Kwanini Mkuu wa Majeshi hapewi heshima?

jeshi lipo kwa ajili ya ulinzi wa raia, yani kwa kifupia wanajeshi ni walinzi, sasa unataka mlinzi nae alindwe?
 
ni kweli, ila tusiwakatishe tamaa askari wa jeshi letu la polisi, kwani kazi wanayofanya si rahisi kama mtu anavyo weza dhani, sana sana wanasheria hebu jaribuni kusoma sheria zinazo tawala jeshi la polisi napia tufanye mijadala ya wazi hasa kwenye vyombo vya habari ilikuboresha sheria za jeshi la polisi, sheria za jeshi hili la polisi zinamkandamiza sana askari wa chini kwa kiwango ambacho nayeye anakuwa na stress nyingi na matokeo yake ni kuharibu kazi.
Sheria za kazi wa kuzirekibisha ni wao sio wananchi, kwani hao wa chini hawapandi, kazi za majeshi Duniani kote zinahusisha zaidi nidhamu na ni lazima, labda ungeongelea maslahi madogo hapo ningekuelewa. Kuomba rushwa, kubabikia watu kesi, uonevu kijumla zidi ya raia, hakuna uhusiano na sheria jeshi kukandamiza ngazi za chini.
 
Hisia za kichwani kwako. Kwa taarifa yako kila chombo hapo kina wajibika kivyake kutoa taarifa ngazi za juu. Huwezi kusema mfano mkuu wa magereza atoe taarifa ya WAFUNGWA kwa mkuu wa Majeshi.
Wewe lazma utakuwa polis maana hampenzi kuona kuwa mnazidiwa na hawa wenzenu wa mabakamabaka
 
ukisoma kifungu cha 56(4) cha sheria ya ulinzi wa taifa Tz, kinawataka jeshi la ulinzi, kutoa taarifa ya mazoezi yao kwa wakazi wa maeneo husika kama mazoezi hayo yataingia kwenye makazi ya watu, basi na mtu atakaye kaidi au kuingilia mafunzo yao atakamatwa na askari wa jeshi la polisi au ofisa wa jeshi la ulinzi au na askari yeyote wa jeshi la ulinzi kwa amri kutoka kwa ofisa wa jeshi la ulinzi, natena mafunzo hayo yanapaswa yawe na kibali cha maandishi kutoka kwa waziri wa ulinzi s.56(1), na pia kwa waziri wa mambo ya ndani kwa mujibu wa penal code, sasa ni mara ngapi jeshi la kudumu au jeshi la ulinzi hufanya mafunzo karibu na makazi ya watu bila kutoa taarifa kwa wakazi? na tena jeshi hili la kudumu la ulinzi huwa hawatoi hata taarifa ndani ya jeshi la polisi chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kuhakikisha watu hawaingilii mafunzo yao, kwa mujibu wa kifungu nilicho kitaja. nilazima dhana ya kudharauliana katika majeshi yetu yote iondolewe kila askari amuheshimu mwenzie kwa mujibu wa majukumu aliyo pewa na nnchi.

na hata kama ni kutafuta kwamba chombo kipi kina mamlaka juu ya chenzie bado jeshi la polisi litakuwa namba moja kimamlaka kwani ndiyo chombo pekee cha kusimamia sheria zote za nchi, ukisoma sheria ya usalama wa taifa letu utaona kwamba TISS hawana uwezo wa ku enforce sheria bali kuchunguza tuu lkn jeshi la polisi linachuguza na ku enforce, je ? nani zaidi kimamlaka ?

ukisoma kifungu cha 77(1) cha sheria ya ulinzi wa taifa, askari wa jeshi la polisi (police constable) ambaye kimsingi ni police officer anamamlaka ya kumkamata askari wa jeshi la ulinzi ambaye anasadikika kuwa ni mtoro katika jeshi hilo, au ni mtoro kabisa, kisha kumfikisha mahakamani au kumpeleka kwenye kambi yao, sasa mpaka hapo nani ni kiranja wa mwenzie kati ya jeshi la polisi na jeshi la ulinzi ? ingawa nao askari wa jeshi la ulinzi huweza kuwa na mamlaka ya askari wa jeshi la polisi pale watakapokuwa wanasaidia mamlaka za kiraia (yaani ku enforce civilian laws)kwa Kifungu cha 22 cha sheria ya ulinzi wa taifa Tz

ukisoma C.40 ya kanuni ya adhabu ndani ya jeshi la ulinzi (CODE OF SERVICE DISCIPLINE) inatamka kuwa kitendo cha askari yeyote yule wa jeshi la ulinzi kuzuia askari mwenzao au ofisa wao asikamatwe na askari polisi, wa jeshi la polisi ni kosa tena lina stahili adhabu ya miaka isiyopungua miwili, hii ni sheria ya jeshi la ulinzi lenyewe, swali ni kwamba ni mara ngapi askari wa jeshi la ulinzi hugoma kukamatwa na askari wa jeshi la polisi ? kwa kisingizio kuwa wao hawa wezi kamatwa na polisi ? na kwa mujibu wa kifungu hiki nani ni zaidi ya mwenzie ? any way TANZANIA POLICE FORCE IS THE ORIGIN OF MILITARY CIVILIZATION IN TANZANIA, DRAW ITS HISTORY FROM THE GERMANS IN COLONIAL PERIODS , FOLLOWED BY THE NATIONAL SERVICE, UKIACHANA NA KINGS AFRICAN RIFLE YA MWINGEREZA AMBAMO JESHI LA ULINZI HUPATA CHANZO CHA HISTORIA YAKE, NA TENA HATA VIONGOZI WA KWANZA WA JKT WALIKUWA NI POLICE, 'majeshi yote yanamajukumu ya ulinzi wa taifa letu na kuhakikisha usalama, ni lazima askari (wanajeshi) wote wa vyombo vyote muheshimiane na kuthaminiana.

NAHATA KAMA NI MFUMO WA VYEO VYA KIJESHI AMBAO ASKARI WA JESHI LA ULINZI HUTAMBIA SANAAAAAA, BADO WANAPASWA KUKUMBUKA KUWA MKUU WA KWANZA WA JESHI LA POLICE TANZANIA ALIKUWA NA CHEO CHA "MAJOR" ALIITWA "MAJOR DAVIS " alikuja Tanganyika akitokea South Africa (hiki kilikuwa kipindi ambacho tanganyika ilikuwa chini ya uangalizi wa muingereza), BAADA YA HAPO COMMISSIONER ELANGWA SHAHIDI AKAWA MKUU WA KWANZA WA POLICE KWA WAZAWA, NA BAADAYE TULIPO UNGANA NA ZANZIBAR ELANGWA SHAHIDI AKAWA "IGP" WA KWANZA WA POLICE TANZANIA
Mkuu japo hii thread ni ya zaman lakin nimekuelewa sana. Kiuhalisia na kivitendo jeshi la polisi ndo lipo juu kimamlaka kuliko majeshi yote labda tu nguvu yake inapungua kwenye kitengo cha siraha maana halina siraha nzito kama JWTZ
 
Co kwamba hapewi heshimaa kupeawa heshimaa ni maamuzii ya mtu tambua yule ni mwanajeshi tena mkuu then Hana makuu hata kidogo mwenye chembe chembe zilizojaa hekima na busara kiufupi huyu mshua ikitokea dharura hulazimika kufanya hivyo ila kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo hujumuika nasi katika JOTO hasiraa na hasa kwa foleni ya dar inshort namkubali ksanaaaa kama aendelee kuwepo miaka mia
 
msafara huo wa ma MP ni zaidi ya kuwa na walinzi (askari) wa CCM10000,...
askari jeshi wanaomlinda major general ni wale kutoka ngelengele special forces,....
hao askari wenu kaki ni wa kuakikisha ulinzi wa CCM na viongoz wake na kuzuia maandamano ya CDM.......
Nadhani Majeshi yote yaani JWTZ,POLISI,MAGEREZA NA JKT yako chini ya CCM.Amri yoyote toka CCM kwenda kwa Jeshi lolote lazima itekelezwe.Nipo tayari kurekebishwa kama ninachoongea ni uwongo.
 
Nadhani Majeshi yote yaani JWTZ,POLISI,MAGEREZA NA JKT yako chini ya CCM.Amri yoyote toka CCM kwenda kwa Jeshi lolote lazima itekelezwe.Nipo tayari kurekebishwa kama ninachoongea ni uwongo.
Unamaanisha kinana ana amri juu ya majeshi?
 
Unamaanisha kinana ana amri juu ya majeshi?
Nimesema CCM kama chama sio mtu.Kumbuka kuna Jamaa hapo juu alisema kuhusu wanajeshi ambao wana nguvu kuliko askari elfu wa CCM.Sasa nikataka kujua kama kuna Jeshi tanzania hii ambalo lina uwezo wa kukataa amri ya CCM.NIPO TAYARI KUREKEBISHWA.
 
Niswala kujiuliza

TUTOE kingora KWA MKUU WA MAJESHI

IGP ANAKIGNGORA

SIRRO NAE ATAKE KINGORA

MPINGA ATAKE KINGORA MWISHO MWITACHACHAA NAE SIATATAKA VINGORA
 
acha kudanganya watu, wewe hujui hata maana ya mwanajeshi, soma ibara ya 147(4) ya katiba ya Tanzania 1977, mwanajeshi maana yake ni askari wa majeshi yetu yote yaani polisi,magereza,jeshi la ulinzi, na jeshi la kujenga taifa. na pia unaposema JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA maana yake ni pamoja na polisi, magereza, jeshi la kudumu, maarufu hujiita jwtz kitu ambacho si sahihi kisheria, kwani wenyewe jina lao halisi ni REGULAR FORCE, huwezi kuwa na kitu TPDF kwa kuwa tenga polisi na magereza, (UNAPOSEMA TPDF NI PAMOJA NA POLISI+MAGEREZA) nenda kasome sheria ya ulinzi wa taifa (NATIONAL DEFENCE ACT 1966) Kifungu cha 10(1)a-d , pia soma sheria ya majeshi ya akiba ya mwaka 1965 part iii, (RESERVE FORCES ACT), Pia kuna kasumba ya kutamba kwamba kombati za mabakabaka zina maanisha eti ni jeshi kamili, hii kasumba haina ukweli tena inaonesha weledi mfinyu ktk masuala ya kijeshi, nguo zile za mabakabaka ni CAMOUFLAGE HASA UTAKAPOKUA UNAPIGANA MAENEO YENYE UOTO UNAO LINGANA NA VAZI HILO, (KIJANI KIBICHI CHENYE MCHANGANYIKO), HIYO ITAKUSAIDIA USISHAMBULIWE KIRAHISI NA ADUI, lakini kwa ujinga wetu tuna amini kombati za baka ndiyo uanajeshi kamili. huwezi kwenda pigana jangwani then ukavaa kombati za bakabaka , mtapigwa mchana kweupe, kwani itakuwa ni rahisi kwa adui kuwagundua kutokana na kwamba jangwani huwa akuna uoto wa kijani kibichi, kombati sahihi kwa jangwa itategemea na nature ya jangwa lenyewe na lazima itakuwa kaki, n.k
Zipo kombati za aina nyingi mkuu hii nikutokana na eneo mnalokwenda so kama ni jangwani mtavaa kombati zinazolandana na eneo huwa tunaziita MSADAMU
 
huelewi unacho ongea , nashida yako ni kwamba hujui mamlaka ya jeshi la polisi,kumbuka masuala yote ya "internal security" (IS) yapo chini ya jeshi la polisi, ngoja nikupe mfano mmoja "mfano ndani ya kambi ya jeshi la ulinzi la kudumu (maarufu jwtz) kumetokea kifo cha mashaka hapo ni jeshi la polisi ndilo litakalo kuwa na mamlaka ya kuchunguza kifo hicho ikiwa ni pamoja na kusimamia taarifa ya kitabibu (POSTMORTEM) juu ya kifo hicho na si jeshi la ulinzi la kudumu (maarufu jwtz), polisi wanamamlaka hata ya kusimamisha na kukagua magari yote ya hao wanao itwa jwtz kwani si kila gari la bakabaka basi ni gari la jeshi la ulinzi la kudumu, au si kila aliyevaa gwanda la bakabaka basi ni askari wa jeshi la ulinzi la kudumu, (lakini cha ajabu hao wanao itwa jwtz huwa wanabisha kukaguliwa na polisi, kwa kisingizio kuwa wao hawatakiwi kukaguliwa. (HUU NI UFINYU WA KUFIKIRI)

kitu kingine unaonesha kudharau jeshi la polisi kwa kusema eti ni la askari wa ccm huku ukijipotosha kuwa hao mnao waita jwtz si askari wa ccm, sasa ndugu yangu nikukumbushe tu kuwa majeshi yote yapo chini ya tawala za kiraia hivyo ni amri za watawala wa kiraia ndizo zinazo endesha majeshi yetu, sasa basi kile kitu kinacho fanywa na polisi halafu wewe ukipendi kumbuka kitu hichohicho chaweza fanywa na hao the so called jwtz, tena kinaweza fanywa vibaya zaidi kuliko hata jeshi la polisi, NIKUJIDANGANYA KUSEMA KWAMBA POLISI WANATETEA CCM, HALAFU HAPOHAPO UWATOE HAO REGULAR FORCE (MAARUFU KAMA JWTZ)
aya bhna ila vitu viko wazi..........
 
Umemaliza yote kaka/ mdau. Inavyosemekana ni kuwa daily briefing ya hali ya Usalama hutolewa nae baada ya kupata kutoka Idara zote yaani Jeshi, UWT, Polisi, Magereza nk. Hivyo yeye ndo humpatia mkuu wa nchi. Hivyo ni kweli kabisa akawa ni Chief of Joint Security Organs kama Marekani wanavyofanya. Kule Marekani mwafrika pekee aliyewahi kushika cheo hicho ni Collin Powel.

Kama kuna anaejua zaidi atueleze lakini kwa asilimia kubwa ni sahihi kabisa yale uliyoyasema.
Mkuu wa majeshi kila anapokuwa kuna msafara ...gari yake Ina Nyota Nne ...na gari Moja au Mbili nyuma Zenye namba private ...uwepo wa kimuli muli hutegemea Hali ...especially kwa Mkuu tulie naye Hana Makuu na hutumia sweepers tu pale anapokuwa na uharaka ...Zaidi ukiwa nyuma yake hata bila sweeper traffic wanakuwa wamepewa signal na utaona wanaita Magari ya upande wake .....anapita
Hata Mkuu wa TISS naye kwa wanaojuwa wanaweza ku spot msafara wake wa Magari meusi yenye private number ...hadi UWE unajuwa Ndio utaweza ku spot ..entourage yake .

Mkuu wa Majeshi nafasi yake ni namba mbili Baada ya Rais ....yeye Ana ripoti Moja kwa Moja kwa Rais ...sio kwa waziri ,waziri Mkuu au Makamu wa Rais ...ambao anawatii tu..., Ana access na Rais 24/7 ....hata usiku akiwa amelala Anao uwezo wa kuagiza aamswe ili waongee au amuone ...ikitokea hatari yeyote ya ulinzi na Usalama au maafa ..yeye Ndio mwenye jukumu la kukusanya taarifa Za vyombo vyote na kumpelekea Rais taarifa Rasmi ..muda wowote ...wakuu wote wa vyombo Vya Usalama ( Polisi ,Usalama ,magereza ,zimamoto etc ) yeye Ndio joint chief ..au mwenyekiti wa ulinzi na Usalama ( national security council )

Kwa Nguvu kubwa alionayo ...anatakiwa kuwa humble ...ili asionekane..kuwazidi waziri wake ,waziri Mkuu na Makamu HADHARANI ....kwenye Protocal arrangement ..anawapigia saluti ..lakini behind the scene wanajuwa yeye ni nani ...na anawazidi ...Sasa akianza kutembea na misafara Marefu ....na Nchi Hii ni ya kidemokrasia..atakuwa Ana send wrong message ...

Mko sahihi wakuu, lakini kitu kimoja tu ni kuwa Mkuu was UWT anariport moja kwa moja kwa raisi na siyo kwa CDF kama mlivyoelezea, na ndio maana uWT wana watu wao jeshini.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom