tetesi: rais kikwete amewapa maagizo wanajeshi kuingilia shell binafsi kuzikagua na kuwalazimisha na ikibidi MPs wa jeshi wauze kwa nguvu
note:bado sijaweza kuzithibitisha habari hizi
serikali ikiamua kukaa pembeni kutakuwa na athari gani? Maana bei ikipanda sana watu hawatanunua! Hapa ndio suala la UDA linapokuja!!
Yesu Wangu!
Hii ibaki kuwa rumour kwa sababu itakuwa ni kosa kubwa sana mbele ya dunia.
Chonde, chonde, chonde! Kama serikali inataka kuingilia kati, basi iwe ni kuiamuru EWURA iondoe agizo la bei hii ya 2,004/=. Warudishe ile bei ya 2,090/=, ambayo ndiyo bei itayowawezesha hawa wa mafuta kupata faida waliotarajia.
Kisheria, haya mafuta ni ya hao wafanya biashara pamoja na principals wengine kama mabenki yaliyowakopa kuagizia mafuta. Hauwezi ukawalazimisha wayauze, lakini unaweza ukaweka mazingira yatayowafanya wasione faida ya kuyauza kama walivyofanya EWURA na hili agizo lao la 2,004/=.

Sema kwa vile serikali yenyewe ni legelege lakini serikali makini haiwezi kurudia matapishi yake maana ni kujinyonga yenyewe, haitakaa isikilizwe tena na hawa wafanyabiashara.
Viko wapi vyombo vya dola, usalama wa Taifa uko mashakani ili hali taasisi tuloijua miaka ile imelala.
Leo wamegoma kuwauzia wananchi mafuta vipi kesho tukiwa vitani wakagoma ku-supply mafuta itakuwaje??
naona jinsi gap kati ya walionavyo na wasionavyo linavyowapofusha watawala ..kwanini hawakuboresha uda? Kwani watu wote dar wanahitaji kuwa na magari na pikipiki?
lakini tambua kitendo cha wenye mafuta kukataa kushusha bei si cha kizalendo kwani wakati serikali haijashusha kodi wao walikuwa wanauza sh 2090 lakini serikali wameshusha kodi na tozo kwa zaidi ya sh 150 sasa kwanini wao wasishuke japo kidogo ili tuone kuwa nao ni wazalendo badala ya kusimama kwenye vyombo vya habari na kuipa serikali masaa 24
hii si sahihi na kama tuna rais basi na tuone nguvu zake sasa na ata ikibidi kujiingiza kwenye biashara ya mafuta na sasa iingie

tetesi: rais kikwete amewapa maagizo wanajeshi kuingilia shell binafsi kuzikagua na kuwalazimisha na ikibidi MPs wa jeshi wauze kwa nguvu

note:bado sijaweza kuzithibitisha habari hizi

Kwani tangu watangaze kuondoa 150, na leo, zimepita siku ngapi? Jee Shilingi imeanguka kwa kiasi gani katika kipindi hicho?
Je, unafikiri kuwa hawa wa mafuta wanapata faida gani kugomea kuuza mafuta kwa wiki nzima? Au ni ule mtazamo wa kuwa bepari yoyote ni mbaya, anapenda kutesa watu, anakula watoto kwa breakfast na anayonya
watu damu?
serikali ikiamua kukaa pembeni kutakuwa na athari gani? Maana bei ikipanda sana watu hawatanunua! Hapa ndio suala la UDA linapokuja!!
Tofautisha kati ya serikali per se na EWURA.
Serikali (Wizara) inaweza kabisa ikaiagiza EWURA, ambayo ni Executive Arm yake, kubadilisha determination yake bila ya kuonekana kuwa imekula matapishi yake.
Kiongozi unakuwa kama si mwenye kufuatilia mambo.
Katibu mkuu wa wizara alifanya kikao na hao wafanyabiashara na akasisitiza msimamo wa serikali, sasa sijui unataka serikali ipi hapo.
Mwanakijiji tupeleke taratibu, unatembea na agenda nyingi sana at pa.Kwanini hawakuboresha UDA? kwani watu wote DAR wanahitaji kuwa na magari na pikipiki?
kanuni ya demand na supply inafanya kazi kwenye free market lakini kilichotokea katika soko la mafuta ni wafanyabiashara wameunda catel yani ushirika wa kudhibiti bei na sheria za tume ya ushindani inaipa nguvu serikali kuingilia inapoamini kuna nanma yeyote ya umoja wa wafanyabiashara kudhibiti bei
katika suala la upungufu wa mafuta linatokana na sababu mbili kubwa sasa.
1. kiburi cha wafanyabiashara dhidi ya serikali kwani wanaamini kuwa serikali lazima isalimu amri na haina nguvu na uwezo wa kuwadhibiti
2.kutokana na kushuka kwa bei watumiaji wengi hawaamini kuwa bei itaendelea kubaki chini na wanadhani kuwa ni wakati mfupi tu itabaki kwenye bei hii na ndio maana wamenunua na kuweka stock yao kwa siku za karibuni kwa niliweza kuzungumza na mkandarasi wa barabara anayetarajia kufanya kazi zake muda wa karibuni yeye ameweza kununua zaidi ya lita 700,000 za diesel na kuziweka akiba kwa ajili ya mitambo yake ili pia linaongeza upungufu wa mafuta
imefika wakati ambao serikali haiwezi kukwepa kuunda mfumo wa upatikanaji wa mafuta wa uhakika kwani katika nchi ambayo umeme ni shida na mafuta nayo yakiwa shida basi lazima ife
serikali lazima ifikirie kufufua kiwanda cha kusafisha mafuta cha tipper ili kupunguza bei za mafuta na kuongeza ajira kwa vijana wetu la sivyo haitaweza kusalimika kutoka katika janga la mfumuko wa bei na usalama wake yenyewe