Rais Kikwete na Lowassa hawakukaa chini kuzungumza baada ya tuhuma nzito zilizotolewa Bungeni na hasa maneno makali ya Wabunge mbalimbali. Kwa yeyote aliyesikiliza hoja za Wabunge ni wazi kuwa Waziri Mkuu alikuwa implied na kuna waliothubutu kutaja na majina kabisa.
Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu si jambo dogo hata kidogo hata kama mtu humpendi. Moja ni kwa sababu za kikatiba na jingine ni suala la gharama.
Kikatiba, Waziri Mkuu anapojiuzulu Baraza la Mawaziri linavunjika na hivyo Rais anatakiwa kuanza mchakato mpya wa kupata Waziri Mkuu mpya na Baraza jipya la Mawaziri. Sasa kama Taifa hatuwezi kuruhusu iwe rahisi kwa Waziri Mkuu kujiuzulu na kuanza moja kila inapotolewa tuhuma dhidi yake. NI lazima Rais (anayemteua Waziri huyo) kuwa na msimamo unaoeleweka ili wananchi waridhike kuwa kweli kosa fulani la Waziri Mkuu linamstahilisha kujiuzulu.
Sasa Waziri Mkuu anapotolewa tuhuma nzito ni wajibu wa Rais kumuita na kumsikiliza kabla Waziri huyo hajafanya uamuzi wowote wa papara (kama wa Lowassa). Kwa wanaokumbuka Rais alikuwa mikoa ya Kusini na Makamu alikuwa sehemu nyinyine na wao kama Taifa zima walisikia kujiuzulu kwa Lowassa "radioni". Kwanini Kikwete hakumuita Waziri wake Mkuu na kuhoji tuhuma dhidi yake na kusikia utetezi wake?
Kigharama, kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kunasababisha gharama zisizo za lazima za kuunda Wizara mpya au kuingiza mawaziri wapya. Kikwete alilazimika kuunda wizara mpya na kuleta mawaziri wapya na yote hayo yana gharama. Hivyo, hatuwezi kuchukuliwa kwa urahisi tu kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kana kwamba ni kitu kidogo.
Pia watu wanasahau kikao alichofanya Rais Kikwete na wazee wa Dar kuelezea mshtuko wake wa kujiuzulu kwa Lowassa. Tukumbuke kuwa Kikwete hakusema Lowassa amefanya makosa yoyote na alisema kuwa kujiuzulu kwa Lowassa kulikuwa ni kwa "ajali ya kisiasa". Sasa kama Rais alijua Lowassa hakufanya makosa kwanini hakusimama naye na kuepusha maamuzi ya kisiasa?
Je, tunaweza kukubali hizi "ajali za kisiasa" kwa kushindwa kuzizuia?
Kidemokrasia, naamini Watanzania tulinyimwa nafasi ya kuona demokrasia yetu inavyoweza kufanya kazi unapotokea mgongano kati ya Bunge na Rais. Kikwete angeweza kukaa na Lowassa, kuangalia ushahidi uliotolewa na Kamati Teule, kupima uzito wa hoja za wabunge na kuandaa majibu kwa kila hoja.
Ninaamini hakuna mwanasiasa wa Tanzania ambaye angeweza kupangua hoja za kamati teule kwa urahisi na kwa umahiri kama siasa (na hapa namaanisha). Ingekuwa vizuri kweli kwa Rais Kikwete kuchukua upande wa Waziri wake Mkuu ili tuone mgongano kati ya Mwenyekiti wa CCM na wabunge wa CCM! Je, kweli mnafikiri Bunge la CCM lingeweza kwenda kinyume na Rais wake? Je wale waliokuwa vinara wangeweza kuendelea kuwa vinara baada ya Rais kuchukua msimamo wa kumtetea Lowassa? Je yawezekana ushujaa wao ni kwa sababu Kikwete hakuchukua msimamo na hivyo ni kuwa kama bingwa ambaye hakutaka kuingilia mapambano ya ridhaa!?
Kama hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa Lowassa kunufaika na mkataba wa Richmond, kama hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kuonesha kuwa Lowassa ndiye Richmonduli, kama Kamati haikuweza kuonesha kuwa mtoto wa Lowassa ndiye alihusika na Richmond na kwa mujibu wa sheria ya Maadili huo ni mgongano wa Maslahi kwa Lowassa, ninajiuliza Lowassa alijiuzulu kwa sababu gani hasa?
Jibu ni kuwa Lowassa alijiuzulu ili kumkomoa Kikwete! Alijiuzulu kama spite ya Kikwete na urafiki wao; hakujiuzulu kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa kwa sababu rafiki yake, mtu aliyehangaika kumuweka madarakani na mtu ambaye kwa kiasi kikubwa ni mshirika wake wa kisiasa alimtosa wakati alipotakiwa kusimama naye.
Je, ina maana kwa Kikwete kusimama na Lowassa kunamfanya Lowassa asiwe na makosa? Na kama alikuwa na makosa ni kweli yalimstahilisha ajiuzulu kwa namna ile ya utekaji nyara nchi?
Mzee mwanakijiji salam na heshima natangliza;
Ninachosoma hapo juu kinanizungusha kichwa kidogo na naamini sitakua peke kwani nimeona wachangiaji kadhaa wameleweshwa na main Thread uliyotuwekea hapa.
Hivi KWELI UNA HAKIKA NA IMANI kuwa LOWASA ni **** wa mtaani kiasi hichooooooo??? awe hana KOSA LOLOTE na AKAACHE NAFASI KAMA WAZIRI MKUU ati kwa KUMKOMOA KIKWETE!!! kumkomoa for WHAT???
Ati lowasa kasaidia kumuweka Kikwete madarakani (pengine) Lakini Lowasa huyo ana kura moja tu Hata ukijumlisha familia yake marafiki na hao atakaowapa hongo wakati wa kampeni bado walikuwa na hiyari ya kutumia kura zao watakavyo.Na kama alikuwa na nguvu na uwezo huo kwa nini asingeutumia na kugombea yeye nafasi ya Urais. Jibu liko wazi WATANZANIA wote tunakumbuka alivyoumbuliwa na Baba wa Taifa hayati Mwl Nyerere kuwa nafasi hiyo haimfai kutokana na TABIA zake in fact Kikwete ni wa kujilaumu mwenyewe kwani the WRITING WERE ON THE LOWASAS FACE kwa kipofu kuweza kuona na kujua kuwa hafai. Kwa hiyo Kikwete asingejitendea HAKI kama angeruhusu URAFIKI UMPONZE kwa mara ya pili.Kama siasa na dhamana zina fadhila basi Kikwete alilipa kwa Lowasa, ilikuwa ni wajibu wa Lowasa kutambua na kuafanya KAZI ALIYOPEWA KWA ADABU. Sasa MMJJ Lowasa kaonewa ??? au Kajionea??? na wewe unaonaje arudishiwe ofisi yake?? AU unamenej kampeni yake ya 2010??