Kwanini Kawambwa asifanye hili...!?

Shomoro

Senior Member
Aug 22, 2010
111
26
Kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha kwa mwaka 2010 na mambo mengi yaliyosemwa na wadau wengi kuhusu kushuka kwa kiwango cha elimu Tanzania. Binafsi nitavutiwa na hoja hii;

*Kwa nini Tanzania kama nchi tusifikirie kufundisha watoto wetu kwa lugha moja ambayo tutaichagua na kuisimamia toka shule ya awali mpaka chuo kikuu!?

Ni dhahiri kuwa kwa sasa Kiswahili hakina mpinzani kama lugha inayozungumzwa na watanzania wengi sasa karibu asilimia 90 na zaidi.
Kiswahili pia kinatumika kama lugha ya kufundishia kwa shule zetu za msingi lakini lugha huja kubadiklika kuwa ya kiingereza mara mtoto anapofika sekondari.
Niliwahi kupata kuzungumza na mgeni mmoja aliyetaka kujua mfumo wa elimu ukoje nchini kwetu na alishangaa sana kusikia kuwa wanafunzi wanabadili lugha ya kujifunzia wakati wanakaribia utu uzima.
Jamani najua kuna siasa nyingi sana katika swala hili lakini ikumbukwe kwamba lugha fasaha watu hujifunza wangali watoto na huu uchanganyaji wa lugha sisemi kuwa ndio umekuwa chanzo pekee cha kurudisha nyuma maendeleo yetu ya elimu lakini kwa mtazamo wangu lugha imekuwa ni kikwazo kikubwa.
Kwa hilo basi natoa wito kwa Mheshiwa Waziri na wadau wote wanaotatizwa na hili kuwasilisha pendekezo la kuwa na lugha moja ya kufundishia. Mimi ningependa kuona kiswahili kinapewa nafasi kwa sababu hii lugha imekua kwa kiasi kikubwa na inatumiwa na wananchi wengi wa Afrika Mashariki na Kati.
Tukijiamini tutashinda.
 
Kwanza kawambwa ajiuzulu hafit wizara yeyote au kwa sababu ni mbunge wa jimbo la kwa mkwere?
 
Si tu ni mbunge wa Bagamoyo atokako mkwere bali ni nduguye ndio maana anambeba mpaka mbeleko inamchanikia!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom