Kwani ni lazima? au...

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Wanandoa wameoana na wamefanikiwa kuwa na watoto wote wa kiume ama watoto wote wa kike. Inatokea kwamba wanandoa kuona familia yao hajakamilika pasipokuwa na watoto wa jinsia tofauti yaani wa kike na wa kiume. Na huendelea kuzaa pasipo mafanikio na kujikuta na lundo la watoto na wanazidiwa uwezo wa kuwatunza. SWALI: Je ni lazima kuwa na watoto wa jinsia tofauti kwenye familia? ama si lazima?
 
Si lazima, ingawa familia nyingine zinaona kama hazijakamilika kuwa na watoto wa jinsia moja.
Pia hii kasumba ya kutaka kulazimisha kupata mtoto wa jinsia tofauti inasababisha kuwa na watoto wengi tofauti na mipango ya wanafamilia. Kuna mfano wa dada yangu ambaye baada ya kuolewa walipanga kuzaa watoto wawili tu lakini kutokana na kuzaa watoto wa kiume tu waliendelea kuzaa ili wapate mtoto wa kike. Mungu si Athmani uzao wao wa sita wamefanikiwa kupata mtoto wa kike. Sasa unaona madhara wao walikuwa hawajapanga kuwa na watoto sita lakini kwa kuwa walikuwa wanataka mtoto wa kike walijiona kama hawajakamilika!
Lakini si lazima familia kuwa na watoto wa jinsia zote!!!
 
Wanandoa wameoana na wamefanikiwa kuwa na watoto wote wa kiume ama watoto wote wa kike. Inatokea kwamba wanandoa kuona familia yao hajakamilika pasipokuwa na watoto wa jinsia tofauti yaani wa kike na wa kiume. Na huendelea kuzaa pasipo mafanikio na kujikuta na lundo la watoto na wanazidiwa uwezo wa kuwatunza. SWALI: Je ni lazima kuwa na watoto wa jinsia tofauti kwenye familia? ama si lazima?
Si lazima.Watoto ni majaliwa ya Mungu
 
Hii inawasumbua wengi jamani yaani mkiwa na wa kike baba haridhiki anataka mpate japo wa kiume au mkiwa na wa kiume mama haridhiki anataka japo apate 1 wa kike duh tutafika kweli
 
Its a good idea to have your ideal family, but dont get all broken if its otherwise....
 
Hii inawasumbua wengi jamani yaani mkiwa na wa kike baba haridhiki anataka mpate japo wa kiume au mkiwa na wa kiume mama haridhiki anataka japo apate 1 wa kike duh tutafika kweli
Wengine na familia nazo zinachangia, kwa mfano baba katoka katika familia ambayo ina watoto wa kiume tu either atapendelea kupata mtoto wa kike au wa kiume, na inavyokuwa tofauti na matarajio yake ndio matatizo yanaanza.
 
kwenye kadamnasi unaweza ukasema mtoto ni mtoto,lakini deep down unakuwa unapenda upate watoto wa jinsia tofauti
 
Nakumbuka kuna jamaa yangu mmoja alikuwa anajigamba bado kuna dume la ng'ombe linakuja kama bile ana makubaliano na muumba baada ya kupata wa kike wawili. Mimba iliyofuata akadai akipata wa kiume basi ndiyo kamaliza kazi akawa wa kike mwingine. Akaendelea kujaribisha dume la ng'ombe, kuja kushtuka ana mabinti sita.
 
kwenye kadamnasi unaweza ukasema mtoto ni mtoto,lakini deep down unakuwa unapenda upate watoto wa jinsia tofauti

Siyo uwongo lakini ukikumbuka kwamba huna makubaliano na muumba basi unakubali majaliwa yenu maana kuna wengine hata mtoto mmoja tu wa dawa wanahangaika huku na kule hawampati.
 
kwenye kadamnasi unaweza ukasema mtoto ni mtoto,lakini deep down unakuwa unapenda upate watoto wa jinsia tofauti

Sasa ukiendeleza utafutaji wa mtoto wa jinsia unayoipenda na inazidi kushindikana utafika mahala yaani una timu ya futiboli au netiboli hapo sasa mambo ya kulea
 
Nakumbuka kuna jamaa yangu mmoja alikuwa anajigamba bado kuna dume la ng'ombe linakuja kama bile ana makubaliano na muumba baada ya kupata wa kike wawili. Mimba iliyofuata akadai akipata wa kiume basi ndiyo kamaliza kazi akawa wa kike mwingine. Akaendelea kujaribisha dume la ng'ombe, kuja kushtuka ana mabinti sita.

Alikuwa anazalisha NGO'MBE?
 
mkabidh allah haja ya moyo wako naye atakupa hitaji la moyo wake ili jina lake liinuliwe!!
 
Back
Top Bottom