Kwanini Dr Ndalichako asijiuzuru?

Status
Not open for further replies.

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,323
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imemsimamisha kazi na itamchukulia hatua za kinidhamu Mkuu wa Idara ya Utafiti, Tathmini na Huduma za Kompyuta, Joseph Mbowe baada ya uchunguzi kubaini kuwapo kwa dosari katika ukokotoaji wa alama za mitihani ya somo la Islamic Knowledge katika kompyuta.

Aidha, Wizara hiyo imeagiza Necta kukokotoa upya alama za mitihani ya wanafunzi wa kidato cha sita ya somo hilo waliofelishwa kwa bahati mbaya mwaka huu kutokana na dosari hiyo na tayari matokeo ya alama hizo yametolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo na Ufundi, Philip Mulugo alisema Mei 28, mwaka huu, Wizara ilipokea malalamiko kutoka Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu, dhidi ya matokeo ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka huu katika somo hilo.

Source: Habari leo

Kwa mantiki hii ilitakiwa na Dr Ndalichako ambaye ndio Mtendaji mkuu wa baraza hilo ni lazima kwa aina yoyote ile ajiuzuru kutokana na kadhia kubwa kama hiyo. Kwani athari walizopata wanafunzi hao walio athirika kisaikologia kutokana na makosa yao ni kubwa sana na vile vile gharama watakazo chukua kufanya marekebisho hayo. Huu ni uzembe mkubwa sana kwa mtu muungwana lazima kujiuzuru .
 
Kwanini Nchimbi , IGP Mwema, Kamanda Kamuhanda hawajiuzulu kwa tukio la Iringa, hivi tukio na NECTA na Islamic knowldge lipi Ni baya na ambalo linahitaji watu wawajibike, Hivi nyie ndugu zetu (Waislam ) Baadhi yenu Vichwa vyenu vimejaa Madudu au Matope
 
Tungeanza na mafisadi papa kwanza, nchi ingekuwa ishanyooka!! Kuna viongozi wengi zaidi wanafanya mambo ya kuiumiza jamii zaidi ya hili. Sipingi kumng'oa Dr. lakini tuangalie sababu zinazotolewa!!
 
Kwanini Dr Ndalichako asijiuzuru?
Inabidi ushiriki maandamano yetu kuelekea NECTA ili kumshinikiza ajiuzuru, vinginevyo hausaidii lolote kukaa kwenye keyboard huko Oman na kujidai una uchungu. Njoo tuandamane wote!
 
watu wengine bana.....ajiuzuru kwa lipi labda? Matokeo ya islamic exams....? Hauko serious mkuu..
 
Binafsi sioni sababu ya yeye kubakia hapo. Kwano kosa kama hilo la kiutendaji ni kubwa sana kwa jamii hasa ukizingatia kuwa limefungamana na mambo ya kiimani. Ikumbukwe ni siku nyingi sana waislam hao hao wa Tanganyika wamekuwa ma msururu wa malalamiko ya kudhurumiwa haki zao na Serikali yao.

Lakin ni funzo sana kwa Serikali ya JMTz kujifunza zaidi ikiwemo pamoja na kulifanya Baraza hilo la Mitihani kuwa na SURA YA MUUNGANO. Kwa kuamua kama Katibu mtendaji atatoka upande mmoja wa muungano basi naibu wake atoke upande wa pili wa Muungano kama ilivyo kwenye taasisi na wizara zote zenye sura ya Muungano kama BOT etc.

Lakin vile vile ikumbukwe tokea kuanzishwa kwa baraza hilo viongozi wake wakuu kama katibu mtendaji mkuu na naibu wake wote wamekuwa wakristo. Hakuna muislam hata mmoja na hapo ndipo panapozidisha mashaka kwa chombo hicho.

lakin mwisho za mwizi arobaini. sasa ukweli umedhihiri. Laazima Katibu mtendaji mkuu wa Baraza hilo lazima awajibike kwa kujiuzuru ikiwemo pamoja na kuwafikisha mahakamani kutokana na kuwa athri watoto hao kisaikologia na kuwapotezea muda wao.

Hatua zimechukuliwa dhidi ya aliyefanya kosa na huu ni utaratibu unaokubalika kwa mtumishi wa serikali (Civil Servant). Hivyo hawezi kujiuzuru kwa matakwa ya Ponda na kwa kuzingatia kosa hilo halihusiani na utendaji wa Ndalichako moja kwa moja.
 
Barubaru, kuna waziri aliyekuwa akiingoza hii wizara naye vipi? amefaurisha wanafunzi zaidi ya 5,000 hawajui kusoma na kuandika, mi napendekeza Dr. Shukuru Kawambwa nae angejiuzuru, kwasababu kama zaidi ya madenti 5000 wamefauru while hawajui kusoma wala kuandika sasa hao waliofeli hawajui nini?
 
Barubaru, kabla Dr Ndalichako hajaondoka natagemea boss wake- Dr Shukuru Kawambwa atatangulia. Unaweza kuniambia kwanini Dr Kawambwa hatajwi kwenye hii issue? Tuliona TBS ambapo both Waziri na mkuu wa TBS waliondolewa, sasa kwa nini kwenye hii wizaraya elimu wananyoa katikati lakini shina linabaki?
 
watu wengine bana.....ajiuzuru kwa lipi labda? Matokeo ya islamic exams....? Hauko serious mkuu..

Kwani Dogo hilo?

Lakin msingi mkuu wa kujiuzuru kwake ni kurejesha hishma ya Barza hilo kwa wananchi hususan wale waliodhurumiwa matokeo yao.
 
Binafsi sioni sababu ya yeye kubakia hapo. Kwano kosa kama hilo la kiutendaji ni kubwa sana kwa jamii hasa ukizingatia kuwa limefungamana na mambo ya kiimani. Ikumbukwe ni siku nyingi sana waislam hao hao wa Tanganyika wamekuwa ma msururu wa malalamiko ya kudhurumiwa haki zao na Serikali yao.

Lakin ni funzo sana kwa Serikali ya JMTz kujifunza zaidi ikiwemo pamoja na kulifanya Baraza hilo la Mitihani kuwa na SURA YA MUUNGANO. Kwa kuamua kama Katibu mtendaji atatoka upande mmoja wa muungano basi naibu wake atoke upande wa pili wa Muungano kama ilivyo kwenye taasisi na wizara zote zenye sura ya Muungano kama BOT etc.

Lakin vile vile ikumbukwe tokea kuanzishwa kwa baraza hilo viongozi wake wakuu kama katibu mtendaji mkuu na naibu wake wote wamekuwa wakristo. Hakuna muislam hata mmoja na hapo ndipo panapozidisha mashaka kwa chombo hicho.

lakin mwisho za mwizi arobaini. sasa ukweli umedhihiri. Laazima Katibu mtendaji mkuu wa Baraza hilo lazima awajibike kwa kujiuzuru ikiwemo pamoja na kuwafikisha mahakamani kutokana na kuwa athri watoto hao kisaikologia na kuwapotezea muda wao.

Hapo ndipo ninapowadharau waislam. Ajira na Dini wapi na wapi??. Au ndio maana umeenda omani ili upate ajira kirahisi kwa kutumia dini yako?
 
Ponda ni katibu wa Jumuiya na Tasisi za Kiislamu Tanzania, hivi Mwenyekiti wake ni nani? Nimejaribu kugogle lakini kila mahali inakuja "Katibu". Barubaru tusaidie jibu
 
Binafsi sioni sababu ya yeye kubakia hapo. Kwano kosa kama hilo la kiutendaji ni kubwa sana kwa jamii hasa ukizingatia kuwa limefungamana na mambo ya kiimani. Ikumbukwe ni siku nyingi sana waislam hao hao wa Tanganyika wamekuwa ma msururu wa malalamiko ya kudhurumiwa haki zao na Serikali yao.

Lakin ni funzo sana kwa Serikali ya JMTz kujifunza zaidi ikiwemo pamoja na kulifanya Baraza hilo la Mitihani kuwa na SURA YA MUUNGANO. Kwa kuamua kama Katibu mtendaji atatoka upande mmoja wa muungano basi naibu wake atoke upande wa pili wa Muungano kama ilivyo kwenye taasisi na wizara zote zenye sura ya Muungano kama BOT etc.

Lakin vile vile ikumbukwe tokea kuanzishwa kwa baraza hilo viongozi wake wakuu kama katibu mtendaji mkuu na naibu wake wote wamekuwa wakristo. Hakuna muislam hata mmoja na hapo ndipo panapozidisha mashaka kwa chombo hicho.

lakin mwisho za mwizi arobaini. sasa ukweli umedhihiri. Laazima Katibu mtendaji mkuu wa Baraza hilo lazima awajibike kwa kujiuzuru ikiwemo pamoja na kuwafikisha mahakamani kutokana na kuwa athri watoto hao kisaikologia na kuwapotezea muda wao.

Mi napendekeza hii mitihani ya Dini ifutwe kabisa, kama ni Kipaimara, Ikaristi ushindani wa kusoma Koroani n.k vifanywe kwenye nyumba za Ibada, leongo langu ni hili, tunaweza ku include matokeo ya dini then ikampandishia mtu division yake, say alistahili kupata Division 4 lakini labda kwenye Bible knowledge au hiyo ya Madrasa akawa mtu ana A, so atavushwa hadi Division 2, hapa huoni tutapeleka watu vyuo vikuu wakiwa kichwani watupu? kwasababu huko hawaendi kujifunza mambo ya dini but Elim dunia.
 
..Kwa mantiki hii ilitakiwa na Dr Ndalichako ambaye ndio Mtendaji mkuu wa baraza hilo ni lazima kwa aina yoyote ile ajiuzuru kutokana na kadhia kubwa kama hiyo. Kwani athari walizopata wanafunzi hao walio athirika kisaikologia kutokana na makosa yao ni kubwa sana na vile vile gharama watakazo chukua kufanya marekebisho hayo. Huu ni uzembe mkubwa sana kwa mtu muungwana lazima kujiuzuru .
Actually huyo sio wa kujiuzuru ni wa kusimamishwa au kufukuzwa. Aliyetakiwa kujiuzuru ni mwenye dhamana ya kisiasa, Waziri wa Elimu Dr Shukuru Kawambwa! Inashangaza hakuna anayemgusha huyu katika suala hili. Inaweza kuwa ni kwa sababu ya dini yake?
 
Barubaru, kabla Dr Ndalichako hajaondoka natagemea boss wake- Dr Shukuru Kawambwa atatangulia. Unaweza kuniambia kwanini Dr Kawambwa hatajwi kwenye hii issue? Tuliona TBS ambapo both Waziri na mkuu wa TBS waliondolewa, sasa kwa nini kwenye hii wizaraya elimu wananyoa katikati lakini shina linabaki?

Wote ni vizuri sana na uungwana zaidi kwao kujitathmini na kuona uzito wa kosa kwa jamii na ukizingatia jamii ndio iliyogundua kosa hilo sio wao. Basi kiungwana walipaswa kujivua gamba.

Labda kwa kuwa utaratibu huo siku hizi haupo huko Tanganyika. Lakinkwa aina yoyote wote walitakiwa kung'oka ili kulinda hishma ya baraza hilo kwa watahiniwa na wananchi kijumla..

  • Thanks
Reactions: SMU
ok yaliyotokea ni makosa ya kiufundi so wahusika wanapaswa kuwajibishwa kwa sababu wanalipwa kwa kazi hiyo. Kitu cha pili ni kwamba kumekuwa na hisia za kudhulumiwa tunazoziingiza katika masomo yote , mimi nadhani hawa ndo wachochezi nataka nikuhakikishie tu kwamba A level ni darasa mashuhuri kama Hausomi utafeli uwe muislamu au mkristu . mbona al muntazir,feza boys ,marian girls zinafanya vizuri??? hapa naomba tujiulize . pale haendi kilaza . kuna utafiti naendelea kuufanya mwishowe nitaleta hapa tuujadili sio tunafanya siasa kila kitu
 
Inabidi ushiriki maandamano yetu kuelekea NECTA ili kumshinikiza ajiuzuru, vinginevyo hausaidii lolote kukaa kwenye keyboard huko Oman na kujidai una uchungu. Njoo tuandamane wote!
Maandamano sawa lakini msisitizo wa kuzingatia elimu katika ujumla wake ni laazima iwe agenda kuliko kusimamia tu hilo tukio moja. Nadhani yalishafanyika maandamano tayari wakati ule juu ya Ndanda, kuna mengi ya kushinikiza watu wajiuzuru katika nyaadhifa zao, laakini nachelea kusema Tanzania hatuna utamaduni wa aina hiyo, wa kujiuzuru na ahata wa kushinikizaa, ni mahakama tu ndiyo inaweza. Vinginevyo nawatakia maandamano mema, niko Indonesia, huku mambo yanaenda kwa mbele kufaanya maendeleo ya kumkomboa mwanadamu kiuchumi na siyo kufikiria kuandamana kila siku kama hapo nchini kwetu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom