Kwanini ni vigumu sana kupata "A" katika vyuo vyetu? Tunawahujumu wanafunzi wetu?

Kama seminar ni sehemu ya kuelewa mbona seminar leader akifika anatupiga Quiz kila tuendapo Seminar yaani kati ya vipindi vitano nilivyohudhuria vitatu katupiga Quizes, semister ikaisha na hivyo vipindi viwili alitumia kutupiga majungu na mashushu! Kuna matatizo makubwa sana hasa kwa walimu wa accounting!
 


Aagh wapi nchi gani yenye utaratibu mbovu kama huu wa bongo?? huko mbele hawafanyi hivi na wameondoa confusion nyingi tu...mfan mzuri kwa first degree nchi nyingi hazitolewi kwenye University bali zinatolewa kwenye College ambazo ziko linked/affiliated na University na pepa zote zinasahishwa main campus ie University na sio kwenye college...so walimu walimu wa college hawahusiki tena, nyie mnapewa syllabus tu mnafundisha pepa zinatungwa na university na zinasahihishwa na university

Labda unipe mifano ya nchi gani wanafanya kama hapa bongo lecturers wa darasani ndio haohao wanakupa GPA...??

If you won't mind naomba tofauti ya college na university
 
Not kuomba kazi hiyo itachukua muda sana...........atapatiwa tu booklet asome then yeye ataona picha halisi

Hivi huyu kaongelea tofauti ya upatikanaji wa materials huku na huko alikosomea yeye?

Mbona wengi tu waliosoma huko ulaya wanakuja na A zao hapa lakini material wise ni vuguvugu sana ?

Kwa tuliosoma UD some mtakumbuka kuwa na wanafunzi wa kutoka huko ulaya na america (xchange program) na wengi ni normal temperetures sana tu?

Cha muhimu kwa sasa ni kusimamia hizo A zao na ku proove wewe ni A material sio kuja nazo huku na hatuoni hilo joto la A...... as leo Prof Mchome kasema TCU wanaanza kutafuta jinsi ya ulinganifu wa madaraja ya ughaibuni na huku. B plain ya huku yaweza kuwa ndo A ya huko

Umenikumbusha kisa cha mzungu mmoja toka eastern europe tulisoma nae masters hapo mlimani, tulikuwa tunamgaragaza sana darasani, ila alama zake za bachelor zilikuwa zinatisha kweli bachelor aliisomea kwao huko huko
 
Wakati nipo kidato cha tatu shule ya Aldersgate tena nikiwa kwenye mtihani wa Historia mwezi Novemba,
alikuja mzungu ambaye kwao huko Marekani ni Mwl wa sekondari,
akaingia darasani na kupewa kopi ya mtihani tuliokuwa tukiufanya akalalamika sana na kusema mtihani mgumu sana kwa wanafunzi wa kidato cha tatu,
akabanabana pua wewee wanaf. Wakamuona hana maana yeyote. Katika mtihani huo swala mojawapo tuliloulizwa ni

Precisely explain the modes of production and account for their characteristics'

ndo muone wenzetu wanapata 'A' kwa mitihani tuifanyayo pia?
Ninachokifahamu wenzetu akisoma Bailojia ni mwanzo mwisho tena anakuwa specific labda Blood cells tu basi, ukimuuliza nutrition ama growth ugomvi. Na kuna mwingine alikuja anafahamu Algebra tu ukimuuliza circle ama Trig mnakosana. Yapo mambo mengi sana hawawezi kufanana nasi kielimu.
 
If you won't mind naomba tofauti ya college na university

University is an institution where students study for degrees and where research is done
College is an institution where students study after they have left school.


Hivi ushawahi kusikia Phd inatolewa kwenye college?? Kwa mimi ninavyojua nchi nyingi za wenzetu first degree ZOTE zinatolewa kwenye college...this simply to avoid ile kitu uchakachuaji toka kwa mwalimu wako wa darasani. Au mwenzangu unaelewaje?
 
Nimeguswa sana na hii mada,

Kwa ufupi hali ya Tz ni mbaya sana.....Kuna mwalimu wangu mmoja alikuwa analalamikia sana suala hili kwamba walimu wanaua Watanzania kwa makusudi au bila kujua! Alinambia kuwa enzi za 1980, B walikuwa wanapewa wanafunzi ambao tayari waliandaliwa kuwa ma-TAs!!

Inawezekanaje unafundisha wanafunzi 100, halafu wanapasi 10 tu na wewe unafurahi na kushangilia??

Babu DC!!
 
what matters is not A's but how competence these students they are, kung'ang'ania A ni kukaribisha wanazuoni wenye "theories" zaidi kiliko elimu ya vitendo, tunao wengi wenye A, but ukiwapeleka ktk application ya ujuzi waloupata ndipo utajua nini maana ya A za hapa nchini.
 


matokeo ya mwaka wa nne mlimani
1. Kwa shahada ya kwanza pale mlimani gredi zenyewe zimekaa hivi (kama hazijabadilika) a: 75-100, b+: 70-74, b: 60-69, c: 50-59, d: 45-49 na e: 0-44 2. Gredi za hapa marekani (kutoka katika silabasi yangu katika darasa la language and african society) zimekaa hivi: a: 93-100, a-: 90-92, b+: 87-89, b: 83-86, b-: 80-82, c+: 77-79, c: 73-76, c-: 70-72, d+: 67-69, d: 63-66, d-: 60-62, e: 0– 59. japo profesa unaweza kujipendekezea gredi zako mwenyewe, mfumo huu wa alama ndio umependekezwa na chuo kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza. 3. Hali ilivyo kule nyumbani (kama bado haijabadilika)
  • utakuta darasa lina wanafunzi 100, na kati ya wanafunzi hawa pengine wawili, watatu na hata mmoja tu ndiyo atapata "a". Hata madarasa makubwa yenye wanafunzi 300, eti wanafunzi wanne au watano tu ndiyo wanapata "a". kwa nini? Ni kwa sababu masomo ni magumu sana? Wanafunzi hawajisomei sawasawa (na kama hawajisomei ni kwa nini?), maprofesa hawafundishi vizuri kiasi kwamba wanafunzi hawawaelewi? Au maprofesa wanatunga mitihani migumu kupindukia? Au pengine wanafunzi wa vyuo vikuu vyetu ni mbumbumbu na hawana uwezo wa kupata a?
  • ninacholalamikia hapa siyo kila mwanafunzi kupata a bali ule ugumu uliopo wa kupata alama hizi kwani siamini kama kweli eti katika darasa la wanafunzi 300, ni wanafunzi watatu au wanne tu ndiyo wana uwezo wa kufaulu vizuri. Kama hivi ni kweli basi ni wazi kuna tatizo kubwa katika mfumo wetu wa elimu.
4. Hali ilivyo hapa marekani
  • hapa kupata a ni jambo la kawaida na maprofesa na wanafunzi wanalijua hili. Mahusiano kati ya wanafunzi na maprofesa ni ya wazi na wanafunzi wanaweza kuuliza maswali na kujadili masuala ya gredi watakazozipata na maprofesa wao kwa uwazi. Hali hii inasababisha matatizo fulani na haya nitayaongelea siku nyingine.
  • kwa wanafunzi wanaotegemea kuendelea na shahada za uzamili na uzamivu ni lazima wahakikishe kwamba wanapata a kwa sababu ushindani wa kupata ufadhili ni mkubwa sana na vyuo vingi vinataka wanafunzi ambao ni bora kabisa. Kwa ujumla alama za b, na hata b+ na pengine a- hazimsaidii sana mwanafunzi kuweza kujiunga na vyuo vikuu vyenye hadhi kama harvard, yale, columbia, ucla, stanford, berkeley na vinginevyo
5. Uzoefu wangu
  • nina uzoefu na uteuzi wa wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu hapa marekani na huwa nashangaa sana kugundua kwamba kwa kawaida waombaji kutoka afrika huwa na alama za chini sana hasa ikilinganishwa na waombaji kutoka sehemu zingine duniani kama china, korea, ulaya, amerika ya kusini na hata nchi za uarabuni. Maprofesa hapa huwa wanajiuliza inawezekanaje mwanafunzi mwenye azma na ari ya kujisomea ashindwe kupata a (75) ambayo hapa ni c? Na kama hakuna profesa wa kuwafahamisha wanakamati wenzie wanaofanya uteuzi kuhusu mambo yalivyo, mara nyingi maombi ya wanafunzi kutoka afrika huwa hafifu sana na huishia kutupiliwa mbali. Ndiyo maana nahoji hapa kwamba pengine tunawahujumu vijana wetu kwa kuwapa alama za chini na kuishia kuwakosesha ufadhili ambao ungewawezesha kusomeshwa bure. Na sijui mfumo huu unamsaidia nani.
6. Ilivyokuwa kwangu
  • mwaka 1997 nilipata nafasi ya ufadhili wa kusoma shahada za uzamili na uzamivu katika idara ya isimu pale ucla ambapo pia nilitakiwa kufanya kazi kama mwalimu msaidizi wa kiswahili. Barua ya mwanzo niliyopata ilikuwa na masharti mawili yaliyonichanganya na kuninyima usingizi. Sharti la kwanza lilisema kwamba ilikuwa ni lazima nipate "first class" katika shahada yangu ya kwanza na la pili ni kufanya mtihani korofi wa gre.
  • sharti la kwanza liliwashtua watu wengi sana na niliambiwa kwamba kwa muda mrefu kulikuwa hakujawa na mtu aliyepata hiyo "first class". Niliambiwa kwamba pengine hawa jamaa wa ucla walikuwa hawataki niende na niliambiwa kuachana nao kwani walichokuwa wananiomba kufanya kilikuwa hakiwezekani. Kilichonishangaza ni kwamba kulingana na matokeo yangu ya miaka mitatu iliyopita, ningeweza kupata hiyo first class kama ningepata angalau a nne tu katika mitihani yangu ya mwisho ya mwaka wa nne. Na kupata a nne katika masomo 10 niliyokuwa nikisoma eti ilikuwa haiwezekani. Sikukubali!
7. Nilichokifanya na matokeo yake
  • sijawahi kusoma kwa nguvu zaidi, ari zaidi na kasi zaidi kama katika kipindi kile katika maisha yangu yote mpaka nikapachikwa majina ya "librarian", mkazi wa "special reserve", "aliyetumwa na kijiji" na mengineyo. Sikujali!
  • matokeo ya mwaka wa nne yalipotoka nilikuwa nimepata a tisa, b+ moja na b moja. Nilikuwa nimeipata hiyo "first class!" tena nzuri. Haraka haraka niliyatuma matokeo hayo ucla na msimamizi wangu (ambaye anafahamu ugumu wa kupata first class) alifurahishwa sana kiasi kwamba aliiomba kamati ya ufadhili kufuta sharti la mimi kufanya mtihani wa gre. Habari hizi kuhusu gre hata hivyo zilikuwa zimechelewa kwani tayari nilikuwa nimeshaanza maandalizi na nilikuwa nimeshalipia ada (dola 120). Niliufanya mtihani huu ili kujipima nguvu tu lakini first class tayari ilikuwa imesharekebisha mambo. Na hivi ndivyo nilivyoweza kusomeshwa ucla kwa miaka sita (mitatu shahada ya uzamili na mitatu shahada ya uzamivu) huku nikilipiwa karibu dola 30,000 kwa mwaka.
risti ya malipo ya gre
  • ati, kwa nini ni vigumu sana kupata a na hatimaye "first class" katika vyuo vikuu vyetu? Tatizo hasa ni nini? Ni mfumo wa elimu tuliorithi kutoka kwa waingereza? Pengine inabidi tulifikirie jambo hili kwani inawezekana tukawa tunawahujumu wanafunzi wetu kwa kuwapotezea nafasi za ufadhili katika mashirika mbalimbali vikiwemo vyuo vikuu, jambo ambalo si jema hasa katika kipindi hiki ambapo kusema kweli mambo yako wazi sana kuhusu masuala ya ufadhili wa kimataifa.
source:matondo: Kwa nini ni vigumu sana kupata "a" katika vyuo vyetu? Tunawahujumu wanafunzi wetu ???
wa
naowavua chupi awapati a mpwa we upate kirahisi umetunga nao mtihani??ingawa niko na wewe kukomoana kupo pale udsm ndio maana wengine tulipotoka tukhja uraiani tukaona tuduri tena kwingine tutoke...wazo jema ila huko nje marekani kupata a nayo ni hujuma labda hujui sababu wao wanaamini umekuja kufaulu so hata ukifeli wanajua ukiona d hata ndugu zako unaowachangia kwenda marekani awaji tena so ni muhimu ukija huku kama una phd nenda upitishwe na wazee wa kazi uone cha moto kama yako halalii halwaliiiiiiiiiiii
 
ni errors ambazo hata comp ilinikumbusha kuwa nimekosea but sikujali hilo...ni maamuzi. Na we nawe unachanganya mambo, nani amekuambia A za Archaeology zinahusika na hayo mambo? Sikuelewi unapohusisha A na hapo.

Kama we ni msomi usingehukumu elimu ya mtu kwa vitu kama hivyo, siku hizi tunaangalia ujuzi mkuu sio maandishi.

Mimi huanza kuhisi umakini au kukosa umakini kwa mtu kupitia anachokiandika hapa JF.Kama neno la kawaida tu unashindwa kuandika kwa usahihi vipi uaminiwe kwa mambo ya msingi? Jirekebisheni vijana hizi "shorthands" zisizo rasmi na "typos" za maneno ya kawaida hazikusaidieni bali zinakuonesheni ni watu mliokosa umakini.Usiendelee kubishana jirekebishe!
 
sithan kama hizo ndio grade ambazo tunazitumia hapa ud. Nadhani sasa hivi wamebadilisha. Ninakataa. Ila mbona kupata a inawezekana tu ukiamua? Ukiingia na coursewrk ya maana ue mbona unapata tu. Mbona mimi kuna masomo nimeipata?

a zinapatikana sana lakini kwa anaye stahili na si vinginevyo.
 
Nadhani hii ni perception mbovu ambayo wanafunzi wanaijenga towards their LECTURERS. Kama wangebahatika kuona madudu yanayoandikwa kwenye scripts za wanafunzi UE/Tests basi wasingeamini. Kuna wanafunzi hawawezi hata kuandika complete sentence ya kiingereza/swahili. Inakuwa ni vigumu kumuaward mwanafunzi marks ambazo hastaili. Better few A ambazo ni competitive na zinazoreflect quality ya chuo, kuliko A nyingi ambazo ni aibu kwa Institution husika. Imefikia hatua baadhi ya raia wanaotaka kujiendeleza kielimu hasa shahada za uzamili na uzamivu (wengi waliosoma shahada za kwanza vyuo tofauti na UDSM)wanasema bora wakasome MZUMBE/ SAUT kuliko UDSM maana UDSM wamekaa kitaaluma (academics) zaidi. Kule wanauhakika na mambo fulani kama vile kupata A's kwa njia wazijuazo wenyewe (ni tetesi na maelezo kutoka kwa baadhi ya wahusika). Issue UNIVERSITY siyo kupata A issue ni je wewe ni A material? Elimu endelevu kwa Taifa haihitaji kuwekewa siasa na mzaa mzaa. Kama LECTURERS wanabania ili wabaki wachache mbona wapo wengi wanaopata hizo nafasi za kuwa LECTURERS siku hizi? Na isitoshe siyo kila mwenye A anauwezo wa kuwa LECTURER...
 
Back
Top Bottom