Kennedy
JF-Expert Member
- Dec 28, 2011
- 49,022
- 54,306
Wakuu jamii ya Mbilikimo wengi wamekuwa wakipatikana katika misitu ya Jamhuri ya Congo, ingawaje hata hapa Tanzania kuna wachache mfano kuna Dada mmoja ktk kundi la VITUKO SHOW.
Sasa mwenye kujua hasa kule Kongo kwanini huwa wanapatikana kwa idadi kubwa anaweza tujuza.
Mwanamuziki hayati PEPE KALE nae alikuwa anawashirikisha katika kazi zake za muziki enzi za uhai wake.
====
Majibu
Sasa mwenye kujua hasa kule Kongo kwanini huwa wanapatikana kwa idadi kubwa anaweza tujuza.
Mwanamuziki hayati PEPE KALE nae alikuwa anawashirikisha katika kazi zake za muziki enzi za uhai wake.
====
Majibu
Swaali zuri sana;
Kwanza fahamu kuwa kuna mbilikimo wa aina mbili: mbilikimo wa asili (pygmy) na mbilikimo wa ugonjwa (dwarf). Wale wa kongo ni mbilikiko wa asili kwa maana ya kuwa maumbile yao ni asili yao na yanatokana na mazingira yao ya asili. Umbilikimo wa aina hii ni hereditary kwa maana ya kuwa huzaliwa na mbilikimo pia. Ni kama ambavyo maumbile ya asili ya waachina yalivyo tofauti na maumbile ya asili ya wazungu, na pia wachina huzaliwa na wachina tu.
Kuna mbilikimo wa aina nyingine ambao wanapata matatizo ya mwili kushindwa kutengeneza hormones zinazohitajika mwili kukua, na hivyo kubaki na umbo la kitoto maisha yao yote; hawa wanajulikana kama dwarfs. Mbilikimo wa aina hii huweza kutokea katika familia yoyote ile, wazazi wawili warefu wanaweza kuzaa mbilikimo wa aina ya dwarf.
Theories zinazonyesha kuwa evolutionary process iliyosababisha waafrika wakawa na ngozi nyeusi kutokana na mazingira ya joto la tropical, ndiyo pia iliyosababisha watu waliokuwa wakiishi kwenye misitu mizito kama vile Kongo kuwa wafupi kwa vile miili yao ilikuwa inakosa mwanga wa jua kutengeneza vitamin D; kwa hiyo miili yao ikawa haiwezi ku-absrob calcium ya kutosha, jambo liliosababisha wawe na mifupa midogo na hivyo kuwa na miili midogo. Misitu ya Kongo ndiyo yenye mbilikimo wengi wa aina hiyo ikifuatiwa na misitu ya Amazon huko Brazili. Kuna sehemu nyingine za dunia kama Papua New Guinea na Australia ambako pia kuna mbilikimo waliotokana na misitu mikubwa iliyokuweko maeneo hayo.