally at the central square.
kwanini aliihisi hivo? Mimi sikuwepo enzi za mwalimu kwa kweli lakini hii philosopy unazani ingeweza kuapply kwake? Si alikuwa anapendwa sana mwalimu enzi hizo
 
za-10 katoa majibu sahihi sana. Nyerere hakuachia madaraka mapema, alikaa madarakani kwa zaidi ya miaka 20; huo ni muda mrefu sanakwa kiongozi mwenye akili timamu kuendelea kuwapo madarakani ukitoa maamuzi makubwa ya kitaifa. Alikuwa anaplani kuachia madaraka mwaka 1980 baada ya kuunganisha tanu na asp, na akafanya mojawapo ya majukumu yake katika kipindi cha 1975-1980 kuwa ni kuunganisha tanu na asp, jambo ambalo lilikamilika mwaka 1977 chini ya usimamizi wa pius msekwa. Hata hivyo ile vita ya mwaka 1979 dhidi ya amin iliharibu mambo mengi kiasi kuwa nyerere alisema ataendelea kuyasimamia tena kwa miaka mingine mitano, ndiyo maana mwaka 1985 akaondoka ingawa alikuwa hajayanyoosha mambo hayo.
nashukuru kwa majibu mkuu swali langu ni kwamba kwanini asingeendelea kushikilia madaraka tu kama kina mugabe wanadai hawajaona watu wenye uwezo wa kuachiwa kuongoza nchi? Au huku kwetu kipindii hicho aliona watu wenye uwezo zaidi yake wapo?
 
nashukuru kwa majibu mkuu swali langu ni kwamba kwanini asingeendelea kushikilia madaraka tu kama kina mugabe wanadai hawajaona watu wenye uwezo wa kuachiwa kuongoza nchi? Au huku kwetu kipindii hicho aliona watu wenye uwezo zaidi yake wapo?
Uchumi wa Zimbabwe ulikuwa mzuri tu hadi hivi majuzi baada ya Mugabe kuya seize mashamba ya mabepari wakizungu.

Nasisitizia hili la uchumi kuwa the main reason why mwalimu didnt do it like Mugabe, kwasababu kwenye majibu yote uliyopewa uchumi umetajwa kama the main thing.Mwalimu left, but Mugabe isnt kwasababu mwalimu alishajaribu hilo la kuziweka rasilimali kwa umma/serikali,lakini halikufanya kazi.Anachofana Mugabe sasahivi, mwalimu yeye alishafanya, lakini ilishindikana.

Pia on the other hand however, muda aliokaa madarakani mwalimu ni almost the same as Mugabe, sema vipindi tofauti, Mugabe kachukua nchi mwaka 1980 kama sikosei.
 
Nadhani kilichomfanya aachie madaraka mapema ni baada ya kuona sera zake za ujamaa na kujitegemea zimefeli na hivyo akaamua kuwaachia wenye mawazo mbadala..

kitu hicho alichofanya ni cha busara angalitaka kukaa kimabavu asingalishindwa.na ikumbukwe kuwa yeye aliheshimika na jeshi na watendaji wengine vizuri zaidi.
 
nashukuru kwa majibu mkuu swali langu ni kwamba kwanini asingeendelea kushikilia madaraka tu kama kina mugabe wanadai hawajaona watu wenye uwezo wa kuachiwa kuongoza nchi? Au huku kwetu kipindii hicho aliona watu wenye uwezo zaidi yake wapo?

Smile,

Kwani kushikiria madaraka na kubaki kiongozi nyuma ya panzia kuna tofauti?
 
Uchumi ulikuwa ukiyumba ... Akaamua asepe... na pia amekaa madarakani zaidi ya miaka 20 ... Hana tofauti na Mugabe ..
 
Mtu kakaa 23 years bado mnasema aliwai?
Infact aliondoka bse alijua yu mtu safi na awaachie wengine pia walisukume ili gurudumu la maendeleo ya Tz.
Na pia ideology zake nyingi zilikuwa zapata upinzani hasa ktk ulimwengu huu wa kibepari so ili asipate KISUKARI NA BP akaona alete damu mpya!
To it was a brilliant idea!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom