Ozzanne Issakwisa
JF-Expert Member
- Mar 7, 2016
- 288
- 239
Utolewaji wa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi, sio kitu rahisi.
Nilikuwa nasoma gazeti la Jamhuri, nikashangaa kuona BAKWATA ni kati ya taasisi ambazo zina kibali cha kuagiza sukari toka nje ya nchi. Na kwamba wana kibali cha kuagiza tani 2,500/=. Nikajiuliza hii sukari wanayoagiza ni kwa ajili ya uji wa watoto katika vituo vya watoto yatima? Au kuna watu wanatumia taasisi kujinufaisha na kuichafua taasisi?
Source: Tunazuia Sukari Kutoka Nje Kwa Maslahi Ya Nani? | Gazeti La Jamhuri

Labda ni vizuri tukajua ni kina nani hawa waliokuwa wakipewa hivi vibali maalumu vya kuagiza sukari. Nao ni wafuatao: Tanzania Commodities Trading Co. LTD (tani 26), TPM LTD (tani 12), Matunda B.C. LTD (tani 12), East Coast Oils and Fats Ltd (tani 1,292) na New Tradeco Investment Ltd.
Wengine ni, Mohamed Enterprises (T) LTD (tani 8), Decent Investment Ltd (2,116), Rubab Investment Ltd (tani 12), Multi Modal Transport Africa (tani 2), Trade Logistics (EA) Ltd (tani 12), Ngawaiya Stores (tani 100), DRTC Trading Company Ltd (tani 2,522) na Market Makers (T) Ltd (tani 480).
Wengine ni Supermarket (tani 910), Power Roads (tani 1,170), A. O. K. Investment (tani 500), B. F. K. Company Ltd (tani 500), Kigwaza Holdings (tani 500), Sofia International (tani 500), Conti Africa Ltd (tani 260), Masooma Supermarket (tani 208), BAKWATA (tani 2,500), Saddique Supper Service Station (tani 1,700) OLAM Tanzania Ltd (tani 832), United Youth Shipping Co. Ltd (tani 494) na EDISABA General Supplies Ltd (tani 1,000).
Inawezekana wengi kati ya hawa ni wafanyabiashara wa sukari, isipokuwa Bakwata. Mimi sina hakika kama wao pia wanafanya biashara ya kuagiza na kuuza sukari. Labda wahusika watatueleza.
Source: Tunazuia Sukari Kutoka Nje Kwa Maslahi Ya Nani? | Gazeti La Jamhuri