ney kaaya
JF-Expert Member
- Jun 27, 2016
- 447
- 352
acha kuangaika utatangatanga hadi lini Imani ya kweli ni kumwamini YESU KRISTO KUWA ALIKUFA NA AKAFUFUKA BASI HAKUNA IMANI NYINGINE.ibrahimu alihesabiwa haki mbele za Mungu kwa imani ya kumwamini Kristo na ndio imani itupasayo kuiamini na wala sio dini.Katika maisha mkuu lazima tuwe open minded. Akili yetu iwe huru kufikiri. Kila tunaposoma na kujifunza turuhusu challenges na elimu mpya. Tuzisome kwa moyo wa kuelewa na nia. Then tukishasoma tunatumia akili zetu binafsi kuchambua na kuangalia facts zinavyosema. Yaani kwa maana kuwa tusi-settle katika elimu na kuridhika.
Ukiwa mtu wa namna hiyo utajikuta unasoma mengi na kuanza ku connects dots na unaelewa vitu katika ufahamu mbalimbali. Mfano mkristu anayeamini biblia tu na hajasoma vingine atatofautiana na mkristu anayeamini biblia na amesoma vingine. Elimu inamfanya mtu anakuwa juu na anaiona vizuri view ya chini. Sawa na ukiwa keleleni unaona bonde vizuri.
The more unavyojifunza vingi, the more unavyoona uhalisia vizuri.
Hata yule ambaye amebahatika akazaliwa na baba mwenye hekima na akafundishwa elimu ya kweli bado anatakiwa asome na elimu za uongo na atambue fahamu zilizopo ili ajue thamani ya ile elimu ya kweli. Pia atajua kujadiliana na watu kwa sababu anajua fahamu zao.
Hata mimi ambaye bado najifunza, hivi sasa bado kuna imani ambayo naona ina ukweli fulani kwa kiasi kikubwa. Na nikiona kuna nyingine inaizidi imani niliyonayo na ina ushahidi, nami nitaifuata na kuzidi kujifunza.