Mimi bado nashangazwa na sababu hasa ya kwanini Gharama za Internet za Tanzania ziko juu sana ukilinganisha na Kenya. Cable ambayo tunatumia ni hiyohiyo Kenya inatumia, wote tumepakana na bahari. Sasa ni sababu gani ya kufanya ghrarama hasa za Internet ziwe juu hivyo. Wafanyabiashara wanaotumia Internet wanasema ndiyo gharama kubwa kuliko hata kodi ya office. Kuna manufaa mengi sana ya kuwa na Internet ya bei ya chini kama Kenya kwani pamoja na biashara inasaidia sana kwenye elimu. Kuna biashara tunashidwa kuja kufanya Tanzania kwasababu gharara na speed ya internet ziko juu sana. Badala ya kwenye kufungua kampuni nyumbani tusaidie inatulazimu tuwape kazi za Internet India!!. Tanzania inabidi tubadilike maana matatizo mengi ni ya kujitakia ndugu zangu.