Kwanini Kikwete huyakimbia matukio?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Rais Jakaya M Kikwete amekuwa na hulka isiyovutia.

Linapotokea tukio ambalo yeye kama Rais anatazamiwa kuonyesha njia yeye hutingwa na safari tena za nje ya nchi.

Matukio ninayoyakumbuka kuwa Rais alikuwa Tanzania wakati yanatokea lakini akasafiri ni yale ya mlipuko wa mabomu ya Gongolamboto na la juma lililopita la mauaji ya Polisi Songea.

Kwanini Rais huyakimbia matukio kama haya na badala yake hutingwa na matukio ya kawaida kama uzinduzi wa benki na hoteli?
 
Niliwahi kuona katika documentary moja ya Snoopy, mmojawapo wa wahojiwa akisema, 'Snoopy has one trait, he does not follow trends but he sets trends'. Hii ni kweli ukisikiliza maneno yake, hata mavazi na staili za nywele.

Sasa tatizo la JK ni ku follow trends/matukio. na siku zote mtu anaye follow trends ni reactive. Therefore the guy is weak. Simaanishi kuwa kila afuataye trend ni weak na reactive, but exclucively speaking, jk is weak and reactive. Na hii inawapa 'wapambe' wake na adui zake nguvu za ku set trends, and they become proactive, therefore they are strong.
 
Nadhani anaamini kwa dhatri kabisa kuwa matatizo huwa yana tabia ya kujitatua yenyewe, kwa hiyo anaamini kuwa akiondoka, atakaporejea atakuta matatizo yameshajitatua
 
Anatudhihirishia kuwa hajachaguliwa kututumikia bali kwa ajili ya safari za kutalii huko anakoona kuna maslahi yake zaidi
 
Anatudhihirishia kuwa hajachaguliwa kututumikia bali kwa ajili ya safari za kutalii huko anakoona kuna maslahi yake zaidi

kwa safari ya botswana isiyo na msingi nilitegemea raisi angeahirisha kwenda huko na kurudi nyumbani
 
Umesahau sakata la mgomo wa madaktari alitimkia Davos,labda hapendistress

Haya yote yanaendana na imani za kishirikina; sangoma wake wamemwambia kuwa yanapotokea matatizo makubwa asijitokeze kwani yanaweza kumfanya aondolewe madarakani!!Hakuwa na sababu ya kukimbilia Davos ambako alishindwa hata kujibu maswali wakati maelfu wa wananchi walipoteza maisha kwasababu ya mgomo wa madaktari!
 
Visit Horney and Relational Theory utagunduwa ni kwanini JK happened to be that way.
 
Mzee mzima anakimbia ili kikiwaka huko nyuma asirudi! Kule kwa wapare wana msemo kua ukipanda kwenye mti, hakuna kuanguka na kushuka, ukianguka umesha shuka. Kikiwaka jamaa akiwa nnje itakua kama Balali tu.
 
Wanangu msihangaishwe na Kikwete. Maskini siku zake simeishajiishia na hili analijua. Ndiyo maana anajiridhisha kwa kujilisha upepo. Muoneeni huruma mja huyo. Siku akianguka hataamka. Muombeeni aende kumuona muungu wake shehe Yahya aliyekuwa akimtumia kuwatisheni. Baba yenu nasema: muoneeni huruma mahluku huyu anayejiishia taratibu.
 
yuko biroo standard arafu hana shida na wewe we nani anaenda majuu kwaza chadema hoyeeeee 2015 chadema zamuyetu kitu slaa bwana yule ataphubutu kusema chochote
 
Mlipomchagua hamkujua hulka yake?ukikosa umakini utalipia gharama hiyo so hii ndo bei ya u kealess wa wa Tz,jk tangu zamani anajulikana kwa ubitoz,nilikuwa nauza nguo kipindi cha bunge enzi zile akiwa foreign affairs,yan yeye kaz yake ilikuwa kuwachagulia pamba wabunge na mawazir,kwake masihara ni sehem ya maisha yake,anahusudu sketi kama ana jini mahaba,so kila mnaloshangaa leo ni tabia yake ya longtime!!
 
Rais Jakaya M Kikwete amekuwa na hulka isiyovutia.Linapotokea tukio ambalo yeye kama Rais anatazamiwa kuonyesha njia yeye hutingwa na safari tena za nje ya nchi.Matukio ninayoyakumbuka kuwa Rais alikuwa Tanzania wakati yanatokea lakini akasafiri ni yale ya mlipuko wa mabomu ya Gongolamboto na la juma lililopita la mauaji ya Polisi Songea.Kwanini Rais huyakimbia matukio kama haya na badala yake hutingwa na matukio ya kawaida kama uzinduzi wa benki na hoteli?


Rais anao watendaji wengi wanaomsaidia kazi hivyo si lazima kila tukio awepo yeye... uwe mwelewa!
 
Back
Top Bottom