Kwanini habari za chama cha wananchi CUF haziandikwi wala kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari?

Mtoa hoja acha uzush,ujio wa Lipumba nimeu0nea on star tv,then few days later akaongea na waandish juu ya CUF
 
Ukitaka habari za CUF muulize Nape ,ukitaka za CCM muulize Mtatiro, hao wana majibu yooote ya maswali yako bila majashooo!
 
Hi ni kwani nini siku hizi vyombo vingi vya habari hapa nchini vimekuwa havitoi habari kuhusiana na chama cha wananchi (cuf) nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu sasa cuf wamekuwa wakifanya mikutano mikubwa ya hadhara lakini kesho yake hakuna hata chombo kimoja cha habari kitakacho kuwa kimetoa habari ya jumapili tarehe 11/03/2012 walifanya mapokezi makubwa sana ya kiongozi wao kwa takwimu za haraka hakuna mapokezi makubwa kama yale kutokea tanzania ukiondoa msiba wa baba wa taifa labda ndio yanaweza fanana kwani yaliyazidi mapokezi ya papa mwaka 1990 na mandela pia alipotembelea tanzania lakini chakushangaza jumatatu yake hakuna hata sehemu yalipotangazwa mbaya zaidi nilikuwa naangalia taarifa ya habari waandishi wa itv walisema wameshindwa pata habari zaidi kutokana na kutishiwa kupingwa na mashabiki wa cuf japo jambo hili si kweli kwani toka kampeni za uhaguzi mwaka 2010 itv imekuwa haitohi kabisa habari za cuf labda tbc ndio imekuwa ikionyesha habari za cuf japo kwa udogo

sasa huwa najiuliza chanzo ni nini? Mpaka tumekuwa tunalazimishwa kusikilizishwa sera za kukopi za vyama viwili tu. Au wahariri nao siku hizi wamekuwa kama madj hawatohi habari mpaka kitu kidogo kwanza

maana kama wanachama cuf bado wako wengi na mapokezi yalidhililisha hilo hata slaa alijionea umati ulivyo jaa irport tarehee 11/3 2012 kweli bongo hakuna wasomi wenye kujijua watu wote wamekuwa watumwa wa wana siasa
kwa sababu kutoandika habari za vikao au mikutano ya vyama vingine ni kutunyima haki yetu wananchi kuchagua chama chenye sera nzuri.

Shakeel,

..hata kwenye mtandao wa wa-Zanzibar[haswa CUF],Mzalendo.net, sikuona habari za Prof.Lipumba kurejea nchini.

..mimi nadhani kwasababu CUF wamewa-ignore wa-Tanganyika kwa muda mrefu, wa-Tanganyika nao wameamua kuwapotezea.
 
"Waandishi wa Habari wa Tanzania ni Makanjanja"-BENJAMIN W. MKAPA, lakin tuwatendee Haki kama kauli mbiu ya Chama chako ya "haki sawa kwa wote",Habari ya mapokezi ya Prof Lipumba yaliripotiwa ipasavyo na karibia na vyombo vyote vya habari lakini pia mchezo wa Siasa ni mchezo wa mbinu cha kufanya mkikutana sio mnajadili kuvunja muungano na kufukuzana,kweye na "mengineo" kwenye agenda ya vikao vyenu mjadili kwa kina sababu na suluhu ya kutopewa nafasi na vyombo vya habari!!!!
 
Wewe jamaa kumbe mnafiki kiasi hiki! Kila siku unapika kelele humu JF za udini kumbe huna lolote, mdini mkubwa wewe tena mnafiki, kwa hiyo CDM yenu ni kwa ajili ya Wakirstu nyie ndiyo mnaemualibia Dk Slaa, kwa style hii CDM hawawezi kuchukuwa nchi kwa kutegemea wakiristu peke yao.
Hahaha.....watu mnachekesha sana, kuna mtu kamtukana Slaa kwa sababu ya udini hujakemea, mwehu mwingine katukana wahariri wa vyombo vya habari kiudini udini, hujakemea. Huyu nae katumia haki yake ya kikatiba kueleza anachokiona kinafaa umekuja juu! Kwani nani asiyejua kuwa KAFU ni chama cha MISIKITINI? Ukweli hata kama ni mchungu upokee tu mkuu
 
Majority ya wahariri wa vyombo vya habari Tanzania ni Wakorintho! Na wakoritho wana chama chao cha siasa, Corithians Democratic Movement (CDM). Usitegemee waandike habari yeyote inayo-promote CUF! Ikiwa ni negative news utashangaa wanavyoipa kipau mbele! Refer ile saga ya HR na ' Kifo Cha CUF'!
Tungekuwa tumesha anzisha TV yetu ile tuliyochangishana mamilioni uwanja wa taifa Chama chetu cha KAFU kingepata kavereji pana sana
 
Habari za CUF huandikwa pindi likitokea lenye mwelekeo hasi kwa chama, lakini lenye mwelekeo chanya haliandikwi na wala halitangazwi abadan.

Sasa mbona waislam wako very updated na habari za za KAFU? Wanazipata wapi hizo habari?
 
Hawa ndio wapinzani wa Tanzania, wanajigawa wenyewe CUF waislam Chadema Wakiristo CCM walivyokuwa mafia wamewagawa na wao wamekubuli kugawika.
 
tuongee ukweli, CUF is no longer. wengi wemechangia kishabiki, lakini ukweli CUF hakina mvuto tena. hata ukiangalia takwimu za kura za urais, simekuwa zikishuka mwaka hadi mwaka. sasa nani aandike habari zake? za nini? na ili iweje? kilichoimaliza CUF ni ndoa yake na magamba. magamba yemifunika kabisa CUF. baada ya Maalim Self kupata kula, nae ametulia bora hata maji ya mtungini, maana yakiguswa yanatikisika. badala ya kukifufua chama, yeye amekaa ofisini na kuendelea kula bata. unategemea nini? yaani asimame na kuipinga serikali anayoiongoza? AIBU, hakuna chama kinaitwa CUF tz, labda hadi uchaguzi wa 2015.
 
[h=1]Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba Awashukuru Wananchi na Kuwataka Kujipanga Vyema Kutoa Maoni Katiba Mpya[/h]


DSC_0786.JPG

Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba akiwahutubia maelefu ya wanachama na wapenzi wa Chama hicho katika viwanja vya Muembe Yanga Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambako kulifanyika mkutano wa hadhara.
DSC_0648.JPG

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akimkaribisha Mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba katika viwanja vya Muembe Yanga Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambako kulifanyika mkutano wa hadhara wa Chama hicho. Katikati ni Makamu Mwenyekiti Mhe. Machano Khamis Ali.
DSC_0625.JPG

Wafuasi wa CUF waliopata ajali siku ya mapokezi ya Prof. Lipumba tarehe 11/03/2012, wakiwasili katika viwanja vya Muembe Yanga Temeke Dar es Salaam kwa ajili ya kumuona na kumsikiliza Mwenyekiti huyo wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.Picha na Salmin Said-Ofisi Ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar
---

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amewataka watanzania kusimama imara na kujipanga katika kutoa maoni ya katiba mpya, ili kuhakikisha kuwa katiba inaweka wazi suala la maliasili kuwa rasilimali za Watanzania.

Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na maliasili nyingi zikiwemo dhahabu, almasi, Tanzanite, copper na madini mengine kadhaa, lakini bado rasilimali hizo hazijawanufaisha wananchi kutokana na kutokuwepo utaratibu unaoeleweka juu ya mgawano wa rasilimali hizo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho wenye lengo la kuwashukuru wananchama na wakaazi wa Dar es Salaam pamoja na Mikoa jirani kutokana na kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi yake tarehe 11/03/2012 Prof. Lipumba amesema iwapo kutawekwa utaratibu maalum kikatiba, maliasili hizo zinaweza kuwanufaisha Watanzania wote.
Katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Muembe Yanga Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Prof. Lipumba amewapongeza wanachama na wananchi waliojitokeza kwenye mapokezi hayo, na kutaka moyo waliounyesha kwake siku hiyo uendelezwe katika kukijenga chama hicho na kuwa dira ya uchaguzi mkuu ujao.

Prof. Lipumba amefahamisha kuwa kutokana na kutokuwepo kwa mipango imara ya kiuchumi nchini, kumepelekea kuwepo kwa mfumko mkubwa wa bei kwa zaidia ya asilimia 50, jambo ambalo linadumaza maendeleo ya Watanzania waliopata uhuru miaka 50 iliyopita.
Amesema kipindi cha miaka 50 ni kikubwa kuweza kuleta mapinduzi ya kweli yw kiuchumi na maendeleo endelevu, na kwamba nchi nyingi tayari zimefanikiwa zikiwemo Singapore, Malaysia na Korea ya Kusini.


“Tunahitaji uongozi wenye dira ya kuikomboa Tanzania kiuchumi, nchi yetu ina utajiri mkubwa lakini hakuna mipango imara kutokana na ombwe ya uongozi uliopo”, alisema Prof. Lipumba ambaye alirejea nchini mapema mwezi huu kutoka Marekani alikokuwa alifanya utafiti kuhusu mambo ya demokrasia na maendeleo ya kiuchumi.


Amewaeleza maelfu ya wanachama na wapenzi wa Chama hicho kuwa tayari amepata mwaliko mwengine wa kwenda nchini Barcelona mwishoni mwa mwezi huu, ambako atakutana na wataalamu wawili wa kuchumi kutoa nchi za Urusi na Ubelgiji kwa lengo la kujadili matatizo ya kisiasa ya nchi za kiarabu na athari za kiuchumi na kisiasa zinazoweza kujitokeza kwa nchi nyengine.


Mapema Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad amepongeza mapokezi makubwa aliyopewa Prof. Lipumba ambayo amesema yanathibitisha kuwa CUF kweli ni Chama Cha Wananchi, sambamba na wanachama kuwa na uchungu na Chama chao.
Maalim Seif amekebehi kwa wale wanaodai kuwa CUF ni CCM ‘B’ kwamba wana wivu wa kisiasa, na kutoa wito kwa wanachama kutokubali kuyumbishwa katika kukiendeleza chama hicho.


Katika hatua nyengine mjumbe wa baraza kuu la uongozi la Chama hicho aliyepewa onyo kali wakati Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Mhe. Hamad Rashid Mohd pamoja na wenzake walipofukuzwa uanachama Bw. Yassir Mrotwa, ameibuka na kuomba radhi kutokana kukifikisha Chama hicho mahakamani.


Amesema atafuatilia mwenendo wa kesi hiyo ili kufuta saini yake isitumike kwenye mwendelezo wa kesi hiyo.


Wakati huo aliyekuwa naibu mkurugenzi wa uchaguzi wa CUF taifa Bw. Khamis Katuga ambaye alikihama chama hicho na kuhamia CCM, amerejea tena CUF ambapo amerejesha kadi ya CCM na kukabidhiwa kadi ya CUF.


Ametahadharisha kuwa tatizo kubwa linalorejesha nyuma maendeleo ya chama hicho ni kutokanyika kwa vikao katika ngazi ngazi mbali mbali, huku akieleza sababu zilizomrejesha tena CUF kuwa ni uimara na sera zinazotekelezeka za chama hicho, huku akifunga maelezo yake kwa usemi “asiyejua kufa achungulie kaburi”.

Na
Hassan Hamad
Ofisi Ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar
 
Hi ni kwani nini siku hizi vyombo vingi vya habari hapa nchini vimekuwa havitoi habari kuhusiana na chama cha wananchi (cuf) nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu sasa cuf wamekuwa wakifanya mikutano mikubwa ya hadhara lakini kesho yake hakuna hata chombo kimoja cha habari kitakacho kuwa kimetoa habari ya jumapili tarehe 11/03/2012 walifanya mapokezi makubwa sana ya kiongozi wao kwa takwimu za haraka hakuna mapokezi makubwa kama yale kutokea tanzania ukiondoa msiba wa baba wa taifa labda ndio yanaweza fanana kwani yaliyazidi mapokezi ya papa mwaka 1990 na mandela pia alipotembelea tanzania lakini chakushangaza jumatatu yake hakuna hata sehemu yalipotangazwa mbaya zaidi nilikuwa naangalia taarifa ya habari waandishi wa itv walisema wameshindwa pata habari zaidi kutokana na kutishiwa kupingwa na mashabiki wa cuf japo jambo hili si kweli kwani toka kampeni za uhaguzi mwaka 2010 itv imekuwa haitohi kabisa habari za cuf labda tbc ndio imekuwa ikionyesha habari za cuf japo kwa udogo

sasa huwa najiuliza chanzo ni nini? Mpaka tumekuwa tunalazimishwa kusikilizishwa sera za kukopi za vyama viwili tu. Au wahariri nao siku hizi wamekuwa kama madj hawatohi habari mpaka kitu kidogo kwanza

maana kama wanachama cuf bado wako wengi na mapokezi yalidhililisha hilo hata slaa alijionea umati ulivyo jaa irport tarehee 11/3 2012 kweli bongo hakuna wasomi wenye kujijua watu wote wamekuwa watumwa wa wana siasa
kwa sababu kutoandika habari za vikao au mikutano ya vyama vingine ni kutunyima haki yetu wananchi kuchagua chama chenye sera nzuri.
Kwenye familia za kiafrika anayesikika ni baba sasa CUF si wameolewa na CCM ndio maana anayesikika baada ta ndoa ni mume wake CUF ambaye ni CCM,ndio raha ya ndoa hata jina la asili linapotea,CUF sasa kwishney ni historia
 
Back
Top Bottom