Kwanini madaktari (baadhi) huenda kinyume na mahitaji ya wagonjwa wao?

Luo

Senior Member
Jan 19, 2012
139
92
Poleni na mihangaiko ya siku itifaki ikiwa imezingatiwa sitaki niwachoshe na maneno mengi.

Hivi ni kwanini Madaktari(baadhi) huenda kinyume na mahitaji ya wagonjwa wao? mfano halisi ni kwangu hapa nilienda hospitali moja ya rufaa ya serikkali hapa mwanza (sek ture) nikamwelezea dactari shida yangu.

Nilishangaa aliponiambia eti nikapime damu na mkojo(moyoni nikisema huyu daktari hajui nimeacha labaratori ngapi hadi kufika hapa?) ilihali sina homa wala nini nikasema isiwe shida labda itakuwa ni hatua ya mwanzo ya matibabu yangu.

Nilienda lab. majibu yakatoka malaria sina bali leucocytes...(U.T.I), akaniandikia dawa sawa japo nikamweleza vipi mimi nilikuja nataka vipimo flani dactari kwa madaha kanijibu hivi: MIMI NI DAKTARI WEWE NI MKULIMA HIVYO HUNIFUNDISHI KAZI. Mimi niliondoka pale sababu nilijua maamuzi ya hasira siku zote sio mazuri. Bahati yake sikupata jengo la utawala nimreport.

Nilichogundua;
1. Usugu wa ugonjwa sababu anaweza kuwa daktri pia.

2.Baadhi ya vyombo vya upimaji hakuna katika hospitali(kama cha kupima choo(stool) kimeharibika (sek ture).

3.Majibu ya ajabu ajabu ya baadhi ya madaktari hupelekea kupigwa na wagonjwa.

4.Wagonjwa hutumika kama experimental units(majaribio) kwa madawa ya hospital na kujaza sumu nyingi mwilini.

Suluhisho;
Madaktari acheni fanya kazi kwa mazoea kwani mnavyosema ni medern madicinal na iwe kweli sio mnakua kama mnapiga ramli.

Mwenye hela zake atafute tiba sahihi na ya wakati mahala anapoweza.

Serikali itoe ajira kwani baadhi tunaangamia kwa kukosa gharama za matibabu kwa sababu elfu 10 yangu imekwenda bure sababu sikupata huduma ninayohiitaji.
 
stool tunapima kwa kutumia microscope(hookworm, giardia,amoeba, ascaris nk) the same to urinary tract infection (UTI)
 
Malaria huna bali leucocytes!

Sijui unaamanisha nini kwa sababu wanadamu wote tuna leukocytes.

Au ulitaka kumaanisha nini?.
 
Kuelekezwa kipimo cha damu ilitegemea ulijieleza vipi.
Kwenda hosp.huku umeshajipa ugonjwa hata ukiambiwa huna ugonjwa ni ngumu kuridhika.
Maelezo sahihi yaliyonyooka ndiyo yatamfanya dkt.atoe tiba sahihi.
 
Hii dhana ya mimi nimesema ipo kwetu Africa tu. Daktari anaamua na hasemi kwanini anaamua!! Huyu bwana angeelezwa sababu ya maamuzi hayo na matokeo ya kipimo kuendana na anavyojisikia asingekuja kulalamika. This is simply the usual poor customer care.
 
MIMI NI DAKTARI WEWE NI MKULIMA HIVYO HUNIFUNDISHI KAZI.
Nawaza wakati huo ulikuwa katika hali gani mpaka akakutambua kwamba wewe ni mkulima??
 
Ila we jamaa mshenzi sana, yaani unaenda hospital kichwani ukiwa na vipimo vyako duuuu, ukija hospital unamueleza daktari shida yako then atakupima na kukutibu kulingana na diagnosis aloipata kulingana na symptoms zako
 
Mgonjwa anayeweza kuongea ni msaada wa kwanza kwa daktari katika kupata matibabu sahihi,ila sio kila utakachosema ndio kitafanyiwa kazi mkuu.
 
Usiende hospital na majibu yako kichwani, dr ndie anaeamua upimwe nini sio mgonjwa
 
1472802139027.png
1472802162647.png
km ulijua unaumwa nn hospital ulifata nini....
 
Daktar anaangalia complain zako na akipata medical history history yako vizur ndo atajua akufanyie investigations zip,ww km mgonjwa huna nafas ya kusuggest vipimo vya kufanya,tatizo tushazoea kwenda maabara za vichochoron kutaka kupima malaria typhoi etc so tunajua na hospitali ni hvyohvyo.......
 
Poleni na mihangaiko ya siku itifaki ikiwa imezingatiwa sitaki niwachoshe na maneno mengi.

Hivi ni kwanini Madaktari(baadhi) huenda kinyume na mahitaji ya wagonjwa wao? mfano halisi ni kwangu hapa nilienda hospitali moja ya rufaa ya serikkali hapa mwanza (sek ture) nikamwelezea dactari shida yangu.

Nilishangaa aliponiambia eti nikapime damu na mkojo(moyoni nikisema huyu daktari hajui nimeacha labaratori ngapi hadi kufika hapa?) ilihali sina homa wala nini nikasema isiwe shida labda itakuwa ni hatua ya mwanzo ya matibabu yangu.

Nilienda lab. majibu yakatoka malaria sina bali leucocytes...(U.T.I), akaniandikia dawa sawa japo nikamweleza vipi mimi nilikuja nataka vipimo flani dactari kwa madaha kanijibu hivi: MIMI NI DAKTARI WEWE NI MKULIMA HIVYO HUNIFUNDISHI KAZI. Mimi niliondoka pale sababu nilijua maamuzi ya hasira siku zote sio mazuri. Bahati yake sikupata jengo la utawala nimreport.

Nilichogundua;
1. Usugu wa ugonjwa sababu anaweza kuwa daktri pia.

2.Baadhi ya vyombo vya upimaji hakuna katika hospitali(kama cha kupima choo(stool) kimeharibika (sek ture).

3.Majibu ya ajabu ajabu ya baadhi ya madaktari hupelekea kupigwa na wagonjwa.

4.Wagonjwa hutumika kama experimental units(majaribio) kwa madawa ya hospital na kujaza sumu nyingi mwilini.

Suluhisho;
Madaktari acheni fanya kazi kwa mazoea kwani mnavyosema ni medern madicinal na iwe kweli sio mnakua kama mnapiga ramli.

Mwenye hela zake atafute tiba sahihi na ya wakati mahala anapoweza.

Serikali itoe ajira kwani baadhi tunaangamia kwa kukosa gharama za matibabu kwa sababu elfu 10 yangu imekwenda bure sababu sikupata huduma ninayohiitaji.
kama ulikuwa unajua tatizo lako kwa nini ulienda hospital?
 
Mwingine tumbo linauma anataka xray, ni vizuri ukienda jieleze vizuri kwa daktari, ukiona ni tiba ulizowahi pata pia usisite kumwambia
 
utakuwa una hypochondria tatizo tanzania madaktari wenyewe wachache mlangoni wagonjwa kibao wanasubiri kuingia kwa daktari. we katumie dawa ulizopewa ukiona hazikusaidii rudi tena hospital, ukiona umepona kaa utulie
 
Dr yupo sahihi, tunapata tabu sana siku hizi... mgonjwa anafika na diagnosis zake alafu anataka akuelekeze, utasikia nipime malaria na typhoid, mwingine anafika anasema mimi nipe dawa ya kutibu UTI, so unamjibu mtu kutokana na anavyositahili kujibiwa
 
Back
Top Bottom