Kwanini mtu apewe sifa nyingi baada ya kufa?

Kashaija

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
255
58
Mara nyingi tumesikia na kuona marehemu akipewa sifa chungu mzima. Sasa nauliza, kwa nini iwe ni baada ya kufa?

Maana huyu mtu utakuta tumeishi naye kwa muda mrefu sana na wala hatukuwahi kumwambia kama yeye ni mtu muhimu sana kwenye jamii, hatukuwahi kumwambia kwamba akifa pengo lake haliwezi kuzibika n.k.

Ila akishakufa tu, tunaibua sifa nyiiiiiiiingi, ambazo kama tungemueleza kabla bila shaka angefurahi sana na angeweza baadhi ya sifa kuzikataa kwamba tunamvisha kilemba cha ukoka ama tunajipendekeza kwake.

Hivi hawa mafisadi papa siku yeyote akifa {kila mtu kuna siku atakufa}, tutegemee kusikia sifa nzuri tu kwao au hata mbaya zitatajwa?

Mimi naona kwamba ni unafiki tu umetuzidi.
 
Last edited:
Hili ndio swali kuu kuliko yote duniani. Zambi kuu kuliko zote ni unafiki. Uwoga wetu wa kurudi tulikotoka ndio unadumisha unafiki huo.kama mtu alikuwa mzuri ni mzuri tuu kama alikuwa ni mbaya ni mbaya tuu. Hii tabia ya kusifia marehemu inawazidishia machungu marehemu wetu kwani imejaa unafiki uliokithiri . Tuwe kama tulivyo tukikosea tukoseane. Tuombeane mema mapito yetu yasafishike ukisha kuwa hivyo utapeta vikwazo vyote mpaka ufike kwa baba juu sayuni.
 
kwa sababu mtu asipokuwepo ndo tunaona umuhimu wake.
Kama kuna mema alikuwa anatenda kwa sababu tuko naye kila wakati hatuyaoni, lakini akishakufa ndo tunagundua kwamba alikuwa na umuhimu wake ndo sifa za marehemu zinaanzia hapo.
 
Ra alikuwa ni mtu wa watu,
mwenye kupenda p[esa kuliko utu,
mwenye uchu wa madaraka na kujilimbikizia mali...
Asiye na huruma kwa wananchi wake..
Naomba muongeze sifa zake nyingine..
Pia mafisadi wengine pia
 
Mbona wampa sifa zote hizo RA , ashakufa nini?
 
Ndio unafiki wa binadamu kwa maana wafu hawajui lolote.Mtu akiwa hai hawezi kupewa sifa sana kwasababu ya roho za "KWANINI".
 
Mara nyingi tumesikia na kuona marehemu akipewa sifa chungu mzima. Sasa nauliza, kwa nini iwe ni baada ya kufa?

Maana huyu mtu utakuta tumeishi naye kwa muda mrefu sana na wala hatukuwahi kumwambia kama yeye ni mtu muhimu sana kwenye jamii, hatukuwahi kumwambia kwamba akifa pengo lake haliwezi kuzibika n.k.

Ila akishakufa tu, tunaibua sifa nyiiiiiiiingi, ambazo kama tungemueleza kabla bila shaka angefurahi sana na angeweza baadhi ya sifa kuzikataa kwamba tunamvisha kilemba cha ukoka ama tunajipendekeza kwake.

Hivi hawa mafisadi papa siku yeyote akifa {kila mtu kuna siku atakufa}, tutegemee kusikia sifa nzuri tu kwao au hata mbaya zitatajwa?

Mimi naona kwamba ni unafiki tu umetuzidi.

Tena akifa Fisadi papa hata shughuli za kitaifa zitasimama!!! Kwani unashangaa nini wakati mtu utakuta alikuwa jambazi sugu tena la silaha halafu akifa tu utasikia katika wasifu......... yaani alikuwa mtu wa kuigwa. Tena hasa hasa kama atakufa kifo cha kuugua tu na wala si kutwangwa risasi katika pambano. Binadamu tu wanafiki sana, hasa watanzania. Kama vile serikali ilivyo na unafiki kwa Mzee Reginald Mengi, JK anamchekea kumbe ana dukuduku moyoni, anahiti maswahiba!!!! Jana RM alisema Rais wangu.... alikosea hapo. Ajue Rais hamtaki, kwa hilo namhakikishia na asirudie tena kusema hivyo.
 
Na mkapa nae akifa ...atapewa unabiii wenzetu ukiamua tu uwe nabii wanakufuata..lol

nabii lakwatare

nabii sumaye

nabii kakobe

je nabii osama hamumtaki ..kama vipi nije. Muniabudu na mimi.
 
Watu wengi hupenda mabishano, sasa kwa kuwa mtu akiwa ameshakufa hawezi kujibizana, basi watu hawawezi tena kumtamkia sifa mbaya (kwa kuwa hawezi tena kujibishana), so iliyobaki ni kumpa sifa nzuri za kinafiki.
 
Tangu nizaliwe mpaka kufikia umri huu nilionao sijawahi kuona marehemu anasemwa kwa mabaya msibani hata kama alikuwa malaya...,,mchoyo...,,,mvivu au mapungufu yoyote ambaye alikuwa nayo kwa sababu hatujaumbwa wakamilifu,,.....sijui wenzangu huko kwenu.....LAKINI LEO KWA MARA YA KWANZA NIMESHUHUDIA.....#HAPAKASITUJAPOKUWATUPOMTEREMKONIITATUUAJAMANI
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom