Kwanini majina ya Kiingereza, na Uigizaji wa Kiswahili

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Hivi kwanini filamu kadha wa kadha za kiswahili, zenye lengo la kuwafikia wazungumzaji wa Kiswahili, zinapewa majina ya Kiingereza. Ni sawa sawa na mtu anatunga wimbo unasema "Forever Together" halafu wimbo mzima uko katika Kiswahili! Naomba mnisaidie, hivi hizi filamu zinauzwa sana nchi ambazo wanazungumza sana Kiingereza?
 
wanadai kiswahili hakijitoshelezi na kinarefusha jina :confused3:
 
wanadai ni katika kutafuta soko la nje zaidi na kuwa kimataifa zaidi, na ndio maana wanaweke subtitle za kiingereza
 
industry nzima bado inafikira za kikoloni wanadhani wakiandika kwa kiingereza ndo wataonekana wameendelea ,hata film zao hazina uhalisia ,maisha ya kitajili ambayo wabongo wanaishia kuyaota tu, they are gud 4 nothing
 
Tatizo ni elimu ndogo na kuwa na ushamba fulani hivi

wa kufikiri kila mtanzania ana mawazo ya watu wa magomeni magomeni
ambao kwa kuongea maneno mawili ya kiingereza ina maana ya kuendelea....

Stpid mentality....thats it..........
 
Tatizo ni elimu ndogo na kuwa na ushamba fulani hivi

wa kufikiri kila mtanzaniaana mawazo ya watu wa magomeni magomeni
ambao kwa kuongea maneno mawili ya kiingereza ina maana ya kuendelea....

Stpid mentality....thats it..........


mzee mbona unatutukana....
 
wanadai ni katika kutafuta soko la nje zaidi na kuwa kimataifa zaidi, na ndio maana wanaweke subtitle za kiingereza

Hawana lolote......Ni ujinga/kutokujiamini na utumwa wa Kiingereza vinawasumbua...............Mimi huwa siangalii sinema/filamu zao
 
Hawana lolote......Ni ujinga/kutokujiamini na utumwa wa Kiingereza vinawasumbua...............Mimi huwa siangalii sinema/filamu zao
balantanda utakuwa umeniiga mimi.....! mimi ni mpenzi mzuri wa kiswahil,afrika,tanzania,utamadun wetu,nyimbo zetu,mashairi yetu,ngoma zetu n.k.!
Na DAIMA SI MPENZI WA VYA "KWETU ILA VYA KWAO"...........mfano nyimbo ya kiafrika mavazi ya kiarabu, nyimbo inaitwa BONGO FLEVA midundo ya ki-maghrib, mmashindano ya urembo ya kikwetu mavazi,miondoko, vigezo vya KWAO.......DOWN...DOWN ......TO THEM.....!
 
hawajui target group, kama unatafuta masoko ya nje si ufanye filamu yote kwa kingereza tu?
 
Majina ya Kiswahili hayana mvuto wa kibiashara,ndivyo wenzetu wanavyodhani kumbe ni ukoloni wa mawazo na ujinga mkubwa!
 
Mkuu Mwanakijiji

Wewe mkorofi sana kuna watu lukuki hapa wanatumia nick names za kiingereza yaani wote hawa ... .... duh! Amakweli wajinga ndio waliwao. Vipi itabidi sasa tuanze kuwa invisible au Boss ataanza kupiga kelele pengine reverend naye atajibu hili. Vipi Avatar za kithungu? Mkuu naona hapa utaleta balaa ngoja tumuulize JK kama bado ile safari yake ya kukinga bakuli bado ipo maana Wajerumani wamesema wao watatoa fweza tu kwa Ugiriki hata kama Cameron hakubali.

BTW mkuu wa kaya huoni anavyojikombakomba kwa kina Sin bin Clair, RA na wa-iran, anajenga Culture tegemezi oooops si unaona hata culture kwa kiswa-english sijui ni nini? When this embecile leaves Magogoni pengine tutakuwa ahueni.
 
nami nakubaliana na wachangiaji wengine kuwa hawa waigizaji wetu hawana lolote zaidi ya ushamba na kuwasumbua,
kwanza wanavyodai wanaweka subtitles kiukweli hizo subtitles ni kama wamezigandisha tu kwani sio optional ila lazima zitokee kwenye screen hata kama we huzitali
pili wengi wanakosea mno kiingereza mpaka wanaudhi maneno mengine wanayokosea ni madogo mno hat mtoto wa darasa la tatu tulipokuwa tukianza kusoma kiingereza enzi zile angeyajua
mfano juzi nilikuwa naangalia filamu iitwayo my dreams-ndoto zangu,humo neno baba wamelitafsiri farther na wameliandika hivyo zaidi ya mara kumi mpaka inachefua unatamani hizo subtitles usizione lakini kwa kuwa zimegandihwa lazima zitokee
ingefaa watafute wahariri wazuri au waende darasani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom