Nadhani imefika wakati wa kuligawa Bunge letu katika sehemu mbili ili kuongeza ufanisi na kupunguza madhaifu yanayojitokeza kwa sasa kwani bunge moja linakuwa limeshehena kazi nyingi kupita uwezo wa mipango yake . nionavyo mimi tunaweza kuwa na mabunge mawili ambayo kila moja linaweza kuwa na wawakilishi kama 120 na kuwa na majukumu yake kuliko kuendelea kuwa na bunge moja ambalo zaidi ya asilimia 90% ya wabunge wake wanakuwa wamelala wakati miswada ikiwa inaendelea. tukiwa na mabunge mawili yenye wajumbe wachache inaweza kufanya wabunge wengi kuwa wafuatiliaji na kuongeza ufanisi na usimamizi na ata ufuatiliaji wa mikataba inayoliumiza taifa letu.