Kwani ni kosa kumsimulia mume/mkeo juu ya mpenzi wako wa zamani?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Kuna mambo huwa yanashangaza na pengine kuchekesha, ni kisa cha
huyu Jirani yangu.
Kila siku amekuwa akimsimulia mkewe juu ya wapenzi wake wa zamani
hasa pale anapowaona akiwa na mkewe, atamweleza tu "ah! yule nimetembea naye, lakini
hivi na vile......" ni kitu ambacho amekuwa akipenda kusimulia. Lakini mwanamke
hajaonyesha kukerwa na simulizi hizo badala yake amekuwa akicheka.

Jioni ya juzi J'tano, wakakutana na Lori ambalo lilikuwa linaendeshwa na
jamaa mmoja ambaye alileta Mzigo pale Buguruni Sokoni, huyo dereva
ni mwembamba, mweusi mfupi.
Mwnamke akaanza kumzungumzia akifikiri kuwa litakuwa jambo la kawaida
kwa mumewe.
"Mume wangu, yule jamaa nimewahi kutembea naye mwaka juzi, usimuone
vile na wembamba na ufupi wake yaani ana****** kubwa mpaka nilikimbia
gesti yaani siwezi kumsahau yule baba." Ile simulizi ilimchukiza mumewe
na hivi ninavyozungumza leo saa 10 Alfajir yule mwanamke ameachwa kisa
ni hiyo simulizi tu!
Jamani kwani ni kosa kusimulia mambo yaliyopita?
 
Tit for tat is a fair game lakini ku*ya anye kuku ila aki*ya bata kaharisha ..nijuavyo mie mwanzoni mwa mahusiano ndio wakati muafaka kuelezana kuhusu mambo mliyopitia kabla ya kuwa pamoja..sasa hiyo ya kuhadithiana kila siku au kila mnapokutana na maex wenu to me it doesn't make sense..
 
Ni upuuzi sana kuongelea mahusiano ya nyuma na especially kama mmeshakubaliana kuwa katika uhusiano wenye mwelekeo wa maana. Ingawa wanaume huwa tunajifanya vinara wa kusimulia na kudai kuelezwa mahusiano ya wenzi wetu, ukweli ni kwamba huwa hatuna kifua cha kumeza yale tunaoelezwa.

Kuna mambo niliwahi kumuuliza Bibi au kumweleza wakati tunashawishiana, hadi sasa najiona mjinga. Kama ningepewa nafasi ya kuanza upya, hakika nisingefanya makosa hayo ya kiufundi.

Kwa hiki kisa, mwanamume kalianzisha na kwa hiyo hana sababu ya kumuadhibu mkewe!!

Babu DC!!
 
Hapo kwenye red nakupa 100% yaani sijui inakuwaje huwa tunataka kujua
sana walikopita n.k lakini ukishajua tu ndo GUBU linaanzia hapo.
 
Hapo kwenye red nakupa 100% yaani sijui inakuwaje huwa tunataka kujua
sana walikopita n.k lakini ukishajua tu ndo GUBU linaanzia hapo.

...If you want my future, forget my past... nimekakumbuka kakipande ka wimbo huu wa miaka ya 90s. Kwakweli hata mimi sijui kwanini tunahadithiana past; zinasababisha unnecessary insecurities. Zenye children involvement sawa, lakini zile ambazo hazileta matunda ya kuonekana; ni uncalled for.
 
U can't change the past,na pia jana imepita yanini uilete leo?
 
Kosa kubwa kama hujaulizwa swali na mke wako kuongelea mambo yalio pita, if you are asked about past relationships, then you have an obligation to be honest..Mimi naona huyo mwanaume ni wale wanaume wanao penda kujisifu na mke wake kampatia sawa sawa...Nakupa sure huyo mwanamke hajatembea na huyo mwanaume ni kiasi cha kuchoka na ujinga wa huyo mme wake.

Huyo mwanamke ningemuona, ningempa zawadi..wacha nimpigie :A S 41:
 
Hapo kwenye red nakupa 100% yaani sijui inakuwaje huwa tunataka kujua
sana walikopita n.k lakini ukishajua tu ndo GUBU linaanzia hapo.

Hata mimi nimekuwa nikijiuliza sana, kwa nini watu wanawashwa washwa kujua vitu ambavyo mwisho wa siku vinaishia kuwaumiza. Halafu wanaume hudai details nyingine za kipuuzi kweli, ..like size za maumbile, frequency of sexual contacts, sometime wanauliza hata walipokutana!! I wish tungeweza kutojiingiza kwenye hiyo kitu inayopasua kichwa!!

Trust me...baada ya kuambiwa roho huwa inauma sana tena sana!!

Babu DC!!
 
...If you want my future, forget my past... nimekakumbuka kakipande ka wimbo huu wa miaka ya 90s. Kwakweli hata mimi sijui kwanini tunahadithiana past; zinasababisha unnecessary insecurities. Zenye children involvement sawa, lakini zile ambazo hazileta matunda ya kuonekana; ni uncalled for.
Sipendi kuvaa T-shirts zenye maandishi lakini nimeamua kudizaini
moja lenye maneno haya, Yamenikuna sana.
 
Kaunga,

Past relations zenye watoto ni kiroba cha misumali...Zinasumbua sana.

Sina hakika, ila wahusika wanatakiwa kuwa na limits za mambo ya kusimuliana. It doesn't make sense kumweleza current BF/GF au mume/mke wako jinsi ulivyofurahia maisha na mzazi mwenzio. Pia ni muhimu kueleza mambo ambayo yanawafanya muendelee kuwa karibu!!

Babu DC!!
 
Sipendi kuvaa T-shirts zenye maandishi lakini nimeamua kudizaini
moja lenye maneno haya, Yamenikuna sana.

Mkuu,

Inabidi pia uwe muangalifu kwani pia mwenzi wako anaweza kuja na tafsiri ya ajabu ajabu, akakugeuzia kibao!! May be umezungusha sana Ki-hiace hadi mwenyewe unaona aibu kukumbuka past yako!!

Haya mambo ni magumu sana,

Babu DC!!
 
Nyie vijana nyie!!
Kwamba yule jamaa alinisugua balaa
Halafu na wewe unasema yule demu alinipaga tigo yule, nikaifumulia mbali!

Hapo kuna ndoa hapo? Hata uchumba haumo wala ugeli frendi haupo!
Hapo kuna malaya flani na gumegume flani wanaishi pamoja!!
 
What if anapokuhadithia unagundua kua mwenzako alikuzidi viwango?utachukua kama changamoto?au naww utajienguay
 
Huwezi simulia list ya wachezaji wote wa zamani, utaonekana kilaza.

Ila kuna baadhi ya vitu vidogo vidogo waweza jikuta umesema lakini sio kila kitu
Hasa wakati mnapoanza mahusiano mtu anaweza uliza kwa nini mliachana na wa zamani.

Anyway, lazima kuwe na mpaka sana wa kusema mahusiano ya zamani katika mahusiano mapya.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom