Kwanini Edward Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania 2015

Lowassa kipenzi cha watanzania hata msemeje tunampenda tu huo ufisadi mbona toka 2008 mpaka Leo mmeshindwa kumshtaki?
 
Vijana wa El wanapaswa waelewe kuwa mazingira ya kujiuzulu Mzee Mwinyi ni tofauti na mazingira ya kujiuzulu Lowassa.Lowassa alijiuzulu kwa tuhuma ya wizi uliogharimu taifa na kuharibu uchumi wa nchi.Richmond ni kichefuchefu hadi leo kwa mwananchi wa Tanzania.Gharama za umeme kupanda ni chimbuko la uwepo wa Richmond.

Kamati teule ilitoa ripoti yenye ushahidi,ikapendekeza ajipime.Akasema kaonewa,Lucas Selelii akasimama na kumwomba Lowassa ale kiapo cha kuwajibika kisiasa kama itagundulika hajaonewa na wao wanakula kiapo cha kuwajibika kisiasa ikiwa itagundulika wamemwonea Lowassa ila Lowassa hakula kiapo hicho kwahiyo hapa anatupa uhakika kuwa Richmond ni misumari ya moto aliyoibeba na itamchoma 2015.Mzee Mwinyi hakujiuzulu kwa wizi bali uzembe wa surbodinates wake.Na kama Lowassa anajifananisha na Mwinyi katika kujiuzulu je anatuaminisha Msabaha na Karamagi ni wakosaji?Na kama ni wakosaji kwanini yupo nao kwenye timu yake ya kampeni?Bado kwenye Richmond hana usafi wa kujisafishia.

Niwaase vijana wa El wajifunze kufanya analysis za kisiasa kwa manufaa ya El.El hata kama anasema anawazidi uwezo Pinda na Sumaye bado anajidanganya.Iko hivi,kumfananisha Pinda na El ni dhambi kubwa kwasababu Pinda ana uzoefu na utumishi wa ikulu tangu 1974.Amehudumu kama Katibu wa rais kwa awamu zote nne za serikali zote Tanzania.Anakijua chama kabla ya Lowassa kuingizwa katika siasa na Jk,Jaka Mwambi na Ditopile.Lowassa hakijui chama kulinganisha na Pinda.Kwahiyo kiuzoefu ndani ya chama na serikali Pinda ni bora kuliko Lowassa.

Lowassa hana pumzi ya kisiasa kumzidi Sumaye.Sumaye ana wasifu wa kuhudumu miaka 10 kama Pm wa Tanzania bila kuchafuka na hata alipochafuliwa mahakama ilimsafisha na fidia aliyopewa alisaidia mfuko wa vyombo vya habari nchini kwahiyo hata New Habari Cooperation ilifaidika na msaada huo.Kete ya uadilifu ndio bao pekee Sumaye analomzidi nalo Lowassa.

Ni ukweli El yupo nje ya serikali kwa karibu ya miaka 10.Hii ni sababu tosha ya kumwengua 2015 kwasababu hatujaona kazi yake wizara yoyote kwakuwa ameshapewa fursa ya Upm akaondoka kwa aibu.Na historia yake mbaya akiwa waziri wa ardhi na waziri wa sera,uratibu na bunge chini ya Pm Malecela kwenye tenda ya ununuzi wa magari ya serikali(mashangingi)ni sababu tosha ya kuionesha dunia kuwa El ni mzigo kwa chama na serikali.Ushahidi usio na mashaka ni kwamba hata jimboni Monduli hali sio nzuri,ufisadi katika halmashauri na ardhi ni pigo tosha kwake.

Mjibu hoja wa El anasaidia kumsafishia njia rafiki yetu BM ya kuelekea ikulu 2015 katika suala la List of shame.List of shame inamtaja El haimgusi BM.Aliyesema List of shame ni asilimia 90 ya wanamtandao wa Jk 2005 anamweka kando BM kwasababu hata kama ni kweli wanamtandao wenzake wanahusishwa ila yeye haonekani mahali.Eti El hawezi kushughulikiwa na wachafu wenzake,huu ni upuuzi kabisa.

Lowassa kugombea Nec wilayani ni ishara ya uoga kwasababu kundi la kifo ndio kundi pekee ambalo linapigiwa kura na wajumbe wote wa Ccm.Wilayani unapigiwa kura na watu wa eneo lako tu unalotoka.Waliopigiwa kura kundi la kifo ni washindi hadi Zanzibar kwasababu Zanzibar nao waliwapigia kura.Kuwa rais lazima ukubalike na Zanzibar maana huwezi kuwa rais wa Monduli,Monduli sio nchi.

Lowassa anaumwa huo ndio ukweli.Ugonjwa wake unaongezeka kila siku.Vijana wake hawana lugha ya kutueleza tukaelewa.Sio wa kupewa nchi.Wametoa mfano wa Michael Sata wa Zambia mimi naona ni mfano dhaifu kuwahi kutokea katika siasa za Tanzania.Mfano unaomfaa Lowassa ni wa Levy Mwanawasa au Omar Odimba Bongo.Hatutaki gharama za uchaguzi mdogo au matibabu kila siku ulaya na India kuelemea walipa kodi wa Tanzania.
Vijana wa ulipo tupo ujumbe huu unawahusu
 
Haya tumekusikia lakini team Lowassa tunaanda speech ya kuwashukuru watanzania kwa kutuunga na mkono na imani wanayoonyesha kwa rais wetu mtarajiwa.2015 safari ya matumaini inaebdelea....
Naona umeendelea nae hadi CDM
 
Mgombea yoyote wa uraisi wa ccm atabakia na historia tu kwamba aligombea uraisi na kubaki mwenyekiti wa ccm. TANZANIA HATUHITAJI NA HATUTAKI NA HATUMCHAGUI RAISI YOYOTE KUTOKA CCM HATA AWE NANI. Jifurahisheni tu kwamba huyu fisadi kidogo, huyu wizi wake haujulikani, huyu ana fweza nyingi n.k. Hatutaki.

TUNACHAGUA RAISI KKUTOKA UKAWA BILA KUJALI NI NANI KWA AJILI YA MFUMO!. UKAWA NI MFUMO SAHIHI UTAKAOTOA MAJIBU YA MATATIZO NA MWELEKEO SAHIHI NA HALISI WA TAIFA LETU.

HAKUNA RAISI ANATOKA CCM, HATA KAMA WANGESIMAMISHA MALAIKA, MAADAM ANATOKA CCM, HATUTAKI!. CCM NI WAHUNI TU!.

MUNGU NA WAUNGWANA UKAWA,
SHETANI NA WAHUNI CCM.
Dekio
 
Nimeamini elimu kweli mali.Hasa unapoutumia weledi wako ipasavyo. Ndivyo ilivyo kwa mmoja wa wagombea watarajiwa wa Urais kupitia CCM,Edward N. Lowassa. Lowassa ni msomi wa shahada mbili.Ya kwanza ni ya Sanaa za Maonesho na Maigizo (Fine and Perfoming Arts) na ya pili ni Shahada ihusuyo Maendeleo ya Jamii (Development Studies). Shahada yake ya kwanza ndiyo hasa anayoitumia vyema

Yeye pamoja na wapambe wake wanamchora Lowassa kama mtu mwenye nguvu kubwa ndani ya CCM na asiyeepukika na asiyeweza kukatwa jina na CCM. Eti, Lowassa ni mwenye idadi kubwa ya wajumbe wa NEC na hata Kamati Kuu watakaompitisha kugombea Urais kupitia CCM kirahisi. Huku ni kujidanganya.

Lowassa ni mwanachama wa kawaida sana wa CCM. Hana upekee wowote kiuanachama na kisiasa ndani ya CCM. Anasaidiwa tu na weledi wake wa sanaa. Hana nguvu zinazochorwa na wapambe wake ambao wanasimamiwa kisanii na kiumahiri na yeye mwenyewe. CCM haina mkubwa wala mdogo. Haina maarufu wala asiye maarufu. CCM yetu inaongozwa na Katiba na Kanuni za chama.

Mchakato ukianza, maneno yangu haya yatajidhihiri.Kuwa Lowassa ni mwanachama wa kawaida chamani.Uteuzi utafanywa kwa ustadi na mahitaji ya Taifa. Hakuna maarufu kuliko chama. Yeyote anaweza kukatwa na kusitoee chochote. CCM ni taasisi kubwa na komavu.

Sifa mzichuje. Shahada ya Sanaa inafanya kazi yake!


Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Wasalaam wana Jamvi


Wananchi wanaanza kufumbua macho baada ya kauli za waasisi kama Mwl jk Nyerere alipomkemea Lowassa kuwa hafai kuwa Rais kwa hoja kubwa kuwa mali alizonazo,zinawalakini.


Watanzania wanapima muda wa utumishi wake tangu aingie madarakani mwaka 1990 akimshinda mpinzani wake kwa rushwa ya ng'ombe wanane waliochinjwa wakati wa kampeni zake.

Unaweza kujiuliza sana,kwa nini Lowassa anautaka urais kwa udi na uvumba hadi anaamua kuvunja sefu ili kuhakikisha anashinda?, kwa nini anafanya sherehe na kuwakaribisha viongozi wa ccm ambao kila wakiondoka Monduli mifuko yao huwa imevimba?,hebu tuangalie nafasi zake mbili za utumishi.

WAZIRI WA MAJI

Itakumbukwa kuwa mwaka 1984, chini ya utawala wa Mwl Nyerere nchi hii ilikuwa imesambazwa mabomba ya maji na visima vingi bora vya HESAWA.Inakumbukwa kuwa watanzania maji haya yalikuwa yanawekwa dawa ili kuua vijidudu.

Ni wakati huo,ugonjwa hatari wa kipindupindu,homa ya matumbo ulidhibitiwa.Ni wakati huo tulishuhudia uhai wa upatikanaji wa maji.

1993-1995, Edward Ngoyaye Lowassa alipewa kazi ya waziri wa nyumba na Maendeleo, wakati huo tulishuhudia ujenzi holela wa Dar es salaam,maeneo ya segerea,Buza,Mbagala na kigamboni. Akiwa msukuma ajenda za wananchi kujijengea makazi bora,lakini hakufanya hivyo.Nenda Mbeya,Songea, Mwanza maeneo ya Pansiasi ni hatari hakuna mpango mji unaoonesha uso wa nchi.

Kuanzia mwaka 2000 alibahatika tena kuteuliwa kuwa waziri wa mifugo na maji.Kipindi hiki kwenye maji tulishuhudia miradi ya kusambaza maji inakufa kukaanzishwa mpango wa DAWAzSCo ambayo ingesambaza maji vijijini na mjini.

Ni Shairose Bhaji ndio alipewa mradi huo,hadi anapewa kazi hiyo hakuna hata boma lililosambazwa .

Bhaji kwa sasa ni mbunge wa afrika mashariki.
Mifugo itakumbukwa kuwa Tanzania hatuna maeneo rasmi yaliyotengwa kwa kufugia.Tumeanza kupata migogoro hii ya ufugaji.

Wataalam wakiishauri nchi kutenga maeneo ya kufugia,kuimarisha viwanda vya ndani ilitutumie nafasi kuzalisha nyama,kutengeneza bidhaa za ngozi,nta nk.Edward ameondoka wizara hiyo ikiongoza kuwa na mifugo huku kukiibuka migogoro ya wakulima na wafugaji nchi nzima.

Najiuliza Lowassa huyu aliyeshindwa kutuhakikishia maji ya uhakika,ambapo hata jimbo lake tu hakuna maji? ,kwa nini michango hiyo anayotoa si aanzie vijiji,shule na Dispensari zake?

* huyu Lowassa ambaye,ameacha mapigano ya wakulima na wafugaji kugombea maeneo leo anasaka Urais.

Akiwa waziri Mkuu,anakumbukwa ziara yake aliyoifanya kule Nansio Ukerewe,mwanafunzi mmoja alimuuliza swali gumu kwa nini nchi yetu ni maskini lakini viongozi ni matajiri?

Lowassa badala ya kuona mtoto anahoja aliagiza kijana akamatwe aeleze nani anamtuma?

Hilo halitoshi,akiwa waziri alishiriki kumshauri rais,kufanyia marekebisho sheria ya maadili na utumishi ya 1995, iliyokuwa inaeleza kuwa" kiongozi wa umma,anawajibu wa kutangaza mali zake kwa kujaza fomu maalum ambayo itatunzwa ikulu" Lakini baada ya kuijaza hairuhusiwi mtu yeyote kuweka maelezo hayo mbele ya wananchi,au kuuona kwa waandishi hadi idhini ya rais tu.

Leo hii anataka urais.

Kuna watu wanadhani anafaa,wamuulize iko wapi miradi ya maji chini ya wajerumani?


Kuna watu wanadai Rais sasa awe tajiri,niwaoneshe biongozi maskini na waliongoza nchi zao vyema kabisa.

Mahattam Ghandi

Huyu alikuwa mwanasheria,aliyeishi Afrika kusini,kisha alienda kuwafurusha waingereza nchini India,mzee huyu anakumbukwa na wahindi kwa msimamo wake kudai usawa na haki,

Alifunga kula,kuishinikiza serikali ya waingereza kusikiliza kilio chao.

Franklin Rooserverty huyu Alikuwa Rais wa Marekani,alikuwa maskini, lakini alihakikisha Rais waafrika utumwa unakoma,haki ya kupiga kura na kupigiwa,usawa katika sheria.

Nelson Mandela
Akiwa m/ kiti wa ANC,alifungwa gerezani kwa kudai haki,umoja na usawa mbele ya sheria,1994 aligombea urais akashinda,hskutoa fedha na hakuwa tajiri.

Mareksni huko ambako raia wengi wanajiweza kiuchumi, walimchagua Bill Clinton Rais mwalimu wa chuo kikuu na kumwacha tajiri milionea,sembuse sisi?

Uingereza,zipo familia za Mc Donald matajiri wa makampuni ya kutengeneza mikate na vinywaji vikali duniani hawajawahi kuendekeza tajiri anayehonga.

Ikumbukwe sasa,wakati inaletwa sheria ya TAKRIMA Lowassa akiwa waziri wa maji na Mifugo aliunga mkono sheria hii iandikwe.Ndugu Chenge akiwa mwanasheria wa serikali na Edward Lowassa wanaweza kutupa majibu kwa nini rushwa iligeuzwa kuwa Takrima?

Anayewaza Lowassa kuwa Rais wa Tanzania, kwa kisa cha Maamuzi magumu,angefikiria sana,kwa nini miradi mingi ya maji, ilikufa na bajeti zilikuwa zinatengwa?

Anaweza kutueleza,kama migogoro ya ardhi,na vigogo kujiuzia nyumba za serikali chini ya uwaziri wake?1993-2000.


Nyumba hizi za NHC ziliuzwa,na yeye akiwepo,je ziko wapi?

Mwaka 200-2005 ,ndio wakati wanyama wetu wakawa wanapanda ndege kwenda nje,tunamkumbuka yule mtoto wa mfaume wa Saudia alivyojichukulia Tausi na Tembo kwenda nje na yeye waziri wa mifugo!

Anayewaza hisani ya Lowassa kanisani na miskitini,ajiulize kwa nini nguvu ya pesa inatumika sana?,

Lakini ajiulize,wanyama wetu,wakati wanabebwa
Walikuwa wachukuliwa kweli Mh.Lowassa haujui ?
Hatutawaamini tena, vyakubimbi nyie
 
Back
Top Bottom