Kwanini Lowassa anaiponda CHADEMA?

chama cha kususa na kuandamana kina tabu sana aisee..ngoja na nyie mpate dola tutawaona kama mtayapenda maandamano yasiyo na msingi,watu hamfanyi kazi kuuutwa barabarani kuandamana na kususa plus kupinga pinga kila jambo halafu mnategemea shilingi eti iwe strong...kwa uzalishaji upi?
Masaburi masaburi masaburi harufu chaaffuuuuuuuu!!!
 
Kauli iliyotolewa hivi karibuni na mbunge wa monduli bwana Edward Lowassa ni ya kufedhehesha na kusikitisha sana. Ni kauli iliyojaa dharau kubwa kwa wanyonge wanaolazimika kutumia nguvu ya sauti yao kudai stahili zao.Kauli hiyo pia inamuonyesha mheshimiwa mbunge kama ni kiongozi muoga asie na ujasiri wa kukabiliana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi.

Kasoro ya kwanza katika kauli hiyo ya Lowassa aliyoitoa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya kanisa la FCTP huko Bigabiro, mkoani Kigoma, ni kuyaeleza matumizi hayo ya nguvu za umma kuwa yanaendeshwa na CHADEMA.

Kwa nini Lowassa hayuko sahihi katika hili? Hivi chama kisicho na dola kama CHADEMA kinawezaje kulazimisha utashi wa wananchi kushiriki kwenye harakati hizo? Kumshawishi mlalahoi akatishe siku yake shambani akahudhurie maandamano yanayokihusisha chama cha siasa ni suala gumu mara kadhaa ya urahisi alionao Lowassa kuwakusanya marafiki zake matajiri kumwaga fedha kwenye harambee zao.

Hivi Lowassa anadhani wananchi wanaojitokeza kwenye maandamano au harakati nyingine kushinikiza masuala mbalimbali wanafanya hivyo kama anasa, hasa ikizingatiwa kuwa wanafahamu fika uwezekano wa kulala rumande kama si kufunguliwa mashtaka pindi Jeshi la Polisi likijisikia kuwanyanyasa?

Tunaweza kumhurumia Lowassa katika hili kwa vile sidhani kama ameshawahi kulazimika kutumia nguvu kudai haki yake. Yeye ni miongoni mwa kikundi kidogo cha wateule wachache ambao miaka nenda miaka rudi wapo madarakani, huku mahitaji yake yakishughulikiwa na wasaidizi wake.

Raha ya kuwa na wasaidizi, wapambe na watoa huduma ni kwamba kwa kiasi kikubwa jukumu la kuhakikisha kila jambo lipo sawa kwa ‘bosi' linakuwa mikononi mwa watu hao.

Katika hotuba yake kwenye harambee hiyo Lowassa alikaririwa akidai (namnukuu) "Nguvu ya umma tunayoshuhudia kwenye maandamano ya chadema, ingekuwa inatumika kwa kiwango kile kile kufanya kazi za kujitolea kwenye miradi ya maendeleo kama ujenzi wa sekondari zetu, hakika taifa lingepiga hatua kubwa ya maendeleo, lakini linapokuja suala la kufanya kazi nguvu ya umma hutoweka."

Kwa lugha nyingine Lowassa anahitimisha kuwa mahala pekee ambapo nguvu ya umma inatumika ni kwenye maandamano ya baadhi ya vyama vyetu. Huyu ndiye ambaye licha ya kuwa Waziri Mkuu huko nyuma ameshika nafasi kadhaa za uongozi serikalini na ndani ya CCM kwa miaka kadhaa.

Je, ni kweli hajawahi kuona nguvu inayotumika na Watanzania kujiletea maendeleo yao licha ya kukwazwa na majambazi wanaotumia fursa zao kuwafisadi?

Moja ya mambo yanayotufanya Watanzania tuendelee kumlilia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ni jinsi alivyotuunganisha bila kutumia dini au urafiki na matajiri kuhamasisha maendeleo ya jamii na nchi yetu kwa ujumla.

Nyerere alitambua umuhimu wa nguvu ya umma katika kuleta mabadiliko yanayokusudiwa hususan kukiwa na usimamizi mzuri usioambatana na maslahi binafsi.

Uhuru wetu kutoka kwa mkoloni ulipatikana kutokana na wanyonge wa Tanganyika kuchoshwa kunyanyaswa na kukandamizwa na wakoloni na kuunganisha nguvu zao wakihamasishwa na Nyerere na wapigania uhuru wenzie na hatimaye tukapata uhuru wetu. Leo hii Lowassa anabeza harakati zenye mwelekeo kama huo.

Historia imetuonyesha jinsi nguvu ya umma ilivyoweza kuangusha tawala mbalimbali za kidhalimu, mifano mizuri ikiwa ni huko Afrika Kusini walivyopambana na utawala wa makaburu na Ulaya ya Mashariki walivyokabiliana na udikteta wa kikomunisti.

Na hivi karibuni tumeshuhudia nguvu ya umma ikiwang'oa madikteta Hosni Mubarak wa Misri, Ben Ali wa Tunisia na Muammar Gaddafi wa Libya.

Lakini kwa kile kinachoweza kutafsiriwa kama unafiki wa Lowassa ni ukweli kwamba yeye alikuwa miongoni mwa waliopongeza nguvu za umma nchini Misri huku akishauri watawala wetu kujifunza katika kilichojiri nchini humo. Ikumbukwe kuwa harakati za Misri zililenga zaidi kuutokomeza utawala wa kidikteta wa Mubarak ilhali nguvu ya umma huko nyumbani imeelemea zaidi kwenye kudai haki za msingi sambamba na kukemea maovu, hususan ufisadi. Sijawahi kusikia kuwepo kwa maandamano yenye wito wa kumng'oa Rais Kikwete madarakani kwani kwa mujibu wa sheria zetu kufanya hivyo ni uhaini pasipo mjadala.

Lakini licha ya kupongeza nguvu za umma huko Misri, ingekuwa miujiza kwa Lowassa kuunga mkono harakati kama hizo huko nyumbani kwani yeye ni miongoni mwa waathirika wake. Nguvu ya umma ikihamasishwa na CHADEMA ilimtaja mwanasiasa huyo kwenye orodha ya mafisadi (list of shame) na hadi leo hajachukua hatua za kisheria kudai amekashifiwa.

Tukiweka kando kauli hiyo ya Lowassa, labda tujiulize kidogo kuhusu hayo mamilioni yanayochangwa na marafiki zake kwenye hafla mbalimbali makanisani. Hivi Watanzania wenzetu hao wenye uwezo wa kutoa sadaka za mamilioni wanatoa wapi fedha hizo?

Na katika hili ninayalaumu sana makanisa yanayoweka mbele fedha pasipo kujiuliza fedha hizo zinazomwagwa kwao zinatoka wapi.
Wakati wa uhai wake, Baba wa Taifa alionyesha upinzani mkubwa kwa wanasiasa wenye utajiri wa kupindukia lakini usio na maelezo ya kutosheleza. Ifahamike kuwa utajiri si dhambi iwapo umepatikana kihalali.

Lakini kila mwenye uelewa anaweza kupatwa na wasiwasi kuona mwanasiasa mmoja akizunguka huku na kule kumwaga mamilioni ya shilingi makanisani. Huyu mtu ana fedha kiasi gani? Amepata wapi?

Lowassa kama muumini yeyote yule ana uhuru wa kutoa michango ya fedha nyingi na marafiki zake matajiri. Kadhalika, ni haki yake ya kikatiba kuongea lolote lile alimradi havunji sheria za nchi. Sasa kama yeye ana uhuru wa kumwaga mamilioni makanisani na kukemea walalahoi wanaotumia nguvu ya umma kushinikiza mambo mbalimbali, kwa nini basi asitambue kuwa walalahoi hao wanaotumia haki hiyo hiyo anayotumia yeye?

Wanasema uhuru bila nidhamu ni uhuni, na kwa msingi huo japo ninatambua uhuru alionao Lowassa kuzungumzia masuala ya kisiasa kwenye nyumba za ibada, uhuru huo unaweza kuwa na madhara makubwa katika taifa letu. Kama walalahoi anaowakemea Lowassa ni werevu na wanafanya harakati zao nje ya nyumba za ibada basi ni vema wanasiasa wetu nao wakaepuka kugeuza sehemu hizo takatifu kuwa majukwaa ya kisiasa.
Nguvu ya UMA ielekee kwa huyu jambazi mkuu arudishe pesa zetu katika mfumo wa ukusanyaji kodi badala ya kuzihonga kutafuta kura 2015.
 
Huyu si alipongeza yale maandamano ya egypt huyu tena akatoa na wito viongozi waache kujilimbikizia mali?kweli nimeamini watu waongo wanaongoza kwa kusahau haraka,si ajabu alishasahau kama aliwahi kusema hivyo huko nyuma.
 
Jina la Lowassa limekuwa kubwa sana kiasi kwamba lolote analotamka linapewa tafsiri nyingi tofauti. Kwa jinsi nilivyomuelewa, Lowassa hakuelekeza kauli zake kwa Chadema, bali kwa wananchi pale akihimiza kwamba nguvu ya umma sio njia sahihi ya kujiletea mabadiliko/maendelo, bali kufanya kazi ya kujenga uchumi, kwa bidii.

Sasa kosa lipo wapi hapo? Huu ni mtazamo sahihi, kwani matatizo yanayotukabili taifa sasahivi ni pamoja na uwepo wa serikali legelege, isiyo na dira yoyote wapi inataka kuipekeka nchi. kama hilo ndio tatizo, kabla ya kufikia matumizi ya nguvu ya umma, kwanini tusijishughulishe na ujenzi wa taifa na kusubiri mwaka 2015 ambapo wananchi wanakuwa na fursa ya kuchagua chama gani kikamake madaraka?

Inaweza ikawa Chadema, inaweza ikawa CCm, lakini kutokana na siasa zetu holela, inaweza ikawa coalition ya vyama vya sasa, au pengine chama kipya kabisa. Pale ambapo itabainika wananchi wameporwa haki yao ya kuchagua chama na viongozi wanaowataka mwaka 2015 ndipo suala la nguvu ya umma linaweza kuwekwa mezani kama mjadala.

Sio sasa. Vinginevyo, Lowassa anaweza kuwa na mapungufu yake lakini katika hili ni kukuza tu mambo kwa sababu aliyetamka ni Lowassa.

Well said mkuu;tupime hoja ya mtu sio kuanza kuleta mizani za kina Ndugai
 
Utakula ban ya kujitakia wewe kijana halafu uanze kulia lia...hiyo kwanini usiipeleke chit-chat?hapa tunaongea politiki dogo!kuhusu maofisini sawa,lakini nchi haijengwi maofisi peke yake na kwanza toka lini watu wa maofisni wakawa na muda wa kuandamana barabarani,sana maandamano yenu ni humu jf!

Hahahahahaaaaaaaa...naona limekupata mwenyewe hapo kwenye red
 
Mtu aliumwa na nyoka akiona jani tu hushituka vivyo hivyo kwa fisadi akiona mandamo ya wazalendo tumbo joto. Na bado ngoja uchaguzi ufike awamu hii hakuna wizi wa kura kila mtu atapata zake za halali kura zitalindwa mpaka pumzi ya mwisho na atakayecheza na kura ajiandae kumtokea yale ya Kenya ys kins Kenyatta na wenzake
 
chama cha kususa na kuandamana kina tabu sana aisee..ngoja na nyie mpate dola tutawaona kama mtayapenda maandamano yasiyo na msingi,watu hamfanyi kazi kuuutwa barabarani kuandamana na kususa plus kupinga pinga kila jambo halafu mnategemea shilingi eti iwe strong...kwa uzalishaji upi?
Toa haki za watu uone kama utamuona mtu barabarani!
 
Kwasababu kwenye ile LIST OF SHAME ya CDM yeye (Lowasa) yumo. Hivyo anafanya "pre-emptive strike"
kama atabahatika kupeperusha bendera ya CCM 2015.
 
acheni ushabiki wa vyama,hivi kweli wengine kazi yao iwe ni kujenga nchi na wengine kazi yao kutumia walivyozalisha wenzao bila kutoka jasho, kumbukeni sasa hivi kila mtu amechoshwa na ugumu wa maisha.Lakini msile mkajisahau maana mwisho wake mbaya
 
kwani rwanda ina viwanda vingapi ambavyo tanzania haina?au visiwa vya shelisheli,madagascar n.k. Wana viwanda vingapi?angalia pale arusha kipindi cha zile vurugu kile kiwanda chao cha utalii kiliathirika kiasi gani na tulikosa pesa ngapi za kigeni?huo ni mfano mmoja tu nimekupa ili upanue fikra zako kidogo,sio lazima u export product ndio upate foreign currency,u can sell service na ukapata mamilioni ya dola kama shelisheli na madagascar..

lazima tufike mahala tujiulize maswali mengi juu ya huyu mtu, kwa nini kipindi hiki anakuja kasi kupitia makanisa kwenda ikulu? Anatafuta nini mtu mwenye mali yote yenye maelezo yasiyojitosheleza? Leo tumesahau baada ya kusota kutokana na makosa yake kibao na washirika wake? Migogoro ya ardhi imeisha aliyosababisha, leo mmesahau? Mmesahau mmesahau leo ufisadi alioufanya? Hamjiulizi kwa nini na kwa nini ikulu anapalilia?tuwe na akili jamani huyu ni nyoka tona swira!hafai hafai hafai kuwa kiongozi wa hii nchi!msithubtu hata siku moja nawaambia watanzanai!
 
Maendeleo hayaletwi na mtu mmoja mmoja kuchangia mabati na vyumba vya madarasa,hakuna nchi duniani iliyowahi kuendelea kwa harambee,huyo tajiri anayejitolea kila harambee yupo ,yeye utajiri wake alichangiwa na nani?ni vizuri kujitolea lakini asione kuwa anasaidia sana jamii ki hivyo.
 
Kauli iliyotolewa hivi karibuni na mbunge wa monduli bwana Edward Lowassa ni ya kufedhehesha na kusikitisha sana. Ni kauli iliyojaa dharau kubwa kwa wanyonge wanaolazimika kutumia nguvu ya sauti yao kudai stahili zao.Kauli hiyo pia inamuonyesha mheshimiwa mbunge kama ni kiongozi muoga asie na ujasiri wa kukabiliana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi.

Kasoro ya kwanza katika kauli hiyo ya Lowassa aliyoitoa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya kanisa la FCTP huko Bigabiro, mkoani Kigoma, ni kuyaeleza matumizi hayo ya nguvu za umma kuwa yanaendeshwa na CHADEMA.

Kwa nini Lowassa hayuko sahihi katika hili? Hivi chama kisicho na dola kama CHADEMA kinawezaje kulazimisha utashi wa wananchi kushiriki kwenye harakati hizo? Kumshawishi mlalahoi akatishe siku yake shambani akahudhurie maandamano yanayokihusisha chama cha siasa ni suala gumu mara kadhaa ya urahisi alionao Lowassa kuwakusanya marafiki zake matajiri kumwaga fedha kwenye harambee zao.

Hivi Lowassa anadhani wananchi wanaojitokeza kwenye maandamano au harakati nyingine kushinikiza masuala mbalimbali wanafanya hivyo kama anasa, hasa ikizingatiwa kuwa wanafahamu fika uwezekano wa kulala rumande kama si kufunguliwa mashtaka pindi Jeshi la Polisi likijisikia kuwanyanyasa?

Tunaweza kumhurumia Lowassa katika hili kwa vile sidhani kama ameshawahi kulazimika kutumia nguvu kudai haki yake. Yeye ni miongoni mwa kikundi kidogo cha wateule wachache ambao miaka nenda miaka rudi wapo madarakani, huku mahitaji yake yakishughulikiwa na wasaidizi wake.

Raha ya kuwa na wasaidizi, wapambe na watoa huduma ni kwamba kwa kiasi kikubwa jukumu la kuhakikisha kila jambo lipo sawa kwa ‘bosi’ linakuwa mikononi mwa watu hao.

Katika hotuba yake kwenye harambee hiyo Lowassa alikaririwa akidai (namnukuu) “Nguvu ya umma tunayoshuhudia kwenye maandamano ya chadema, ingekuwa inatumika kwa kiwango kile kile kufanya kazi za kujitolea kwenye miradi ya maendeleo kama ujenzi wa sekondari zetu, hakika taifa lingepiga hatua kubwa ya maendeleo, lakini linapokuja suala la kufanya kazi nguvu ya umma hutoweka.”

Kwa lugha nyingine Lowassa anahitimisha kuwa mahala pekee ambapo nguvu ya umma inatumika ni kwenye maandamano ya baadhi ya vyama vyetu. Huyu ndiye ambaye licha ya kuwa Waziri Mkuu huko nyuma ameshika nafasi kadhaa za uongozi serikalini na ndani ya CCM kwa miaka kadhaa.

Je, ni kweli hajawahi kuona nguvu inayotumika na Watanzania kujiletea maendeleo yao licha ya kukwazwa na majambazi wanaotumia fursa zao kuwafisadi?

Moja ya mambo yanayotufanya Watanzania tuendelee kumlilia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ni jinsi alivyotuunganisha bila kutumia dini au urafiki na matajiri kuhamasisha maendeleo ya jamii na nchi yetu kwa ujumla.

Nyerere alitambua umuhimu wa nguvu ya umma katika kuleta mabadiliko yanayokusudiwa hususan kukiwa na usimamizi mzuri usioambatana na maslahi binafsi.

Uhuru wetu kutoka kwa mkoloni ulipatikana kutokana na wanyonge wa Tanganyika kuchoshwa kunyanyaswa na kukandamizwa na wakoloni na kuunganisha nguvu zao wakihamasishwa na Nyerere na wapigania uhuru wenzie na hatimaye tukapata uhuru wetu. Leo hii Lowassa anabeza harakati zenye mwelekeo kama huo.

Historia imetuonyesha jinsi nguvu ya umma ilivyoweza kuangusha tawala mbalimbali za kidhalimu, mifano mizuri ikiwa ni huko Afrika Kusini walivyopambana na utawala wa makaburu na Ulaya ya Mashariki walivyokabiliana na udikteta wa kikomunisti.
Na hivi karibuni tumeshuhudia nguvu ya umma ikiwang’oa madikteta Hosni Mubarak wa Misri, Ben Ali wa Tunisia na Muammar Gaddafi wa Libya.

Lakini kwa kile kinachoweza kutafsiriwa kama unafiki wa Lowassa ni ukweli kwamba yeye alikuwa miongoni mwa waliopongeza nguvu za umma nchini Misri huku akishauri watawala wetu kujifunza katika kilichojiri nchini humo. Ikumbukwe kuwa harakati za Misri zililenga zaidi kuutokomeza utawala wa kidikteta wa Mubarak ilhali nguvu ya umma huko nyumbani imeelemea zaidi kwenye kudai haki za msingi sambamba na kukemea maovu, hususan ufisadi. Sijawahi kusikia kuwepo kwa maandamano yenye wito wa kumng’oa Rais Kikwete madarakani kwani kwa mujibu wa sheria zetu kufanya hivyo ni uhaini pasipo mjadala.

Lakini licha ya kupongeza nguvu za umma huko Misri, ingekuwa miujiza kwa Lowassa kuunga mkono harakati kama hizo huko nyumbani kwani yeye ni miongoni mwa waathirika wake. Nguvu ya umma ikihamasishwa na CHADEMA ilimtaja mwanasiasa huyo kwenye orodha ya mafisadi (list of shame) na hadi leo hajachukua hatua za kisheria kudai amekashifiwa.

Tukiweka kando kauli hiyo ya Lowassa, labda tujiulize kidogo kuhusu hayo mamilioni yanayochangwa na marafiki zake kwenye hafla mbalimbali makanisani. Hivi Watanzania wenzetu hao wenye uwezo wa kutoa sadaka za mamilioni wanatoa wapi fedha hizo?
Na katika hili ninayalaumu sana makanisa yanayoweka mbele fedha pasipo kujiuliza fedha hizo zinazomwagwa kwao zinatoka wapi.
Wakati wa uhai wake, Baba wa Taifa alionyesha upinzani mkubwa kwa wanasiasa wenye utajiri wa kupindukia lakini usio na maelezo ya kutosheleza. Ifahamike kuwa utajiri si dhambi iwapo umepatikana kihalali.

Lakini kila mwenye uelewa anaweza kupatwa na wasiwasi kuona mwanasiasa mmoja akizunguka huku na kule kumwaga mamilioni ya shilingi makanisani. Huyu mtu ana fedha kiasi gani? Amepata wapi?

Lowassa kama muumini yeyote yule ana uhuru wa kutoa michango ya fedha nyingi na marafiki zake matajiri. Kadhalika, ni haki yake ya kikatiba kuongea lolote lile alimradi havunji sheria za nchi. Sasa kama yeye ana uhuru wa kumwaga mamilioni makanisani na kukemea walalahoi wanaotumia nguvu ya umma kushinikiza mambo mbalimbali, kwa nini basi asitambue kuwa walalahoi hao wanaotumia haki hiyo hiyo anayotumia yeye?

Wanasema uhuru bila nidhamu ni uhuni, na kwa msingi huo japo ninatambua uhuru alionao Lowassa kuzungumzia masuala ya kisiasa kwenye nyumba za ibada, uhuru huo unaweza kuwa na madhara makubwa katika taifa letu.
Kama walalahoi anaowakemea Lowassa ni werevu na wanafanya harakati zao nje ya nyumba za ibada basi ni vema wanasiasa wetu nao wakaepuka kugeuza sehemu hizo takatifu kuwa majukwaa ya kisiasa.

Asante kwa hoja.Tatizo ni hao walalahoi wengi wao bado hawajaamka toka usingizi.Ebu jaribu kuangalia kwenye mjumuiko wa harambee hiyo wenye nazo ni wangapi na bado wengi wa walalahoi waliohudhururia nao wanapiga vigelegele.
Hata hivyo tatizo kubwa lililopo nayo nikuwa viongozi wa nyumba hizi za Ibada nao wamegeuka na kufanya shughuli tofauti na masuala ya imani na kukemea maofu.Ebu fikiria unamwalika mtu kama Lowasa kwenye nyumba ya Ibada pamoja na tuhuma zote zinazomzunguka na ambavyo yeye mwenye hajaoata kujitokeza na kujitetea hata kama si mahakamani.
 
Kwa hiyo kwa akili yako unataka kutuambia kuwa viwanda vyetu vimekufa kutokana na maandamano?

Viwanda vyetu vimekufa kutokana na Uongozi na usimamizi mbovu. CCM daim ni "CHUKUA CHAKO MAPEMA' na kwa kudhihirisha hili turudi nyuma kidogo tutafakari kuhusu MRADI WA MABASI YA WANAFUNZI" hapa DSM kwenye miaka ya 90's

Mradi uliopewa jukumu la kusimamiwa na UVCCM, hatimaye haukudumu ule mradi kwani "MTOTO WA NYOKA NI NYOKA'

Wale vijana walikumbuka kuwa Wazee wao "WANA CHUKUA CHAKO MAPEMA" nao vijana wakachukua. Mwishowe hata mabati ya yale mabasi hakuna sijui nani alichukua hadi mabati kufanya SCREPER.

Hivyo endapo uongozi wa Serikali utabadilika na kuwekwa watu wenye msimamo na uchungu wa nji kweli kwa nini tuwe na maandamano???????

Endapo kama Madaktari watapewa haki zao kwanini wagome kufanya kazi na kuuwa wagonjwa wetu tulio maskini, kwani viongozi hawatibiwi katika Hospitali zetu na hata hii migomo wanaisikia katika vyombo vya habari. Mtoto akiumwa anapanda ndege kutibiwa nje ya nji.

Endapo wafanya kazi wote watapewa haki zao kwa nini wagome, walimu hakuna kugoma watoto wetu watasoma bila hofu. Lakini walimu wanaogoma na wa shule zetu za walalahoi, watoto wa wakubwa hawasomi shule hizo. Hivyo hawaathiriki na migomo ya Waalimu.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!!!
 
Back
Top Bottom