Kwanini Chadema wanasafiria nyota ya Mwangosi?

Nicholas,

Awali ya yote nakupa pole sana kwa kutofahamu lugha yako ya asli ambayo mimi mgeni nimeibainisha kiufasaha zaidi. Lakin pia ulitakiwa uelewe kuwa kuna kitu kinaitwa lugha ya PICHA ambayo nimeibainisha.

Nastahajabu sana yanapokutoka mapuvu na kupomosha matusi kwa hoja ambayo ni dhahir shahir. Siku zote msomi au mwerevu anajadili hoja iliyopo mezani na sio kumjadili mtu. Huo ni upungufu niliouona kwako na ndio ulionipelekea nikupe POLE SANA.

Nakushauri rejea katika mada na ijadili kwa kina. Punguza jazba na soma kwa nia ya kuelewa pasi na shaka mola atakujaalia utaelewa na kuleta hoja zako ambazo tutakua tayari kuzisoma na kuzijadili kama zitakuwa na mashiko.

Pole sana

Barubaru :kwanza nikupe pole kwa lugha unayosema unaijua.Pili nakupa pole sana kama ni mgeni halafu unaingilia mambo ya nchi isiyo yako huku ukiwa na nia mbaya namna hii.Nani kakupa hiyo mamlaka?
Pia ujue lugha ni art na arts huhitaji talents,kila mtu ana talents zake za kuweza mpatia edge over his/her fellows.Na hii haithibitihsi kuwa kujua lugha ndio kutambua mambo.

Sioni hiyo lugha ya picture unayotaka iweka hapa wala umuhimu wake.By the sidhani kama umejibu hoja zangu instead umereside ktk distractions.Huwa mimi nawadharau sana watu wanotegemea distractions km defense zao ktk hoja za msingi.Distractions ni very primitive tricks ambazo hata wanyama/ndege huzitumia kwa hiyo sioni jipya kwako.Kuhamia katika issue ya lugha na jazba ni distractions.

Sidhani km unafahamu ukisemacho.Ulipokuwa ukiwasema watanganyika wanakosa elimu sijui ulikuwa unaongelea nini?Ulipokowa unasema hatuna uelewa ulikuwa unamsema nani?Unafiki ni kosa lichukiwalo katika ulimwengu wengu ila ndilo liwatafunalo sana.

By the way, waamini nyota ni mushrikin sana na huamini mambo ya hovyo sana yasiyo ya kisayansi.hizo blah blah za kujifanya kuwa upo makini sana ni kwa vile umepata domain yako ya porojo katika jamii ikuzungukayo.Kujifanya kuwa huna jazba ni kwa muda tuu na kunazuia kwa vile upo katika internet na si ana kwa ana.
 
Kumbuka Mwangosi aliuawa wakati akifuatilia jinsi polisi wanavyoinyanyasa CDM kwa hiyo si tatizo kwa CDM kuonyesha sympathy. sasa barubaru ulitaka wakae kimya wakati tukio lenyewe lilitokea kwenye mkutano wao? Acha hizo.
Wa Ukumbi.

Kwanza kabisa napenda kutoa Pole zangu kwa Familia ya Mwangsi kwa kumpoteza mpendwa wao wakti akitekeleza majukumu ya kazi yake.

Pili natoa pole kwa wanahabari wote wa Tanzania hususan Upande wa Bara kwa kumpoteza mwanachama wenu mahiri katika mazingira ya kusikitisha akiwa akitekeleza wajibu wake kisharia wa kupasha habari.

lakin pia WaTanzania wote kwa kumpoteza mwananchi mwenzenu makini sana .

Baada ya salam hizo za Pole napenda pia kutoa mshangao wangu kwa baadhi ya vyama vya Siasa huko Tanzania kwa kulivalia njuga suala ma kifo hichi na kuvisahau vifo vingine. Hapa nimeshangazwa sana na Chama Cha Chadema ambachi kimekuwa mstari wa mbele sana kulishadidia hili.

Ikumbukwe kuwa wenye haki kamili ya kulishadidia hili ni waandishi wa Habari ambao ndio sio tu kwa kupewa pole lakin wanajitetea na kudai haki zao za msingi pindi wanapokuwa katika utendaji wa shughuli zao. Ikimbukwe kuwa Wanahabari kwa nchi zinazofuata Rules of Law wao wanakuwa ni muhimili mkuu wa nne lakin usio rasmi katika uongozi wa nchi. Mihimili iliyo rasmi kwa mujibu wa Rules of Law ni mahakama, Bunge na Serikali.

Mimi nilitaraji chama cha Chadema walitakiwa kujua kuwa Mwangosi aliuawa katika tukio hilo akiwa kazini kama Mwandishi wa habari na si kama mshabiki au mwanachama wa Chadema. Chadema walitakiwa wayashadidie mauaji ya wanachama wao ambao wamekuja kushiriki katika tukio la kichama kama yale ya Arusha au hata yaliyotokea hivi karibuni huko Morogoro. Lakin hili si muswiba wao ni muswiba wa wanahabari japo tukio lilitokea katika hadhwara yao.

Kwa lugha ya Pwani tunasema Chadema wanasafiria Nyota ya Mwangoso katika kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Kwani hata katika baraza kuu lao Jana walishikiria kifo hicho na kuonyesha mpaka video yake lakin hawakuonyesha video ya mauaji ya Mwanachama wao Morogoro. Hivyo kuzidisha thamani kwa Mwangosi ambaye ni mwanahabari na kumsahau mwanachama wao wa Pale morogoro. Sote tunaamini watu wote ni sawa lakin familia ni sawa zaidi. Na kila muswiba una wenyewe wengine wote mnakuwa wasindikizaji. Ni vizuri Chadema wajue kuwa katika Muswiba wa Mwangosi wao ni wasindikizaji tu lakin muswiba ni wa wanahabari.

Kijumla ninalaani mauaji ya watu hususan haya ya mwandishi akiwa anatekeleza majukumu yake lakin napinga sana watu kutumia muswiba huu kwa kujitafutia umaarufu na kusahau mauaji ya wanafamilia wake. Tukumbuke kila muswiba una wenyewe. Muswiba wa Mwangoso ni wa wanahari wote sio tu Tanzania bali Dunia nzima na wengine wote tunakuwa wasindikizaji tu.

Tussafirie nyota za wengine katika kutafuta umaarufu wa kisiasa.
 
Barubaru :kwanza nikupe pole kwa lugha unayosema unaijua.Pili nakupa pole sana kama ni mgeni halafu unaingilia mambo ya nchi isiyo yako huku ukiwa na nia mbaya namna hii.Nani kakupa hiyo mamlaka?
Pia ujue lugha ni art na arts huhitaji talents,kila mtu ana talents zake za kuweza mpatia edge over his/her fellows.Na hii haithibitihsi kuwa kujua lugha ndio kutambua mambo.

Sioni hiyo lugha ya picture unayotaka iweka hapa wala umuhimu wake.By the sidhani kama umejibu hoja zangu instead umereside ktk distractions.Huwa mimi nawadharau sana watu wanotegemea distractions km defense zao ktk hoja za msingi.Distractions ni very primitive tricks ambazo hata wanyama/ndege huzitumia kwa hiyo sioni jipya kwako.Kuhamia katika issue ya lugha na jazba ni distractions.

Sidhani km unafahamu ukisemacho.Ulipokuwa ukiwasema watanganyika wanakosa elimu sijui ulikuwa unaongelea nini?Ulipokowa unasema hatuna uelewa ulikuwa unamsema nani?Unafiki ni kosa lichukiwalo katika ulimwengu wengu ila ndilo liwatafunalo sana.

By the way, waamini nyota ni mushrikin sana na huamini mambo ya hovyo sana yasiyo ya kisayansi.hizo blah blah za kujifanya kuwa upo makini sana ni kwa vile umepata domain yako ya porojo katika jamii ikuzungukayo.Kujifanya kuwa huna jazba ni kwa muda tuu na kunazuia kwa vile upo katika internet na si ana kwa ana.

Ahali yangu ngoja nikudarsishe kidogo kwa kudurusu kile nilichoandika hapo chini mpaka kufikia hitimisho la kusema wamesafiria nyota ambalo ndio nimelitumia kama kichwa cha habari changu. Soma nilipoRED kama ufafanuzi na nilipo BLUE kama hitiomisho.

Baada ya salam hizo za Pole napenda pia kutoa mshangao wangu kwa baadhi ya vyama vya Siasa huko Tanzania kwa kulivalia njuga suala ma kifo hichi na kuvisahau vifo vingine. Hapa nimeshangazwa sana na Chama Cha Chadema ambachi kimekuwa mstari wa mbele sana kulishadidia hili.

Ikumbukwe kuwa wenye haki kamili ya kulishadidia hili ni waandishi wa Habari ambao ndio sio tu kwa kupewa pole lakin wanajitetea na kudai haki zao za msingi pindi wanapokuwa katika utendaji wa shughuli zao. Ikimbukwe kuwa Wanahabari kwa nchi zinazofuata Rules of Law wao wanakuwa ni muhimili mkuu wa nne lakin usio rasmi katika uongozi wa nchi. Mihimili iliyo rasmi kwa mujibu wa Rules of Law ni mahakama, Bunge na Serikali.

Mimi nilitaraji chama cha Chadema walitakiwa kujua kuwa Mwangosi aliuawa katika tukio hilo akiwa kazini kama Mwandishi wa habari na si kama mshabiki au mwanachama wa Chadema. Chadema walitakiwa wayashadidie mauaji ya wanachama wao ambao wamekuja kushiriki katika tukio lhuko Morogoro. Lakin hili si muswiba wao ni muswiba wa wanahabari japo tukio lilitokea katika hadhwara yao.

a kichama kama yale ya Arusha au hata yaliyotokea hivi karibuni
Kwa lugha ya Pwani tunasema Chadema wanasafiria Nyota ya Mwangoso katika kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Kwani hata katika baraza kuu lao Jana walishikiria kifo hicho na kuonyesha mpaka video yake lakin hawakuonyesha video ya mauaji ya Mwanachama wao Morogoro. Hivyo kuzidisha thamani kwa Mwangosi ambaye ni mwanahabari na kumsahau mwanachama wao wa Pale morogoro. Sote tunaamini watu wote ni sawa lakin familia ni sawa zaidi. Na kila muswiba una wenyewe wengine wote mnakuwa wasindikizaji. Ni vizuri Chadema wajue kuwa katika Muswiba wa Mwangosi wao ni wasindikizaji tu lakin muswiba ni wa wanahabari.

Inaitwaje tena hiyo nyota? Simba, Mashuke, Nng'e, Ng'ombe, Mbuzi ...... Nafikiri Chadema wanayo magari wanayoyatumia katika shughuli na safari zao za kila siku.

Daudi Mwangosi kauwa kikatili na kinyama sana. Sasa kifo chake na kutokuwepo kwake tena, kusitumike kumdhalilisha kwa mifano na maneno yasiyo na tija kwa yale aliyokuwa akiyatetea na kusababisha kuawa. Ni mategemeo yangu kuwa kifo cha Daudi Mwangosi kitahamasisha au kuleta madiliko makubwa ya sheria kandamizi dhidi ya uwazi na ukweli kwa vyombo vya habari na Taifa kwa ujumla.
 
Wa Ukumbi.

Kwanza kabisa napenda kutoa Pole zangu kwa Familia ya Mwangsi kwa kumpoteza mpendwa wao wakti akitekeleza majukumu ya kazi yake.

Pili natoa pole kwa wanahabari wote wa Tanzania hususan Upande wa Bara kwa kumpoteza mwanachama wenu mahiri katika mazingira ya kusikitisha akiwa akitekeleza wajibu wake kisharia wa kupasha habari.

lakin pia WaTanzania wote kwa kumpoteza mwananchi mwenzenu makini sana .

Baada ya salam hizo za Pole napenda pia kutoa mshangao wangu kwa baadhi ya vyama vya Siasa huko Tanzania kwa kulivalia njuga suala ma kifo hichi na kuvisahau vifo vingine. Hapa nimeshangazwa sana na Chama Cha Chadema ambachi kimekuwa mstari wa mbele sana kulishadidia hili.

Ikumbukwe kuwa wenye haki kamili ya kulishadidia hili ni waandishi wa Habari ambao ndio sio tu kwa kupewa pole lakin wanajitetea na kudai haki zao za msingi pindi wanapokuwa katika utendaji wa shughuli zao. Ikimbukwe kuwa Wanahabari kwa nchi zinazofuata Rules of Law wao wanakuwa ni muhimili mkuu wa nne lakin usio rasmi katika uongozi wa nchi. Mihimili iliyo rasmi kwa mujibu wa Rules of Law ni mahakama, Bunge na Serikali.

Mimi nilitaraji chama cha Chadema walitakiwa kujua kuwa Mwangosi aliuawa katika tukio hilo akiwa kazini kama Mwandishi wa habari na si kama mshabiki au mwanachama wa Chadema. Chadema walitakiwa wayashadidie mauaji ya wanachama wao ambao wamekuja kushiriki katika tukio la kichama kama yale ya Arusha au hata yaliyotokea hivi karibuni huko Morogoro. Lakin hili si muswiba wao ni muswiba wa wanahabari japo tukio lilitokea katika hadhwara yao.

Kwa lugha ya Pwani tunasema Chadema wanasafiria Nyota ya Mwangoso katika kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Kwani hata katika baraza kuu lao Jana walishikiria kifo hicho na kuonyesha mpaka video yake lakin hawakuonyesha video ya mauaji ya Mwanachama wao Morogoro. Hivyo kuzidisha thamani kwa Mwangosi ambaye ni mwanahabari na kumsahau mwanachama wao wa Pale morogoro. Sote tunaamini watu wote ni sawa lakin familia ni sawa zaidi. Na kila muswiba una wenyewe wengine wote mnakuwa wasindikizaji. Ni vizuri Chadema wajue kuwa katika Muswiba wa Mwangosi wao ni wasindikizaji tu lakin muswiba ni wa wanahabari.

Kijumla ninalaani mauaji ya watu hususan haya ya mwandishi akiwa anatekeleza majukumu yake lakin napinga sana watu kutumia muswiba huu kwa kujitafutia umaarufu na kusahau mauaji ya wanafamilia wake. Tukumbuke kila muswiba una wenyewe. Muswiba wa Mwangoso ni wa wanahari wote sio tu Tanzania bali Dunia nzima na wengine wote tunakuwa wasindikizaji tu.

Tussafirie nyota za wengine katika kutafuta umaarufu wa kisiasa.

Hakuna mahali popote kwenye utetezi wa cdm panapo onyesha kuwa mwangosi alikuwa mwanachama wala yule wa moro.Mawazo yako ni mwendelezo wa mgando wa mawazo yanayowasumbua magamba!Hili la mwangosi litawaacha vipande vipande.
 
Mkuu Barubaru naona baada ya kumuua balozi wa US huko Libya umeamua kurudi Zenji na ni kweli kuwa mambo ya Tanganyika utakuwa huyajui.

Kwa ufupi ni kuwa kama ule mpango wa kumuua Mwangosi ungefanikiwa bila intelijensia ya Chadema kufahamu na kama waandishi wasingepata ujasiri wa kurekodi lile tukio, KUNA UWEZEKANO MKUBWA KUWA CHADEMA INGESHAFUTWA AU INGEKUWA INAMALIZIWA KUFUTWA NA JOHN TENDWA KWA KUSHIRIKIANA NA CCM NA SERIKALI YAKE.

Ni lazima CHADEMA iuweke ukweli kwa jumuia zote juu ya mauaji ya Mwangosi kama inavyofanya sasa ili kuweka rekodi sawasawa na kuendeleza mapambano ya kumtetea Mtanzania (Mtanganyika na wewe Mzanzibari)
 
Ahali yangu ngoja nikudarsishe kidogo kwa kudurusu kile nilichoandika hapo chini mpaka kufikia hitimisho la kusema wamesafiria nyota ambalo ndio nimelitumia kama kichwa cha habari changu. Soma nilipoRED kama ufafanuzi na nilipo BLUE kama hitiomisho.

Baada ya salam hizo za Pole napenda pia kutoa mshangao wangu kwa baadhi ya vyama vya Siasa huko Tanzania kwa kulivalia njuga suala ma kifo hichi na kuvisahau vifo vingine. Hapa nimeshangazwa sana na Chama Cha Chadema ambachi kimekuwa mstari wa mbele sana kulishadidia hili.

Ikumbukwe kuwa wenye haki kamili ya kulishadidia hili ni waandishi wa Habari ambao ndio sio tu kwa kupewa pole lakin wanajitetea na kudai haki zao za msingi pindi wanapokuwa katika utendaji wa shughuli zao. Ikimbukwe kuwa Wanahabari kwa nchi zinazofuata Rules of Law wao wanakuwa ni muhimili mkuu wa nne lakin usio rasmi katika uongozi wa nchi. Mihimili iliyo rasmi kwa mujibu wa Rules of Law ni mahakama, Bunge na Serikali.

Mimi nilitaraji chama cha Chadema walitakiwa kujua kuwa Mwangosi aliuawa katika tukio hilo akiwa kazini kama Mwandishi wa habari na si kama mshabiki au mwanachama wa Chadema. Chadema walitakiwa wayashadidie mauaji ya wanachama wao ambao wamekuja kushiriki katika tukio lhuko Morogoro. Lakin hili si muswiba wao ni muswiba wa wanahabari japo tukio lilitokea katika hadhwara yao.

a kichama kama yale ya Arusha au hata yaliyotokea hivi karibuni
Kwa lugha ya Pwani tunasema Chadema wanasafiria Nyota ya Mwangoso katika kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Kwani hata katika baraza kuu lao Jana walishikiria kifo hicho na kuonyesha mpaka video yake lakin hawakuonyesha video ya mauaji ya Mwanachama wao Morogoro. Hivyo kuzidisha thamani kwa Mwangosi ambaye ni mwanahabari na kumsahau mwanachama wao wa Pale morogoro. Sote tunaamini watu wote ni sawa lakin familia ni sawa zaidi. Na kila muswiba una wenyewe wengine wote mnakuwa wasindikizaji. Ni vizuri Chadema wajue kuwa katika Muswiba wa Mwangosi wao ni wasindikizaji tu lakin muswiba ni wa wanahabari.

Kwanza kwa haraka kwako mafanikio ya chadema si furaha kwako.Kwa hiyo huna chema cha kuwashauri,nhia zao ni bora ndio maana wamekuwa consistency.Hakuna mtu duniani mwenye akili timamu anayeweza ondoa kitu kinachofanya kazi vizuri bila sababu.

Tukirudi katik mada nilishakujibu kuwa Chadema walikuwa na kila sababu ya kushughulikia hili suala.Tofauti na wapiga soga wanvyotaka tuaminisha kwa tafsiri zao duni.

-Kwanza chadema ndio walikuwa wameandaa tukio.(Kifo cha mgeni katik sherehe yako ni suala unahitaji kuwa concerned).

-Pia proganda zilizojengwa zilifanya chadema wawe katik hali ama wachukue lawama na kufutwa ama wathibitishe kutohusika na kuweka kumbukumbu sawa.Wote ni wahanga wa lile tukio.Kwa urahisi ili uelewe ni kwamba "si busara kutomjulia hali ,mtu mliyepata naye ajali katika safari" na ikibidi kumsaidia kwa hali na mali kama una afadhali kidogo.

-Vyombo vya habari kuwa mhimili mwingine hakuaaminishi hakuna mambo ya kushirikiana.Wala kusaidiana.Ndicho chadema walichofanya na si kuwapangia jambo waandishi wa habari.

-Sijui kwa nini hujawa mkweli au ndiko kutokujua kuwa hujui kitu.Yule jamaa wa morogoro hakuwa mwanachadema ni muuza magazeti.Na CDM walijituma sana ingawa CCM iliingiza siasa ili CDM wasipewe ushirikiano wa kutosha.Nona umekoroga sana mboga hapa.Kuwa mwangosi hakuwa mwanaCDM sijui ulijuaje kama hakuwa mwanachama na mwandishi.Kama alivyo Tendwa mwana CCM na msajili wa vyama. Pengine next time inabidi uwakaribishe na CUF.

-Pia chadema kam chama cha kisasia kina haki ya kuliweka hilo jambo kisiasa ili kuongez amashinikizo kwa wauaji.Bila hivyo watakuwa wanaitafuta ikulu ya nini kama hawana faida kwa wananchi wote au mmojamoja.
 
Wee Barubaru!!, kwani yule aliyeuawa Morogoro alikuwa katika ule mkutano wa Chadema au alikuwa pembeni kabisa akiuza magazeti(kama siyo hivyo nirekebisheni)? Chama kikubwa kama Chadema hawawezi kufanya msiba wa Mwangosi kuwa mtaji wake kisiasa na kama utafuatilia vyema utagundua kuwa malalamiko ya Chadema siyo kwamba kwanini Mwangosi ameuliwa na Polisisiemu bali ni kwanini Polisisiemu wanatumia nguvu kubwa sana kuzuia mikutano ya Chadema. Hata hivyo hakuna ubaya wowote kwa Chama chenye kujali watu kupigia kelele mauaji ya aina yoyote ile, nahisi unajitoa kumbukumbu pia maana Chadema walitaka kugharamia shuhguli zote za mazishi ya yule jamaa wa Moro. Inaonyesha Barubaru hufurahishwi na jinsi Chadema wanavyotetea haya mauaji, hongera kaka kwa kuthibisha kuwa wewe ni mtaji wa ustawi na uwepo wa CCM madarakani kwa kufurahia dhuluma ya uhai wa watu
 
Ahali yangu.

Ni vibaya sana kuizungumzia mauti. Lakin kwa mtu makini na mwandishi yoyote anaejua taaluma yake utaona wazi kuna mengi sana yamebainishwa katika ile picha.

Personal natilia shaka ueledi wa Marhum katika hii tasnia ya habari. naomba mwenye CV yake kama ipo aiweke tuione.

mapungufu niliyobaini kutokana na picha ni kuwa mwandishi hakuwa na taaluma hiyo. Kwani kuna kitu kinaitwa UANDISHI WA PENYE VURUGU/VITA (V J) ambao siku zote unamsisitiza mwandishi kuchukua position nzuri na iliyo salama katika kupiga picha/ kuona tukio zima. Na hapa inasisitizwa mwandishi kukaa nyuma ya vyombo vya usalama ili kuona wanausalama hao wanafanya nini na raia wanafanya nini.

Lakin ukiangalia picha ile utana marhum amekaa mbele ya vyombo vya usalama kama walivyo wanachama wa Chadema. Kumbuka kuwa vurugu haina macho na lolote linaweza kutokea. Na kufa kwa mwandishi ni pigo kwa jamii kwani itakosa habari.

Kila siku nashauri ni lazima Tanzania ifanye utaratibu wa kusajili waaandhi wake na kuwapeleka internship wanapomaliza skuli ili kujifunza nationa priority, Uzalendo, sharia , mamlaka ya nchi na mazingira ya kazi. Hii iwe kama wanavyofanya me Engineers, ma Doctors na wanasharia.

Poleni sana

ule haukuwa uandishi wa kwenye vita wala vurugu,polisi ndo walifanya shambulizi la kushtukiza kwa kupiga mabomu watu waliokuwa tayari chini ya ulinzi,marehemu aliuwawa akiwa tayari under police custody,think my friend kabla hujaudhalilisha utu wako kwa maneno yasokuwa ya kibinadam.

Halafu kwanini unachukuwa almost a week kila mara kujibu post yangu moja?Please don't be that slow,people are moving on with other issues.Respond propmptly and if not potezea maana najuwa message sent...
 
Kwa sababu Imeonyesha mumiani (wamwaga damu za watanzania ) ni nani! Yaani kifo cha Mwangosi kimeivua nguo serikali na chama chake!
 
Mkuu, nakubaliana na wewe kwa baadhi ya hoja ila si zote.

Kwanza nikiri kuwa mimi ni CCM sana ila sipendi unafiki.

Ni kweli Mwangosi died while he was on duty za kiuandishi na si mwanachama wa wapinzani wetu Chadema. Nadhani kinachowaconnect Chadema ni kama ifuatavyo:

1. Mwangosi alikufa katika shughuli ya ufunguzi wa tawi la chama chao, mtu akifa kwenye shughuli hiyo si jambo la kuacha hata kidogo, kifo ni jambo kubwa na kama political party mnahitaji kulichukulia kuwa sensitive otherwise watu watashangaa kuhusu moral values za chama chenu/viongozi wenu!

2. Ukiachana na kifo, hawa chadema wamepigwa mabomu na kunyanyaswa na police bila sababu za msingi. Kushadadia hii ishu inawapa attention kama chama kinachogandamizwa na dola na kufanya wananchi wachukie utawala uliopo na chama chetu cha CCM. Publicity hiyo inawajenga wapinzani wetu Chadema, so its worth it kama wakipigia debe ishu ya maonezi na kifo kilkichotokana na maonezi hayo.

3. Kumetokea msururu wa vifo kuanzia Arusha, Singida, Morogoro, Iringa; pamoja na watu kuwekwa ndani, nk katoka operations za wenzetu Chadema. Kupaaza sauti kwa kifo hiki ni kuonyesha kutoridhika kwao na issue nzima ya kuonewa na kugandamizwa. Kumbuka publicity kwa vyama vya siasa ni muhimu sana (mhimili wa 4 kama ulivyosema hapo juu)

4. Morogoro kwa marehemu bwana ally (mchuuzi wa magazeti), walitaka kufanya publicity ila familia ya marehemu ilikataa. Inawezekana sie CCM tumewawahi mie sijui. mwangosi, familia ilikubali chadema washiriki kikamilifu.

My friend, siasa ni kujaribu always kuwin wapiga kura kwa namna yoyote iliyo halali bila kuvunja sheria. Mara nyingi sisi CCM tunawapa mwanya chadema wa kupounce na kupata cha kusema kutokana na makosa yetu mengi sana Mfano kumfukuza Zitto bungeni kwenye issue ya Buzwagi ilitugeuka na ikawa lulu kwa chadema (wakatumia helicopta kupata wapiga kura).

Nadhani utakuwa umeelewa.

Kidumu chama cha mapinduzi

Ubarikiwe huko ulipo! You are a free thinker unlike most of your colleagues.
 
Jazba za nini? lete hoja si matusi wala kejeli.

Nitakusaidia kidogo kwa kukufafanulia mambo fulani hapa.

Kwanza Nimetoa Pole kwa wanahabari wote wa Tanzania lakin nikabainisha hususan wale wa Tanganyika kwa sababu SUALA LA HABARI kwa mujibu wa mkataba wenu wa Muungano wenu halimo katika mambo ya Muungano. Kila nchi inajitegemea katika masuala haya ya habari na ndio maana kuna waziri wa habari Znz na waziri wa habari Tanzania Bara.

Pole sana nakuombe nisome vizuri utanielewa tu nini nimekusudia. Punguza jazba.

Akikusoma vizuri atakutukana zaidi...............
 
Wa Ukumbi.
Kwanza kabisa napenda kutoa Pole zangu kwa Familia ya Mwangsi .....

.....Nyota ya Mwangoso ......

......Muswiba wa Mwangoso .....

Yakhe, ulikuwa unamzungumzia nani hapo juu tafadhali?

Sisi tulifunzwa kuwa ni lazima ujue na uandike vizuri majina ya vitu kwa usahihi ili wakati unafikiri/unapotoa maana basi uwe na msingi na mtiririko usio na madoa doa.

Pia kwa ufupi juu ya makala yako hii; nina shaka kama uko karibu na ulimwengu huu tuliopo. Sasa kwa vile uko mbali kijiografia ni vizuri ukajongea panapo uhalisia na ukweli; kabla ya ulichofanya.
 
Baru baru sijui labda ungepoteza muda kuangalia ni busara gani ilitumika kuyapa maeneo ya zanzibar majina.Majina yake kama mtu ni mwepesi wa kucheka basi hutoacha waudhi wale watu.Hii pi ainaambata na majina ya kipuuzi kabisa kama Duni, Ntumwa na mengineyo mnayowapa watu wenu.Sidhani kama zanzibar waanaweza weka mipaka ya mizaha.
 
ule haukuwa uandishi wa kwenye vita wala vurugu,polisi ndo walifanya shambulizi la kushtukiza kwa kupiga mabomu watu waliokuwa tayari chini ya ulinzi,marehemu aliuwawa akiwa tayari under police custody,think my friend kabla hujaudhalilisha utu wako kwa maneno yasokuwa ya kibinadam.

Halafu kwanini unachukuwa almost a week kila mara kujibu post yangu moja?Please don't be that slow,people are moving on with other issues.Respond propmptly and if not potezea maana najuwa message sent...

Nafikiri unahitaji kuuona ule mkanda mzima wa kadhia huo ambao Chadema waliutumia na kuuweka katika Mkutano wao wa dharula.

Kifupi walifuata taratibu zote ambazo Polisi anatakiwa kuzifuata katika kutawanya watu kwa mujibu wa PGO.

usikurupuke wala kuweka ushabiki kwa hili.
 
Barubaru,

..kwa hiyo unataka kusema Polisi walifuata taratibu zote ktk kumuua Daudi Mwangosi!?

..hivi ndiko unakotaka kuelekea huko?? kuwa na ubinadamu hata kidogo. suala hili linahusisha maisha ya mtu, tena mwenye watu wanaotegemea.
 
Last edited by a moderator:
Barubaru,

..kwa hiyo unataka kusema Polisi walifuata taratibu zote ktk kumuua Daudi Mwangosi!?

..hivi ndiko unakotaka kuelekea huko?? kuwa na ubinadamu hata kidogo. suala hili linahusisha maisha ya mtu, tena mwenye watu wanaotegemea.

Nilipo RED.

Ahali yangu naomba unisomevizuri sananimeandikanini siokunizulia.

Kwakukusaidia nimebainisha kwamujibu wa Videoya kadhia hiyoinaonekana wazi polisi walifuata taratibu zoten zinazowaongoza yaani PGO katika kukabilianana kadhia hiyo. Ingawa kosalinaloonekana kwamujibu wa Videohiyo ni kuwa walitumia nguvu kubwa sana kupambana na watu wasio na silaha.

Nisome vizuri unielewe na sio kusingizia.
 
Baru baru sijui labda ungepoteza muda kuangalia ni busara gani ilitumika kuyapa maeneo ya zanzibar majina.Majina yake kama mtu ni mwepesi wa kucheka basi hutoacha waudhi wale watu.Hii pi ainaambata na majina ya kipuuzi kabisa kama Duni, Ntumwa na mengineyo mnayowapa watu wenu.Sidhani kama zanzibar waanaweza weka mipaka ya mizaha.

Vipi jina kama Tundu ?
 
Back
Top Bottom