Kwanini Kikwete hakusimama na Lowassa?

Wanajamii

Tatizo hapa jina la hii thread na haya malumbano yaliyo hapa jamvini ni vitu viwili tofauti.wengi wanaonekana wako more interested na malumbano than the actual thread.

Ni wazi kuwa JK alimteua EL pasi na kujua histtoria ya ufisadi wake.Alimteua just kulipa fadhila ama aliamua tu kumpa second chance G-d knows.Lakini hakuchaguliwa kwa kuwa alikuwa more qualified.Tusidanganyike hata kidogo kwamba Rais anamuogopa Lowassa ama Lowasa ana sauti kumpita Rais,This is not true.Katika serikali yetu ya Tanzania kiongozi ambaye ana nidhamu ya kiuongozi sijaona zaidi ya Makamu wa Rais Shein.Wengine wote kila kukicha wanateleza.Kinachowaweka madarakani ni blessing ya Rais.

Sasa ndugu yangu MWANAKIJIJI Rais huyu atawatetea wangapi ikiwa kila kukicha awe anatizama amtetee yupi maana kila siku viongozi wanakuja na mpya.Loe waziri mkuu anataka kuuwa wanaotuhumiwa kuuwa maalbino,kesho ainuke kumtetea Masha na uzembe wake,keshokutwa kuna mkuu wa wilaya anacharaza watu viboko.I think Mr.President was right kwa lile la Lowasa.

Mwisho bwana WILIAM nimeipenda hii staili ya KATA ISHU. THINK TWICE.

SAHIBA.
 
Kuwa mtu wa siku nyingi au wa jana haijalishi kitu hapa JF. Wewe kata issue usilete za kujuana wala kutaka sifa na recognition. Huna cha kuchangia soma post ujikate zako ukacheck homework za watoto.

Acha kulialia na mods, wana kazi nyingine za kufanya na pia kuna members wengine wanahitaji kusikilizwa matatizo yao. Ugeni wako usitake kubadilisha maisha ya wenyeji, kama vipi jiondoe hadi hapo utakapokuwa na cha maana cha kuchangia au hadi hapo utakapokubali kuwa hapa haliangaliwi jina, inaangaliwa hoja. Leta hoja acha viroja.

Ukileta uongo, unasimamishwa nao immediately, ukileta hoja imepindapinda utabanwa vile vile. Kaa mkao wa kula challenges. Kama huwezi kuhimili challeges na criticism nenda kwenye TV, huko kuna kiongozi wa mada na maswali yako limited na muda.

MUHESHIMIWA,

Tafadhali jaribu kutumia hekima kidogo katika kumfahamisha mwenzio hisia zako.hatuko hapa kwa malumbano wala kupoteza muda tupo haha kukata issue.Lugha ya masimango na kejeli haisaidii kujenga inabomoa Taifa.Respect ndio kitu cha kwanza katika forum hii na tunajitahidi kuipigania ingawa ni vigumu.Ni vigumu kumuheshimu usiyemjua hasa kama humuoni lakini tujitahidi ndio mwanzo wa ustaarabu mengine yatafuatia. THINK TWICE.

SAHIBA.
 
Let this discussion carry on in peace. I will not hesitate to act whenever it is necessary especially when the discussion move into personalities. Please refrain.
 
Ninaamini, hakuna wakati ambapo Kikwete alionesha udhaifu mkubwa kama kiongozi kama kushindwa kusimama na Waziri wake Mkuu au kupanga naye mkakati wa kujibu mashambulizi ya Bunge. Ndiyo maana ninaamini Lowassa hana sababu ya kumlaumu mtu mwingine yoyote (siyo Spika, CCM au Mwakyembe) kwa kujiuzulu kwake bali mtu mmoja tu ambaye alishindwa kuchukua msimamo mgumu!

Ewe Mwana wa Kijiji, kumbuka Mwalimu alianzisha huu mfumo wa kuwa na Wakulu 2 Watendaji, yaani Rais na Waziri Mkuu, makusudi kabisa ili kumlinda Rais na mitikisiko kama hii. Kwa lugha nyingine, cheo cha Waziri Mkulu ni kuwa ngao ya Mkulu ya kuzuia mikuki isifike Ikulu. Hebu sikia tena maneno haya ya Mwalimu aliyoyatoa wakati hali tete ilipotokea kati ya Mkubwa wa Awamu ya 2 na Waziri Mkubwa wake:

"Kuwajibika kuna ngazi zake. Hatuwezi kusema ati kwa sababu Mkuu wa Nchi yetu ni Rais Mtendaji, basi atawajibika kwa kila kosa la Serikali yake na Mawaziri wake, hata pale, ambapo mkosaji halisi na wa wazi wazi ni Waziri. Rais hawezi kuwajibika kwa makosa ya Uongozi wa Serikali Bungeni, kana kwamba naye ni Mbunge. Viongozi wa Chama na Serikali waliomo Bungeni, hasa Waziri Mkuu na Katibu Mkuu, ndio wanaostahili kuwajibika moja kwa moja. Kwa vyovyote vile hatuwezi kujenga utaratibu ambapo Waziri akikosa Rais ndiye anayewajibika. Mara mbili sasa Rais amelazimika kukiri hadharani makosa ya Serikali yake; na Mawaziri wahusika hawana wasi wasi...Katiba ya Nchi yetu, na utaratibu tunaojaribu kujenga, vinataka kuwa katika hali kama hiyo Mawaziri ndio wawajibike, na hivyo kumlinda Rais, si Rais awajibike, na kuwalinda Mawaziri wake, na tena kwa kosa ambalo si lake...Kosa kubwa la Rais (na ni kosa kubwa), ni kule kukubali kushirikishwa kosa, badala ya kuwafukuza wale waliomshauri ashiriki kosa lao" - Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania Ukurasa wa 44

"Narudia: kumbadili Waziri, hata Waziri Mkuu, si jambo la ajabu. Anaweza kujiuzulu, anaweza kufukuzwa, na Nchi isitikisike. Lakini huwezi kumtikisa Rais wa Nchi bila kuitikisika Nchi yenyewe" - Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania Ukurasa wa 46
 
Companero.. kuna kitu kikubwa sana nimekisema; tatizo watu wamekikosa na mimi sitojaribu kufafanua kwa sababu wakivuka tu kuwa "mwanakijiji anaandika vitu gani tena" they'll get it! few have.
 
Jobo,
Ulisikiliza vizuri ripoti ya Mwakyembe dhidi ya Richmond? Lowasa alikuwa ndo kasimama kidete akiagiza nini kifanyike mpaka Richmond wakapewa hiyo tenda. Na kwa taarifa yako ni kwamba aliamua kuiweka pembeni tenda bodi ya TANESCO katika manunuzi hayo akaunda tenda bodi yake ya watu watatu special kushughulikia suala hilo na akafanikiwa, hapo bado unasema hakuhusika? Pia usisahau uswahiba wa EL na Rostam, na huo ilikuwa mradi wao.

Siyo kusikiliza tu nimeisoma page to page, is not worth the paper it is written on my friend. Richmond report is one of the poorest researched documents ambazo nimewahi kuziona.

Nilisubiri nione cogent evidence ya jinsi ambavyo wawili hao wanavyohusika na Richmond, only to get statement like: Tulimwita Rostam lakini tukaambiwa amesafiri! When was he called? A day after x-mass ambapo tume ilitakiwa iwe imeshakamilisha kazi yake kama wasingeongezewa muda! Lowassa yeye anaambiwa apime!!! uchafu wa Lowassa ambao uko wazi kwenye report ni barua ya Msabaha na maneno ya Msabaha nje ya kiapo kuwa yeye ni mbuzi wa kafara!

Irudie tene hiyo report na utagundua ninachosema. By the way, I am not here to defend lowassa, naweza kweli akawa alifanya ufisadi katika sakata hili, but where is the evidence?????
 
........then hukuielewa ripoti nzima.........na kama hukuielewa sijui tukusaidieje.....pengine tafuta majadiliano hapa JF kuhusu hiyo ripoti ndio utaelewa........
 
Companero.. kuna kitu kikubwa sana nimekisema; tatizo watu wamekikosa na mimi sitojaribu kufafanua kwa sababu wakivuka tu kuwa "mwanakijiji anaandika vitu gani tena" they'll get it! few have.

Siku zote huwa vitu vyako unajifanya hadhira haikuelewi, na kwa hayo maneno ina maana labda:-
1. una akili kuliko watu wote hapa JF.
2. ama unaandika vitu viko nje ya kile kitu ulichokusudia kukiandika.
3. unajaribu kuchezea akili za watu ili upate "points" za kuweka katika maandishi yako.
 
haya ni mashambulizi dhidi ya mtoa hoja na si dhidi ya hoja.
siungi mkono....
 
haya ni mashambulizi dhidi ya mtoa hoja na si dhidi ya hoja.
siungi mkono....

Nani aliyekwambia kwamba umelazimishwa kuniunga mkono, mbona HAUJIAMINI?. Huu si mjadala kila mtu ana haki ya kuchangia, kama unaona kuandika kwangu humu inakuuma, muwe muna PM hii mijadala ili isiwe public ili tusichangie. Lakini ukienda public tutatoa mawazo. Naomba unioneshe hayo mashambulizi.
 
..pia ni haki yangu kuunga au kutounga mkono mkuu.
Najiamini sana ndo maana natoa mawazo na maoni yangu publicly. Kitu kingine huwezi kulazimisha kuwa hoja zijadiliwe kupitia PMs, ninaanza kunusa kuwa wewe mheshimiwa hauna tofauti na Mkuchika, mtafungia vyombo vyote ila msichoweza ni kuifungia hii baraza yetu.
mashambulizi uliyoyafanya nimeyacopy ktk post yangu iliyopita.

Umesoma kitabu cha POSTAMASTA?
 
Rais Kikwete na Lowassa hawakukaa chini kuzungumza baada ya tuhuma nzito zilizotolewa Bungeni na hasa maneno makali ya Wabunge mbalimbali. Kwa yeyote aliyesikiliza hoja za Wabunge ni wazi kuwa Waziri Mkuu alikuwa implied na kuna waliothubutu kutaja na majina kabisa.

Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu si jambo dogo hata kidogo hata kama mtu humpendi. Moja ni kwa sababu za kikatiba na jingine ni suala la gharama.

Kikatiba, Waziri Mkuu anapojiuzulu Baraza la Mawaziri linavunjika na hivyo Rais anatakiwa kuanza mchakato mpya wa kupata Waziri Mkuu mpya na Baraza jipya la Mawaziri. Sasa kama Taifa hatuwezi kuruhusu iwe rahisi kwa Waziri Mkuu kujiuzulu na kuanza moja kila inapotolewa tuhuma dhidi yake. NI lazima Rais (anayemteua Waziri huyo) kuwa na msimamo unaoeleweka ili wananchi waridhike kuwa kweli kosa fulani la Waziri Mkuu linamstahilisha kujiuzulu.

Sasa Waziri Mkuu anapotolewa tuhuma nzito ni wajibu wa Rais kumuita na kumsikiliza kabla Waziri huyo hajafanya uamuzi wowote wa papara (kama wa Lowassa). Kwa wanaokumbuka Rais alikuwa mikoa ya Kusini na Makamu alikuwa sehemu nyinyine na wao kama Taifa zima walisikia kujiuzulu kwa Lowassa "radioni". Kwanini Kikwete hakumuita Waziri wake Mkuu na kuhoji tuhuma dhidi yake na kusikia utetezi wake?

Kigharama, kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kunasababisha gharama zisizo za lazima za kuunda Wizara mpya au kuingiza mawaziri wapya. Kikwete alilazimika kuunda wizara mpya na kuleta mawaziri wapya na yote hayo yana gharama. Hivyo, hatuwezi kuchukuliwa kwa urahisi tu kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kana kwamba ni kitu kidogo.

Pia watu wanasahau kikao alichofanya Rais Kikwete na wazee wa Dar kuelezea mshtuko wake wa kujiuzulu kwa Lowassa. Tukumbuke kuwa Kikwete hakusema Lowassa amefanya makosa yoyote na alisema kuwa kujiuzulu kwa Lowassa kulikuwa ni kwa "ajali ya kisiasa". Sasa kama Rais alijua Lowassa hakufanya makosa kwanini hakusimama naye na kuepusha maamuzi ya kisiasa?

Je, tunaweza kukubali hizi "ajali za kisiasa" kwa kushindwa kuzizuia?

Kidemokrasia, naamini Watanzania tulinyimwa nafasi ya kuona demokrasia yetu inavyoweza kufanya kazi unapotokea mgongano kati ya Bunge na Rais. Kikwete angeweza kukaa na Lowassa, kuangalia ushahidi uliotolewa na Kamati Teule, kupima uzito wa hoja za wabunge na kuandaa majibu kwa kila hoja.

Ninaamini hakuna mwanasiasa wa Tanzania ambaye angeweza kupangua hoja za kamati teule kwa urahisi na kwa umahiri kama siasa (na hapa namaanisha). Ingekuwa vizuri kweli kwa Rais Kikwete kuchukua upande wa Waziri wake Mkuu ili tuone mgongano kati ya Mwenyekiti wa CCM na wabunge wa CCM! Je, kweli mnafikiri Bunge la CCM lingeweza kwenda kinyume na Rais wake? Je wale waliokuwa vinara wangeweza kuendelea kuwa vinara baada ya Rais kuchukua msimamo wa kumtetea Lowassa? Je yawezekana ushujaa wao ni kwa sababu Kikwete hakuchukua msimamo na hivyo ni kuwa kama bingwa ambaye hakutaka kuingilia mapambano ya ridhaa!?

Kama hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa Lowassa kunufaika na mkataba wa Richmond, kama hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kuonesha kuwa Lowassa ndiye Richmonduli, kama Kamati haikuweza kuonesha kuwa mtoto wa Lowassa ndiye alihusika na Richmond na kwa mujibu wa sheria ya Maadili huo ni mgongano wa Maslahi kwa Lowassa, ninajiuliza Lowassa alijiuzulu kwa sababu gani hasa?

Jibu ni kuwa Lowassa alijiuzulu ili kumkomoa Kikwete! Alijiuzulu kama spite ya Kikwete na urafiki wao; hakujiuzulu kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa kwa sababu rafiki yake, mtu aliyehangaika kumuweka madarakani na mtu ambaye kwa kiasi kikubwa ni mshirika wake wa kisiasa alimtosa wakati alipotakiwa kusimama naye.

Je, ina maana kwa Kikwete kusimama na Lowassa kunamfanya Lowassa asiwe na makosa? Na kama alikuwa na makosa ni kweli yalimstahilisha ajiuzulu kwa namna ile ya utekaji nyara nchi?

Mwanakijiji ,

Kuna kitu kimoja tu ambacho kinasomeka vizuri kwenye post zako!!! unatamani sana Tanzania kuwa na political unrest!!!!

Kwa hiyo sishangai baada ya kuona issue ya Mh. Edward imeishia bila kuleta tatizo sasa umeanzisha issue ambayo itafanya Mh.Edward na Mh. Jakaya waonane hawakusaidiana wakati wa shida.

Umeelezewa vizuri sana na Mh. William kwa nini sio vyema kuingilia issue za mhimili mwingine!

Rais, Head of state anatakuwa kuwa mtu mwenye subra sana!!! Sio mtu wa kuzamia kwenye mijadala ambayo ni hot na yenye hisia za watu... Ndio maana ile cheo sio rahisi kiasi hicho mkuu!
 
..pia ni haki yangu kuunga au kutounga mkono mkuu.
Najiamini sana ndo maana natoa mawazo na maoni yangu publicly. Kitu kingine huwezi kulazimisha kuwa hoja zijadiliwe kupitia PMs, ninaanza kunusa kuwa wewe mheshimiwa hauna tofauti na Mkuchika, mtafungia vyombo vyote ila msichoweza ni kuifungia hii baraza yetu.
mashambulizi uliyoyafanya nimeyacopy ktk post yangu iliyopita.

Umesoma kitabu cha POSTAMASTA?

Kama ulijua kuwa una haki hiyo. Hukuwa na haja ya kuandika kuwa mimi ninafanya mashambulizi, halafu hapo hapo unaniambia "sikuungi mkono". Wewe jadili mada iliyopo kwa kutoa vigezo, nimekuuliza ni yapi mashambulizi yangu. Unanirudisha kule kule, hujasema kwa mambo 3 niliyoandika vipi hayo mambo ni mashambulizi. Haya mjadala mwema.
 
Mwanakijiji ,

Kuna kitu kimoja tu ambacho kinasomeka vizuri kwenye post zako!!! unatamani sana Tanzania kuwa na political unrest!!!!

Kwa hiyo sishangai baada ya kuona issue ya Mh. Edward imeishia bila kuleta tatizo sasa umeanzisha issue ambayo itafanya Mh.Edward na Mh. Jakaya waonane hawakusaidiana wakati wa shida.

Umeelezewa vizuri sana na Mh. William kwa nini sio vyema kuingilia issue za mhimili mwingine!

Rais, Head of state anatakuwa kuwa mtu mwenye subra sana!!! Sio mtu wa kuzamia kwenye mijadala ambayo ni hot na yenye hisia za watu... Ndio maana ile cheo sio rahisi kiasi hicho mkuu!

Did I sniffed something here?
Napenda kama subra ya muungwana italeta heri, maana amekuwa kimya mno kana kwamba haguswi na kilio cha wengi.
ningelikuwa mie ningetumia methali ya mchelea mwana....
 
Did I sniffed something here?
Napenda kama subra ya muungwana italeta heri, maana amekuwa kimya mno kana kwamba haguswi na kilio cha wengi.
ningelikuwa mie ningetumia methali ya mchelea mwana....

Jamaa anaguswa sana lakini anatakiwa kuingia kwenye mijadala hiyo wakati muafaka... sio anazama tu wakati ambao sio... asipokuwa makini anaweza kuweka petrol kwenye moto badala ya kuweka maji kwenye moto.

Sijui una umri gani ndugu lakini jiulize subra yako ulipokuwa na miaka 7, 14 na 21...

You will see different wisdom....

Kuna vitu vingine ni rahisi kung'amua especially kama umekuwa kiongozi mdogo tu... nakupa scenerio moja rahisi sana.

Customer is complaining of your staff kwamba ametoa bad service, huyo staff yako ndio customer service manager, in other words ndio expert wako wa customer care... je ukiwa CEO... unaingilia huo mgogoro hakaraka na kusema customer is wrong and therefore customer service manager wako super na kumu-loose customer...au unasema manager wako ni bull-shit na unashusha self-esteem yake... hivyo unamfanya a-resign na ubaki na customer?

Kwenye issue kama hizo unatakiwa uingie wakati ambao hutashusha self-esteem ya customer na pia ya staff wako!!! you need hekima na timing.

Over
 
Kilichomponza EL ni kujiamini kutokana na umaarufu alioupata kupitia kwa JK alijua kuwa JK atamlinda kwa vyovyote vile kwa kuwa alijua JK hawezi kusimama bila yeye(EL).Pia alijiamini kutokana na mizizi aliyojiwekea nchi nzima na alijua angeweza kumtikisa JK kama ilivyotokea Madagasca.Hata hivyo hadi sasa mtikisiko wa serikali ya JK ni kutokana na mizizi ya EL na kundi lake,ili JK awe salama katika uendeshaji wake wa nchi ni vizuri ayang'oe mizizi hiyo.
 
Jamaa anaguswa sana lakini anatakiwa kuingia kwenye mijadala hiyo wakati muafaka... sio anazama tu wakati ambao sio... asipokuwa makini anaweza kuweka petrol kwenye moto badala ya kuweka maji kwenye moto.

Sijui una umri gani ndugu lakini jiulize subra yako ulipokuwa na miaka 7, 14 na 21...

You will see different wisdom....

Kuna vitu vingine ni rahisi kung'amua especially kama umekuwa kiongozi mdogo tu... nakupa scenerio moja rahisi sana.

Customer is complaining of your staff kwamba ametoa bad service, huyo staff yako ndio customer service manager, in other words ndio expert wako wa customer care... je ukiwa CEO... unaingilia huo mgogoro hakaraka na kusema customer is wrong and therefore customer service manager wako super na kumu-loose customer...au unasema manager wako ni bull-shit na unashusha self-esteem yake... hivyo unamfanya a-resign na ubaki na customer?

Kwenye issue kama hizo unatakiwa uingia wakati ambao hutashusha self-esteem ya customer na pia ya staff wako!!! you need hekima na timing.

Over

...kama claims ni nyingi sana and kama reputation ya company inadrop lazima nifanye maamuzi sahihi.
Mkuu Kaseshe, unajua kwamba hizi subira hizi zina uzito na mahala pake, kuna masuala ambayo reaction yake lazima iwe haraka ili kuzuia madhara na kuna masuala ya kusubiri.
Kwa mfano kama unamwona kiongozi aliyeteuliwa na muungwana anamwaga pumba mbele ya jamii na hata tija yake haionekani ktk nafasi aliyomo zaidi sana sana hali inazidi kuwa mbaya, itakuwa uvumilivu wa kifisadi kuendelea kumkumbatia kiongozi aina hii.
shehe nilipokuwa nina umri ulioutaja nilikuwa najifunza methali na hivi sana ndo nazitumia ili kuendesha maisha yangu.
....Endapo Muungwana angekuwa anaguswa basi tungeona moto unavowawakia mawaziri maana siyo mpaka aseme directly kwa umma bali hata indirect kupitia wasaidizi wake ingelikuwa mbolea pia. Sitaki kuamini kwamba anawashauri wasiomfaa ktk kipindi hiki.
kumbuka tupo ktk kipindi cha TIA MAJI-TIA MAJI ohoo!
 
Jk akikuteua ujue you are on your own
Hata kama nitakubaliana na usemi huu, sitaki kukubali kama ni mapungufu, naamini ndiyo style yake ya kazi. JK is a populist politician, yeye atafanya chochote kinachowezekana ili mradi asihusishwe na jambo lolote ambalo in the public eye, ni negative. Kitu kikifanyika na kufanikiwa, he will be there to support fully, lakini hatatokea kwenye tukio mpaka ajue outcome ya jambo ni negative au la, kwahiyo kufanya maamuzi ni ngumu. Maoni yangu ni kwamba Tanzania needed a president like Kikwete kwa wakati huu, kwasababu people needed to be united and started feeling good about their government & country. He is the kind of the guy that make people feel good, na amefanikiwa sana kujenga uzzalendo wa watu – which is good, kwasababu inakuwa rahisi kwa serikali kufanya mabadiliko na maamuzi magumu wakati you have support ya wananchi. Kipaji kikubwa cha uongozi ni kujua strength & weaknes zako na za wateule wako na viogozi wenzako, mimi naamini katika kumteua EL kuwa PM alionyesha hichi kipaji dhahiri. JK alisema bungeni kwenye hotuba yake kwamba nimemteua siyo kwasababu ni rafiki bali ni mfuatiliaji na msimamizi mzuri sana wa mambo ya nchi, kwahiyo team ya Jk ilitakiwa iundwe na watu wote wenye guts za kufanya kazi na maamuzi magumu kama EL, wakati JK akitoa support yake iliyo na public backing nyuma yake. Unfortunately, vurugu za mchakato 2005 nadhani zilikuwa under-estimated na JK na administration yake yote, maadui wake walirudi kwenye drawing table na kuandaa master plan ya kuisambaratisha administration yote na mtandao kwa ujumla, na kwa asilimia kubwa sana wamefanikiwa almost 90%. Adiminsitration ilisambaratika 2006, malengo yote na mipango ya regime yaka-colapse, kwasababu ya richmond – hili jambo tukilijadili leo baada ya hasira kushuka baada ya mwaka mmoja, unaona clearly kwamba ilikuwa political move, lakini ambayo ilichezwa vizuri, wananchi waliweza kuaminishwa mambo. Suala la Richmond/Dowans ni mwaka wa tatu sasa inaisumbua nchi, hivi kweli is it a worthy issue ya ku-engage nchi nzima siku zote hizi, halafu je hatima yake ni nini? Any benefits kwa wananchi? Watapata maji zaidi? NO, shule bora? NO, i hope Rais anakaa na Bunge kulimaliza hilo suala ili yaongelewe mambo ya wananchi.
Leo lakini JK is on his own, a lonely man in the office, hii siyo nzuri kwa CCM na siyo nzuri kwa nchi, ni rahisi kusema aondoke 2010, lakini wote tunajua hiyo siyo realistic and the country is hurting. Ni viongozi wachache sana wanoamini kwenye agenda yake sasa hivi, kwasababu imesambaratishwa na maadui, all through out the country watu wanasubiri uchaguzi tu, hamna discussion ya maendeleo. I believe JK needs a re-launch ya administration, public opinion is bad as it is, lets not fool ourselves, just go for a do or die, for the country and the party. JK AKAE CHINI NA WAZEE NA WATAALAMU ANAOWAAMINI WAPANGE RE-LAUNCH, aende kwenye uchaguzi na agenda of the ‘new administration’ ambayo itakuwa tayari imejiestablish na imeleta a new wave of optimism kwa wananchi.
EL alikuwa anaamini 100% kwenye agenda ya JK, hamna mtu ataniambia zile ziara kule vijijini zilikuwa hazina maana, they were ENGAGING ziaras, zile enzi za wenyeji kusafisha barabara na kuchinja kuku tu kwaajili ya mgeni ziliisha. Vikao vyote vilikuwa intensive na maswali ya kutosha, back & forth, na ma-DC wanasema hata jamaa wakiondoka wasaidizi wanaendelea kufuatilia kwa karibu makubaliano yote. Hii ilikuwa inamfanya JK kuwa POWERFUL zaidi, kwasababu kama PM amepita ndiyo hivi, tutafanyeje mwenye nyumba mwenyewe akija?? It was working perfectly, hata posture ya JK in public was that of a ‘powerful president in deep thought’, sasa hivi its all gone. Either ni urafiki wanao au ushirikiano tu, sijui, lakini i believe Tanzania needed a bit more of the partnership btn JK & EL. All in all we wish them both the best of luck, lakini nchi inaumia sana.
 
ninanusa propaganda za Salva humu.
Kwa hivyo unahubiri kwamba dhambi ya Richmond ilikuwa ni bambikizo tu na kiinimacho? wizi mtupu.
Jamaa ameshindwa kucontrol adiministrative yake na sana sana he wearing a smile than being serious and firm on issues.
 
Back
Top Bottom