Kwanini CCM hawataki midahalo kwenye TV kisa sio Wtz wote wana TV ila mikutano wanataka TV?

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Mara zote CCM wakati wa midaharo iwe ya Uchaguzi au mambo yoyote yahusuyo wananchi huwa wanapinga kwa herufi kubwa kuwa hawataki kusikia habari za midaharo na mbaya zaidi kurushwa moja kwa moja kwa Luninga au media mbalimbali kwa kisingizio kuwa watanzania wengi hawana tv na redio kuwasikiliza.

Najiuliza mbona kwenye mambo yao ya ajabu ajabu hasa wanapogeuka wapinzani wanataka coverage ya media kwa gharama zozote?
 
hawana ushawishi tena kwa wananchi.wanaogopa kuaibishwa na 'vichwa' vya upinzani vyenye hoja. kumbuka walipowakataza wagombea wao wote kutoshiriki midahalo! kwa ile michache waliyokuwa wameshiriki waliaibika sana....salama yao waliona waipige stop.
 
Mara zote CCM wakati wa midaharo iwe ya Uchaguzi au mambo yoyote yahusuyo wananchi huwa wanapinga kwa herufi kubwa kuwa hawataki kusikia habari za midaharo na mbaya zaidi kurushwa moja kwa moja kwa Luninga au media mbalimbali kwa kisingizio kuwa watanzania wengi hawana tv na redio kuwasikiliza.

Najiuliza mbona kwenye mambo yao ya ajabu ajabu hasa wanapogeuka wapinzani wanataka coverage ya media kwa gharama zozote?

Hii CCM naona ni kama coward boxer; anapenda aonekane akifanya mazoezi makali akiidunda punching bag mangumi mazito. Taabu akiambiwa kuingia ulingoni kupigana; kama mbwa kaona chati-visingizio elfu kidogo ili basi tuu asiingie ulingoni akaonwa mapungufu yake....
 
Wewe umeliona vizuri sana. Na hilo ndilo lililo wafanya akina kambona kukimbia. Misingi mibovu. Hata ndani ya chama wako hivyo.
 
Sasa watazungumzia nini,au watawambia wanchi wametekeleza ahadi gani? Pili kuruhusu midahalo ktk TV ni hasara maana hakuna wakuangnalia sababu haina mvuto,na inabidi kuwa na hekima ya kutosha kuongea na wanachi walio kupa ridhaa ya kuongoza dola maana nimasikini wakutupwa wanakula mlo mmoja kwa siku miaka nenda rudi wanazidi kudidimia kuichumi vile vile uwezo wa kiakili wa kujenga na kuchambua hoja na mwisho walisha katazwa na wakubwa wao kutoshiriki midahalo.
 
CCM inayoongozwa na mafisadi hawana uwezo wa kujenga hoja ndio maana hawataki midahalo. Pale jangwani walihutubia bila kuulizwa maswali.... Hicho ndicho wanachotaka; kutokuulizwa maswali maana hawana majibu yenye mashiko. Mfano waziri anayeongoza kulala bungeni, mh. wasira aliwaambia wana-CCM waliokusanywa kwa malori pale jangwani kuwa CCM imefanya kazi kubwa ya kusomesha watoto wetu... wakamshangilia. Lakini ingekuwa kwenye mdahalo angeulizwa ubora wa elimu wanayopata watoto wetu.
 
Wamezoea kuulizwa maswali waliyokwisha yapanga, wauliza maswali wao sehemu mbalimbali ni watu waliokuwapaid kufanya hivyo, maswali wanakuwa wanayajua tayari

Back
Top Bottom