Kwanini Bunge halitaki kusomwa kwa Ripoti kamati ya bunge juu ya mgogoro wa madaktari

Na sio tu hivyo, kwa nini wabunge wa CCM wanatumia nguvu kubwa sana kuziba watu midomo kuhusu huu mgomo na hata unyama aliofanyiwa Dr Ulimboka?
 
Nafurahi kwamba wanadhani Watz ni wale wa enzi zile kudanganywa kirahisi. Ngoja uchaguzi uje wapigwe chini ndo tujue!!!!!!!!
 
HKIgangallwa njoo utupe ukweli
 
Last edited by a moderator:
Sababu wananji wanaowasupport wakijua ukweli imekula kwao.Japo bunge la leo lilikuwa vurugu tupu lakini meseji imewafikia walengwa,baada ya Mh.Mnyika kuuliza kwa nini serikali haitaki ripoti hiyo ijadiliwe.Nadhani ITV waweke kipima joto kuuliza wananchi kama wanahitaji ripoti hiyo isomwe au la,labda itasaidia Spika wetu msikivu kupata nini watanzania tunataka.Ukweli na uwazi la sivyo kama kiti kinamshinda kama mwenyekiti wa leo aseme basi nimeshindwa aondoke.
 
Nauliza kwanini au kuna nini nyuma ya ripoti hiyo?A

Inashangaza sana! Nadhani kuna mambo hawataki yajulikane lkn siku inakuja tutajua ukweli wote. Inashangaza kuona kamati imepewa kazi ya kufuatilia kuhusu ukweli wa mambo yote kwa kutumia mahela ya kodi zetu lkn report imefichwa! Bob Marley aliwahi kusema: " You can fool some people sometimes but you can't fool all the people all the time" inakera sana
 
Serikali inapokosa uhalali wa kutawala option ya mwisho huwa ni udikteta kwa sas kikwete hana jinsi ni lazima atumie hiyo silaha ya mwisho hata mimi nakubaliana naye kufanya hivyo, maana hakuna njia mbadala watu hawaitaki tena CCM na wala hawataki tena kuongozwa na CCM, HILO liko wazi.
Miaka mitatu iliyobaki ni safari ndefu sana kwao.Kashfa zinazowakabili CCM na serikali yao si mchezo mdogo haya hapa machache;
  • Mgomo wa madaktari
  • Mgomo unaonyemelea wa waalimu
  • 300BILION zilizoko Uswizi za wanasiasa(wanaccm)
  • Meli ya Iran inayofanya biashara ya mafuta kwa kutumia bendera ya Tanzania
  • Uchaguzi uliojaa ubabe na rushwa wa ccm ngazi ya tawi na taifa
  • Wimbi la kuhama wana ccm kwenda M4C direction
Haya machache tu lazima yanaumiza ubongo na kumfanya mtu mzima kuchanganyikiwa
 
Hiyo ni sawa na kumwambia JK aunde TUME HURU kuchunguza utekaji na uteswaji wa Dr. Ulimboka. In a nutshell is like asking them (CCM) to shoot on their foot!
 
Usijisumbue sana, ni kawaida ya Serikali ya Tz; haiwezi kutoa taarifa kwa uchunguzi wowote uliofanywa na tume au kamati zake pindi inapojua kuwa imehusika kufanya madudu hayo. Jiulize iko wapi taarifa ya uchunguzi wa moto uliouwa binti zetu kule Shauritanga? Iko wapi taarifa ya Meremeta? Iko wapi taarifa ya kifo cha Mwaikusa?

Usitegemee hii taarifa kujadiliwa bungeni; kwani Serikali ilituma kamati hii kama kiini macho kwa umma kwa kuwa wanajua wo ni wahusika wakuu wa mgogoro huu. Bahati yao wamejipanga vema; m/kiti wa kamati hii ni Mrs M. Sitta; kama mumewe alivyozima mjadala wa Richmond na kuzawadiwa uwaziri ndivyo afanyavyo. Na kwa bunge hili la Makinda na wadogo zake, Ndungai,,na J.Mhagama. Pembeni wakiwepo kaka yao wa Isimani (Lukuvi) hakuna kutoka kwa taarifa hii. We angalia style iliyopo. Makinda alisema hakuna kujadili suala la mgomo wala kusoma taarifa ya kamati kwa kuwa suala liko mahakamani. Wenye ufahamu tukajua hii zengwe jingine. Kamati ilionana na madaktari wakati awamu ya kwanza ya mgomo. Mahakama imeingizwa hivi juzi; kuna uhusiano gani? Why kamati haikupewa fursa kuwasilisha taarifa yao before mgomo huu kuanza au kupelekwa mahakamani?
Kituko cha pili; mahakama inalalamika kuingiliwa (kwa mujibu wa maelezo ya Makinda) pale tu Mnyika anapoomba spika kuruhusu kuwasilishwa kwa taarifa hiyo bungeni. Lakini aliyehongwa ukuu wa mkoa kwa kuwasaliti waTz (Stella Manyanya) (si ndivyo alivyodai kaka yake Mwakyembe kuwa walificha mengi ili kuokoa serikali ya Jk??) akiongea bungeni ni OK. HAPA UHURU WA MAHAKAMA HAUINGILIWI! "CHEMBA" likifunuka na kutapika , mahakamani haiguswi!


Tusidanganyane taarifa hiyo haitasomwa hadi kiama. Na ikifika mahali ikaletwa basi "itaficha mengi ili kuokoa serikali yao"

EJL
 
Unaambiwa kifo hicho kwenye kona kinakuja kukuchukua wakati unapasua mikuku ya ukweli utaacha kuchanganyikiwa
 
Back
Top Bottom