Kwanini naamini CHADEMA itashinda Arumeru.

FortJeasus

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
603
397
Wiki moja tangu kuzinduliwa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki, nimeamua nifanye tathimini juu ya mwelekeo na mwenendo wa vipengele (components) 6 kama vilivyojidhihirisha na kisha kufuatiliwa na kuzingatiwa.Ili kuweza kuelewa mantiki iliyo nyuma ya hitimisho hapo juu,tuangalie viashiria (indicators) ambavyo kwazo mwenendo mzima wa kampeni umepimwa:

1.Kama kawaida,kampeni za CDM zimekuwa,kutokana na kuongozwa na wajenzi mahiri wa hoja, hususani Nassari, zikiongozwa kwa nguvu za hoja,zenye kushawishi akili,zinazovuta hisia za wasikilizaji, zikiambatana na masuluhisho ya matatizo mbalimbali ya wana -Arumeru.Kwa mfano ,tatizo la ukosefu wa ardhi linalotokana na kumilikishwa wawekezaji huku wananchi wakiachwa bila rasilimali hiyo muhimu.

2.Upepo mbaya unaovuma dhidi ya CCM kwa kushindwa kutatua matatizo yanayowakumba wakazi wa Arumeru Mashariki kama vile maji na ardhi,huku makada kadhaa wa CCM wakiwaaminisha wananchi kuwa sasa umefika wakati wa kutatua matatizo hayo kwa sharti kwamba wapewe kura za ubunge kwa mara nyingine tena.Inavyoelekea ,wananchi wengi wameikataa hoja hii.Hili lina mfanano wa kimantiki na harakati za miaka ya 1960 za kudai uhuru wa Tanganyika , ambapo mkoloni alitaka akubaliwe kuendelea kutawala licha ya kushindwa kuboresha maisha ya Watanganyika, kwa kutotoa huduma bora za jamii ,pamoja na kushindwa kuheshimu na kuthamini ubinadamu wetu.Sote tunafahamu Kambarage na wanaharakati wenzake ,wakiungwa mkono na Watanganyika wenzao, hawakuwa tayari kuendelea kuwapa wakoloni fursa ya kututawala,wakiamini kuwa haiwezekani kupata jibu tofauti kwa kuendelea kutumia mbinu zile zile.

3.Udhaifu wa kampeni za CCM, unaochangiwa , kwa kiwango kikubwa na uwezo mdogo wa kujenga hoja za kiakili unaoonyeshwa na mgombea wake, pamoja na udhaifu wa haiba na kimaadili miongoni mwa baadhi ya makada wa CCM wanaoongoza kampeni Arumeru.Aidha makada hao,tena wanaoonekana wamepata kupita shule,wanawaghilibu wananchi kuwa eti CHADEMA hawana serikali na hivyo hawapaswi kupewa nafasi ya kutoa mbunge Arumeru Mashariki!!Iwapo hoja hii ina ukweli wowote, inashangaza kwa nini wahusika hadi sasa hawaelezi kwa nini serikali hiyo hiyo ya CCM ,imewapa wana Arumeru fursa ya kuchagua mwakilishi wake!Wala hawataki kueleza kuwa maendeleo (uwekezaji ktk huduma za kijamii na kiuchumi) ni haki ya msingi ya wananchi, kwanza kama walipa kodi wa nchi hii, na pia kama watu wenye uhalali na mamlaka ya kikatiba kupata ama hata kudai haki za kiuchumi,kisiasa,na kijamii ,pasipo kuzingatia ufuasi,uanachama wa chama cha kisiasa.

4.Kama ilivyo hulka yake,CCM inaendelea kuamini na kutumia muda mwingi kwa kupiga nyimbo za mipasho kanakwamba hii ni silaha kuu mikononi mwake -ingawa ni sehemu mojawapo ya kampeni -na kupoteza muda ambao ungeweza kutumika kujadili masuala muhimu na kuvutia kura.

5.Faida ya kijiografia.Arumeru Mashariki inapakana kwa karibu kabisa na jimbo la Arusha Mjini, Hai na Moshi Mjini, na kupelekea majimbo haya kuwa na maingiliano makubwa ya kijamii ,kibiashara na kisiasa sawia. Imedhihirika, sasa, wana- Arumeru wamehamasika na sasa wapo tayari kufanya kile kilichopata kufanywa na jirani zao:kuikataa CCM na matendo yake.

6.Kutokana na pointi namba 5 ,upo uwezekano mkubwa wa kupata mawakala waaminifu kwa kutilia maanani kuwa, pamoja na umuhimu wa kufanya kampeni makini, ni lazima wapatikane mawakala imara na walinzi wa kura .Kwa kuwa Arumeru ipo jirani na Arusha Mjini na Moshi Mjini - maeneo yenye Vyuo kadhaa vya Elimu ya Juu ,na ambapo CDM ina makada wa kutosha - kuna uhakika wa kupata mawakala waaminifu kwa chama. John Mnyika ,mwaka 2010, pamoja na kutumia wananchi wa kawaida walio waaminifu kama mawakala, alitumia pia na vijana wa Vyuo vya Elimu ya Juu wa Dar er Saalam walioimarisha usalama wa kura.
Nawasilisha.
 
ushauri wa bure :chadema lazima wawe hatua mbili mbele ya tume ya uchaguzi.
tatizo siyo kukubalika ila ni kutengeneza mtandao mzuri wa kuweza ku monitor usambazaji wa masanduku, upigaji kura kwa kuhesabu watu wote wanaopiga kura maana yangu ni kuwa chadema lazima wawe na agent wa ziada wa kuhesabu kila mtu anayekuja kupiga kura, na zoezi la kuhesabu kura hapa lazima kura zihesabiwe na matokeo kutumwa kwa haraka kwa wahusika wa chadema ili kufanya majumuisho kwahiyo ni lazima kila polling agent wa CDM lazima awe na cell phone ya kuweza kuwasiliana na wahusika in case of anything including kutuma matokeo ya kituo mara baada ya kuhesabiwa ili kabla ya matokeo kutolewa na tume sisi tayari tuwe na matokeo ahead of tume ya uchaguzi ili ktk majumuisho ya kura ya mwisho tume isitupige bao.
 
Mkuu,ni imani yangu kuwa ushauri wako makini utafanyiwa kazi na wahusika.
Ulinzi wa kura ukiimarishwa, Nassari atatangazwa mbunge wa Arumeru mashariki
 
Cdm kazana!! Karibu kitowewo (ccm) kinastop kuhema. Weka makucha chini.
 
Kujipa moyo sio mbaya hata kidogo ila kujidanganya kwa kiasi hiki ni hatari
 
Kujipa moyo sio mbaya hata kidogo ila kujidanganya kwa kiasi hiki ni hatari

Lazima wewe utakuwa cyo mtanzania.Uko hapa Tz kwa muda tu baadae utarejea kwenu somalia.Haiwezekani kijana mdogo kama wewe uwe na mawazo mgando kama hayo.Watu wa uhamiaji inatakiwa wafanye kazi yao kwa umakini zaidi ili wakupate na wewe.Mzalendo wa Tz hawezi kuwa kama wewe.
 
ccm wanajipaka mfano leo tume imetoa taarifa kuzuia utumiaji wa form no 17 hii ina maana kuna watu zaidi ya 4000 watashindwa kupiga kura kwani kwa taarifa za viongozi wa ngazi za juu wa chadema wanasema kuna kadi zaidi ya 4000 kwenye vituo 3 vya polisi yaani tengeru, usa, maji ya chai......
 
Attachments

  • Mpasuko%5B1%5D%5B1%5D%5B1%5D.jpg
    Mpasuko%5B1%5D%5B1%5D%5B1%5D.jpg
    19.5 KB · Views: 49
Uzini , igunga maneno yalikuwa haya haya . Tarehe 1 siyo mbali .
 
Hivi kwa akili yako unadhani CDM watashinda Arumeru?

Mimi natoka Arumeru Mashariki kata ya Mbuguni. Kwa taarifa yako kata za ushindi ni Mbuguni, Makiba, Kikwe, Karangai na Usa River. Kule ccm ilishazikwa. Licha ya ccm kutenga pesa zaidi ya 30million kwa ajili ya hongo, bado kauli mbiu ya Kula ccm Kura CDM itawaumbua. Ni suala la muda tu kabla ccm haijapotea kabisa kama chama cha siasa.
 
Wapiga kura wengi ni CCM, wahudhuriaji mikutano ya kampeni wengi ni wafuasi wa CDM. Pasipo shaka CCM inaungwa mkono katika kata nyingi dhidi ya hizo chache za CDM; HIVYO CCM atapeta!!!!!
 
CDM haikuwa na ngome Uzini na Igunga na ikatikisa kiasi cha CCM kukosa usingizi. Vipi kuhusu Arumeru penye ngome na mtandao ulioimarika?
 
Back
Top Bottom