Elections 2010 Kwanini ni vigumu kuiba kura katika Uchaguzi Wetu - Tusitafute visingizio

Kwenye hili Mzee Mwanakijiji hatupo pamoja hata kidogo ebu tuangalie hoja yako hii:-

Mtu yeyote ambaye anaweza kutumia muda kufikiri ataona kuwa kama kuna wakati ambapo CCM ilihitaji kuiba kura ni katika uchaguzi wa Dr. Slaa ambapo mara tatu amewaangusha Karatu (na madiwani akapata), Uchaguzi wa Mzee Ndesamburo (Moshi Mjini) au hata uchaguzi wa Arfi kule Mpanda Mashariki. Katika sehemu zote hizo CCM ilikuwa na sababu kubwa zaidi ya kuiba kura kuliko majimbo mengi nchini, kama kweli upo wizi wa kura, kwanini sehemu hizi nyingine na muhimu wameshindwa?

Siyo hapo tu, kama kweli Kura zingekuwa zinaibwa kirahisi hivyo, kwanini wameshindwa kuiba kura Pemba ambapo CUF imeendelea kutesa kwa miaka 15 sasa tangu mfumo wa vyama vingi uende na kwanini kura za Jimbo la Darajani (ambalo nadhani sasa limegawanywa - niko tayari kusahihishwa) haziibwi na matokeo yake zinakuwa za karibu sana?

Majimbo haya tuyaite ni majimbo maalumu ambapo wagombea wa upinzani wanamtandao mkubwa sana wa kuweza kulinda kura zao lakini huwezi sasa ukachukulia mifano hii kiduchu ndiyo hali ya upinzani kwenye majimbo yote.

Hoja hizi haziwazuii mawakala na wasimamizi ambao siyo waaminifu kuiba kura kwa kutoyaheshimu matoeko ya hesabu za kura na kumbeba mgombe asiyekubalika ili mradi tu ana uwezo wa kifedha.


Kwanza kabisa, ieleweke kuwa kura zinapigwa, kuhesabiwa na matokeo yake kutangazwa kituoni (kwa kura za wabunge). Hii ina maana ya kwamba, mwisho wa kura washindi wa kila kituo watajulikana kituoni hapo kwa utaratibu uliowekwa wazi ambapo fomu mbalimbali zinatakiwa kujazwa mbele ya watu wote.


Masanduku yanaletwa kituoni na yote yanakuwa na mihuri (seals). Mihuri inapovunjwa kwa utaratibu maalum na mbele ya watu wote (wawakilishi wa vyama, waangalizi wa ndani na wa kimataifa kama wapo). Masanduku yakishafunguliwa hayahami tena hadi mwisho wa kura na kuhesabu kura na hayaruhusiwi kabisa kutoka hata kwenye jengo yalipo. Masanduku hufunguliwa hadharani, wawakilishi wa wagombea na waangalizi wanaruhusiwa kuyakagua si kwa macho tu hata kwa kuyashika na kuyapapasa ili waone kuwa hayaharibiwa au kuchezewa, wakisharidhika na hatua zote za ufunguzi wawakilishi wote hujaza fomu ya kuonesha kuwa wameridhishwa. Masanduku huwekwa mahali pa kupigia kura ambapo panampa mtu hifadhi. Lazima yawe mahali ambapo yanaweza kuonekana, hivyo hayawezi kuwekwa kwenye chumba kilichofichwa.
Kwenye uchaguzi wa jimbo la Starehe nchini Kenya, Askofu Magreth Wanjiru ndiye aliyetangazwa kuwa alikuwa ni mshindi wa jimbo hilo wakati ambapo mgombea wa PNU Bw. Maina Kamana alipoenda mahakamani na kudai kura zirudiwe kuhesabiwa ndiyo ikaja kubainika ya kuwa kumbe Askofu Magreth Wanjiru hakushinda kiti kile mbali ya kuwa tayari alikwisha kuapishwa hata kuwa Naibu Waziri.

Hivyo hoja zako juu ya uhimili wa Mahakama haupo kabisa kwa sababu hakuna hoja zilizowahi kwenda mahakamani kuchunguza kama kweli fomu ya majumuisho ya kura ndiyo iliyo na matokeo halisi ya kura kama zilivyopigwa kwa maana ya kuhakikiwa.



Hivyo hoja zako hizi hapa chini ambazo hazijawahi kupimwa na mahakama zetu hazitusaidii sana katika kutuongezea ufahamu wetu wa nafasi ya mahakama zetu katika kuthibitisha uchakachuaji wa matokeo:-

Ipo imani ambayo imejengeka kuwa ni rahisi kwa kikundi cha watu au watu kuiba kura na kumuongezea mtu mwingine kura kinyume cha sheria. Watu wenye imani hii (naiita imani kwani hakuna ushahidi wowote kuwa kura zimewahi kuibwa, yaani ushahidi unaoweza kusimama Mahakamani!) huwa na wasiwasi kuwa uchaguzi unapofanyika basi kuna makundi ya watu ambayo yanakula njama kuiba kura na kubadilisha matokeo.
Uchakachuaji wetu wa matokeo huwa sana sana ni kughushi fomu ya matokeo na kumtangaza mgombea ambaye wapigakura walimkataa. Kwa kufanya hivyo wanakuwa wasimamizi na mawakala wameshirikiana katika kupika matokeo kwa manufaa yao wenyewe ya kuhongwa. Hata wewe hili umeliona kama ulivyosema hapa chini:-
Lakini, kura zaweza kuchezewa lakini ili zichezewe kunahitaji ushirika wa zaidi ya mtu mmoja. Yaani, msimamizi wa kituo, wawakilishi wa wagombea, waangalizi wa ndani na wa nje na vile vile wapiga kura wenyewe.
Njia hii wapigakura hatuna sauti nayo sana kwa sababu hatumo ndani ya vituo vya kupigia kura ambako huwa kura zinahesabiwa kama wenzetu wa Kenya.

Njia mbadala ya kuchakachua matokeo ni ile ya kuingiza kura za bandia baada ya kura kuhesabiwa kwenye vituo. Hili zamani kwetu uwezekano ulikuwa haupo lakini sasa lawezakana sana baada ya NEC kufuta utaratibu wa wapigakura kuwepo mita 200 kutoka kwenye eneo la kupiga kura.

Wapigakura wangeliweza kabisa kuzuia maboski ya kura yasiingizwe kwenye vyumba vya kupigia kura na ieleweke wenye miliki wa chaguzi si vyama vya siasa ila ni raia wote hivyo hoja za kuvimilikisha vyama vya siasa miliki hiyo kama ulivofanya hapa chini si sahihi hata kidogo:-

Chadema imepewa nafasi ya kihistoria kushinda uchaguzi, ilijua kwa miaka mitano kuwa mwaka huu kutakuwa na uchaguzi na inajua taratibu zote za uchaguzi - hivyo walitakiwa wawe wamejiandaa vya kutosha. Kama hawakujiandaa vya kutosha kupata wawakilishi wa kutosha kwenye kila kituo hili si tatizo la NEC wala CCM! Chadema inahitaji kushinda kisiasa kwa kuwafanya watu wengi wakipigie kura kwani ni kura zilizopigwa tu NDIZO zinazohesabiwa siyo zinazoombewa, kunuiwa au kusubiriwa mawazoni.
Kauli zako za kutubeza wenye hofu na mfumo uliopo zinakera na kusikitisha mno kwa sababu tupo kwa ajili ya vizazi vijavyo na wala siyo kwa mahitaji yetu wenyewe:-

Ukweli ni kuwa wenye hofu hii ya "wizi wa kura" ni kwamba hawajui upigaji kura wetu ulivyo na kwanini hatua zilizochukuliwa mwaka huu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi zitachangia sana kuondoa wasiwasi wa wizi wa kura.
 
Mzee Mwanakijiji, Mapembelo/Lamwihe!
Imeniuma kwani tukio lilihusisha jirani zangu.
Mfumo unaweza kuwa tofauti na huu wa sasa lakini bado wizi ulifanyika nab ado naamini unaweza kufanyika.
Msanduku ya kura yalipohitajika kuletwa kwenye central unit ya kufanyia MAJUMUISHO, kilichotokea ni kuwa kwa kuwa masanduku yalikuwa yanatokea sehemu tofauti na hivyo zoezi zima la kuhesabu ( Majumuisho) lilibidi kusubiri hadi kila kituo kiwasilishe masanduku yake, mara vituo vyote vilipotimia kuwasilisha masanduka na kwa kuwa kuna wengi walikaa kusubiri wenzao. Msimamizi Mkuu aliamua kutoa muda wa watu wote kwenda KULA. Na kwa kujiamini aliagiza kila mwakilishi au wakala kufunga ula mlango wa jingo lile kwa kufuli lake endapo atakuwa na mashaka ( kwa maana ya mafukuli ya ziada, ukiachia lile la Msimamizi Mkuu).
Nini kilitokea? Kumbe ndani ya lile jingo kulikuwa na watu ndani ya DALi tangu usiku wa manane na masanduku ya KURA zilizopigwa tayari kwa Mgombea wa chama TAWALA. Na mara baada ya kuondoa wale walishuka CHINI na kubadilisha KURA ,kuondoa za Mpinzani ambaye alipewa nafasi kubwa ya kushinda na kuweka za mgobea wa CHAMA tawala ambaye hakuwa na nafasi KABISA ya USHINDI.
Waliporudi na kuanza kuhesabu kwa jili ya majumuisho, Mawakala waliishia kushangaa na kilichokuwa kinatoka kwenye MASANDUKU. KURA za Mgombea wa UPINZANI zilizotolewe kwenye yale MASANDUKU zilikutwa zimetupwa MTONI.
Fuatilia habari hii kanda za Juu KUSINI utaipata… KURA ZINAIBIWA na siyo STORI…
 
Hivi huwa uwezi kuandika kwa kifupi? Wizi wa kura upo, inasemekana mawakala upewa mlungula halafu matokeo yanapinduliwa! Ila kwa upande mwingine ni watanzania wengi kutokana na uelewa wao mdogo juu ya vyama vingi wanaipigia kura CCM. Mfano, nimemuuliza mtu kama atapiga kura na atamchagua nani. Akasema atamchagua JK ingawaje afanyi vizuri; sababu ni kwamba wapinzani watatuburuza. Hivyo bado kuna ukungu kwenye akili za watanzania wengi hasa less educated (na huu ndio mtaji mkubwa wa CCM) na elimu ya uraia bado sana!

Unakumbuka hadithi ya Bush na Gore kwenye uchaguzi wa USA, computer ilionesha Bush mshindi lakini manually Gore alikuwa anaongoza. Gore aliamua kutunza heshima ya USA kuamua kukubali matokeo.
 
... Wapiga kura tumpigie Dr.Slaa kwa wingi ili wizi wao ushindikane. Margin kati ya Dr.wa ukweli na wa kuchakachua iwe kubwa.
 
Kura zinaibwa! Ukitaka kufahamu hilo;-
ulinza kwanini Channel ten ilifungiwa mwaka ule wa......
kwanini Bakari Kingobi amekuwa mkurugenzi wa Jiji la Dar
na mengine meengiiiii
 
Mwanakijiji;

Mwaka 1995 kulingana na takwimu za mawakala wa CUF kule ZNZ ilionyesha kuwa Maalim Seif kashinda kwa asilimia kubwa dhidi ya incumbent Dr Salmin Amour lkn matangazo ya ZEC yalimpa ushindi Dr Salmi kwa aslimia 50.1 dhidi ya 49.9 za CUF!

CUF walienda hata kwenye jumuia za kimataifa kuomba warudie tena kujumlisha matokeo ya kura ya vituo vya uchaguzi lkn ZEC ikasisitiza tena na tena kuwa matokeo waliyotangaza ni halali na hawatarudia tena kujumlisha matokeo;machafuko yaliyotokea hapo baadae hamna asiyeyajua!

Wasi wasi wangu ni kuwa hata kama Dr Slaa atashinda,na hata kama mawakala wa CHADEMA watafanya kazi nzuri sana ya kuwa makini kwenye vituo vya kura,lkn je kama NEC ikatangaza matokeo jinsi wanavyotaka wao na kwa hiki kipengele kinachosema NEC haipingwi popote pale tutafanya nini?

Hapa ndio penye shughuli je tutakimbilia wapi?
 
Mkuu, to me umetoa somo zuri sana. Nadhani hiki ndicho NEC ilitakiwa kuhubiri. Wengi wetu hatujui huu mchakato. Kwa kweli nimeelewa how it works na umenipunguzia wasi wasi mkubwa wa uchakachuaji. Hongera mkuu kwa kutupa elimu.
 
Mzee Mwanakijiji, Mapembelo/Lamwihe!
Imeniuma kwani tukio lilihusisha jirani zangu.
Mfumo unaweza kuwa tofauti na huu wa sasa lakini bado wizi ulifanyika nab ado naamini unaweza kufanyika.
Msanduku ya kura yalipohitajika kuletwa kwenye central unit ya kufanyia MAJUMUISHO, kilichotokea ni kuwa kwa kuwa masanduku yalikuwa yanatokea sehemu tofauti na hivyo zoezi zima la kuhesabu ( Majumuisho) lilibidi kusubiri hadi kila kituo kiwasilishe masanduku yake, mara vituo vyote vilipotimia kuwasilisha masanduka na kwa kuwa kuna wengi walikaa kusubiri wenzao. Msimamizi Mkuu aliamua kutoa muda wa watu wote kwenda KULA. Na kwa kujiamini aliagiza kila mwakilishi au wakala kufunga ula mlango wa jingo lile kwa kufuli lake endapo atakuwa na mashaka ( kwa maana ya mafukuli ya ziada, ukiachia lile la Msimamizi Mkuu).
Nini kilitokea? Kumbe ndani ya lile jingo kulikuwa na watu ndani ya DALi tangu usiku wa manane na masanduku ya KURA zilizopigwa tayari kwa Mgombea wa chama TAWALA. Na mara baada ya kuondoa wale walishuka CHINI na kubadilisha KURA ,kuondoa za Mpinzani ambaye alipewa nafasi kubwa ya kushinda na kuweka za mgobea wa CHAMA tawala ambaye hakuwa na nafasi KABISA ya USHINDI.
Waliporudi na kuanza kuhesabu kwa jili ya majumuisho, Mawakala waliishia kushangaa na kilichokuwa kinatoka kwenye MASANDUKU. KURA za Mgombea wa UPINZANI zilizotolewe kwenye yale MASANDUKU zilikutwa zimetupwa MTONI.
Fuatilia habari hii kanda za Juu KUSINI utaipata… KURA ZINAIBIWA na siyo STORI…

Mawakala wa Chadema habari ya kwenda kula kula haifai kabisa. Nilikwisha sema chukueni maji ya kunywa ya kutosha, chukua chakula cha safari cha kutosha, chukueni huduma ya kwanza (panadol), msipokee chakula cha aina yoyote kutoka kwa mtu yoyote, sheria haisemi kama kutakuwa na muda wa kula, pia mchunguze mazingira yote ya kupigia kura chumba kilivyo na mianya yote.
 
Ibara ya 41 (7) "Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake." ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inabariki wizi wa kura kwenye ngazi ya Urais. Kama wizi hakuna Ibara hii kwa nini isisomeke kinyume?
 
Ni dhahiri kuwa, CHADEMA na vyama vingine vya upinzani kuna haja ya kuhamasisha wananchi umuhimu wa kujitokeza kupiga kura. Hilo ni jambo ambalo kweli ni wajibu wetu sasa na liko kwenye uwezo wetu. Kuna watu wasiojua hata vitambulisho vyao vilipo wakati huu. Naendelea kusema, wewe Mtanzania chukua nafasi yako kufanya kile kilicho kwenye uwezo wako kwa sasa, hicho ni kuhakikisha unampa kura yako kiongozi unayeona anastahili, na si kwa mazoea. Hebu fikiri iwapo hizo mbinu zote za kuiba au kubadili hayo matokeo zisipofanikiwa na wote tukawa tumepiga kura kwa hekima na si mazoea!!!!
Wako wanaosema ati iwapo chama kama CHADEMA kitachaguliwa, viongozi watakuwa watu wasio na elimu wala uzoefu, naomba hili nalo tulijadili, Je katiba ni msahafu au biblia ambayo haiwazi badilika? What are the possibilities? Mimi naamini kuna watu wengi ambao wanabaki kuwa wanachama wa CCM kwa sababu za hofu na kimazoea, ati ili nitoke au niwe kwenye nafasi fulani nahitaji kuwa mwana CCM! Mtanzania mwenye utashi na elimu ya kutosha unaishi kwa jinsi hiyo! Tunaelekea wapi?
 
Hapa ndipo nawakumbuka... Rais Mugabe na Waziri Mkuu Tsvangarai, namkumbuka Rais Kibaki na Waziri Mkuu Odinga....oh bado niko Afrika....labda nikimbilie Iran sasa......no mbona harufu ya Bush na hotdog za florida inanijia....no no no narudi Zanzibar...1995 jinsi mwalimu alivyosafiri ghafla kuelekea Zanzibar muda mchache kabla ya tume ya uchaguzi kutangaza matokeo huku maneno yakipita chini chini kuwa Seif kashinda...........oh.....nimesahau....nakumbuka sasa....mzee Kingunge alivyosafiri kwa mtindo huo huo mwaka 2005....loh jamaa walivyokimbilia mombasa na kuwa wakimbizi!!!!!!....inatosha...mzuka usije ukapanda.....

Kura tutapiga tu.....lakini hatutakuwa vipofu...wala viziwi.....'don't even dare'
 
mzee mwanakijiji.
kwanza nashukuru kwa hii thread yako, imenielimisha sana, wengi wetu tumakalia kusema kura zitaibwa lakini seriously hakuna hata mmoja anaesema ZINAEBWAJE? kimantiki. so idea imebaki kuwa too hypothetical kiasi kwamba kwa mimi mpiga kura kwa mara ya kwanza najazwa tu hofu za kufikirika lakini sijathibitishiwa kiuhalali kwamba hicho kitu hufanyika. so wale ambao mmeshapiga kura hapo kabla like 2005, tuelezeni kimantiki huo wizi ukoje kiuutaaalam, na si kusema mara masanduku darini,tiki ya huku inahamia huku nk. asanteni.
 
Anachosema mwanakijiji ni kuwa...Jukumu letu watanzania ambao tumejiandikisha kupiga kura ni kwenda kutumia haki yetu ya kupiga kura siku ya Jumapili tarehe 31 Oktoba; Period!
Hofu ya kuibiwa kura iliyopo miongoni mwa wanajamii ni kubwa na ndio itakayopelekea wananchi wengi waliojiandikisha kukata tamaa ya kupiga kura. Kuna watu wengi sana, hususan vijana ambao walikosa kujiandikisha, kwa kuwa waliona hamna maana yoyote ya kufanya hivyo kwani kwa mtazamo wao hata wangejiandikisha na baadaye wakapigia kura vyama vya upinzani, CCM itashinda tu (kwa hofu hiyo hiyo ya kuibiwa kura)

Na sasa kuna baadhi ya wengi waliojiandikisha wameshaanza kuwa na hofu ya kuibiwa kura na kuona kwamba hata siku ya uchaguzi ukifika hawataenda kupiga kura kwani CCM itashinda tu, na hata kama watapigia kura upinzani, CCM wataiba kura na kuwa washindi.

Hii hofu ni mbaya na ndio maaana Mwanakijiji anasema kazi yetu sisi tuliojiandikisha ni kwenda kupiga KURA siku ikifika.
 
Sasa Mwanakijiji kama uwazi wote huo na ulinzi wote huo ni wakulinda kura zisiibwe why can't you think other way round kwamba hata wale wezi nao wamebuni mbinu mpya ya kuibia ambayo hata wewe hujaijua? Maana naamini kwamba hakuna jambo ambalo linaweza kusemwa wakati hata sampuli yake au mfano wake haupo. Hata hiyo imani unayosema kama haina matendo hiyo siyo imani kwa hiyo imani lazima iwe na base na kwa base hiyo ndio maana tunasema kuna wizi wa kura.Haya wakati huu wa uchaguzi kuna watu wananakiri namba za shahada na wengine wananunua shahada zenyewe sasa tunajiuliza wanataka kuzifanyia nini? Sio kuibia kura?
 
Mawakala wengi wanakuwa uwt awe wa upande gani ni mapandikizi tu wachache wanakuwa warahisi kuhongwa tu na kuahaidiwa Ukuu wa wilaya nk. MKJJ usilinganishe nchi nzima na Moshi au Tarime, maana huko watu wanamwamko wa kipekee kisiasa. Huko CCM imeadabishwa sawa sawa maana mpiga kura anapewa hongo na anaahidi kabisa kuwa atawapigia kura lakini anafanya kile anachoona kinaifaa jamii. Zaidi ya hapo wahusika kulinda kura hawalali. Fanya utafiti utajua nguvu wanayotumia kuhakikisha haki yao haiibiwi wala kununuliwa. Kwa sasa kuna mwelekeo kuwa sehemu nyingi nguvu hii ya uamuzi wa hiari inaanza kuenea. Mungu ibariki Tanzania.
 
jamani.. zinaibwaje? zamani ilikuwa rahisi kwa sababu sanduku linapakizwa kwenye baskeli kwenda kuhesabiwa sehemu nyingine.. siyo mnasema "wizi upo" kinadharia inawezekana lakini mtu aniambie unawezekana vipi? Wildcard anasema kuwa Zanzibar waliiba ah wapi!, kuna suala la Tume ya Uchaguzi kuingiliwa hilo limetokea Kenya na ninaamini ndilo lenye uwezekano mkubwa wa kutokea Tanzania mwaka huu..

MKJJ
Siku zote mamuluki hutumia njia nyigi za kuingia madarakani, mojawapo ni kuiba kura.
Uchaguzi wa serikali za mitaa pale Mbagala masanduku ya kura yaliibwa na kufichwa na baada ya wiki mbili yakaonekana yamechimbiwa chini na yalikuwa na kura. Na CCM walishinda hiyo mitaa.

Hivyo basi wizi wa kura upo. Wakijua kuwa eneo hilo uwezekano wa kushindwa ni mkubwa wako tayari kuiba masanduku ya kura. Hivyo basi kulinda kura ni mhimu. Kama wao wenyewe kwenye kura za maoni wameibiana sembuse kwenye uchaguzi huu
 
Mzee Mwanakijiji,

Umeeleza kwa ufasaha lakini mbinu za wizi ni nyingi. Mwaka 1995 UDSM masanduku ya kura yalifika saa 7 mchana watu wakapiga kura mpaka usiku kwa shinikizo maalum maana upinzani ulikuwa juu. Mimi nilipiga kura saa mbili na nusu usiku. Wakati tunajiandaa kushangilia matokeo, Tume ikazuia matokeo na badala yake ikatangaza uchaguzi kurudiwa DSM. Watu wakakata tamaa kwenda kurudia uchaguzi na mbinu hii ikafanikisha CCM kushinda. Mwaka huu wapiga kura kwenye ngome za vyama vya upinzani wajiandae na mizengwe, mara masanduku yamechelewa, mara karatasi hazitoshi, mara umeme kukatika wakati kura zinaendelea kupigwa, mara uchaguzi urudiwe n.k Haya tumeyaona kwenye kujiandikisha tu: mara kamera haitoi picha kwa sababu ya mawingu nk

TUKOMAE HATA IKIBIDI MAWAKALA WAWE NA KURUNZI KWENYE VYUMBA VYA KUPIGIA KURA KWA AJILI YA DHARURA. HAKUNA KULALA

Endapo mgombea anapiga kura na matokeo yanaonyesha hajapata kura yoyote inahitaji zaidi ya akili ya kawaida kuelewa!

Just thinking aloud!!!
 
Wizi hupo tu msibishe endapo Chadema haitapata mawakala waaminifu wenye kuweka uzalendo mbele jamaa watawadakisha mshiko mzuri na watafunga macho na chochote kinawezekana. fedha sabuni ya roho. Yesu alisalitiwa kwa vipande 30 vya fedha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom