Kwanini historia ya Zanzibar ya kweli haisomeshwi?

Masopakyindi,
Maalim wangu alonisomesha mbinu za mnakasha Sheikh Haruna
akiniasa kila siku akisema, ''Mohamed jihadhari na ghadhab,'' tena
akirudiarudia neno, ''ghadhab.''

''Ghadhab inaondoa umakini.''
Wapi nimetukuza utumwa?
Unafanya kosa kubwa sana.
You are misjudging kibri ya Watanzania katika kukumbuka mababu zao walivyofedheheshwa.
Na pengine hujajiridhisha kuwa ghadhabu iliyozimwa kwa miaka yaweza kuamshwa kirahisi sana kwa mada kama hizi.
 
teh teh teh,yaani historia ya ukweli ya zenji iandikwe na ibrahim noor sharrif??,sio ndio ndugu zao hao waliokuwa wanafanya biashara ya utumwa kipindi hicho,atakuwa fair kweli kwenye majarida yake?,mi naona hyo historia angalau ingekuwa ya ukweli kama ingeandikwa na mzawa halisi wa zenji asiye na mchanganyiko wowote ule na waarabu,tuletee chapisho la mzawa halisi asiye na mihemko ya udini tuone ukweli ulipo
 
Labda nikuulize.
Hao unaowasemea ni watu gani?

Kwani wako waliodhulumiwa leo si karne zilizopita na
hawajapigana.

Wamefedheheshwa mwisho wa kufedheheshwa na

Steveachi,
Unataka kumsoma mwandishi ambae hajachanganya damu.
Nimekuelewa.

Ni udhaifu huu unaoonyesha wewe ndiyo ulioiponza historia
ya TANU kuandikwa kwa kufutwa wazalendo wangine kwa
hofu kama hii unayoonyesha wewe.

Ikawa historia ya TANU inaanza na Nyerere 1954 ilhali historia
hiyo inatoka tokea miaka ya 1920.

Turudi kwenye mjadala.

Kuna kitabu cha Dr. Ali Sendaro lakini huwezi kumkubali pia
kwani yeye pia ana ''kasoro.''

Hata hivyo itakuongezea maarifa kumsoma Sendaro ''Utumwa na
Biashara ya Utumwa : Mtazamo wa Ukristo na Uislam,'' (2009).

Ikiwa humkubali Prof. Ibrahim Noor kwa kuwa kachanganya
damu ya Kiomani na Mwafrika basi nakuwekea rejea uitakayo
ya Mzungu - Sir John Gray, ''History of Zanzibar from the Middle
Ages to 1856,'' London : Oxford University Press 1962 uk. 255.

Gray kawataja na mataifa mengine yaliyoshiriki katika biashara ya
utumwa pamoja na Waarabu.

Steveachi,
Mwisho nakupa indhari.
Unapojadili ondoa hizo ''teh teh...'' ili tujadili kwa heshima na adabu.
 
mkuuu hujanielewa abadan,hata huyo sijui mzungu uliyemtaja hawezi kuleta historia sahihi ya zenji kwa kuwa lazima kuna vitu vibaya alivyovifanya hataweza kuvisema kwa sababu ya historia yake,ukweli uendelee kuwa ukweli milele,historia ya ukweli ya mwafrika itasimuliwa na kuandikwa kwa uzuri zaidi na mwafrika mwenyewe na sio mchanganya damu
 
Nadhani ni rahisi. Soma haya machapisho ya wazungu na wachanganya damu halafu kama hayakidhi, basi ingia kazini. Fanya research kisha tuletee tutasoma na tutaelimika zaidi. Kupinga kazi za wengine kwa hisia tu bila kuja na kazi nyingine inayopinga kazi za wengine haijengi sana.
 
mkuuu hujanielewa abadan,hata huyo sijui mzungu uliyemtaja hawezi kuleta historia sahihi ya zenji kwa kuwa lazima kuna vitu vibaya alivyovifanya hataweza kuvisema kwa sababu ya historia yake,ukweli uendelee kuwa ukweli milele,historia ya ukweli ya mwafrika itasimuliwa na kuandikwa kwa uzuri zaidi na mwafrika mwenyewe na sio mchanganya damu
Steveachi,
Hii ndiyo raha ya barza hii yetu.

Hakuna mwandishi anaeweza kuepuka yeye kutawaliwa na
''values.''

Hili ni somo linalojitegemea.

Ili wewe ujielewe kwa nini unafikiri hivyo itabidi usome lau
kidogo umuhimu wa ''values,'' katika kuandika na kuelewa
mambo.

Ukilifahamu somo hili utajua mengi na hutakuja tena na hoja
ya rangi ya mtu bali utasoma kile alichoandika na utakipima
kwa ukweli uujuao katika somo hilo.

Jussep kakufungulia mlango.
 
Steveachi,
Hii ndiyo raha ya barza hii yetu.

Hakuna mwandishi anaeweza kuepuka yeye kutawaliwa na
''values.''

Hili ni somo linalojitegemea.

Ili wewe ujielewe kwa nini unafikiri hivyo itabidi usome lau
kidogo umuhimu wa ''values,'' katika kuandika na kuelewa
mambo.

Ukilifahamu somo hili utajua mengi na hutakuja tena na hoja
ya rangi ya
mtu bali utasoma kile alichoandika na utakipima
kwa ukweli uujuao katika somo hilo.

Jussep kakufungulia mlango.

teh teh teh,values ndo zikutoe utu mkuu?
 
teh teh teh,values ndo zikutoe utu mkuu?
Steveachi,
Jitulize na unisome upya ili uelewe maudhui.

Hakuna lolote kuhusu utu katika niloandika.

Yawezekana hujui ninayosema hivyo shida
kwako kuelewa.

Nilichokuwa naeleza ni kuwa kuelewa au hata
mtu anapoanza utafiti kuna kinachomsukuma
kwa nini afanye utafiti huu na kwa nini usiwe
ule.

Hapo ndiyo inapingia, ''values.''
''Teh teh teh,'' zinakupunguzia umakini.

Achana na vitu hivyo na ikite akili yako katika
kusoma na kuandika kwa dhamira yake halisi.

Hii ndiyo tofauti ya wasomi ''teh teh teh'' na
wasomi makini.

Msomi ambae kila mtu anapoona jina lake basi
anajua hapo kuna cha kujifunza ndiye mwenye
tija.

Hawezi mtu kupoteza muda kusoma, ''teh, teh,
teh.''
 
Mzee muhamed watu wengi wa dunia ya leo hassa vijana hawahukumu kosa la mtu bali wanahukumu mtu kwa rangi yake dini yake na hata kabila lake.
Mtu anthubutu kukuambia maandiko ya prof nour ni maandiko ya kuegemea rangi yake na kabila lake mtu huyo utafanyaje mpaka aamini na akubali kama prof alifanya tafiti na kazi kubwa mpaka kufikia kutoa kitabu na kikasomwa dunia nzima.
Mm sioni akili za ziada utakazo tumia kumuelewesha mtu waina hiyo mtu mwenye mitazamo ya rangi ya mtu na kabila la mtu.
Mtu anafika kuandika chotara sio kwao znz mtu huyo hajui hata chanzo cha jina ASP hajui ASP ni african na shiraz hivi shirar ninani kama sio chotara.
Leo humtaki mtu ulieungana nae ukakombowa nchi utamtaka nani?
 
Sahimtz,
Hapa barzani kuna tatizo kubwa sana la watu kutojua.
 
Sio kutojua tu na hata kutaka kujua hawataki.
Laiti wangetaka kujua wange jiongeza kidogo hata kusoma vitabu tofauti au kukubali yale wanayo ambiwa na watu kama nyinyi.
Lakini leo mtu anawekewa pandiko lililoandikwa na mtu mwenye ilmu na heshima mbele za wasomi analikataa kwa hoja ya kikaburu kabisa eti muandishi ni muislam muwarabu.
Kwani waliambiwa usomi hautopatikana kwa muwarabu na muislam?
 
Masopakyindi,
Labda nikuulize.
Hao unaowasemea ni watu gani?

Kwani wako waliodhulumiwa leo si karne zilizopita na
hawajapigana.

Wamefedheheshwa mwisho wa kufedheheshwa na
hawajapigana.
Mkuu acha kuzunguka mbuyu katika kuwatetea waarabu waliokuwa wafadhili wa utumwa.
Wafadhili wa utumwa hawatarudi tena Zanzibar wala pande hizi za Afrika.
Kama mzee Mandela alivyosema alipotoka gerezani na kupata urais wa Afrika Kusini....

Mandela , May 10th 1994
"Never, never and never again shall it be that this beautiful land will again experience the oppression of one by another and suffer the indignity of being the skunk of the world."

Zanzibar baada ya 1964........Never, and never again will the arabs be left to return.
 
Mtu yeyote kabla hajasoma falsafa au msimamo au kazi ya mwandishi au mwana falsafa au mwanahistoria lazima ajue background ya huyo mtu. Alizaliwa wapi, alikulia wapi, alipatwa na matukio gani muhim, iman zipi zilimkuza.

Background ndo hushape kila kitu tunacho kisoma ni sawa tuu kwa mtu yeyote kuhusisha dini, rangi, makuzi na vitu vingine, na ni uchambuzi muhimu unatakiwa kifanyika ili kujua una tegemea kupata kitu gani toka kwa mtu huyo unaye soma kazi yake.

Na hiyo ndo njia ya kisasa kusoma kazi za watu wengine
 
upo sahihi sana mkuu,katika mukhtadha huo,historia nzuri haiwezi kamwe kuandikwa na anayetuhumiwa kufanya udhalimu ktk utawala wake,naamini itaandikwa vizuri zaidi na mhanga wa huo udhalimu kwani atasema kwa uwazi kila kibaya alichofanyiwa na kama kuna mazuri pia atayasema
 
ENOUGH..YATOSHA....MSHAPATA MLIYOPATA...KAMA MATESO MSHAWAPA..WAACHIENI MASHEKH WETU
MASH.jpg
 
Mkuu acha kuzunguka mbuyu katika kuwatetea waarabu waliokuwa wafadhili wa utumwa.
Wafadhili wa utumwa hawatarudi tena Zanzibar wala pande hizi za Afrika.
Kama mzee Mandela alivyosema alipotoka gerezani na kupata urais wa Afrika Kusini....

Mandela , May 10th 1994
"Never, never and never again shall it be that this beautiful land will again experience the oppression of one by another and suffer the indignity of being the skunk of the world."

Zanzibar baada ya 1964........Never, and never again will the arabs be left to return.
Masopyakyindi,
Hili la Waarabu kurudi Zanzibar kutawala wala si la kulisemea ukalitolea
na shingo kwani enzi ya mambo ya usultani yamepita.

Na hao Waarabu unaowazungumza hawapo Zanzibar sasa takriban karne
mbili.

Huwezi sasa kumuadhibu Mzanzibari wa leo kwa makosa ya mababu zake wa
karne ya 18.

Na kingine hiyo nukuu ya Mandela wala hapa si mahali pake kamwe na kama
unataka kuitumia falsafa ya Mandela kujipa nguvu nakushauri umsome katika
''Long Walk to Freedom,'' utaona hata aibu kwa kumleta hapa kutetea hoja hii
yako.

Mandela ameunganisha nchi yake na Makaburu wanamheshimu kwa hilo.
Sasa hebu rejea nyuma utazame hawa wanamapinduzi nini walifanya mara baada
ya kushika dola.

Waliweka jela za mateso za akina Mandera.
Hadi hapa hilo hapo juu linatosha kukufikirisha.
 
Mkuu kama humwelewi Mandela na "Never, never.. Never again..."
Pengine utaielewa "Mapinduzi Daima..."
 
Kitendo cha waarabu kuwachukua mababu zetu utumwani ni cha kishenzi tofauti na ustaarabu.
Kutetea hali hiyo napata shida kumwitaje mtu kama Mohamed Said.
Jisomee Zanj Slaves Rebellion ya mwaka 869 - 883 kwenye bara Arab, ina hiki unachojitahidi kuongea. Tumia internet.
 
Back
Top Bottom