Kwanini JK asiwe shupavu kama Rais Sata wa Zambia na kutoa maamuzi mazito kama haya ya Sata

Hivi masharti ya kuomba uraia wa Zambia yakoje ,nataka niukane U Tz bana maana mizaha imekuwa mingi hapa ni porojo tu mara nitaleta bajaj ambazo ni ambulance ,mara walioiba EPA tunawaomba warudishe ,mara wauza unga tunawajua tafadhali hiyo biashara waache ,haya ni masihara ngoja tuhamie kwa walio serious
 
Kuna kitu ambacho wana CCM hawataki kusikia kinasemwa na JK ame manage kuwakwepa nacho .JK uozo wote wa madini yeye ni mdau mkubwa sana .Kuna ushahidi mwingi kwamba Barrick walimpa JK pesa za kuingia madarakani na ndiyo maana hawezi kusema lolote .Si hao tu kuna IPTL na wengineo leo tunasikia suti za bure nk .Haya yote ukisha fanya huwezi kuwa na sauti hata mara moja .Alisha tuweka rehani .

Kwa kifupi Kikwete aliingia madarakani kifisadi kwa kutumia mabilioni ya pesa za mafisadi na yeye pia ni fisadi. Kama mtakumbuka alitoa kauli kwamba hamjui yule Al Adawi anayedaiwa kuwa ni mmiliki wa Dowans kitu ambacho si cha kweli. Miaka sita sasa madarakani ameshindwa kutimiza hata moja ya ahadi zake za kampeni za uchaguzi 2005. Mfano ni mikataba ya uchimbaji wa dhahabu. Miaka ya karibuni bei ya dhahabu katika soko la dunia imeongezeka sana na kusababisha makampuni ya kuchimba dhahabu nchini kuingia mapato ya $1.5 billioni kila mwaka huku nchi yetu ikiambulia $100 millioni tu na makampuni haya yote hayalipi kodi. Kwa maana nyingine kila mwaka wanaondoka na $1.4 billion ambazo zinawanufaisha shareholders wa makampuni hayo na managements zao ambazo wanaongezewa mishahara na marupurupu makubwa kwa "kazi nzuri" ya kuingiza makamounbi hayo faida kubwa sana.
 
Old JK na new JK hawa watu ambao wanatofauti kubwa sana. Kwani kilichompata gaddafi kwa kuweka maslahi binafsi kwani riz1 ni mtoto wake ambaye nae pia baba yake anamfupia macho mwanae kama vile alivyojimilikisha nchi ya libya kama yake na kuishi kwenye handaki na kufa kama *****. Sata bwana ni mfano wa kuigwa hana tofauti na late Mchonga meno, ukichemsha anakufukuza kazi na siyo wanachi wakuhukumu ni uzushi tu na unafiki lakini tangia lini urafiki unajenga bali huwa unabomoa.
 
Thatha ni mlopokagi.
Mi niko huku Zambia. Sata is a true patriot. anajua shida za watu wa Zambia and it hurts him. Juzi niece wake ambae alikuwa mbunge wa Matero kapelekwa police kuhojiwa sababa ya machine 2 zakusaga. Unadhan angekuwa ni ndugu ya JK angenusa hata hiyo police?
Amekata mawizara kutoka 23 hadi 19. angekuwa alafi kama JK angekimbilia kuongeza wizara.
Mishahara za wafanya kazi wa serikali, mashirika makubwa, migodo imepanda hado kima cha chini kimekuwa K2,000,000 (sawa na 600,000/-).
Mafuta yameshuka bei kwa 4.9%.
Sasa hivi umeme and kodi wanaangalia washushe kwa kiwango gani.
Naweza kukwambia vitu million ambavyo amefanya ndani ya mwezi mmoja maekuwa rais. Niambie JK kafanya nini baada yakukaa madarakani miaka 6?

asante.
 
Back
Top Bottom