Kwanini muungano usiongelewe kwenye maoni ya katiba?

Kasimba G

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
3,428
2,609
Nilishangaa kusikia hotuba ya Rais “ikikataza” kuongelea Muungano! Nilifikiri kuwa maoni ya wananchi ndiyo yapewwe kipaumbele kwa kuwa wananchi ndio wenye mamlaka na nchi yao kumbe sio! Mashaka ya wengi juu ya kumpa Rais mwenyewe kutoa hadidu za rejea yameisha dhihilika ni ya ukweli.

Nadhani mambo yooote, yangeongelewa, hata muungano, kwani muungano aliuweka Mungu na kutoa masharti tusiujadiri? Kama ni mawazo ya wanadamu, ni laazima ujadiliwe na kama ikiwezekana uboreshwe kama kuna kitu cha kuuboresha.

Nawasilisha.
 
“Jamani Watanzania wenzangu wa Shinyanga, naomba tuzungumze kidogo hili la Katiba mpya, kwanza nawaomba msibweteke eti kwa sababu tume imeundwa, kuundwa tume hakuleti katiba mpya na bora. Pia tunataka Kikwete ajue kuwa Watanzania hawatengenezi katiba ya Kikwete wala ya CCM. Wanataka Katiba mpya na bora ya kwao.

“Nami namuomba ni bora akajitahidi kujiepusha na matamko ya ajabu, maana anaendelea kutupatia ajenda. Anasema suala la muungano lisijadiliwe wakati wa mchakato wa utoaji maoni. Hapa anataka kutuma ujumbe gani…” alisema Dk. Slaa na kushangiliwa.

Akiuchambua muungano, Dk. Slaa alisema ni haki ya Watanzania kwa maana ya wale wa Zanzibar na wa Bara kujadili muungano wanaoutaka kwani kufanya hivyo hakuna nia ya kuuvunja.

“Sisi CHADEMA tunasimamia nini? Tunataka Watanzania wajadili wanataka muungano wa aina gani, tunataka Zanzibar ipate haki zake kama ilivyokuwa mwaka 1964.

“Hapa hoja si muungano uwepo ama usiwepo, hoja ni aina gani ya muungano wa kisiasa Watanzania wanautaka. Tunaamini kuwa hakuna mwanasiasa mwenye akili timamu anaweza kuhubiri kuvunja muungano.

“Mwanasiasa anayezungumzia kuvunja muungano huyo ni mwendawazimu, maana muungano wa kweli wa Watanzania uko kwenye damu zao. Lakini katika suala la kiutawala wananchi waachwe waamue wanataka aina gani, hii ndiyo hoja hapa,” alisema Dk. Slaa.

Akifafanua, Dk. Slaa alisema wanazo taarifa kwamba tayari CCM kupitia katika Halmashauri Kuu yao ya Taifa wameshafikia hatua ya kuwatumia makada wao, wakiwamo viongozi wa kiserikali kama wakuu wa mikoa na wilaya katika kuhakikisha yale ambayo chama hicho tawala kinayataka, yanaingizwa katika Katiba mpya.

“Napenda kumwambia haya huku akijua kuwa, mkononi kwangu au ofisini kwetu tayari tunao uamuzi wa Halmashauri Kuu ya chama chao, ambayo imewaagiza viongozi ambao ni makada wao, kuhakikisha masuala ambayo chama hicho kinataka yanaingia katika Katiba mpya, hii ni hatari,” alisema Dk. Slaa.
 
Kaka Kisimba mimi nilimsikiliza rais, sikusikia akisema kuwa tusiujadili bali alisema hapa hatuendi kujadili au siyo katiba ya kuvunja muungano. unless nilimquote tofauti.
 
Spot on Dr. once again.

CCM wanajua the least that will happen is the change of Muungano Sturcture. The worst to happen could be the death of it naturally thru malfunctionality due to the existing mechanism.

So what's next? well ccm had to desparately hung on rhetorics and threats, which will soon be exposed as unworkable and hazardious costly.
 
Okay, lakini nadhani dhana iliyopo ni kutokuujadili wakati kwa cases za tanganyika na zanzibar kama nchi mbili ndio theme kubwa zaidi ya kujadiliwa, ndio maana tunajadili hapa ili wajumbe wasitumeze kwa kusema haustahili kuujadili!
 
Mie kama nilimvyomuelewa Raisi ni kwamba watu watapewa kujadili kuboresha muungano na si kuvunja muungano! mie nakubaliana naye kwani kuna wahuni ambao wanakuja na kauli za kibaguzi kama kina jusa! watu hawa hawafai na raisi anajua ndio maana kaweka hicho kikwazo! jadili namna ya kurekebisha na kuboresha muungano na si kuuvinja! hiyo ndoa haitavunjwa ila njoo na mawazo ya kuifanya ndoa imeremete
 
Mie kama nilimvyomuelewa Raisi ni kwamba watu watapewa kujadili kuboresha muungano na si kuvunja muungano! mie nakubaliana naye kwani kuna wahuni ambao wanakuja na kauli za kibaguzi kama kina jusa!

watu hawa hawafai na raisi anajua ndio maana kaweka hicho kikwazo! jadili namna ya kurekebisha na kuboresha muungano na si kuuvinja! hiyo ndoa haitavunjwa ila njoo na mawazo ya kuifanya ndoa imeremete
Ha ha ha ha ha! Hapo kwenye red - bibi yamemshinda anahisi hapati haki yake, kapata libwana lingine la kiarabu sasa anaomba talaka.

Hii ndoa ni "hadi kifo kitutenganishe" wasidhanie ni zile ndoa za kwenda kuchungulia nyumba za wanaume na kuondoka ambazo unakuta "msichana" wa miaka isiyozidi 40 kishaolewa na kuachika mara tano!
 
Kwahiyo ndoa yetu na zenji ni ya kikristo! Haa! Ha ha ha! Hamna kuachana, kuna kuvumuliana tuu
 
mkiita ndoa,mkiita koloni lenu,mkiita muungano, semeni mtakavyo. mshatudhulumu sanaaa sasa wazanzibar washaamka wanataka nchi yao kwa gharama yoyote ile... ao wanosema tusijadili kuvunja muungano wanajifurahisha 2 na mm nadhani hawaijui hisoiria ya zanzibar au wanajitia upofu .TANGA LISHAJAA UPEPO ZANZIBAR IYOO INAONDOKA
kama shida yenu TZ kaunganeni na ZAMBIA ......ndugu zetu wa damu tutakutana New york (UN).
 
:welcome:Lum amethibitisha hili,
mshatudhulumu sanaaa sasa wazanzibar washaamka wanataka nchi yao kwa gharama yoyote ile... ao wanosema tusijadili kuvunja muungano wanajifurahisha 2 na mm nadhani hawaijui hisoiria ya zanzibar au wanajitia upofu .TANGA LISHAJAA UPEPO ZANZIBAR IYOO INAONDOKA

Kwa kweli kwa mwendo huu nasema tena Rais wacha watu wajadili kama wanapenda kuendelea na Muungano na kisha wengi tukikubali tuamue sasa tuendelee kwa muundo upi. Kwa kauli kama za Lum, nami nasema HATUWEZI KUWA TUNATUKANWA KUWA SISI NI WATU WA KUDHULUMU WENGINE wakati hatuoni unafuu au faida ya kuvumilia matusi kama haya.

Speech ya Rais ilimuwa nzuri lakini kuzuia :tape: watu kuamua juu ya Muungano si sahihi kabisa na hata wakibana vipi na kwa mwendo wa hawa watu wa namna ya Lum wanavyotuchukulia sisi wa- Bara, basi nasema na mimi sitaki kutukamwa zaidi. Rais tusome alama za nyakati kutoka kwa Wazanzibar juu ya hili.

Tume mjiandae kutuweka ndani wengi maana tunasema waziwazi kuwa kwanza tunaomba kura ya maoni juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa Muungano na uwe wa aina gani kama tunaukubali. Sitaki tena na tena kutukanwa in the name of preserving our Union in which our partner has systematically decided to defile consistently in public. :disapointed:


SALA KATIKA WILAYA ZOTE ZA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Ehe Mungu nawaheshimu waasisi wa Muungano wetu , sikia kilio chetu na utoe funzo kwa watu wanaoamua kutukana sehemu moja ya Muungano bila sababu.

Fungua macho na mioyo ya Wakuu wetu wa sasa waone umuhimu wa kuwa wazi na kuwapa fursa Wananchi kujadili na kuamua mustakabali wa Muungano wao katika karne hii kama wote tunaridhia kuendelea.

Vinginevyo mapenzi yako yatimie na kila nchi ibaki kivyake tushiriane tu vizuri kama majirani wema wa historia na ndugu tuliozaliana wana hadi vitukuu kama Kenya, Uganda, Burundi n.k

Fisha na legeza nguvu zote za Dora zitakazo jaribu kumtesa yeyote anayetaka kutoa maoni yake juu ya Muungano kwenye Tume ya Marekebisho ya Katiba.

:amen:
 
  • Thanks
Reactions: lum
Back
Top Bottom