Kwanini michezo inawateka wasomi na kusahau mambo muhimu?

Gurti

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
211
59
Ndugu zangu wa jf,

Mimi huwa ninafuatilia sana uelewa watu kuhusu mambo ya msingi ya nchi hii. Kila mara kunapokuwa na mambo muhimu kwenye media asubuhi kwenye vituo vya magazeti, ktk daladala na maofisini ikiwepo ofisini kwetu mjadala unaoongoza bado ni wa michezo. Ninajitahidi kuanzisha mijadala iliyoko uk wa mbele wa gazeti - hawataki- Ni michezo tu. Hata kukiwa na hotuba za rais, Dowans, katiba mpya au uchaguzi bado watu wanajadili michezo kupita kiasi. Mimi inanisumbua sana. Mimi ni mshabiki wa Man U na Simba lakini michezo haipaswi kuwa zaidi ya katiba mpya na downs au siasa kwa ujumla. Kwanini wasomi hawabalance?


Hivi karibuni nimeanza kufuatilia nyendo za great thinkers wa Jamii forums, mwendo ni ule ule. Ninapaandika makala hii, wafuatiliaji wa michezo magazetini ktk jf ni karibu 8000 wakati mambo ya downs na katiba mpya na mengine muhimu yahusuyo nchi wanacheza kati ya 0 hadi 250. Hii maana yake ni nini huko tuendako?

Watu wengi hatujui kuwa siasa ndo inaamua kama sisi tuangalie/tufuatilie michezo kwa amani au tusiangalie kabisa kukitokea vurugu. Tunasahau kuwa hata soka yetu inauawa sana na wanasiasa. Kwa hiyo, kwa kuwa ninapenda sana michezo lazima nipende sana siasa na nifuatilie sana nyendo za siasa aka katiba mpya, uchaguzi, downs, mijadala bungeni ili sote tujue hatima ya upenzi wetu katika michezo pamoja na maeneo mengine katika maisha kama uchumi, afya
 
Tena bora hiyo michezo ingekuwa ni ya nchini kwetu..wengi wetu ni ulaya...a sort of neo-colonialism....
 
Back
Top Bottom