Kwanza ilikuwa ni Rais Bush na Michael Brown kule Lousianna wakati wa Katrina. Wakati kelele zinapigwa za kutaka kichwa cha Brown (mkuu wa FEMA) Bush alifunga safari kujionea na kwa jinsi anavyojua yeye alisimama mbele ya waandishi wa habari na kusema yale maneno ambayo yamebakia kama mwangwi "Brown you are doing a heck of a job".
Bush alisimama na mtu wake aliyemteua licha ya kelele..
Sasa wiki ile iliyopita hata leo hii kumekuwa na kelele za kutaka Waziri wa Fedha wa Marekani Bw. Geithner kujiuzulu. Mara tatu sasa Rais Obama amejitokeza pasipo woga kumtetea mteule wake na kusimama naye na kusema kama kuna mtu anataka wa kumlaumu basi wamlaumu yeye na kamwambia hata akileta barua ya kujizulu hatoikubali (basically asijisumbue).
Obama amesimama na mtu wake aliyemteua!
Ndiposa, nikabakia kujiuliza.. nini kilitokea Februari ile? Kwanini Kikwete hakusimama na mteule wake na kukubali kubeba lawama zote za Richmond yeye mwenyewe? Kwanini hakusimama na Karamagi, Chenge (ya Chenge labda haifai!) au Msabaha?
Je kila watu waliochini yake wakilaumiwa yeye atawatosa tu? NI lini atakubali kubeba lawama na kusema kuwa "mnilaumu mimi"? Je yawezekana tunu hiyo ya kukubali kubeba mzigo kama kiongozi Rais wetu hana na badala yake ni bora watu watoswe ilimradi yeye anaendelea kuonekana ni msafi? Je kuna siku atasimama kuwatetea watu aliowateua au atawaacha wamomonyoke na hivyo kuthibitisha ni jinsi gani asivyo mwangalifu katika uteuzi (maana anashindwa hata kuwatetea!)!
Ninaamini, hakuna wakati ambapo Kikwete alionesha udhaifu mkubwa kama kiongozi kama kushindwa kusimama na Waziri wake Mkuu au kupanga naye mkakati wa kujibu mashambulizi ya Bunge. Ndiyo maana ninaamini Lowassa hana sababu ya kumlaumu mtu mwingine yoyote (siyo Spika, CCM au Mwakyembe) kwa kujiuzulu kwake bali mtu mmoja tu ambaye alishindwa kuchukua msimamo mgumu!
Lakini labda alijua maji yamemwagika? Je kama JK angesimama na Lowassa na kukubali uchafu na lawama zote za Richmond (as a matter of fact nakumbuka mkutano wake na waandishi wa habari nadhani alistahili kuubeba mzigo huo!).
Kama mtu ukiteuliwa na Kikwete jua jambo moja.. you are on your own!!
Watanzania tunataka kiongozi anayehusika na lolote lile liwe baya au zuri ndani ya Serikali na vyombo vingine vya umma.
1. Obama hakumtetea Tom Daschle, wala Bill Richardson, lakini alimtetea Treasury secretary wake.
2. Bush hakumtetea Donald Rumsfield, lakini alimtetea Brown.
3. Rais Kikwete, hakumtetea Waziri Mkuu wake wa kwanza E. Lowassa, lakini Masha ni waziri mpaka leo.
Ahsante.
William.
Masha ni waziri mpaka leo lakini Sio kwa sababu ya kutetewa na Kikwete. Kama alifanya kimya kimya kimikakati kwenye vikao vya bia na totoz, hayo ni mengine. Tunachojua mpaka sasa ni kuwa ukiwa na issue yako utaibeba mwenyewe, dont count on the presidaa.
Kuhani;404790]Lead post ya mleta hoja ina falacy na matatizo lukuki. Imejengwa katika assumption, au niseme premise, kwamba ilikuwa sawa kwa George Bush na Barack Obama kusimama kidete na viongozi wao walipokuwa matatizoni.Kwanza, Bush alipata a vicious backlash kwa kusimama na Brown. Haikuwahi kukubalika hata kidogo.
Baraka Obama alishambuliwa vikali aliposimama kumtetea walioharibu. Mfano ulio wazi -ambao mleta hoja kauficha - ni Tom Daschle, ambae siku moja baada ya kutetewa na Rais mwenyewe akajitoa. Obama akaonekana kachemsha vibaya sana kutoona mabaya ya mteule mpaka mtu anajitoa mwenyewe?
Mleta hoja kaongelea mfano wa Geithner huku akijua fika kwamba kuna mfano wa mtu ambae aliharibu zaidi na uteuzi wake ulimomonyoka kama wa Lowassa, na Rais aka pay a heavy political price for it.
Halafu ni lini Lowassa alimlaumu Spika na, au, CCM kwa kuangushwa kwake? Tunajuaje hakumlaumu Kikwete?
Lead post imesheheni ma assumptions na ma premises yalo pinda pinda, na ma double talk
1.
- Mhhhhh! ni vyema kutoa boriti kwenye jicho lako kwanza.
Aahsante.
William.
Je Rais anatakiwa kumtetea mteule wake hata pale anapofanya makosa makubwa dhidi ya nchi kama ilivyothibitika kwa Lowassa?

huwezi kusema kuwa mtu ni mchafu hadi uwe na ushahidi! Hata kama ni mchafu kwa masuala mengine, hili lililomwondoa halikuwa na ushahidi. Mwakyembe alitaka kupitisha mambo yake mwenyewe. Ukiongeza na chuki za Sitta kuukosa uPM basi likazuliwa zengwe kuwa Lowassa ana nia ya kumwondoa JK 2010. Kikatafutwa kisingizio cha Richmond.
Je Rais anatakiwa kumtetea mteule wake hata pale anapofanya makosa makubwa dhidi ya nchi kama ilivyothibitika kwa Lowassa?
Kwanza ilikuwa ni Rais Bush na Michael Brown kule Lousianna wakati wa Katrina. Wakati kelele zinapigwa za kutaka kichwa cha Brown (mkuu wa FEMA) Bush alifunga safari kujionea na kwa jinsi anavyojua yeye alisimama mbele ya waandishi wa habari na kusema yale maneno ambayo yamebakia kama mwangwi "Brown you are doing a heck of a job".
Bush alisimama na mtu wake aliyemteua licha ya kelele..
Sasa wiki ile iliyopita hata leo hii kumekuwa na kelele za kutaka Waziri wa Fedha wa Marekani Bw. Geithner kujiuzulu. Mara tatu sasa Rais Obama amejitokeza pasipo woga kumtetea mteule wake na kusimama naye na kusema kama kuna mtu anataka wa kumlaumu basi wamlaumu yeye na kamwambia hata akileta barua ya kujizulu hatoikubali (basically asijisumbue).
Obama amesimama na mtu wake aliyemteua!
Ndiposa, nikabakia kujiuliza.. nini kilitokea Februari ile? Kwanini Kikwete hakusimama na mteule wake na kukubali kubeba lawama zote za Richmond yeye mwenyewe? Kwanini hakusimama na Karamagi, Chenge (ya Chenge labda haifai!) au Msabaha?
Je kila watu waliochini yake wakilaumiwa yeye atawatosa tu? NI lini atakubali kubeba lawama na kusema kuwa "mnilaumu mimi"? Je yawezekana tunu hiyo ya kukubali kubeba mzigo kama kiongozi Rais wetu hana na badala yake ni bora watu watoswe ilimradi yeye anaendelea kuonekana ni msafi? Je kuna siku atasimama kuwatetea watu aliowateua au atawaacha wamomonyoke na hivyo kuthibitisha ni jinsi gani asivyo mwangalifu katika uteuzi (maana anashindwa hata kuwatetea!)!
Ninaamini, hakuna wakati ambapo Kikwete alionesha udhaifu mkubwa kama kiongozi kama kushindwa kusimama na Waziri wake Mkuu au kupanga naye mkakati wa kujibu mashambulizi ya Bunge. Ndiyo maana ninaamini Lowassa hana sababu ya kumlaumu mtu mwingine yoyote (siyo Spika, CCM au Mwakyembe) kwa kujiuzulu kwake bali mtu mmoja tu ambaye alishindwa kuchukua msimamo mgumu!
Lakini labda alijua maji yamemwagika? Je kama JK angesimama na Lowassa na kukubali uchafu na lawama zote za Richmond (as a matter of fact nakumbuka mkutano wake na waandishi wa habari nadhani alistahili kuubeba mzigo huo!).
Kama mtu ukiteuliwa na Kikwete jua jambo moja.. you are on your own!!
Kwa wanaokumbuka Rais alikuwa mikoa ya Kusini na Makamu alikuwa sehemu nyinyine na wao kama Taifa zima walisikia kujiuzulu kwa Lowassa "radioni"