Kwanini kila ndoa inayovunjika lawama anatupiwa mwanamke!!!!!

Inatokea kwamba sisi wanaume ndio tunasababisha mengi ila ni wepesi sana kukimbia majukumu maana lolote litakaloharibika ndani ya nyumba lawama zinakuwa kwa wake zetu hata kama sisi ndi wasababishi

umeongea vema
 
Ni kweli kabisa nakumbuka hata mie wangu alinikosea sana, ajabu kwenye kusuluhisha akasema eti namlaumu sana kuhusu kosa fulani hivi kwa hiyo ananikwepa na kuchelewa kurudi, sasa ukiangalia kukosa kakosa yeye, kwa nn asilaumiwe! lakini siku hizi nimekaa na kufikiria kwamba kweli kwa kiazi fulani mwanamke anatakiwa kuilinda nyumba yake isibomoke kama atataka kuwepo milele na mwanamme wake,kamakakosa na umemsamehe usirudierudie kila siku kumlaumu kwa kosa uliloamua kumsamehe, kachelewa kurudi hata uulizi unaanza kung'aka,hata hujui kapatwa na nini
 
kwa mujibu wa jamii yetu anayetakiwa kulinda ndoa ni mwanamke so hata mwanaume afanye nini kitacho sababisha uhuisano kuyumba jamii inakutegemea mwanamke ndio uweke mambo sawa,coz hata sis wanawake wenyewe tuna kasumba mbaya ya kusema wenzetu 'ndio maana kaachika' haijalishi nani alikuwa chanzo cha mfarakano
 
tatizo ni pale wanapoanza kutoa mambo nje ndo wanakutana na ushauri usiofaa .... hasa yey anapoanza kukuelezea ni lazima aonyeshe kwamba wewe ni tatizo

tunayatoa nje walau kupata unafuu ndugu yangu sema sasa wamama wengine wakisha choka sana huwa tunachanganyikiwa na wakishachanga nyikiwa hawajui waanzie wapi ndipo huanza kumweleza kila mtu tatizo lake
 
Sijui kwa nini watu wanawalaumu wanawake pekee, hata hivyo imefikia wakati si kuangalia jamii inakulaumu au vipi, ni vema kuchukua maamuzi kwa maslahi ya wote, kwa mfano mumeo unakupiga na kuku abuse hovyo inatishia moja kwa moja uhai na uwajibikaji wako katika maisha ya kila siku utasema eti unaogopa kuachana naye kwa sababu utaonekana wewe ni failuire?? za kuambiwa tuchanganye na zetu jamani wanawake wenzangu, acha waseme mwisho watachoka, maisha yanaendelea.
 
Mimi nashangazwa na mijadala ya namna hii kwani haiko ballanced! Mtu ametoa case tatu ambazo yeye anaamini kuwa wanawake wanalaumiwa kwa kuvunja ndoa, halafu anatoa mjumuisho kuwa kila ivunjikapo ndoa basi mwanamke hulaumiwa!!! Hii mie sijaiona. Ndoa inapovunjika, wale wanaojua kilichosababisha ndoa kuvunjika hukisema, na ikiwa mhusika ni mwanamke jamii husema!!

Hizi "sweeeping conclusion" za kuwa mwanamke anaonewa au mfumo dume ndo tatizo lenyewe. Hivi wanawake kwenye ndoa ni malaika na hawasababishi ndoa kuvunjika?? Wenye ndoa wanajua. Hata jamii inaposema aliyesababisha ndoa kuvunjika ni mke, tujiridhishe kwa kufanya utafiti si kwa kupinga tu na kulaumu mfumo dume!!

Hizo case 3 unazotolea mfano inaonekana hauna details za kutosha ila tu umeamua kuwa "FEMINIST" wa kutetea mwanamke kwa kila jamba bila kuangalia uhalisia!! Jamii huwa ina jinsi yake ya kuchambua mambo, hata tukitaka kulazimisha misimamo yetu tutaendelea kuonekana watu wa ajabu!

Wanawake si malaika ndani ya ndoa, na ni kweli kuwa wapo wanaovunja ndoa zao kwa makosa yao! Jamii inapofanya conclusion, imeona kilichotokea! Pale ambapo wenye kosa ni wanaume, jamii husema vile vile!! Tusigeuze jukwaa hili feminism movement, tuongee vitu kwa haki na kuangalia uhalisia wa kila tukio kwa mapana yake!!
 
Jamani wana MMU kuna ndoa zomevunjika nimezishuhudia zaidi ya 3 na zote ukizisikiliza kesi zao nimwanaume kutokuwa mwaminifu yaani kuwa na nyumba ndogo au kutoka na wanawake tofauti tofauti nje ya ndoa lakini cha kushangaza jamii inawahukumu hao wanawake walioachwa kuwa wameshindwa kuipalilia ndoa mara wawaambie mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe. sasa mimi huwa najiuliza WHY??? mwanamke tu jamani??
napinga hiyo tetesi ya wanaume. Inastahili kuwa hivi "Mwanamume mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono na miguu yake miwili". Maana ya kuwa kichwa katika familia ni nini? Yangu haitavunjika ng'o hata kama mwanamke ni kama kinanda najua jinsi ya kumpunguza volume, hata awe moto ntazima kwa CO2 na sio maji. Wanaume tuwe na busara, mwanmke kiumbe kidogo sana, mpeleke taratibu atafika na sio kukanyagia accelerator hadi mwisho
 
mwanamke huwa ndo nguzo ya nyumba na ndo huleta maelewano au kuharibu ... lawama zinakuwa kwa vile kashindwa kuitunza nyumba yake

so ni mkeo ambaye anaenda kukutongozea wanawake wengne nje?
achen justfcation zenu zisizovaa ndala....ukadig nje et lawama umpe mkeo?

ni km vile uamue kukojoa seblen afu useme ni uyu mwanamke kanifanya nikojoe apa cz kashindwa kunishtua kwenda chooon....try to admit MNAPOKosea ahh inakera...yaan kafanya yeye then lawama kwako
 
Kumbe na wewe umeshaligundua hilo mamaa.
hata sisi wanaume tunalifahamu hilo ila ujeuri tu. Mungu turehemu sisi wanaume, hawa wanawake wametuvumili vya kutosha.
ngoja kwanza tausi, unaonaje hii thread -"https://www.jamiiforums.com/jf-chit-chat/175215-i-have-to-do-ila-isiwe-arusha" wakulaumiwa ni nani?
 
so ni mkeo ambaye anaenda kukutongozea wanawake wengne nje?
achen justfcation zenu zisizovaa ndala....ukadig nje et lawama umpe mkeo?

ni km vile uamue kukojoa seblen afu useme ni uyu mwanamke kanifanya nikojoe apa cz kashindwa kunishtua kwenda chooon....try to admit MNAPOKosea ahh inakera...yaan kafanya yeye then lawama kwako
andaeni migomo ( sex strike). hii mifumo dume itokomee mbali
 
Jamani wana MMU kuna ndoa zomevunjika nimezishuhudia zaidi ya 3 na zote ukizisikiliza kesi zao nimwanaume kutokuwa mwaminifu yaani kuwa na nyumba ndogo au kutoka na wanawake tofauti tofauti nje ya ndoa lakini cha kushangaza jamii inawahukumu hao wanawake walioachwa kuwa wameshindwa kuipalilia ndoa mara wawaambie mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe. sasa mimi huwa najiuliza WHY??? mwanamke tu jamani??
Ndoa isipoanza na misingi ya kumjua Mungu huleta shida na matokeo yake ni kuvunjika au kuwa na kesi zisizoisha katika ndoa hiyo.Wanandoa pekee wanaweza kuokoa ndoa yao au kuifanya isiwe na amani.Kukosa uaminifu kwa wanandoa nitatizo kubwa sana katka dunia ya sasa iliyojaa matamanio ya kila aina .Kujenga ndoa juu ya misingi ya dini huepusha matatizo mengi kwenye ndoa.Kwa wakristo lazima watambue mke na mme wanapooana wanaambatana na kuwa mwili mmoja.Kwahiyo lazima watambue wameanza maisha mapya ya kuacha wazazi wao,lazima waambatane pamoja(kuacha kutamani nje ya ndoa) na lazima wawe na umoja.Ndoa yenye umoja hustawai na haiwezi kuvunjwa na upepo wa dunia hii.ndoa iliyojengwa katika misingi ya Mungu wanandoa watatumia maneno ya upole ,watafanyakazi kwa kushirikiana na kila ,wanachopata wataweka wazi na kupaga namna ya kukitumia,wanakuwa na makusudi mema,watapendana kama nafsi zao,watasameheana .Haya yote ni matunda ya roho ya upendo kwa ndoa .Mungu aziponye ndoa zote zenye shida ya kutoelewana
 
Mimi nashangazwa na mijadala ya namna hii kwani haiko ballanced! Mtu ametoa case tatu ambazo yeye anaamini kuwa wanawake wanalaumiwa kwa kuvunja ndoa, halafu anatoa mjumuisho kuwa kila ivunjikapo ndoa basi mwanamke hulaumiwa!!! Hii mie sijaiona. Ndoa inapovunjika, wale wanaojua kilichosababisha ndoa kuvunjika hukisema, na ikiwa mhusika ni mwanamke jamii husema!!
kwani wewe ni suspect No. 4. Mtoa mada ameeleza vizuri sana kuwa the real issue ya hizo case 3 ni infidelity lakini badala ya jamii kuona hilo inawalaumu wanawake. jamii inakuwa impartial, partisan kumfavour mwanume.

Hizi "sweeeping conclusion" za kuwa mwanamke anaonewa au mfumo dume ndo tatizo lenyewe. Hivi wanawake kwenye ndoa ni malaika na hawasababishi ndoa kuvunjika?? Wenye ndoa wanajua. Hata jamii inaposema aliyesababisha ndoa kuvunjika ni mke, tujiridhishe kwa kufanya utafiti si kwa kupinga tu na kulaumu mfumo dume!!
mtoa mada hajasweep into conclusion ila ameeleza alichosikia na judgement ya jamii sasa anauliza iweje basi mwanamke ndo anatupiwa lawama zote. mkuu kwani wewe unaishi dunia ipi huelewi mambo haya. hujawahi kusikia mtu amehukumiwa miaka 30 kwa kosa ambalo halijui bali kapewa?
Hizo case 3 unazotolea mfano inaonekana hauna details za kutosha ila tu umeamua kuwa "FEMINIST" wa kutetea mwanamke kwa kila jamba bila kuangalia uhalisia!! Jamii huwa ina jinsi yake ya kuchambua mambo, hata tukitaka kulazimisha misimamo yetu tutaendelea kuonekana watu wa ajabu!
duh! hii mada yaonekana imekuchoma sana ila sijui kwa nini. kuwasupport wanawake haimaanishi ana feminist ideology. samahani kama amekukwaza
Wanawake si malaika ndani ya ndoa, na ni kweli kuwa wapo wanaovunja ndoa zao kwa makosa yao! Jamii inapofanya conclusion, imeona kilichotokea! Pale ambapo wenye kosa ni wanaume, jamii husema vile vile!! Tusigeuze jukwaa hili feminism movement, tuongee vitu kwa haki na kuangalia uhalisia wa kila tukio kwa mapana yake!
na mwanamume pia sio malaika. tukubali pia makosa na tuwe tayari kuomba msamaha. tatizo letu wanaume ni kujifanya Miungu midogo, iwapo tutabadilisha hii dhana sidhani kuna ndo inaweza vunjika
![/QUOTE]
 
mwanamke huwa ndo nguzo ya nyumba na ndo huleta maelewano au kuharibu ... lawama zinakuwa kwa vile kashindwa kuitunza nyumba yake

Aaaagh! mambo mengine ni kuendekeza ujinga. Kuzini azini mtu mwingine halafu kuhukumiwa ahukumiwe mwingine!!! kwa kweli kwa jinsi hii UKIMWI utatumaliza watu weusi!.. Kweli "Miafrika ndivyo tulivyo..........." N.N.
 
mwanamke mpumbavu huvunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom