Kwanini niliomba muongozo-Sakata la Mgomo wa Madaktari by J J MNYIKA

Kama wenzangu waliotangulia, hoja ya ni nzuri ina mashiko na ni halisi. Lakini tatizo ni hilo silly bunge. Udhaifu wa ccm umedhihirika na unaendelea kuonekana kila iitwapo leo.

Sisi wananchi tunaona na tunachukua hatuastahiki ili kuendena na kazi ya M4C. Hitimisho la hatua zetu hizi ni kwenye sanduku la kura mnamo 2015 and beyond. Hakika bunge la 11 litakuwa tofauti sana na hili la sasa.
 
Nasikitika kuwa CCM wanajua kuwa wanatuhadaa, na wananchi tunajua kuwa tunahadaiwa, CCM wanadhani tuko 1947 lakaini nawaambia ole wenu, kiyama kinakuja...
 
Makinda alishageuza bunge kuwa sehemu ya serikali. Uswaiba wake na waziri mkuu nao ni kero kwa demokrasia lakini ni hatari zaidi kwa CCM maana anapotumia mabavu kuziba hoja muhimu madhara yake anachonganisha ccm na wananchi.

CCM na hasa wabunge wanatakiwa wajiandae kumeza madhara ya ubabe wa Makinda maana ni wao waliosema wanata 'mwanamke' badala ya spika.

Ni masikitiko makubwa kwa watanzania kwa kitendo cha spika wa bunge mama anne makinda kuibeba mno serikali hata mahali pasipostahili.
Mathalani hili suala la mgomo wa madaktari alitakiwa kulipa nafasi bunge liingilie kati na kujaribu kutafuta ufumbuzi.
Inaonekana serikali na madaktari hawawezi kufikia sehemu ya kuelewana, nahisi kuna mambo fulani ya vitisho kutoka kwa viongozi wa serikali hivyo kuwafanya madaktari kuamua kutumia njia za maumivu kwa wananchi ili serikali itambue wajibu wake kwao.
Chonde chonde spika wa bunge jiangalie upya jinsi unavyoliongoza bunge letu, lipe nafasi liisaidie serikali, inaonekana kwamba imekwama inahitaji msaada wa kuikwamua. Ruhusu bunge lijadili na kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa madaktari na serikali.
 
Yan umenena kamanda lakini hapo ni kumpigia mbuzi gitaa.

Kweli ulisema ukweli maana hata mgimwa bungeni ana kushukuru kwa kusema ukweli.
 
Chadema ni rahisi kuandaa bajeti ya harusi si bajeti ya nchi "Ngeleja"
 
Tume ya katiba imetengewa billion 40 na madaktari wametengewa motisha ya billion 20 kwa mwaka (embu tuweke ratio yao hawa watu na majukumu yao), kaazi kweli kweli.

Bado hata ujaangalia bajeti ya anasa waliojitengea wakuu wa nchi hii, tutafika kweli maana wanajilimbikizia miela mpaka inaibiwa chini ya raisi mpaka nayeye astuliwe haki ya mungu only in Tanzania.
 
Tatizo serikali imejitoa ktk matatizo ya wananchi na hili limethibitishwa na kauli aliyotoa waziri mwinyi leo bungeni nanukuhu.." madaktari mkigoma watakao athirika ni wananchi" . Kwa kauli hiyo serikali imejitoa kuwajibika kuokoa maisha ya wananchi, kana kwamba wananchi wakifa ni kenya au uganda ndio itapungukiwa walipa kodi na wavuja jasho. i wish i could fast foward the election date
 
Madaktari ni alama tu yawataalamu wavyonyanyasika ktk nchi hii kwakulipwa kiduchu!Sekita nyingi ziko hoi tatizo ni uoga!
 
nikikumbuka kauli ya pinda alipokua anajibu swali la mbowe kuhusu sakata hili napata hasira,kauli ilikua hivi..."wakigoma wagome tu lakini watambue kwamba wanatakiwa waoneshe dhamira ya kweli kuhudumia jamii"...jamani wadau hii kauli ipo sawa kweli..?
 
Tafadhari wana JF naomba haraka sana namba ya simu ya mheshimiwa Myika, ninataka kumpa data za udhaifu mwingine wa wizara ya afya! Haraka sana jamani kabla hajapeleka hiyo hoja binafsi.
 
Tafadhari wana JF naomba haraka sana namba ya simu ya mheshimiwa Myika, ninataka kumpa data za udhaifu mwingine wa wizara ya afya! Haraka sana jamani kabla hajapeleka hiyo hoja binafsi.

jaribu kum'PM au kum'inbox facebook.. La nenda kwenye website ya bunge utakuta namba yake.
 
Back
Top Bottom