Kwanini nchi maskini kama tanzania inapoteza raslimali nyingi kwa tafrija?

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Rais wa China yuko Marekani kwa ziara rasmi na jioni hii rais Obama atamwandalia dhifa ya kitaifa, hii itakuwa ni mara yake ya tatu tangu aingie madarakani kufanya hivyo. Viongozi wengine wote wanaofanya ziara rasmi Marekani kwa kawaida anawaandalia cha kawaida "working lunch". Kwetu hapa kila kiongozi wa nchi anayefanya ziara rasmi hapa nchini uandaliwa dhifa ya kitaifa; hivyo kwa mwaka mmoja uandaliwa dhifa nyingi za kitaifa. Tunashindwa nini kujifunza kutoka kwa wenzetu juu ya matumizi mazuri ya raslimali ya nchi.
 
Hakuna vipaumbele sahihi vya jinsi ya kutumia rasilimali na viongozi wetu hawana uchungu nazo wala wa wananchi wao,ndo maan kila mmoja anafanya kufurahisha nafsi yake.....Nakumbuka baada ya kupita kwa katiba mpya Kenya Makamu wa Rais alifanya tafrija,kwenye bunge lililofuata wabunge wakahoji umuhimu wa tafrija na hela zilizotumika zilitoka wapi???Hapo Kenya,sasa nchi hii watu hawako accountable na matumizi ya hela,very few people have guts to ask,ndo maana wataendelea kufanya hayo,pengine KATIBA mpya itakuja na solutions..........:A S 39:
 
Back
Top Bottom