Kwanini nisifanye ngono hadi nitakapokuwa tayari (ndoa)?

apprentice1997

Senior Member
Jun 8, 2016
107
99
Shikamoni wakubwa wangu,

Mimi ni kijana wa kiume umri wangu ni miaka 19. Nimebakiwa na wiki moja kabla sijayaanza maisha yangu mapya ya kimasomo kama mwanachuo. Natambua kuwa mpaka hapa nilipofikia si mimi bali ni Mungu tu na ninashukuru hata kwa kuendelea kunifichia aibu yangu ya kufanya ngono miaka 2 iliyopita na toka hapo sijafanya tena.

Nina nia ya dhati ya kufanikiwa maishani na pia natamani sana kukua nikiwa na heshima inayotakiwa kwa jamii na pia nikue nikiwa sina scandal za mambo yoyote maovu maishani mwangu. Kiukweli mimi sio mlokole na wala sio mshika dini sana ila ninalitunza neno la Mungu ndani yangu na ninaamini kuwa ni yeye tu anayenitunza hivyo basi mimi ni kijana wa kawaida ila sifanyi mambo ambayo vijana wengi wanayafanya.

Ninamuomba Mungu nisifanye ngono hadi siku nitakapooa nikiamini kuwa sihangaiki na maisha na Mungu atanipatia mtu ambaye atakuwa sahihi kwangu kuliko kuhangaika na watu ambao hawatanijali na kunitesa. Ninatamani kufanya hivi ili niweze kufanikiwa katika masomo yangu na kazi zangu.

Naombeni ushauri wenu jinsi gani nitafanikiwa nia yangu na je. faida zipi nitapata kwa maamuzi haya kama una ushuhuda wowote wa kunitia moyo ningependa kuusikia.

Mbarikiwe.

Cc heaven sent Valentina THT
 
huu ndio muda wako muafaka wa kufanya ngono, ukioa tu haufanyi ngono tena; utakuwa kama sisi tunaofanya tendo la ndoa.
 
O'level na advance ushawishi ni mdogo tofauti na mazingira ya chuo.wengi waneharibikiwa au wamebadilika tabia walipokuwa chuoni.kaza buti katika masomo ufanye vizuri umalize na GPA nzuri
 
Umefanya ngono mara moja tu ila "mungu anakufichia" so hadi utakapooa. Labda huyo mungu na sio Mungu. Usifananishe ngono na mambo ya kijinga.


=Usile Mbegu=
 
Kaza Buti kijana , tafuta lyf, mademu hawana ishu (magonjwa , maradhi na umasikini) . Jijenge uwe na mafanikio , mwombe Muumba na muda ukifika utampata mcha Mungu mwenzio..... Acha wafu wazike wafu wao
 
Hongera kwa nia yako hiyo,Mungu akutie nguvu uweze kukabiliana na vishawishi vyote vya ngono tofauti na malengo yako

Faida ya msimamo wako utakua na ndoa imara kwakua Mungu atakuunganisha na wa ubavu wako,mtu sahihi na kwa wakati sahihi...
 
[AsanteE="Valentina, post: 17596280, member: 181383"]Hongera kwa nia yako hiyo,Mungu akutie nguvu uweze kukabiliana na vishawishi vyote vya ngono tofauti na malengo yako

Faida ya msimamo wako utakua na ndoa imara kwakua Mungu atakuunganisha na wa ubavu wako,mtu sahihi na kwa wakati sahihi...[/QUOTE]
Asan
 
Shikamoni wakubwa Wang,
Mimi ni kijana wa kiume umri Wangu ni miaka 19. Nimebakiwa na wiki moja kabla sijayaanza maisha yangu mapya ya kimasomo kama mwanachuo. Natambua Kuwa mpaka hapa nilipofikia si Mimi Bali ni mungu tu na ninashukuru hata kwa kuendelea kunifichia aibu yangu ya kufanya ngono miaka 2 iliyopita na toka hapo sijafanya tena. Nina Nia ya dhati ya kufanikiwa maishani na pia natamani sana kukua nikiwa na heshima inayotakiwa kwa jamii na pia nikue nikiwa sina scandal za mambo yoyote maovu maishani mwangu. Kiukweli Mimi sio mlokole na wala sio mshika dini sana ila ninalitunza neno la mungu ndani yangu na ninaamini Kuwa ni yeye tu anayenitunza hivyo basi Mimi ni kijana wa kawaida ila sifanyi mambo ambayo vijana wengi wanayafanya. Ninamuomba mungu nisifanye ngono hadi Siku nitakapooa nikiamini kuwA sihangaiki na maisha na mungu atanipatia MTU ambaye atakuwa sahihi kwangu kuliko kuhangaika na watu ambao hawatanijali na kunitesa. Ninatamani kufanya hivi ili niweze kufanikiwa katika masomo yangu na kazi zangu. Naombeni ushauri wenu jinsi gani nitafanikiwa nia yangu na je. faida zipI nitapata kwa maamuzi hay a. Kama una ushuhuda wowote wa kunitia moyo ningependa kuusikia. Mbarikiwe.

Cc heaven sent Valentina THT
Hata polisi akishapata mafunzo ya kutumia bunduki na risasi, huwa haanzi kutumia hovyo hovyo popote pale atakapojisikia. Kuna majira.
 
Mdogo wangu naomba ufahamu kuwa nilijiwekea Vow kama wewe na nilijitahidi sana kujitunza sawasawa na neno la Kristo linavyotaka ila kilichonitokea mwaka 2011, sintakaa nimsahau binti mmoja mshirikina aliyenitafuta for years kwa kile alichonifanyia nyumbani kwake kimazingara.

Kifupi ikiwa una hofu ya Mungu wako na umeamua kulitii neno lake basi fanya tu hivyo kwasbb dhambi ya uzinzi wa makusudi ina adhabu kali sana.

Take it from me.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom