Kwanini Biblia imeandikwa kwa lugha ngumu?

moto wa maji

JF-Expert Member
Mar 25, 2016
4,080
2,884
Habari wakuu,

Je, ni kwanini biblia imeandikwa kwa lugha ngumu hadi inapelekea watu wasiielewe na kufanya kila mmoja anakua na tafsiri yake?

Na kwanini wachungaji waliosoma theologia huwa wanaenda Kenya kupunguza au kuongeza maneno kwenye biblia? Na je hayo mamlaka wamepewa na nani?

Naomba tujuzane.
 
habari wakuu
Je ni kwanini biblia imeandikwa kwa lugha ngumu hadi inapelekea watu wasiielewe na kufanya kila mmoja anakua na tafsiri yake? na kwanini wachungaji waliosoma theologia huwa wanaenda kenya kupunguza au kuongeza maneno kwenye biblia? na je hayo mamlaka wamepewa na nani? naomba tujuzane
Kwa sababu inataka kutetea kitu kisichokuwepo. Mungu.

Unapotetea uongo kuna kanuni za obfuscation (kufichaficha vitu kwa kutokuwa clear) inabidi utumie.

Kwa mfano. Biblia imetuambia jino kwa jino. Biblia hiyo hiyo imetuambia mtu akikupiga kofi shavu moja, mpe na jingine. Biblia hiyo hiyo imetuambia kila neno la mungu ni zuri kwa mafundisho.

Sasa hapo mtu akinipiga nifuate lipi?

Jino kwa jino au nimpe shavu jingine?

Na kwa nini kitabu cha Mungu kiwe na utatanishi hivi?

Jibu langu naona ni kwa sababu hiki kitabu si cha mungu, ni cha watu tu. Mungu hayupo kwa sababu dhana ya mungu kuwapo inajikanganya kama pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika Euclidian geometry.
 
asante kwa jibu lako mkuu
 
ukisoma kwa umakini unaona kabisa Mungu wa Agano la kale ni tofauti kabisa na Mungu wa Agano jipya, kana kwamba ni miungu wawili tofauti.

Mungu wa Agano la kale aliwatuma nyoka wakawaume wana wa israel waliozungumza vibaya kuhusu musa na mungu.. halafu hapohapo mungu akamwambia Musa "Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi." ... kana kwamba anataka kuonesha uwezo wake, kwa kizungu wanasema mungu ana SHOW-OFF.

kwanza kabisa mungu aliua, hii kwenye amri kumi zake ni dhambi.

pili, Musa akamtumia nyoka kuwaponya wana wa israel walioumwa na nyoka. lakini tunaambiwa kuabudu nyoka ni ushirikina.

tatu, Mungu anasema akupigae shavu la kushoto mgeuzie la kulia.. sasa mungu mbona alishindwa kuwageuzia shavu la kulia wana wa israel waliomkufuru? na badala yake aliwatumia nyoka wenye sumu kali wawaume na kuwaua wana wa israel?

na kama kwa matendo yake ya agano la kale mungu aliona anakosea na kuona kwenye agano jipya ajirudi na kuwa mwenye huruma, huoni kama huo kwake tayari ni udhaifu na mungu anakua sio mkamilifu kama sisi binadamu, yani kwa kizungu unaweza kusema mungu anahitaji ANGER MANAGEMENT.

tano mungu anasema yeye ni mungu mwenye wivu, na kwenye biblia hio hio inasema wivu ni mzizi wa dhambi..

inakuaje tena dhambi hiohio aliyoikataza mungu, yeye mwenyewe anaifanya? kana kwamba akifanya yeye ni halali, tukifanya sisi tunakwenda motoni..!!

biblia inajichanganya mno, na kutokana na mchanganyo huu wakristo wengi wameona bora wajikite kwenye maandiko yanayowapendeza wao, na sio yale maandiko yaliyokaa kishetani shetani kama musa na nyoka wa shaba, mungu kuua watu nakadhalika.. lakini kumbuka biblia hiohio takatifu ndo imeandika maandiko hayo unayoita ya kishetani, kupitia roho mtakatifu kama wanavyosema.
 
habari wakuu
Je ni kwanini biblia imeandikwa kwa lugha ngumu hadi inapelekea watu wasiielewe na kufanya kila mmoja anakua na tafsiri yake? na kwanini wachungaji waliosoma theologia huwa wanaenda kenya kupunguza au kuongeza maneno kwenye biblia? na je hayo mamlaka wamepewa na nani? naomba tujuzane
ndio ujue hicho si kitabu chenye maneno ya MUNGU, hao wanaoenda kupunguza au kuongeza neno wamepewa mamlaka hayo na nani.....? je wanaushirika na MUNGU.....?wapi waliongea naye akawatuma warekebishe neno.......?ndo maana bw YESU alisema TUSIPOWASHINDA WAANDISHI NA MAFARISAYO KATU UFALME WA MBINGU NI NDOTO, tafuta mwenyewe Mafarisayo ni kina nani, na waandishi ni kina nani.
 
i think ni kwa sababu imetafsiliwa toka lugha zingine, wale watafsiri may be hawapo poa kwenye kiswahili, like you said wanaenda kenya. huo ndo mtazamo wangu, huyo Kiranga asiwapotoshe. imeandikwa siku za mwisho........
Asante mkuu, ila kama umewahi kusoma biblia ya kiingereza ina maneno magumu
na ugumu nnao uzungumzia ni pale sehem nyngn inakinzana na nyngne
 
Lugha inakua kadri jamii inavyobadilika. Kiingereza kwa mfano kilichotumika karne ya 8 si kinachotumika leo. Halikadhalika Kiswahili, mf. jaribu kukitafuta kitabu alichoandika Shaaban Robert ukisome leo hakika katika kila aya moja utapata maneno zaidi ya kumi usiyoyaelewa achilia mbali miundo ya kisarufi. Lugha waliyotumia kina Rebman kutafsiri biblia karne ya17 haiwezi kuwa nyepesi leo.
 
Asante mkuu, ila kama umewahi kusoma biblia ya kiingereza ina maneno magumu
na ugumu nnao uzungumzia ni pale sehem nyngn inakinzana na nyngne
mkuu kama unazungumzia ya kiingeleza, siwez sema chochote sababu sijui how good you are in that language. lakini pia hata kama unajua vizuri kiingereza lazima kuna maneno unaweza usiyaelewe. na ndo maana kuna kamusi za kiingereza kwa kiingereza. na kuhusu kukinzana inategemeana umesomaje, mwingine anaweza soma mstari mmoja tu aka-conlude, bila kuangalia mwanzo mpaka mwisho wa habari husika.
 
Kwa sababu inataka kutetea kitu kisichokuwepo. Mungu.

Unapotetea uongo kuna kanuni za obfuscation (kufichaficha vitu kwa kutokuwa clear) inabidi utumie.

Kwa mfano. Biblia imetuambia jino kwa jino. Biblia hiyo hiyo imetuambia mtu akikupiga kofi shavu moja, mpe na jingine. Biblia hiyo hiyo imetuambia kila neno la mungu ni zuri kwa mafundisho.

Sasa hapo mtu akinipiga nifuate lipi?

Jino kwa jino au nimpe shavu jingine?

Na kwa nini kitabu cha Mungu kiwe na utatanishi hivi?

Jibu langu naona ni kwa sababu hiki kitabu si cha mungu, ni cha watu tu. Mungu hayupo kwa sababu dhana ya mungu kuwapo inajikanganya kama pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika Euclidian geometry.
Wewe ulipogundua kuwa biblia ina mapungufu hivyo si kitabu cha mungu,je ni hoja zipi zilizokufanya ukawa mpinga uwepo wa mungu? Maana biblia kuwa sio kitabu cha mungu ni jambo moja na kuwa hakuna mungu ni jambo lengine kabisa.

Kumbuka wapo wanaoamini mungu ila hawaamini vitabu vya dini.
 
Mungu yupi?
 
habari wakuu
Je ni kwanini biblia imeandikwa kwa lugha ngumu hadi inapelekea watu wasiielewe na kufanya kila mmoja anakua na tafsiri yake? na kwanini wachungaji waliosoma theologia huwa wanaenda kenya kupunguza au kuongeza maneno kwenye biblia? na je hayo mamlaka wamepewa na nani? naomba tujuzane
Decoding machine ya Biblia ni Roho Mtakatifu, unaposema imeandikwa kwa lugha ngumu ni kwasababu unatumia LOGIC ya kibinadamu kuelewa LOGIC ya Mungu. Hapo lazima utoke kapa.

Iko simple sana, Yesu alisema alinampasa Yeye kuondoka ili msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu, Roho Wa Mungu apate kuja na kutusaidia katika kuelewa njia za Mungu.

Kuwa na mahusiano mazuri na Roho Mtakatifu katika maisha yako afu njoo utupe majibu kama kweli Biblia ni ngumu.
 
kumbuka nilikuwa namjibu mtoa maada, ndo lilikuwa lengo langu kuu. hata kama ulikuwa involved bro, sorry
Umeninukuu mimi. Umetumia maneno yangu.

Kwa nini unalianzisha na mimi, halafu nikikuhoji unakimbia?

Kwa nini umesema uongo kwamba nimepotosha bila hata kuweza kutetea kauli hiyo?

Usianzishe malumbano ambayo huyawezi.
 
Back
Top Bottom