Kwanini kuwa na mawaziri toka Zanzibar wakati wao hawana hata mmoja toka bara?

tunachohitaji ni kwaliti ya kiongo na si mkoa... FYI, Nyalandu ni wa singida.. dodoma hakuna kitu pale na kigoma yupo mmoja tu ambaye ni mwizi wa kura kwahiyo sawa tu

labda moro amuondoe mkulo..

Mh. Teu, NW wa Fedha hails from Mpwapwa. Mpwapwa iko Dodoma.
 
Kuna sovereignty.

Wanzanzibari wanatuhurumia na tushukuru. Kinadharia wangeweza kudai, na wangekuwa na hoja, wakisema katika baraza la watu 29 wawakilishwe na mawaziri 14 unusu. Kama Wanzanzibari 5 kwenye cabinet ni wengi, mbona sisi tuna 24?

Tulivyokubaliana nao 1964 , Zanzibar ni sovereign entity ndani ya Muungano. Tuliamua kuungana na kakisiwa ka watu laki moja ushee sisi tukiwa milioni nane wakati huo kutengeneza pande zenye hadhi sawa.

Sovereignty maana yake haijalishi wana watu wangapi, au ukubwa gani, au uchumi kiasi gani, wao ni kitu kamili kisichotawaliwa. Kiongozi wa Tanzania Bara akikataa kuhudhuria ghafla ya Rais analaaniwa kwa kutikisa nchi, lakini Karume anakuja kusikiliza hotuba za Kikwete uwanja wa Taifa anapojisikia. Kwa nini, wao ni sov ereign entity.

Ndivyo tulivyokubaliana nao wenyewe. Na wajanja huwezi kuwala, inakula kwetu kwa sababu sisi ndio wajinga tunaokataa kuangalia upya Muungano kwa vile mawazo yetu ni mgando wa mtindi. Milioni takriban 40 na millioni moja mtaunganaje muwe na hadhi sawa? Wako wachache kiasi kwamba ukiwa na Masters degree we waziri! Na Mtanganyika ukitaka kupanda haraka pitia Zanzibar (Rais Mwinyi). Kanchi kama wilaya, Unguja na Pemba zinaingia Newala na Masasi mara tano! Lakini tumewakubalia sovereignty.

Mawazo mgando kwa sababu hakuna anaeweza kuutetea Muungano kwa kutuambia faida zake. "Adui ataweka himaya visiwani na itatishia usalama wetu." Ndio historia tuliyofundishwa. Nchi masikini ya makapuku hii itazuia aduni gani hii? Kwamba Mmarekani akitaka kukutungua itabidi kwanza apate viwanja vya kupaki vifaru visiwani? Na North Korea akitaka kumtungua Mmarekani itabidi kwanza achukue Jamaica kuhifadhi vifaru, au? Historia. Kikwete akizindua Bunge la kumi ametoa sababu kwa nini tuendelee na Muungano: "Tunalo jukumu la kihistoria la kuhakikisha kuwa Muungano wetu unadumu na unazidi kuimarika."

Muungano wetu ni historia tu, zaidi ya hapo ni mzigo wa hasara kwa Watanzania Bara. Tulikosea.


Na ndio maana watu wanahoji hu muungano una manufaa gani kwetu? inavyoonyesha tunajipendekeza kwa hawa watu kwa kila namna
 
Hivi wazanzibari ni watanzania kumbe?
Niliwahi kuwa ng'ambo wakati fulani, nikakutana na ndugu yangu wa visiwani, wakati tunajitambulisha, nikasema i am from tanzania. yeye akasema he is from Zanzibar tena kwa mbwembwe sana.
kwanini usiseme wewe unatoka Tanganyika...au unaona aibu kusema kama wewe ni Mtanganyika?
 
Wazanzibari wanafaidi sana kwenye huu Muungano ndo maana nashindwa kuelewa wanalalamikaga kwasababu gani hasa za msingi?!!! kila jimbo la Zanzibar lina mmbunge wa kuja Dom! na kwenda barazani kwao, wana makamu wa rais wa serikali ya muungano, Jaji Mkuu, etc. tusisahau kwamba katiba yao inasema Zanzibar ni nchi. nilimsikia Dr. S. Mvungi akiongea kupitia chanel ten wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita kwamba angetaraji ajitokeze Mtanzania bara mmoja aseme uchaguzi ubatilishwe sababu wagombea wenza wote wa urais si rai kama walivyofanya kwa baadhi ya wagombea ubunge. Kazi kweli kweli, tusubiri tuone labda wanafanyakazi zaidi yetu watz-bara.
wazanzibari hawataki Muungano bali wanalazimishwa....vengi nevyo ni uwongo mtupu....
 
Kwa hiyo unamaanisha zanzibar kuna wachapa kazi sana ukilinganisha na Tanzania bara? mbona kwenye baraza la mawaziri zanzibar hakuna mbra hata mmoja?

mkuu kuna mawili yanakuhusu
pengine huna unachojua kuhusu muungano
au unaongelea ushabiki.
Kukusaidia znz ni sehemu ya tz na inamikoa kama bara
 
Kwa hiyo unamaanisha zanzibar kuna wachapa kazi sana ukilinganisha na Tanzania bara? mbona kwenye baraza la mawaziri zanzibar hakuna mbra hata mmoja?

Kianacho matter ni uchapakazi hata kama wangetoka sehemu moja wote ila kama wanafanya kazi kwa maslahi ya taifa hilo sineno. Ukitaka achague kwa kuangalia ia mkoa atakua na constraints nyingi sana
 
Katika Baraza "jipya" la Mawaziri (29) aliowateua JK kuna Mawaziri wanne kutoka Zanzibar wakati huhuo kuna Mikoa mitatu hakuna Waziri hata mmoja...

Kuna nini Zanzibar hadi kuwa na uwakilishi mkbwa kiasi hik katika Baraza la Mawaziri?
!

waliotoka Zanzibar ni maandalizi ya umakamu wa rais 2015....
 
Naomba Kuuliza::

Naibu Waziri ni Waziri? Inaelekea Kiswahili ni kigumu pia?

BTW: Siongelei UKABILA naongelea MIKOA::

Kwa mfano Dar es Salaam: Mwanza : Shinyanga kila MKOA una Waziri mmoja:: Iweje Zanzibar (over 1m population) itoe Mawaziri Wanne?

Note: Baraza la Mawaziri lazime liwawakilishe wa-Tanzania wote.

mkuu jiulize pia hivi zanzibar ni mkoa?
Au ndio kiswahili kigumu
je unawezaje kulinganisha zanzibar na dar au singida? Unaangalia vigezo gani, ukubwa wa eneo au idadi ya watu au tafsiri ya sheria kwamaana ya katiba?
 
tunachohitaji ni kwaliti ya kiongo na si mkoa... FYI, Nyalandu ni wa singida.. dodoma hakuna kitu pale na kigoma yupo mmoja tu ambaye ni mwizi wa kura kwahiyo sawa tu

labda moro amuondoe mkulo..
Eng Chiza jee?si wa Kigoma jamani????Dodoma yupo naibu waziri wa Fedha...Teu anatoka Mpwapwa......tafuteni data kwanza kablsa kuropoka
 
sasa na huyu zakia Megji Jk kaibuka naye wapi tena?, lile nilo la kustaafu halimo kwa msamiati wa Kikwete! wanarudishwa tuu...basi mrudishe na Msuya.
 
Kwa hiyo unamaanisha zanzibar kuna wachapa kazi sana ukilinganisha na Tanzania bara? mbona kwenye baraza la mawaziri zanzibar hakuna mbra hata mmoja?

Muungano huu unazua maswali mengi! Mikoa ya Zanzibar ni kama kata za Tanganyika, Majimbo ni sawa na vijiji vya Tanganyika. Kuna usawa gani hapa!!! Na Tanganyika yenyewe haitambuliwi!! Afadhali Zanzibar ingekuwa mkoa kama mikoa mingine na kusiwe na rais zanzibar. La sivyo tuwe na Tanganyika yetu na tuwe na rais wa Tanganyika kama wao. Serikali ya muungano ndio iwe na watu wa bara na Zanzibar. Hakuna taifa duniani wanaofanya kama sisi! Muungano wetu hauna USAWA, HATA KIDOGO!
 
Let we now discuss social-economic development of tanzania.

Without "clean" political structures in place, you can not have stable and sustainable socio-economic development at all!

Ostritch Algorithm will not help
 
tunachohitaji ni kwaliti ya kiongo na si mkoa... FYI, Nyalandu ni wa singida.. dodoma hakuna kitu pale na kigoma yupo mmoja tu ambaye ni mwizi wa kura kwahiyo sawa tu

labda moro amuondoe mkulo..

True, sure, kweli kabisaaaaaa
 
Ndiyo maana NIMEULIZA - Kama kuna mtu amefanya utafiti then naomba anipatie jibu:

Taso: Sovereignity ya Zanzibar in UTATA mtupu (ref Mjadala wa Zanzibar ni Nchi au Si Nchi?)
TASO ametumia vibaya maana ya sovereignity. huenda alimaanisha kitu kingine. naomba tu aeleze vizuri kwa kiswahili fasaha akiondoa hilo neno sovereign. Zanzibar lost her sovereignity since 2th April 1964 and this is going to last as long as the Union lasts. i may agree that zanzibar has five regions so producing four ministers out of the five regions sound sensible to me. Baba _Enocks argument would have a soundy power if he wouldn't compare the mentioned regions with zanzibar.
 
Huu udini na ukabila mnaoushabikia utatufikisha wapi? Raisi wa JMT ndiye mwamuzi wa mwisho kwenye uteuzi wa mawaziri, suala la baadhi ya mikoa haina mawaziri halina mantiki yeyote, mawaziri wapo kuwatumikia watanzania wote, tukumbuke mfumo wa serikali yetu si majimbo na hata kwenye nchi zinazofuata mfumo serikali za majimbo Raisi hachagui mawaziri wake kwa kufuata wametoka jimbo gani, anachoangalia ni uwezo wao wa kutekeleza sera za serikali.
ZANZIBAR SI NCHI KAMILI NI SEHEMU YA JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA, HAINA UWEZO WA KUFANYA MAAMUZI YAKE BILA KUISHIRIKISHA SERIKALI YA JAMUHURI, HAINA UWAKILISHI KWENYE VYOMBO VYA KIMATAIFA KAMA VILE UN, AU, JUMUIYA YA MADOLA, KUWA NA BENDERA HAIMANIISHI KUWA NI NCHI KAMILI, HATA HUU MUUNGANO WA BARA WENGI HATUUTAKI TUNALAZIMISHWA TU:embarrassed:
 
Hivi wazanzibari ni watanzania kumbe?
Niliwahi kuwa ng'ambo wakati fulani, nikakutana na ndugu yangu wa visiwani, wakati tunajitambulisha, nikasema i am from tanzania. yeye akasema he is from Zanzibar tena kwa mbwembwe sana.


Inabidi Watanganyika nao wadai Tanganyika yao. Hivi wale wa G55 walishakufa wote? Hawaoni kuwa ni wakati muafa wa kuitoa hiyo agenda yao kwenye kabati walipoifungia na kuanza hata kuifuta vumbi. Wananzibari walishamla ng'ombe wao wamebakiza kumalizia mkia. Ile laana ya ubaguzi aliyosema mwl JK haitatutafuna sisi bali wao wailio anza. Tunaidai Tanganyika yetu.
 
Back
Top Bottom