Kwanini kuwa na mpenzi au mwenza kunaathiri uhuru wako wa kuwasiliana na marafiki?

environmental

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,054
137
Uhuru wa kuwasiliana na marafiki ndugu na jamaa unapungua kwa kiasi kikubwa unapokuwa na mahusiano ya kudumu na mwenza wako, je ni sahihi kupoteza uhuru huu muhimu wa asilia?
 
Itakua hivyo kama nyote hamjiamini.Kama unamwamini mwenzako kwa nini uwe na wasiwasi anapowasiliana na marafiki zake?
 
Sioni tatizo kwani huyu mpenzi wako sialikukuta nao hao marafiki vp tena mabadiliko? hawezi kuwajua wote lakini wengine
atawajua na kadri muda unapokwenda na wengine atawajua au kama una vimeo hayo mengine...
 
mmmmh hii itakuwa kwako tu.....

Mbona sie wengine mawasiliano kama kawa?

Mpenzi wako hajiamini? Au ndo aina ya wapenzi wanaotaka kukutawala, na iukuchagulia marafiki? Muone Mtambuzi anajua nyanja hiyo zaidi....
 
Last edited by a moderator:
kama ulikuwa maaarufu wa kuflirt kabla ya kumpata huyo laazizi lazima ukose uhuru,tena simu yako mwenyewe unawezaa kuichukia, ikiingia call tu au message huna amani lakini ule urafiki wa kawaida tu haiwezekani bana hakuna kitu utaongea kimkwaze mwenzio,
 
Uhuru wa kuwasiliana na marafiki ndugu na jamaa unapungua kwa kiasi kikubwa unapokuwa na mahusiano ya kudumu na mwenza wako, je ni sahihi kupoteza uhuru huu muhimu wa asilia?[/QUOTEa ]

ni sahihi kupunguza mawasiliano maana ktk list hiyo kutakuwa na wakaka na wadada waliokuwa alternative, baada ya hapo inabidi ujiheshimu,pia mtu aliye single,uhuru wake hauwezi kufanana na aliyeoa.
 
nahitaji uhuru wote je si haKI YANGU YA MSINGI?
 
kama ulikuwa maaarufu wa kuflirt kabla ya kumpata huyo laazizi lazima ukose uhuru,tena simu yako mwenyewe unawezaa kuichukia, ikiingia call tu au message huna amani lakini ule urafiki wa kawaida tu haiwezekani bana hakuna kitu utaongea kimkwaze mwenzio,
nitakuwa mtiifu kwenye mapenzi yangu, naitaji kudumu na marafiki zangu wa jinsia zote
 
nitakuwa mtiifu kwenye mapenzi yangu, naitaji kudumu na marafiki zangu wa jinsia zote
Huyo mtu wako anatakiwa kufahamu kwamba wewe hukuzaliwa na kukulia kisiwa ambacho hakina watu. Na wewe msaidie kulitambua hilo
 
jamani wanajamii hili jambo wote tuliangalia katika mtizamo wa mawasiliani ya simu tu na vitu kama hivyo ila kuna vitu kama kutembelea ndugu na jamaa nalo pia lahusika maana yake kama umepitia kwa ndugu bila hata kumtaarifu hasa wife inakuwa kosa hata kama hauna historia ya kucheat kwake inakuwa ni big deal na hii mi naizungumzia kutokana na experience yangu kwa wenza kadhaa ambao nimepata kuwa nao. mi naona wengi wa kina dada wanakuwa hawajiamini na hata simu ikiita ile kukata tu lazima kuulizwa nani kapiga.
mwisho wa siku ni kwamba kina wanawake wanapenda kuchukua nafasi kubwa kabisa kuliko kitu chochote kwamba wewe ukitoka tu kazini basi tena.
 
hapa kuna mkanganyiko kidogo wadau, unajua huwa kuna marafiki wema na marafiki washika mapembe. mwenza wako anaweza ku-take advantage ya marafiki wema kuongea na washka mapembe.
My take: timiza wajibu wako kama mke/mume issue ya kufatilia marafk wa mkeo/mmeo ni kujitafutia presha. ushaamua kwa moyo 1 kuoana na huyo ulomchagua. TULIA TULI KAMA MAJI YA MTUNGINI
 
Jamani,ukiamua kuoa,achana na marafiki wa kike kama mwanaume na kama mwanamke achana na wakiume.kwanza,sometimes ukute ulishatembea na hao mnaowaita marafiki,na mkeo au mumeo anajua.as a man be with men friends and woman be with womanfriends.
 
"... Mtu ataachana na mama yake na baba yake, nao watakuwa mwili mmoja"... kama huyo mwenza ni rafiki (mpenzi) kabla ya ndoa unaweza kukaa naye chini na kumueleza yale ambayo unahitaji kutoka kwake na wewe umtimizie anayohitaji. Ila kamamkiingia katika ndoa, basi achana na mahusiano na ukaribu na watu wako wa zamani (wawe marafiki, majirani au wapenzi) kwani haki yenu inakuwa moja, maamuzi yeni mamoja na mambo yenu ni mamoja. Marafiki, ndugu na jamm hao unaowataka kuwasiliana nao kama zamani wakati umempata mwenza ndio wanaosababishaga kuvunjika kwa mahusiano na ndoa nyingi hapa duniani... nakushauri achana nao kwani kila kitu kina wakati wake... ndo maana michezo ya utotoni unapokua huichezi.
 
Uhuru wa kuwasiliana na marafiki ndugu na jamaa unapungua kwa kiasi kikubwa unapokuwa na mahusiano ya kudumu na mwenza wako, je ni sahihi kupoteza uhuru huu muhimu wa asilia?
Ni kweli mawasiliano hayana budi KUPUNGUWA kwa marafiki, ndugu na jamaa kwani wakati huo unakuwa umeunganishwa na yule aliye ASILI ya mawasiliano yako. Yaani alipoumbwa ADAM akaumbwa HAWA na si ndugu/jamaa au rafiki mfano wa ADAMU. But cha msingi ni kupungua kwa mawasiliano haya kwani huamia kwa ndugu yako huyu/mwili mmoja nawe..angalizo Mawasiliano yakifa hapo pana tatizo na panaleta kila haja ya kurejea mwanzo na kutatua hii kitu..
 
Kama mawasiliano yako na marafiki ni yale ya kuitana baby,honey etc lazima ukose uhuru lakini kama ni mawasiliano ya kawaida tu huwezi kukosa uhuru,ukiona hujiamini ujue ulijizoesha vibaya kuflirt hovyo na marafiki wa jinsia tofauti na yako..:coffee:
 
ni sahihi kupunguza mawasiliano maana ktk list hiyo kutakuwa na wakaka na wadada waliokuwa alternative, baada ya hapo inabidi ujiheshimu,pia mtu aliye single,uhuru wake hauwezi kufanana na aliyeoa.

in any case, mawasiliano lazima yali-reflect mahusiano mapya na aghalabu hayawezi kubaki kama yalivyokuwa zamani.... wenzetu wana methali inayosema 'huwezi kula keki yako halafu ukaendelea kubaki nayo', so chagua moja...
 
hiyo nakubaliana na wewe...i've lost so many friends over the years coz of love...bt i guess ndio sacrifice zenyewe hizo..
 
Back
Top Bottom