Kwanini Edward Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania 2015

M.L.

Senior Member
Feb 11, 2012
185
119
Watu wengi wanawaza kuwa yamkini EL angefaa kuwa mgombea urais kupitia CCM mwaka 2015. Kwa upande wangu naona na ninaamini hivi, Edward Lowassa hafai kabisa kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM kwa sababu:-

  1. Tuhuma dhidi yake kuwa ni fisadi mkubwa kwenye sakata la Richmond na hatimaye Dowans. Tuhuma hizi haziwezi kusafishika kwa namna yoyote. Labda tu ataje kwamba hahusiki na akiri hadharani (press conference) kwamba yuko tayari kutoa ushahidi mbele ya umma na mahakama wa kuwezesha kuwatia hatiani wahusika ambao wamemvisha kengere shingoni mwake.
  2. Uvumi kwamba yeye amejitajirisha kwa njia zisizohalali; kwani, utajiri wake hauelezeki ulivyopatikana. Hapa kunatuhuma kwamba akiwa waziri wa Aridhi aliuza na kutoa viwanja vingi vya umma kwa matajiri wa kihindi na wafanyabiashara kadhaa. mf, uwanja wa wazi wa karibu na majengo ya Bora (Kijitonyama-Mabatini). Aidha, tuhuma za kuyatoa maeneo ya kiwanja cha UVCCM akishirikiana na E. Nchimbi pale Dar es Salaam.
  3. Tuhuma za kujenga makundi ndani ya CCM, mathalan, wakati wa uchaguzi uliopita kumpitisha J. Kikwete. Alimpaka matope Salim A. Salim, Philip Mangula, Fredrick Sumaye na wengine wengi.
  4. Katika uchaguzi wa ndani ya chama Edward Lowassa ametuhumiwa kutumia fedha nyingi mno kuhonga wajumbe wa chama kwa ngaszi mbali mbali ili apitishe watu wanaomuunga mkono yeye ndani ya chama, mathalan, wakuu wa wilaya na mikoa; wenyeviti na makatibu wa ccm ngazi ya wilaya na mikoa.
  5. Tuhuma za ushiriki wake katika biashara ya madawa ya kulevya akishirikiana na familia ya mkuu wa kaya.
  6. Ni mpenda vyeo na king'ang'anizi.
  7. Mtoa rushwa kwa kuhonga taasisi za dini ili asafishike na kujijenga na kutengeneza mazingira ya kupigiwa debe na viongozi wa dini.
  8. Ni tu mwenye kupendelea watu wa jamii yake au watu wanaotokea upande wa kwao kaskazini. Kwa ufupi ni mkabila.

Kwa sababu hizo na nyingine ambazo unazijua wewe, EL hastahili kugombea urais wa TZ kupitia hali yoyote wala kupitia chama chochote.


Wana jamvi habari zenu nimekuwa nikifuatilia nikaona nitoe mtizamo wangu kuhusu huu upepo unaovuma kuhusu Edward lowasa,leo natoa sababu 5 zinazomfanya Lowasa asiwe na sifa za kuwa raisi wa nchi yetu

1.Elimu
ikumbuke kuwa EL ndie aliyesimamia ujenzi wa shule za kata ambao hii leo zimesababisha kushuka kwa elimu nchini,hakuna vitabu,miundombinu mibovu,walimu bado ni tatizo,kwa maana hiyo hakuandaa mazingira kwanza na kukurupuka kujenga majengo ambayo leo hii hayana tija, hata waliofeli wanabebwa ili kujaza shule.

2. kashfa ya ufisadi
jamani watanzania tumerogwa haiwezekani mtu aliyekumbwa na kashfa nzito ktk nchi hii leo anaonekana anafaa kuwa raisi, eti sababu ni mtu mwenye mamuz magumu yepi hayo kufukuza wakurugenz wakati mapapa wapo anawaangalia tu,watanzania tusipumbazwe na huu upepo unaotufanya tusimtafakari EL kwa undani na kushabikia.

3.Vision
tokea nmeanza kumfahamu lowassa cjawahi kusikia akitoa mtizamo wa kuifikisha nchi hii mahali fulani zaidi ya kukurupuka kufanya vitu visivyokuwa endelevu, hivyo lowassa anaweza kuwa mtendaji mwenye kuangalia maslai yake, lakini si kiongozi mwenye tafakari na dira.kwa mfano harambee ya bodaboda kumiliki yake haiwezekan kiuchumi ataharibu uchumi kutokana na vijana kutoweza kukaa mashamban kuzalisha na kuhamia mijini kuwa boda boda.

4.visasi
lowassa ni mtu wa visasi na anautaka uraisi ili aje awalipize ubaya waliomtendea walioibua suala la richmond tuliona uchaguzi uliopta jinsi wabaya wake walivohangaika kupita kwenye majimbo yao,hivyo kama kauli yake ya kujiuzuru alivyosema mana yake kuna watu ana vita nao kuhusu PM ambao hadi leo hajawai wataja hivyo mpaka leo kahifadhi moyoni,fikiri nn kitatokea..

5.Rushwa
watanzania tufumbue macho tumekuwa tukinufaika na pesa za Lowasa na kufumba macho kumjadili,haiwezekani hizo pesa zake si angeendelea kufanikisha zoezi lake la shule za kata aliloanzisha,kujenga maabara,vitabu ili tuone kwamba alikuwa na dira gani kuhusu hizo shule alizojenga ili tujue alikwamishwa lakin bado nia yake ilikuwa kumkomboa mtanzania ktka elimu, kulikoni hivi anavogawa pesa km njugu ili kutimiza adhma yake,hii mm naita ni rushwa iliyokomaa na kufanya wananchi tuone ni kitu cha kawaida.
mwisho niseme kwamba tunahitaji raisi ambaye hatuna hofu kuhusu afya yake,ili aweze kufanya kazi na wala sio kila mwezi kwenda kuangalia afya ughaibuni.
''Tunahitaji maamuzi magumu yenye tija na dira na sio maamuzi magumu yasiyo na dira na mipango madhubuti''
ahsanteni nawasilisha

Wasalaam wana Jamvi

Wananchi wanaanza kufumbua macho baada ya kauli za waasisi kama Mwl jk Nyerere alipomkemea Lowassa kuwa hafai kuwa Rais kwa hoja kubwa kuwa mali alizonazo,zinawalakini.

Watanzania wanapima muda wa utumishi wake tangu aingie madarakani mwaka 1990 akimshinda mpinzani wake kwa rushwa ya ng'ombe wanane waliochinjwa wakati wa kampeni zake.

Unaweza kujiuliza sana,kwa nini Lowassa anautaka urais kwa udi na uvumba hadi anaamua kuvunja sefu ili kuhakikisha anashinda?, kwa nini anafanya sherehe na kuwakaribisha viongozi wa ccm ambao kila wakiondoka Monduli mifuko yao huwa imevimba?,hebu tuangalie nafasi zake mbili za utumishi.

WAZIRI WA MAJI

Itakumbukwa kuwa mwaka 1984, chini ya utawala wa Mwl Nyerere nchi hii ilikuwa imesambazwa mabomba ya maji na visima vingi bora vya HESAWA.Inakumbukwa kuwa watanzania maji haya yalikuwa yanawekwa dawa ili kuua vijidudu.

Ni wakati huo, ugonjwa hatari wa kipindupindu, homa ya matumbo ulidhibitiwa. Ni wakati huo tulishuhudia uhai wa upatikanaji wa maji.

1993-1995, Edward Ngoyaye Lowassa alipewa kazi ya waziri wa nyumba na Maendeleo, wakati huo tulishuhudia ujenzi holela wa Dar es salaam, maeneo ya segerea, Buza, Mbagala na kigamboni. Akiwa msukuma ajenda za wananchi kujijengea makazi bora, lakini hakufanya hivyo. Nenda Mbeya, Songea, Mwanza maeneo ya Pansiasi ni hatari hakuna mpango mji unaoonesha uso wa nchi.

Kuanzia mwaka 2000 alibahatika tena kuteuliwa kuwa waziri wa mifugo na maji. Kipindi hiki kwenye maji tulishuhudia miradi ya kusambaza maji inakufa kukaanzishwa mpango wa DAWASCO ambayo ingesambaza maji vijijini na mjini.

Ni Shairose Bhaji ndio alipewa mradi huo,hadi anapewa kazi hiyo hakuna hata boma lililosambazwa .

Bhaji kwa sasa ni mbunge wa afrika mashariki.
Mifugo itakumbukwa kuwa Tanzania hatuna maeneo rasmi yaliyotengwa kwa kufugia.Tumeanza kupata migogoro hii ya ufugaji.

Wataalam wakiishauri nchi kutenga maeneo ya kufugia,kuimarisha viwanda vya ndani ilitutumie nafasi kuzalisha nyama,kutengeneza bidhaa za ngozi,nta nk.Edward ameondoka wizara hiyo ikiongoza kuwa na mifugo huku kukiibuka migogoro ya wakulima na wafugaji nchi nzima.

Najiuliza Lowassa huyu aliyeshindwa kutuhakikishia maji ya uhakika,ambapo hata jimbo lake tu hakuna maji? ,kwa nini michango hiyo anayotoa si aanzie vijiji,shule na Dispensari zake?

*huyu Lowassa ambaye,ameacha mapigano ya wakulima na wafugaji kugombea maeneo leo anasaka Urais.

Akiwa waziri Mkuu,anakumbukwa ziara yake aliyoifanya kule Nansio Ukerewe,mwanafunzi mmoja alimuuliza swali gumu kwa nini nchi yetu ni maskini lakini viongozi ni matajiri?

Lowassa badala ya kuona mtoto anahoja aliagiza kijana akamatwe aeleze nani anamtuma?

Hilo halitoshi,akiwa waziri alishiriki kumshauri rais,kufanyia marekebisho sheria ya maadili na utumishi ya 1995, iliyokuwa inaeleza kuwa" kiongozi wa umma,anawajibu wa kutangaza mali zake kwa kujaza fomu maalum ambayo itatunzwa ikulu" Lakini baada ya kuijaza hairuhusiwi mtu yeyote kuweka maelezo hayo mbele ya wananchi,au kuuona kwa waandishi hadi idhini ya rais tu.

Leo hii anataka urais.

Kuna watu wanadhani anafaa, wamuulize iko wapi miradi ya maji chini ya wajerumani?

Kuna watu wanadai Rais sasa awe tajiri, niwaoneshe kiongozi maskini na waliongoza nchi zao vyema kabisa.

Mahattam Ghandi

Huyu alikuwa mwanasheria, aliyeishi Afrika kusini, kisha alienda kuwafurusha waingereza nchini India, mzee huyu anakumbukwa na wahindi kwa msimamo wake kudai usawa na haki,

Alifunga kula, kuishinikiza serikali ya waingereza kusikiliza kilio chao.

Franklin Rooserverty huyu Alikuwa Rais wa Marekani,balikuwa maskini, lakini alihakikisha Rais waafrika utumwa unakoma,bhaki ya kupiga kura na kupigiwa,usawa katika sheria.

Nelson Mandela
Akiwa m/ kiti wa ANC, alifungwa gerezani kwa kudai haki, umoja na usawa mbele ya sheria, 1994 aligombea urais akashinda, hakutoa fedha na hakuwa tajiri.

Mareksni huko ambako raia wengi wanajiweza kiuchumi, walimchagua Bill Clinton Rais mwalimu wa chuo kikuu na kumwacha tajiri milionea, sembuse sisi?

Uingereza, zipo familia za Mc Donald matajiri wa makampuni ya kutengeneza mikate na vinywaji vikali duniani hawajawahi kuendekeza tajiri anayehonga.

Ikumbukwe sasa,wakati inaletwa sheria ya TAKRIMA Lowassa akiwa waziri wa maji na Mifugo aliunga mkono sheria hii iandikwe. Ndugu Chenge akiwa mwanasheria wa serikali na Edward Lowassa wanaweza kutupa majibu kwa nini rushwa iligeuzwa kuwa Takrima?

Anayewaza Lowassa kuwa Rais wa Tanzania, kwa kisa cha Maamuzi magumu, angefikiria sana, kwanini miradi mingi ya maji, ilikufa na bajeti zilikuwa zinatengwa?

Anaweza kutueleza, kama migogoro ya ardhi na vigogo kujiuzia nyumba za serikali chini ya uwaziri wake?1993-2000.


Nyumba hizi za NHC ziliuzwa na yeye akiwepo, je ziko wapi?

Mwaka 200-2005 ndio wakati wanyama wetu wakawa wanapanda ndege kwenda nje, tunamkumbuka yule mtoto wa mfaume wa Saudia alivyojichukulia Tausi na Tembo kwenda nje na yeye waziri wa mifugo!

Anayewaza hisani ya Lowassa kanisani na miskitini, ajiulize kwa nini nguvu ya pesa inatumika sana?,

Lakini ajiulize, wanyama wetu, wakati wanabebwa Walikuwa wachukuliwa kweli Mh. Lowassa haujui ?

Amani iwe kwenu wanajukwaa,

Juzi nilikuwa namsikiliza mzee wangu Mheshimiwa aliyetukuka kabisa bwana Edward Ngoyai Lowassa. Alizungumzia juu juu kuhusu suala la RICHMOND na mashabiki wake wakasema kabisa "THAT WAS JUST THE TIP OF THE ICEBERG" sinema yenyewe inakuja.

Well i couldn't agree more ila kuna msemo unasema "FOOL ME ONCE SHAME ON ME,FOOL ME TWICE SHAME ON YOU". Mzee wangu Lowassa ni mara mia hata asingezungumzia swala zima la RICHMOND kwa mapema hivi tena kwa kujitia upofu kama hajui serikali huwa inaongozwaje.

Katika serikali yoyote duniani lazima kuwa na Administrative Machinery ambayo huwa haiendeshwi hivihiv tu ila kwa kufuata kanuni na taratibu za kiutawala. Hii inasaidia kudumisha amani na utulivu katika nchi husika.

Mzee Lowassa alisema kwamba yeye hakuhusika na mikataba yeyote ila waziri wa wizara husika ndiye aliyeiandaa na Mamlaka za juu zikaruhusu mkataba kupitishwa. Sasa kwa jambo kama hili mtu Layman anaweza akakubaliana nalo lakini jamii ya wasomi hawawezi kusadiki kitu kwasababu it goes against the common precepts of leadership.

The doctrine of ministerial responsibility huwa inasema kwamba "Whatever belongs to the cabinet is the responsibility of all ministers". Simply to say ni kwamba maamuzi ya Baraza la Mawaziri ni maamuzi ya mawaziri wote regardless ni maamuzi ya wizara ya michezo au Nishati na Madini.

Endapo serikali itavurunda basi wananchi wa kawaida watasema serikali ni mbovu na siyo waziri fulani tu. Hivyo basi The Doctrine of Ministerial Responsibility ipo kwa ajili ya kuifanya serikali iwe accountable kwa watu inaowaongoza na pia kutunza siri za serikali.

Katika Baraza la Mawaziri mambo critical huwa hayapitishwi hivi hivi,.ila ni kwa kufuata procedures na principles. Hili Mzee wangu Lowassa analijua vizuri kabisa. Mfano Mzuri ni pale ambapo Baraza walikuwa wanapinga kuhusu Project ya Maji kipindi cha utawala wa Mzee Mkapa na Mambo yale yalizungumzwa na Baraza zima wakati yeye ni Waziri wa Maji.

Sasa Leo mzee Lowassa anataka kutuambia kwamba yeye hahusiki vipi na RICHMOND wakati alipitisha?

Under Ministerial Responsibility endapo waziri hatakubaliana na maamuzi ya baraza au raisi basi hatapiga kura na maamuzi yakipita basi yatakuwa deemed kama ni ya Serikali.

Endapo waziri kutakubaliana na hayo maamuzi na kutaka Usiwe part ya hayo basi utatakiwa ujiuzulu la si hivyo nyamaza na Uendelee kubaki serikalini.THE DOCTRINE OF MINISTERIAL RESPONSIBILITY inawaruhusu mawaziri wa Upinzani tu ndani ya serikali kuyakosoa maamuzi ya serikali na bado wakabaki madarakani.

Hii huwa inatokea sana kukiwa na Serikali ya mseto kama Zanzibar. Makamu wa Raisi Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad yupo sahihi kabisa kufanya anachofanya kwasababu ni upinzani.

Na ikumbukwe Dhumuni la MINISTERIAL RESPONSIBILITY ni kujenga imani kati ya serikali na wananchi,..ili mwisho wa siku Serikali ikikosea ni Lazima watu wajue nani ni wa kuwajibishwa.

Mzee wangu Lowassa ulitakiwa Ujiuzulu mapema kama kweli ulikuwa na nia ya kulisaidia taifa na usingesubiri bunge lifumue mambo ndiyo useme unabeba msalaba. Kwa mtu mwenye AKILI TIMAMU hili haliingii akilini hata kidogo.

Kama mkataba ulikuwa ni mbaya na wewe unajua kabisa kwanini uluendelea kukaa madarakani??
THIS MAKES YOUR INTEGRITY QUESTIONABLE.

Ikumbukwe Patriotism siyo kupenda CHAMA,WALA KUIPENDA SERIKALI ,WALA SI KULINDANA NA WALA SI KUMTII RAISI ila UZALENDO NI KUONYESHA HESHIMA KWA SHERIA ZA NCHI IKIWEMO KATIBA,NA NIA YA KUILINDA NA KUITUNZA NA KUBWA ZIADI NI KUWAHESHIMU WATANZANIA BILA KUJALI KABILA,ITIKADI,RANGI AU DINI.

Sasa Mzee Lowassa ni lazima ajue kwamba hata ufanyaje hili swala ni lenu wote,..wewe na wana CCM wenzako katika serikali ya Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete. Lilipitishwa na wewe hukuchukua hatua yoyote ile bali ukakaa na kuendelea kupokea Mshahara na kupigiwa Ving'ora kama kawaida.

Sasa leo kwenye uraisi ndiyo utake kuwahadaa watanzani,...kweli???This is not acceptable at all.

Cha kusikitisha ndugu zangu UKAWA wamempokea kwa mikono miwili wakiamini wanaweza kumhandle Lowassa.

Jamani wahenga walisema Kunguru hafugiki.

UKAWA wajifunze kwamba "WHEN FIGHTING VAMPIRES MAKE SURE YOU DON'T TURN INTO ONE OF THEM"



CC: Pasco Lizaboni
 
Nakuunga MKONO Msafi aliyebaki ni Rizwan Kikwete pekee ndie anayefaa kuchukua URAIS - yeye SIO FISADI; Anakiongoza VIZURI UMOJA wa VIJANA... ameshaanza kukutana na VIONGOZI wa DUNIA
 
MZEE EL kwa mfumo wa siasa ya tanzania na hali ya kusahau kwa haraka miongoni mwa watanzania wengi. uwezekano wa EL kupenya tundu la sindano upo 2015, kwani jamii imechoka na siasa ya watanzania inayotembea kwa miguu ya demokrasia mufilisi isiyotafsirika kwa namna yoyote ile mpaka CCM ing'atuke madarakani. kila mtu anakosoro hasizoweza kujisafisha. "Kichwa cha Nyoka kumbe kweli hakistahimili kilemba."
 
CCM nani msafi? tuambie wewe inaonekana yu ndani ya chama wafikiria nani anafaa?? Ukabila ondoa ni uongo sina haja ya kuuzungumzia.

Madawa ya kulevyea ndo twasikia kwako, haina ukweli hata kidogo na wewe unajua hivyo mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.. yeye na mzee wakali it really they are in bad termz.. how could they be partners??

Mpenda vyeo bila shaka haina uhalisia mbona alijiuzulu uwaziri mkuu, acha propaganda!!

Kujenga makundi ni tuluma ambayo ni nyepesi kwani kila mwana ccm yeye mwenyewe imani na upendo wake kwa kiongozi fulani ana ji identify na kundi lake.. aliye jenga makundi ccm ni Nape na Sitta walipokuja na hoja ya ufisadi bila kujua athari yake na sasa wako bize kumbebesha EL mzigo! ccm walipovunja azimio la arusha wakaja na zanzibar wadhani walimanisha nin?? kashifa kwa Sumaye na Salim hawaitaji kusemewa mana wao wanamjua mbaya wao MZEE WA KAYA na hii inathibitisho na kauli ya Sumaye aliyoitoa 2005" mtu anapotumia kalamu kuchafua wenzake ili kupata madaraka bila shaka atatumia risasi kudhibiti wapinzani wake akiwa madarakani" Nadhani unaikumbuka hii kauli..

Kuhonga ccm si El PEKEE ILA NI TABIA NA ASILI YA CCM hata wanachama hafanyi chochote bila kupokea chote, wanachama ccm ni walamba miguu ya WAKUBWA ndo mana utasikia kijana wa Six, Membe, Ridhiwan ndo wanaowalisha hawa.. swali: wewe ni wa nani??

Hyo uvumi kwamba sitaongelea mana ni uvumi kila mtu ana yake hata wewe kuna watu wanakufikiria negative in every success you have achieved in life.. it just rumourz

Tuhuma za ufisadi za richmond na Dowan hapa bado pana kazi ila kwa mwenye upeo anajua kinachoendelea mfano ripoti ya kamati teule ya Mwakyembe ilisema mitambo ile ilikuwa mibovu ila leo symbion wanaitumia na wanatuuzia umeme, Lowassa aliomba swali hili kurudishwa bungeni ama kupelekwa mahakamani ila serikali ilikataa, Tume ya Mwakyembe ilisema ingefumua mambo yote serikali ingekuwa taabani' mhh sas walimanisha nin??

Kazi kwako tafakari why Lowassa?? why he is the threat especially to some fellow in his party?? Ni mtendaji mzuri hawezi linganishwa na Pinda wala wengine wengi he has a very strong leadership calibre.. nakumbuka city water na maji victoria he did play his role
 
Lowasa mchapakakazi sana ,maswala ya mahera yake hayatuhusu,kama una ushaidi mshitaki dada.maneno maneno hata kwenye kanga wanaandika,kenya kachukuwa nchi milionea,wameangalia uwezo wa kazi.
 
Vijana wa El wanapaswa waelewe kuwa mazingira ya kujiuzulu Mzee Mwinyi ni tofauti na mazingira ya kujiuzulu Lowassa.Lowassa alijiuzulu kwa tuhuma ya wizi uliogharimu taifa na kuharibu uchumi wa nchi.Richmond ni kichefuchefu hadi leo kwa mwananchi wa Tanzania.Gharama za umeme kupanda ni chimbuko la uwepo wa Richmond.

Kamati teule ilitoa ripoti yenye ushahidi,ikapendekeza ajipime.Akasema kaonewa,Lucas Selelii akasimama na kumwomba Lowassa ale kiapo cha kuwajibika kisiasa kama itagundulika hajaonewa na wao wanakula kiapo cha kuwajibika kisiasa ikiwa itagundulika wamemwonea Lowassa ila Lowassa hakula kiapo hicho kwahiyo hapa anatupa uhakika kuwa Richmond ni misumari ya moto aliyoibeba na itamchoma 2015.Mzee Mwinyi hakujiuzulu kwa wizi bali uzembe wa surbodinates wake.Na kama Lowassa anajifananisha na Mwinyi katika kujiuzulu je anatuaminisha Msabaha na Karamagi ni wakosaji?Na kama ni wakosaji kwanini yupo nao kwenye timu yake ya kampeni?Bado kwenye Richmond hana usafi wa kujisafishia.

Niwaase vijana wa El wajifunze kufanya analysis za kisiasa kwa manufaa ya El.El hata kama anasema anawazidi uwezo Pinda na Sumaye bado anajidanganya.Iko hivi,kumfananisha Pinda na El ni dhambi kubwa kwasababu Pinda ana uzoefu na utumishi wa ikulu tangu 1974.Amehudumu kama Katibu wa rais kwa awamu zote nne za serikali zote Tanzania.Anakijua chama kabla ya Lowassa kuingizwa katika siasa na Jk,Jaka Mwambi na Ditopile.Lowassa hakijui chama kulinganisha na Pinda.Kwahiyo kiuzoefu ndani ya chama na serikali Pinda ni bora kuliko Lowassa.

Lowassa hana pumzi ya kisiasa kumzidi Sumaye.Sumaye ana wasifu wa kuhudumu miaka 10 kama Pm wa Tanzania bila kuchafuka na hata alipochafuliwa mahakama ilimsafisha na fidia aliyopewa alisaidia mfuko wa vyombo vya habari nchini kwahiyo hata New Habari Cooperation ilifaidika na msaada huo.Kete ya uadilifu ndio bao pekee Sumaye analomzidi nalo Lowassa.

Ni ukweli El yupo nje ya serikali kwa karibu ya miaka 10.Hii ni sababu tosha ya kumwengua 2015 kwasababu hatujaona kazi yake wizara yoyote kwakuwa ameshapewa fursa ya Upm akaondoka kwa aibu.Na historia yake mbaya akiwa waziri wa ardhi na waziri wa sera,uratibu na bunge chini ya Pm Malecela kwenye tenda ya ununuzi wa magari ya serikali(mashangingi)ni sababu tosha ya kuionesha dunia kuwa El ni mzigo kwa chama na serikali.Ushahidi usio na mashaka ni kwamba hata jimboni Monduli hali sio nzuri,ufisadi katika halmashauri na ardhi ni pigo tosha kwake.

Mjibu hoja wa El anasaidia kumsafishia njia rafiki yetu BM ya kuelekea ikulu 2015 katika suala la List of shame.List of shame inamtaja El haimgusi BM.Aliyesema List of shame ni asilimia 90 ya wanamtandao wa Jk 2005 anamweka kando BM kwasababu hata kama ni kweli wanamtandao wenzake wanahusishwa ila yeye haonekani mahali.Eti El hawezi kushughulikiwa na wachafu wenzake,huu ni upuuzi kabisa.

Lowassa kugombea Nec wilayani ni ishara ya uoga kwasababu kundi la kifo ndio kundi pekee ambalo linapigiwa kura na wajumbe wote wa Ccm.Wilayani unapigiwa kura na watu wa eneo lako tu unalotoka.Waliopigiwa kura kundi la kifo ni washindi hadi Zanzibar kwasababu Zanzibar nao waliwapigia kura.Kuwa rais lazima ukubalike na Zanzibar maana huwezi kuwa rais wa Monduli,Monduli sio nchi.

Lowassa anaumwa huo ndio ukweli.Ugonjwa wake unaongezeka kila siku.Vijana wake hawana lugha ya kutueleza tukaelewa.Sio wa kupewa nchi.Wametoa mfano wa Michael Sata wa Zambia mimi naona ni mfano dhaifu kuwahi kutokea katika siasa za Tanzania.Mfano unaomfaa Lowassa ni wa Levy Mwanawasa au Omar Odimba Bongo.Hatutaki gharama za uchaguzi mdogo au matibabu kila siku ulaya na India kuelemea walipa kodi wa Tanzania.
 
Wakati mwingine tunalazimika kujibu si kwamba kwa kuwa tuna majibu mazuri ila kwa kuwa tunaamini mwandishi anaweza kuwa amejivika kilemba cha uelewa finyu hivyo kuhitaji msaada.

Moja ni lazma uelewe kwamba hakuna mtu anayejaribu ati kumsafisha EL manake kwanza hakuwahi kuchafuka bali alichafuliwa na akasafishwa muda huo huo na nukuu hii hapa chini ikusaidie kujua kwamba kama Mwakiyembe ni kijana wa Lowassa basi yeye ndiye aliyeanza kumsafisha.

"Mhe. Spika kamati Teule ilikuwa na ushahidi wa mawasiliano ya karibu kati ya Waziri Mkuu na Uongozi wa Wizara. Ushahidi huo haukutosha kwa uwajibikaji wa sura ile ya kwanza wa kiongozi kukutwa na makosa ya moja kwa moja, aliyoyafanya yeye mwenyewe kwa njia moja au nyingine, lakini ushahidi huo ulitosha kwa uwajibikaji wa sura ya pili, ambao hauhitaji mahojiano, kusikilizwa wala utetezi; Uwajibikaji kwa makosa ya watendaji walio chini yako.-Hiyo ndiyo demokrasi.-Wabunge wengi wametoa mifano mingi hapa ukiwemo wa Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, alipokuwa Waziri wa Mambo ya ndani; aliwajibika kwa makosa ya askari huko Shinyanga wakati yeye alikuwa DSM; hatukumsikia akidai apewe nafasi ya kusikilizwa na hata kama angepewa bado angewajibika yeye mwenyewe.

Mheshimiwa Spika, kamati teule inatamka ukurasa wa 37 wa taarifa yake kuwa Ushiriki wa karibu wa Waziri Mkuu katika kila hatua ya zabuni ya umeme wa dharura si lazima uwe ushahidi wa kwamba, kiongozi huyo wa Kitaifa alihusika katika kuibeba Richmond. Unaweza pia ukawa ushahidi wa style yake ya kawaida kabisa ya Waziri Mkuu katika kufuatilia masuala yote ya Kitaifa kwa karibu sana, tukizingatia kwamba, Nchi wakati huo ilikuwa katika kipindi kigumu sana cha ukosefu wa umeme……………….”

Si lazma kujifanya vichaa ktk mambo yaliyo wazi. Halafu ati leo kabisa unamzungumzia Sumaye na miaka yake 10 mi nadhani ungekuja na takwimu ya yale mashamba aliyojimilikisha Morogoro na kuwapata taabu wananchi utueleze uamuzi wake ni upi..... Huo ni uroho, ulafi , na ishara ya kukosa uzalendo kwa Taifa.

Kwa uzoefu huo wa Pinda kukaa Ikulu basi angemtangulia JK na badala ya kujiita mtoto wa Mkulima angejiita mtoto wa Ikulu..... Tujitahidi sana hoja ziwe nzito.....

Hahaha hili la BM jamani nshasema hata wanaomuuza washapeleka kwamba hauziki wametumia maneno haya ni kofia ya Polisi! Halafu BM hana tofauti ns Martha Karau aliyekuwa mgombea Kenya wewe hata kwenu hukubaliki kwa wenzio utaenda kuwaambia nini.... Tusijitoe ufahamu jamani....

Eti EL kafanya nini mimi sitojibu hili unapotoka kwako muda huu ama utakapokuwa popote pale we mwite mtu yeyote hata kijana wa miaka 14 muulize hilo swali nasisitiza yeyote yule.....

Ugonjwa sibishi manake hata wewe hapo ulipo unaumwa braza ni maiti inayotembea sasa una mamlaka gani ya kunyooshea vidole wenzio?? JK kadondoka jukwaani mara kadhaa mmesema sana kwamba hatomaliza wakati wake jamaa anadunda tu.............

Kazi mnayo
 
Wakati mwingine tunalazimika kujibu si kwamba kwa kuwa tuna majibu mazuri ila kwa kuwa tunaamini mwandishi anaweza kuwa amejivika kilemba cha uelewa finyu hivyo kuhitaji msaada.

Moja ni lazma uelewe kwamba hakuna mtu anayejaribu ati kumsafisha EL manake kwanza hakuwahi kuchafuka bali alichafuliwa na akasafishwa muda huo huo na nukuu hii hapa chini ikusaidie kujua kwamba kama Mwakiyembe ni kijana wa Lowassa basi yeye ndiye aliyeanza kumsafisha.

"Mhe. Spika kamati Teule ilikuwa na ushahidi wa mawasiliano ya karibu kati ya Waziri Mkuu na Uongozi wa Wizara. Ushahidi huo haukutosha kwa uwajibikaji wa sura ile ya kwanza wa kiongozi kukutwa na makosa ya moja kwa moja, aliyoyafanya yeye mwenyewe kwa njia moja au nyingine, lakini ushahidi huo ulitosha kwa uwajibikaji wa sura ya pili, ambao hauhitaji mahojiano, kusikilizwa wala utetezi; Uwajibikaji kwa makosa ya watendaji walio chini yako.-Hiyo ndiyo demokrasi.-Wabunge wengi wametoa mifano mingi hapa ukiwemo wa Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, alipokuwa Waziri wa Mambo ya ndani; aliwajibika kwa makosa ya askari huko Shinyanga wakati yeye alikuwa DSM; hatukumsikia akidai apewe nafasi ya kusikilizwa na hata kama angepewa bado angewajibika yeye mwenyewe.

Mheshimiwa Spika, kamati teule inatamka ukurasa wa 37 wa taarifa yake kuwa Ushiriki wa karibu wa Waziri Mkuu katika kila hatua ya zabuni ya umeme wa dharura si lazima uwe ushahidi wa kwamba, kiongozi huyo wa Kitaifa alihusika katika kuibeba Richmond. Unaweza pia ukawa ushahidi wa style yake ya kawaida kabisa ya Waziri Mkuu katika kufuatilia masuala yote ya Kitaifa kwa karibu sana, tukizingatia kwamba, Nchi wakati huo ilikuwa katika kipindi kigumu sana cha ukosefu wa umeme……………….”

Si lazma kujifanya vichaa ktk mambo yaliyo wazi. Halafu ati leo kabisa unamzungumzia Sumaye na miaka yake 10 mi nadhani ungekuja na takwimu ya yale mashamba aliyojimilikisha Morogoro na kuwapata taabu wananchi utueleze uamuzi wake ni upi..... Huo ni uroho, ulafi , na ishara ya kukosa uzalendo kwa Taifa.

Kwa uzoefu huo wa Pinda kukaa Ikulu basi angemtangulia JK na badala ya kujiita mtoto wa Mkulima angejiita mtoto wa Ikulu..... Tujitahidi sana hoja ziwe nzito.....

Hahaha hili la BM jamani nshasema hata wanaomuuza washapeleka kwamba hauziki wametumia maneno haya ni kofia ya Polisi! Halafu BM hana tofauti ns Martha Karau aliyekuwa mgombea Kenya wewe hata kwenu hukubaliki kwa wenzio utaenda kuwaambia nini.... Tusijitoe ufahamu jamani....

Eti EL kafanya nini mimi sitojibu hili unapotoka kwako muda huu ama utakapokuwa popote pale we mwite mtu yeyote hata kijana wa miaka 14 muulize hilo swali nasisitiza yeyote yule.....

Ugonjwa sibishi manake hata wewe hapo ulipo unaumwa braza ni maiti inayotembea sasa una mamlaka gani ya kunyooshea vidole wenzio?? JK kadondoka jukwaani mara kadhaa mmesema sana kwamba hatomaliza wakati wake jamaa anadunda tu.............

Kazi mnayo

Itatuchukua mda kwa watanzania kujua kuwa, mtu akiwa na tuhuma zozote na ikabainika amehusika kw njia moja au nyingine, hastahili kushika madaraka ya nchi hii. Ndo maana hata katika katiba mpya wanapigania wajibikaji wa viongozi. Lowasa tangu enzi za nyerere ashamuona hafai kwa tabia zake za wizi, na leo anatugarimu na umeme, ila bado hatulioni hili tunaendelea kuziba masikio. Ki msingi, nchi hii kama tunahitaji mabadiliko kwenye uongozi lazima tupige chini ccm na tuweke watu wengine hata kama ni kichaa. Ccm wanahodhi hata katiba ya nchi akiwemo lowasa, hafai kabisa.
 
Back
Top Bottom