Kwanini CCM na CHADEMA tu?

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Nimekuwa nafuatilia sana habari za vyombo vya habari, mara nyingi Kurasa ikiwa na habari ya Siasa inakuwa aidha ya CCM au ya CHADEMA, hii imekaaje mbona vyama vya siasa hapa nchini vipo ishirini(20)? mbona sisikii nini vinafanya vyama vingine? sana sana utasikia chama fulani kinapinga au kinaiunga mkono hoja fulani ya CCM au CHADEMA, mimi nashindwa kujua hivi vyama havifanyi kazi au ni vyombo vya habari havitupashi habari zao? Au ni vyama vya msimu wa uchaguzi tuu?

ORODHA YA VYAMA VYA SIASA TANZANIA
Source: List of political parties in Tanzania - Wikipedia, the free encyclopedia
 
hivyo vingine vyama vya msimu wa uchaguzi - by JK not me. :biggrin1::biggrin1:
 
Sasa unashangaa nini! Majina tu ya hivyo vyama hayatamkiki kwa urahisi, ndiyo mana hata waandishi wa habari wanaachana navyo! Vitawachanganya wateja wao (Wasomaji).
 
CUF na CCM wako pamoja, si unakumbuka ile ndoa yao?

Hata kama vipo katika ndoa lazima CUF japo isikike basi kinafanya nini ndani ya ndoa, maana tunaisikia tuu CCM, kumbuka katika ndoa kila upande unawajibu wake
 
Hata kama vipo katika ndoa lazima CUF japo isikike basi kinafanya nini ndani ya ndoa, maana tunaisikia tuu CCM, kumbuka katika ndoa kila upande unawajibu wake

Kimada hatakiwi kuongea ongea!
 
Hivyo vingine ni vyama vya msimu wa uchaguzi kama alivyowahi kutanabaisha "mkuu". Chadema ndio chama pekee cha majira yote: joto, baridi, mvua, jua, masika, kiangazi. kipupwe, ukame, n.k. Ukisikia chadema inatajwa basi ni kutokana na mapenzi ya nguvu ya umma hivyo vyombo vya habari haviwezi kukaa kimya kwani hiyo kwao huwa ni habari ya kuuza. Ukisikia magamba wametajwa ujue ni kwa kuwa wameitusi cdm au kuna uongo fulani wameutoa.
 
Ndugu yangu mbona unaniangusha? We ujui kuwa ccm wajanja hivyo vyama vingne ni branches tuuu ila upinzan ni chadema ndomana unaona vpo 20 angalia vizuri inaweza kuwa si 20 bali ni 2.0
 
Hivi vyama vingine havisikiki sbb ni branch ya ccm kupunguza kura kwa wapinzani wa kweli CHADEMA
 
Chadema ndio mpinzani pekee wa CCM, CUF na wengine kazi yao kubwa ni kuunga mkono matakwa ya wakubwa zao, CCM inatekeleza ilani ya cdm for sure, from 2015 Cdm inatake over
 
Nimekuwa nafuatilia sana habari za vyombo vya habari, mara nyingi Kurasa ikiwa na habari ya Siasa inakuwa aidha ya CCM au ya CHADEMA, hii imekaaje mbona vyama vya siasa hapa nchini vipo ishirini(20)? mbona sisikii nini vinafanya vyama vingine? sana sana utasikia chama fulani kinapinga au kinaiunga mkono hoja fulani ya CCM au CHADEMA, mimi nashindwa kujua hivi vyama havifanyi kazi au ni vyombo vya habari havitupashi habari zao? Au ni vyama vya msimu wa uchaguzi tuu?

ORODHA YA VYAMA VYA SIASA TANZANIA
Source: List of political parties in Tanzania - Wikipedia, the free encyclopedia

Na vile ukiwa Zanzibar ni CCM na CUF tu
 
Duu!kama ndo hivyo ccm ana wake wengi maana vyama 18 ni wake zake isipokuwa Chadema ambacho ndo chama cha kweli cha upinzani.Cuf aliolewa na ndoa ikashuhudiwa na watanzania wote,hivyo vyama vingine vimeolewa bila kulipiwa mahari ccm kavichukua bure bure.
 
Naomba ujue kwamba Tanzania sasa demokrasia inakomaa.Mbona hushangai Marekani vyama vinavyotajwa ni Democrat na Republican tu??
Tanzania vinaweza hata kufikia vyama 50 lakini watanzania wameamua kuwa vyama viwili ndio vinara wa siasa wa nchi hii.Vingine ama ni matawi ya vyama hivi vikubwa au ni vyama vya msimu au ni vyama vya mfukoni au vyama vya makongamano na warsha au vyama vinavyojikomba kwa watawala.
 
hii ni kweli kabisa lakini kuna kachama kamoja nilikuwa na kasikia wanakiita sauti ya umma(sau)
lakini nao sasa wamelala sijui niukata au ni nini
 
Back
Top Bottom