Kwanini Balali hakuzikwa Tanzania?

Status
Not open for further replies.
Inawezekana Kama kweli amekufa alikuwa ameukana uraia wa Tanzania. Pili labda aliacha wosia kwamba akifa asizikwe Tanzania ni mambo binafsi. Alikaa huko USA kwa miaka mingi na alikuwa na nyumba yake huko. Tumwache apumzike. Tupambane na Ndullu afanye kazi kwa tija yaliyopita SI ndwele tugange yajayo!:A S 465:

Indeed!!!.. Tumuache apumzike... aendelee kula bata mwanawane!!!!
 
Nadhani jibu ni rahisi kwasababu swali lenyewe ni jepesi pia. Hakuzikwa Tz kwasababu BALALI hajafa yuko hai anakula bata tu!! Waliamua kumzushia kifo ili kuficha siri kubwa aliyokuwa nayo juu ya vigogo wa tz ambao alikuwa anakula nao na kuamua asirudi tena bongo. Kwanza familia yake iko wapi? Kumbuka yule jamaa wa Dar alopigwa risasi getini kwake UDSM baada ya kutoa siri kuwa amemwona Balali katika nchi moja.
 
Katika waraka wa kwanza kabisa wa slaa kufichua mafisadi hata kabla ya mkutano wake wa kidongo chekundu..alisema na kuthibitisha kua Balali alikua na mipango ya kuhamia eidha katika visiwa vya Malta ama monaco ambako alikua anamiliki majumba ya kifahari pamoja na washington..ambako alikua anatafuta urahisi wa (endapo angetafutwa na serikali) kidiplomasia..
 
Kijana acha kumchulia kifo mzee mwenzangu. Balali yupo na anaendelea kula kuku tu. Kuna wakati niliwahi kuzungumza na afisa mmoja wa ubalozi wa US hapa Tanzania aliwahi kunidokeza hako kasiri. Lakini lengo lake sio baya sana. Kwani D.Balali si raia wa Tanzania mlimpa u gavana kwa ujinga wetu tu. Ndo shida ya viongozi vichwa nazi.
 
mbona wewe hujazikwa?
mwacheni ale alichochuma kwa jasho lake.
kama mnaona wivu pelekeni cv zenu bot na nyie mle,ujanja kuwahi.
nchi haina mwenyewe halafu mnalalamika badala ya kuchukua chenu mapema?
aliyekuwa anaweka kauzibe alishatangulia mbele ya haki,hamjaona kila mtu anakula kwa nafasi yake?
hamkuwasikia wajasiriamali huko nzega wakiivamia ndege ya madini?au mlifikiri ni nini?wenye madini walikuwa mamepiga dili,wale wajasiria nao walitaka kuwawahi ila polisi kwa kupenda sifa badala ya kuzuia wapiga dili wa kwanza wakaamua kuwabana wapiga dili wazalendo.
kalaghabaho.
 
Mimi nilishangaa sana alipokuja jamaa yangu kutoka USA na kuniambia mmepigwa changa la macho na Serikali kuambiwa Balal kafa na mkakubali siri ikapotea kirahisi kabisa. Wakaamua kumtoa kafara ndogo ya kwenda jela jamaa yetu mambo yakaishilia mbali wahusika wakuu wakiendelea kupeta. Kosa walilofanya walishindwa kutengeneza picha ya vidio ya uongo ya kuthibitisa kifo na mazishi kwa ushahidi, wengi tungeamini tu.
 
Ningependa siku moja kabal mwenyezimungu hajanihitaji nirejee nilikotoka, nimuone kiongozi jasiri ktk nch hii akayafunua haya yoote na kuanika ukweli hadharani!

Kweli kama kweli Balal hajafa ,kasingiziwa tu kifo basi hapa viongozi wetu wamemdhihaki sana mwenyezi mungu. Mungu baba hana budi kuwaadhibu kwa hii dhambi.
 
mkuu unamaanisha prof juan mwaikusa??
Nadhani jibu ni rahisi kwasababu swali lenyewe ni jepesi pia. Hakuzikwa Tz kwasababu BALALI hajafa yuko hai anakula bata tu!! Waliamua kumzushia kifo ili kuficha siri kubwa aliyokuwa nayo juu ya vigogo wa tz ambao alikuwa anakula nao na kuamua asirudi tena bongo. Kwanza familia yake iko wapi? Kumbuka yule jamaa wa Dar alopigwa risasi getini kwake UDSM baada ya kutoa siri kuwa amemwona Balali katika nchi moja.
 
acha kutushusha hadhi wana jf. unapokubali kuingia mkenge ktk maigizo ya ccm na jk basi unaonyesha jinsi ulivyo mdhaifu . sisi waelewa tunajua balali yuko hai na anaendelea kula kuku kwa mrija. ila ccm inajua kuwa mchezo wake wa kuwadanganya wadanganyika umefanikiwa [ loo samahaan ni watanganyika]. ngoja ccm iondoke madarakan alaf chadema wakichukua nchi uone jinsi atakavyo letwa mbele ya mahakama. sijui mtasema amefufuka au?
 
aliyekufa ndo huzikwa,kama hajafa hawezi zikwa,so kama hajazikwa,atakuwa hajafa
 
Kwani kunatofauti ya anaye zikiwa marekani na tanzania.Kama ipo labda walifikiria hilo.Kuhusu pesa ondoa
 
Inawezekana Kama kweli amekufa alikuwa ameukana uraia wa Tanzania. Pili labda aliacha wosia kwamba akifa asizikwe Tanzania ni mambo binafsi. Alikaa huko USA kwa miaka mingi na alikuwa na nyumba yake huko. Tumwache apumzike. Tupambane na Ndullu afanye kazi kwa tija yaliyopita SI ndwele tugange yajayo!:A S 465:

Huu ndio ujinga tunaorithi kwa babu zetu. Eti aliyetuibia tuachane naye tumpe na mwingine aibe. Hayo yooote uliyoyasema hayakumzuia mpenda misiba kwenda huko. Mimi naamini angetia maguu kwa mambo mawili:
1. Kupenda safari: kwa hiyo juu chini angekwenda kuhudhuria huu wa marekani
2. Kupenda kutokea gazetini na maneno haya :Mh. Dokta akiongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Sasa kama wewe ni mmoja wa wanakamati ya kutupiga changa la macho kaa kimya. Sisi hatuamini kuwa JK msiba unaweza kumpita. Kama wakifa waaandishi wa habari tu lzm atie mguu akapige msosi wa msibani itakuwa zulumati mwenzao?
 
Jamani si kuwa naota..Ninajaribu kukumbukia Serikali yetu ya Tanzania na upana wa maamuzi yake..Tulikuwa na Gavana wa BOT na alikuwambwa na Kashfa Lukuki mpaka Macho yoote ya watanzania yakaganda kwenye Sakata Hilo.

Sasa Huyu jamaa alikufa, Nini kilisababisha Maiti isije Tanzania kwa mazishi na uhakika wa kifo Cha mtu huyu???

Serikali kutokuwa na Maamuzi mapana kuhusu sakata la BOT ilikuwa inakusudia nini??

Nimewaza nikatoka na Hili hebu tuuchambue kidogo huu uongozi tulio nao na upana wa maamuzi yake...

Haya njooni tusemezane Asema Bwana.

Waulize watu wa usalama wa Taifa kama kweli balali alikufa au lah!!! inasemekana amewekwa kisiwa fulani kwenye bonge la Makazi amalizie maisha yake humo huku akiendelea kukaa na siri za mauaji makubwa ya Taifa letu Kwa maslahi ya watu wasiozidi hata 100. Ipo siku nitajichukulia sheria mikononi walah tena
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom