Kwanini niliomba muongozo-Sakata la Mgomo wa Madaktari by J J MNYIKA

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
kama kawaida mbunge kijana ndugu JJ MNYIKA anaendelea kuanika ''udhaifu'' wa serikali.
kama serikali ina majibu isisite kutoa taarifa kwa umma!!

[h=6]Kwanini niliomba muongozo-Sakata la Mgomo wa Madaktari
Leo, Juni 22, 2012 nilitaka kuomba muongozo wa Spika kwa mujibu wa Kanuni 49 (2) baada ya Waziri wa Afya kutoa kauli juu ya utekelezaji wa madai ya madaktari. Kanuni hiyo inataka kauli isiwe ya kuzua mjadala lakini aliyoyaeleza waziri juu ya uboreshaji wa maslahi ya madaktari yanazua mjadala kwa kuwa yanatofautiana na majibu ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoyatoa bungeni jana, (Juni 21, 2012) na pia hayana uhalisi. Mathalani, wakati serikali ikidai imeongeza posho ya kuitwa kazini (on call allowance) toka Februari, 2012 na kutumia bilioni 7.9 kwa miezi michache, imetenga kwa watumishi wa Afya bilioni 18.9 tu kwa mwaka mzima wa 2012/2013 kiwango ambacho hakitoshi.

Hivyo nilitaka kuomba muongozo Spika awezeshe kauli hiyo ijadiliwe kama ilivyokuwa kwa kauli juu ya fedha za rada. Nakusudia kumuandikia barua Spika kushauri aelekeze kamati ya bunge ya huduma za jamii kauli hiyo ya waziri.

Pia bunge halipaswi kunyimwa fursa ya kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa ibara ya 63 ya kuishauri na kuisimamia serikali kusuluhisha mgogoro na madaktari ili kuepusha mgomo wenye athari kwa nchi na wananchi kwa kisingizio cha kusudio la serikali kupeleka mgogoro mahakama kuu kwa kuwa mpaka leo taarifa iliyotolewa bungeni bado hakuna shauri katika kitengo cha kazi. Hivyo, Spika anapaswa kutoa jukumu kwa kamati husika ya bunge kuendelea na usuluhishi kabla ya serikali kukimbilia mahakamani.

Wabunge tupewe nakala ya taarifa ya majadiliano ya pande mbili yaliyochukua zaidi ya siku 90 badala ya kupewa hotuba ya nusu saa ya upande mmoja wa serikali pekee.

Hata serikali ikizuia mgomo wa wazi kwa zuio la kimahakama ieleweke kuwa mgomo wa chinichini kwa watumishi wa afya ambao una athari ya muda mrefu kwa maisha ya wananchi nchini.

Mwisho, serikali ipunguze matumizi yasiyo ya lazima na ipanue wigo wa mapato.

John John Mnyika.
Mbunge Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
22 Juni, 2012
[/h]
 
Katika khali ya kawaida serikari inaitaji kutoa majibu haraka kwani imekuwa ikikimbilia Mahaamani kuweka pingamizi, naishauri serikali kuwa si siku zote ni j2 ipo cku wafanyakazi watachoka kuwekewa pingamizi na kitakchofuata ni maafa.
Nawasilisha
 
Mapambano ni lazima yaendelee mpaka kieleweke, maana hawa magamba wanafanya kazi zao bila kufikiria!
 
mm nashindwa kuelewa nafasi ya Rais hasa pale anapoitajika kuchukua maamuzi magumu ya Kitaifa hili linaitaji kuingia katika majadiliano ya katiba mpya
 
...unamwazo na ushauri mzuri sana mweshimiwa Mnyika lakini hao unaowapa huo ushauri wako wapi?...
 
kama kawaida yao.,udhaifu na ubadhirifu ndo wanautanguliza. Wanataka kutuambia malipo ya call allowance za mwezi wa pili mpaka wa nne ni bl 7.9 na bajeti ya wizara nzima ilikuwa bil 30? Huu uwendawazimu wa aina hii sijui tutaachana nao lini watz! Roho yangu inaniuma ninapoona watu wale wale wanatudanganya vile vile na tunaendelea kuwashabikia.
 
Mnyika, kaka umeandika mawazo mazuri lakini serikali yenyewe ndio hivyo goigoi na tetea Chama badala ya kutetea wananchi
 
Duh mke wangu anaweza kujifunggua anytime, ngoja nikambook mkunga wa jadi jirani yangu nisije poteza kichanga changu kitarajiwa maana madoktor wakiazimia kitu uwa hawarudi nyuma
 
Ni ushauri mzuri japo madaktari silaha yao ni kugoma iwe rasmi au hisivyo rasmi....nazani kuna haja ya ku address ishu ya madaktari mapema
 
Makinda alishageuza bunge kuwa sehemu ya serikali. Uswaiba wake na waziri mkuu nao ni kero kwa demokrasia lakini ni hatari zaidi kwa CCM maana anapotumia mabavu kuziba hoja muhimu madhara yake anachonganisha ccm na wananchi.

CCM na hasa wabunge wanatakiwa wajiandae kumeza madhara ya ubabe wa Makinda maana ni wao waliosema wanata 'mwanamke' badala ya spika.
 
Thread kama hizi natamani wale wote waliokua wanamponda mhe Mnyika juu ya kauli yake kuwa Rais ni dhaifu waje na hapa wakanushe,siwanalipwa posho?
 
...unamawazo na ushauri mzuri sana mweshimiwa Mnyika lakini hao unaowapa huo ushauri wako wapi?...mimi naona kama-vile unajaribu kumwongezea damu maiti!,hiyo midude unayojaribu kuisemesha ilishakufa siku nyiiiiiiiiiiiingi,unainayoiona hapo bungeni ni misukule tu...lejea kauli yako uliyoitoa bungeni tarehe 19/06/2012..."Tanzania imefika hapa ilipo kwa sababu ya UDHAIFU wa raisi Jakaya Kikwete,nchi imefikia hapa kwaajili ya upuuzi wa chama cha CCM"...
 
Naamini itachukua muda mrefu kwa viongozi wa sasa toka CCM kuelewa shule hii. Hata hivyo mkakati ni kuzidi kuwaelemisha na kwa njia hiyo kuwafunua mbele ya wananchi na wapiga kura ili wawaelewe na wazielewe mbinu zao za kutaka kuzidi kuwapumbaza, kuwadanganya na kuwadumaza wapiga kura na wananchi kwa ujumla kwa nia na malengo yao binfsi ya kisiasa. Tuzidi kuwaelimisha wananchi kwa njia zote ikiwa ni pamoja na wabunge kama akina Mh.JohnMnika kusema ukweli kwa kuita a spade a spade and not a big spoon!
 
Kwa ufahamu na experience yangu ya migomo ya madaktari iliyopita, ni kwamba hawa jamaa hawaogopi mahakama wala nini, mgomo wao uko pale pale kuanzia kesho, suluhu ni serikali kukaa kuongea nao tena huko mahakamani hakuna solution!
 
Back
Top Bottom