Kwanini Mohamedi Dewji hakupewa hata U-Naibu Waziri?

Pasco_jr_ngumi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,802
282
HABARI WANA JF,
Nimejaribu kufikiri kwa muda mfupi sana, nikaja na hili wazo!
Naombeni tujadiliane, kwa nini huyu jamaa hajapewa hata unaibu uwaziri? kama elimu anayo na ni mtaalamu wa masuala ya biashara. Tena ni kijana matata na hodari anayeikuza kampuni ya MOHAMEDI ENTERPRISE kwa kupanuka vilivyo.....

Je ni kasumba ya kuwa muhindi au? lakini ni mtanzania haswa, nakumbuka babu Nyerere alimpa madaraka mbalimbali Mzee Al-noor Kassum ingawa ni muhindi. Hadi leo ni mkuu wa Chuo Cha Sokoine!!!

haya twende,
Lakini CDM msinitukane, tujadili kiutaifa kwanza!!!!
 
Hivi tu ni mbunge Mohamed Enterprises haiko kwenye top 15 ya tax payers, akiongezewa madaraka itakuwaje?
 
Sioni tatizo Dewji kutopewa unaibu waziri. Kama ana qualifications za kuwa naibu Waziri mbona wapo wengi wenye qualifications kama zake na hawajapewa fursa kama hiyo. Siyo wote wenye sifa za kuwa manaibu waziri watapewa unaibu waziri ... na hakuna tatizo katika hilo. Ni suala la nafasi zipo ngapi na wenye sifa wapo wangapi. Hatuna ushahidi wa kuhusianisha uhindi wake na yeye kutopewa unaibu uwaziri.
 
Ni dhaifu na mchumiatumbo tu. Nilifanya kazi MeTL kama humjui niuluze mimi.
 
Sio Mohamed Dewji tu; Kuna yule wa HAKIELIMU anafaa Uwaziri au Unaibu Amesoma na angeweza kweli kuboresha

Na kutoa his knowhow kwenye ELIMU na kusaidia naona ni bora kuliko Waziri wa Sasa Wa Elimu Mh. Shukuru Kawambwa
 
If u a Great thinker huwezi fikiri Mohamed Dewj kua naibu waziri unahitazi akili za ziada hata 2 kujiuliza ni vipi hata amekua mbunge, jibu rahisi Dhiki zetu na umaskini wetu na kuamini kuwa tajiri nikuwa na akili na uwezo wa kuongoza kumbe Hapana
 
HABARI WANA JF,
Nimejaribu kufikiri kwa muda mfupi sana, nikaja na hili wazo!
Naombeni tujadiliane, kwa nini huyu jamaa hajapewa hata unaibu uwaziri? kama elimu anayo na ni mtaalamu wa masuala ya biashara. Tena ni kijana matata na hodari anayeikuza kampuni ya MOHAMEDI ENTERPRISE kwa kupanuka vilivyo.....

Je ni kasumba ya kuwa muhindi au? lakini ni mtanzania haswa, nakumbuka babu Nyerere alimpa madaraka mbalimbali Mzee Al-noor Kassum ingawa ni muhindi. Hadi leo ni mkuu wa Chuo Cha Sokoine!!!

haya twende,
Lakini CDM msinitukane, tujadili kiutaifa kwanza!!!!

Mkuu Pasco Jr Ngumi naomba unijibu yafuatayo

Je wewe ni kibarua wake?
Una maslahi binafsi gani na hilo gamba au kampuni zake?
Je ulilazimishwa au ulilipwa ku post uzi huu,
 
misamaha yote ya kodi inamnufaisha dewji,mashamba ya katani chai kapewa bila kuyaendeleza,korosho anajipangia bei hafai
 
Moja kati ya mambo yaliyomwondoa Mkulo ni dili ya kiwanja ambayo METL walihusika. Who knows uhusika wake ukoje? Usije ukatoa mbuzi ukaweka kondoo!
 
Mkuu Pasco Jr Ngumi naomba unijibu yafuatayo

Je wewe ni kibarua wake?
Una maslahi binafsi gani na hilo gamba au kampuni zake?
Je ulilazimishwa au ulilipwa ku post uzi huu,

haaaaaa
maswali yako ni mazuriiii
1. mimi sio mwajiri wake, tena sijawahi kumuona kwa macho yangu LIVE..... zaidi kwa picha za mtandaoni
2. sina maslahi na HUYU GAMBA, lakini naangalia utaifa kwanza. CCM na bungeni kuna wahindi wabunge, na hapa Mtwara wapo kibao, mbona hawapewi nafasi ya kiuongozi............. so huyu MO DEWJI namkubali..... msomi, mjasiliamali
3. kulipwa?? sina shida za kutumika na mtu kama kandambili, najitafutie kwa mikono yangu

JIBU WEWE HAYA
1. Kwa nini wabunge wahindi hawaingizwi baraza la mawaziri
2. kwa nini basi mnawapitisha kuwa wabunge?
 
Sioni tatizo Dewji kutopewa unaibu waziri. Kama ana qualifications za kuwa naibu Waziri mbona wapo wengi wenye qualifications kama zake na hawajapewa fursa kama hiyo. Siyo wote wenye sifa za kuwa manaibu waziri watapewa unaibu waziri ... na hakuna tatizo katika hilo. Ni suala la nafasi zipo ngapi na wenye sifa wapo wangapi. Hatuna ushahidi wa kuhusianisha uhindi wake na yeye kutopewa unaibu uwaziri.
. mbali na kuwa mchumia tumbo lakini mimi naona hii mental inclination ya kutaka kila mwenye digrii au mtu maafuru kwenye siasa ni lazima awe waziri ni fikra potofu na inaonesha to want extent we do not have entrepresing attitudes. let aus cherish for productive rather than non productive sector such as politics.otherwise we will not get out of poverty abyss.
.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom