Kwanini hawatajwi mpaka leo?

MmasaiHalisi

Senior Member
Jan 15, 2009
192
23
Vigogo dawa za kulevya watajwa
Written by Mwananchi
Monday, 18 September 2006
*Majina yao yapelekwa kwa Rais Kikwete
*Ni orodha ndefu ya majina ya watu 58
*Wamo wafanyabishara, wanasiasa, viongozi wa dini
*Mbinu wanazotumia nazo zaanikwa hadharani

WITO wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka wananchi wajitokeze kutaja majina ya wahalifu nchini, umepata mwitikio mpya, safari hii watu kadhaa wakijitokeza
kutaja majina ya vigogo wanaoongoza kwa biashara ya dawa za kulevya nchini.

Majina hayo yako katika barua iliyoandikwa na wananchi 15 kwenda kwa Rais Kikwete, ambamo wanadai kwamba walikuwa wakitumiwa na vigogo hao kufanya biashara
hiyo, lakini sasa wameamua kuachana nayo. Barua hiyo iliandikwa Septemba 8, mwaka huu na wahusika wanadai wamekwisha kuiwasilisha Ikulu.

Kwa mujibu wa barua hiyo, majina 58 yameorodheshwa yakiwa katika makundi matatu makubwa, la kwanza likiwa ni waagizaji wakubwa wa dawa hizo; la pili ni
wafadhili ambao majina yao hutumika kusafirisha dawa hizo; na la tatu ni wauzaji walioko Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.

Katika orodha ya waandishi wa barua hiyo wanaodai kusukumwa na uzalendo na uchungu kwa nchi yao, yamo majina ya wafanyabiashara maarufu nchini na wanasiasa,
wakuu wa taasisi nyeti, baadhi ya viongozi wa dini na maafisa wa juu serikalini.

Kundi la kwanza lina majina 12, miongoni mwao ni wafanyabiashara maarufu katika miji ya Dar es Salaam, Morogoro, Zanzibar, Arusha na Bagamoyo na baadhi ya
viongozi wa dini wa madhehebu fulani.

Kundi hili linadaiwa kuwa linaingiza dawa za kulevya kwa njia mbalimbali zikiwamo, kutumia mipira ya kondomu, majokofu, vifaa vya hospitali, meli na
marobota ya mitumba.

Katika kundi la pili kuna watu 19, miongoni mwao wamo wanasiasa wakubwa nchini wakiongoza kundi hili, kutoka taasisi ya fedha nchini na wafanyabiashara maarufu wa
Dar es Salaam na Zanzibar.

Kundi la tatu lina majina 27, ambao si ya watu wenye majina makubwa, lakini ndio wanaotumika kusambaza mitaani kwa watumiaji wa dawa za kulevya.

Mbali ya kushiriki katika kusambaza dawa za kulevya, kundi hili pia lina baadhi ya majina ya watu waliotajwa kushiriki katika kuingiza silaha nzito
zinazotumika kwa ajili ya ujambazi kutoka nchi jirani.

Ufukwe wa Pwani ya Bahari ya Hindi eneo la Muhoro wilayani Rufiji inaelezwa kuwa linatumika kuingizia silaha hizo kutoka nchi jirani pamoja na dawa za
kulevya chini ya ufadhili wa mmoja wa wanasiasa nchini.

Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere unatajwa kuwa unatumiwa na watu hawa kuingiza dawa hizo nchini kutokea nchi za nje, huku baadhi ya maafisa wa polisi
watatu wakitajwa kuwa ndio wanaotoa ulinzi kwa watu wanaopitisha dawa hizo.

Nyumba ya afisa wa juu mstaafu katika idara nyeti iliyopo jijini Dar es Salaam inatajwa kuwa inatumika katika kuhifadhi vijana wanaoingiza dawa za kulevya
nchini, huku nyumba ya mfanyabiashara mmoja iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ikitajwa kuwa ndiyo inayotumika kama kituo cha kutolea pipi tumboni kwa
vijana wanaotumika kuingiza dawa hizo kutoka nje ya nchi.

Vile vile, katika kundi hili mwanamke mmoja anayefanya kazi katika taasisi moja ya fedha anatajwa kuwa anashiriki katika kuhujumu uchumi wa nchi kwa
kusafirisha kwenda nje fedha nyingi za kigeni akitumiwa na mfanyabiashara mmoja maarufu wa dawa za kulevya nchini.

Mipaka ya Tunduma mkoani Mbeya, Horohoro mkoani Kilimanjaro na Namanga mkoani Arusha, nayo imetajwa kuwa inatumika kupitisha dawa za kulevya kwa kutumia
mabasi na magari mengine. Kuna kampuni mbili za mabasi nchini zinazotajwa kuongoza kutumika katika usafirishaji.

Barua hiyo ya kurasa 10, pia inamtaja mwanamke mmoja ambaye anatumika kupitisha dawa za kulevya uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kuwa ni sugu; aliwahi
kuhukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya, lakini hivi sasa yupo mitaani kifungo chake akitumikia mtu mwingine.

Alipoulizwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philip Marmo, alisema hajapata barua hiyo na kwamba atalizungumzia
baada ya kuipata.

Naye Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, alisema hana taarifa za kuwako kwa barua hiyo. Hata hivyo, alisema kuna tume ya dawa za kulevya iliyopo
chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo inayoshughulikia zaidi suala hilo.

Alisema Jeshi la Polisi linafanya kazi za kukamata watu wanaojihusisha na dawa hizo na kwamba mikakati mingine ya kupambana na watumiaji inafanywa na tume
hiyo.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Polisi liongezewe uwezo wa kupambana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha vituo vya kazi askari
waliokaa kituo kimoja kwa muda mrefu.

Pia alilitaka Jeshi hilo lijisafishwe lenyewe kutokana na madai kwamba polisi wanahusika na baadhi ya matukio ya uhalifu nchini.

Rais alitoa wito kwa wananchi wenye taarifa zozote za uhalifu, na wanaojua waliko majambazi wazipeleke taarifa hizo kwake kama wanaogopa kuzipeleka polisi.
Katika kuitikia wito huo, wananchi kadhaa waliandika barua iliyooroshesha majina ya polisi 20, wakiwamo baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa na kuikabidhi
kwa Waziri wa Usalama wa Rais, Bakari Mwapachu.

Tangu wakati huo, mabadiliko makubwa yameshuhudiwa yakifanywa kwenye jeshi hilo, hata hivyo hii ni mara ya kwanza kwa watu kujitolea kuandika barua yenye
majina na maelezo ya kina kama hii kuhusu biashara ya kulevya na kuipeleka kwa Rais.
 
nina uhakika unajua ni kwanini.Ila tu haiingii akilini kuwa hata na wewe pia unadanganywa na unakubali, na huna cha kufanya!Habari ndio hiyo!!Sana sana kelele zikizidi, atatolewa mmoja kafara, kwa muda kiasi, halafu kesi itaisha basi, tutaendelea mbele na kudanganyika kwetu mimi na wewe.Ole wao kizazi cha watoto wasiosomeshwa, au wasiokuwa na nguvu na ujasiri, nawaonea huruma mama zao kilio kikavyokua, huo umasikini na ujinga utakao kiwapo!!!hayo magonjwa!! jamani watanzania tunaambizana tuamke, sasa tukishaamka tunafanya nini? au nitajuaje kama nimelala au nimamka?? Nataka kufanya kitu!!
 
hao wauza hayo madawa mbona wanajulikana nasikia mmoja wa mameya wa manispaa mojawapo hapa jijini dar ni kinara wa kuuza hayo madawa akishirikiana na madiwani kadhaa
 
hahaha by then tulikuwa hatujajua kuwa JK ameingia kwenye number of episodes za usanii tulidhani ni kweli mtendaji kumbe kama Queen of GB.Pres ni RA ndio ana take action
 
Mshawahi kusoma kijitabu cha HEKAYA ZA ABUNUWASI????

karibu tukate ishu
 
hahaha by then tulikuwa hatujajua kuwa JK ameingia kwenye number of episodes za usanii tulidhani ni kweli mtendaji kumbe kama Queen of GB.Pres ni RA ndio ana take action

Naah,

wengine tulimjua tangu kabla ya 95!
 
Hiyo idea ya kuorodhesha majina ilikuwa mbovu tangu mwanzo, tatizo ni ushahidi sio kuwajua tu.
Sana sana serikali itajikuta inawalipa fidia ikiwataja kuwa wanauza unga wakati hawana ushahidi wowote.
 
si watajwe kwani nani asiyewajua hao wauza unga

Mau, bahati mbaya mimi simjui hata mmoja. Kwa wana JF wanaowajua wauza unga, jamani la mgambo limelia tuwataje basi hapa JF forum hadharani kama tunavyowataja mafisadi. Kwa nini imeendelea kuwa siri mpaka leo wakati watoto wetu wanaendelea kuteketea. Naambiwa magorofa mengi yanayojengwa Dar ni matokeo ya biashara hii haramu ya madawa ya kulevya. Hebu tuwataje basi!!!!! Tusiishie kusema diwani fulani au meya fulani, weka wazi hapa!!!!

1.
2.
3.

Tiba
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom