Kwani kila krismas lazima wachaga waende Moshi, je ni kweli kuwa......

Chongeni tu kuhusu the jews of Tanzania mie napata mbege na family members after tht naenda kuzchanga tena niweke mjengo wa pili hapa migombani! Utajiju arifu!
 
Mbona watu wanapenda kutusakama wachaga?tunaenda uchagani december kwasababu wengi wanakuwa likizo na ni vizuri angalau mara1 kwa mwaka uwaone wazazi pa1 na ndugu,vilevile watoto wanatakiwa wapajue walipotokea na sio kuwaacha wajue mjini tu!!thats why wachaga tumejenga sana vijijini ili kuwa na pa kuishi anytime sio watu wengine wanatusema afu mwisho wa siku hata akifa ni aibu kwa watu kupaona nyumbani kwao.
 
Mtakufa na kijiba cha roho mnaowaonea wivu wachaga kwenda kwao.
Kila siku wachaga tunazungumziwa hapa JF,inaonesha ni kabila classic hapa Tz.
 
Mtakufa na kijiba cha roho mnaowaonea wivu wachaga kwenda kwao.
Kila siku wachaga tunazungumziwa hapa JF,inaonesha ni kabila classic hapa Tz.

Mti wenye matunda ndio unaorushiwa mawe. Kama watanzania wote wangekuwa kama sisi wachaga hii nchi ingekuwa moja ya nchi tajiri duniani. Sasa badala ya kujifunza kutoka kwetu wanabaki kuona wivu. Wamechelewa. Mpende msipende tutazidi kuwapeleka sana, na mwisho wa mwaka tunaenda kwetu kama kawa.

Mcheza kwao hutunzwa.
 
wapo wanaodai kuwa wachaga hupenda kwenda moshi wakati wa krismas
kufanya madhambi kama ngono baina ya hata ndugu yaani watoto wa baba mdogo au mkubwa, wajomba hata wakwe hapa hujaingiza ngozo za kawaida.

Kuwa wanakwenda kuonyeshana pesa waliyochuma nje ya mkoa hasa kwa njia haramu na mauza uza mengine. Kweli hapa ukimwi tutaushinda yarabi?

huna adabu kweli wewe...... Umekosa cha kusema ehh?
Watake radhi wenyewe.
 
we ni mzaramo nini au mkweree????!!! upupu+mashudu=pumba. inakuuma sana bac kajinyonge
jawabu sahihi hapo ni takataka zisizo na
kazi maana pumba huweza kutumika

jina lake ni mpayukaji.
Kabila gani wana majina ya ajabu ajabu
kiasi hadi humu jf anafuata jadi?
 
Mtoa mada kaona tu wachaga ila amewasahau wamasai, mkataa kwao ni mtumwa. Ni vizuri kukumbuka asili yako, baba yako amezaliwa upanga au uhuru road? Kutokana na madhambi pamoja na ujinga wa makabila mengine ndio maana wanaona aibu kwenda kwao hadi wanarudishwa wakiwa .......... Ni vizuri kukutana ndugu pamoja na kupatanishwa kama mlipisha kidogo kwani "penye wazee ............."
 
Ni kweli mkusanyiko wa watu lazima uwe na vituko vya hapa napale!lakini,hilo siyo lengo kuu la mkusanyiko wao,na hutendi haki hata kidogo kuzungumzia mabaya tuu ya mkusanyiko huo,wakati pia una mazuri yake!
 
Chongeni tu kuhusu the jews of Tanzania mie napata mbege na family members after tht naenda kuzchanga tena niweke mjengo wa pili hapa migombani! Utajiju arifu!

Jews of Tanzania in terms of what?
Je ni ule uteule waliopewa na mungu?
Je ni kile kipaji walichonacho katika uvumbuzi na utengenezaji wa silaa za maangamizi?
Je ni ule uzalishaji wa matunda kwa kiasi kikubwa?

Sifa za hawa jamaa zinapishana sana na zile za pande yenu,sifa mojawapo ni unywaji wa pombe kama wewew mwenyewe ulivyoainisha,wizi na dhuruma huwezi kuvitenganisha na jamii yenu!
 
Wachaga ni kabila celebrity hapa.......

yani umeniacha mbavu sina! Ivi kwelie??? Manake mijadala ya makabila humu ndani wachaga kweli wanaongoza, hate speeches, kwa kweli wachaga tuko juu kwa kusemwa, hayo mengine mie sijui.
Kwa sasa na mie nimekuja migombani toka mbali sana, gharama ni kubwa ila i do not regret, kila asubuhi na jioni nasali kwenye makaburi ya wakwe zangu napata faraja kuwakumbuka, nawamiss sana.
Ila xmas bila wazazi huku inahitaji kampani sana,
kati ya stori zilizoibuka jana wakati wa kutoka kanisani ni changamoto ya wanaume vijana wa sasa kuleta heshima kama wazazi wao.
Nimezunguka kiasi Tz ni kweli vijiji vingine si vya kwenda kupumzika,
mfano hali ya hewa, huduma za kijamii ni bora kuliko mjini mara dufu.
 
Tatizo lako Mpayukaji, ni jinsi ulivyoliunda swali lako, huenda ulikuwa na nia nzuri ila ukajikuta
umeshindwa kuwakilisha mawazoyako kwa usahihi hapa. Hii ndiyo sababu darasani wakawepo wanaopata
100% na wengine 0%. Sasa usilalamike kwa kushambuliwa kwani wewe ulianza kwa kuwashanbulia Hao Wachaga.
Kwa taarifa yako utamaduni huu wa Wachaga kwa sasa unaigwa na 50% ya makabila mengine ya Tanzania.Kwa sasa nipo huku Nyanda za juu kusini, watu ni wengi kwelikweli, hata foleni za magari tunazishuhudia jambo ambalo halikuwepo kabla, baada ya uchunguzi kidogo nimegundua tuliokuja kula sikukuu huku kwetu ni wengi sana.
Labda tujiulize kwanini Wachaga, walianzisha tabia hii. Ni sababu za kihistoria na Jiografia. Ardhi ni tatizo kubwa Kilimanjaro, hivyo wengi wametapakaa duniani kote kutafuta maisha baada ya kugundua ni hasara kwao kuendelea kuuana kugombea ardhi kidogo
iliyopo. Aidha wengi walijiingiza kwenye ujasiriamali kwa vile utawala uliwanyima fursa, mfano wakati ule alama za ufaulu katika shule za Kilimanjaro zilikuwa za juu kulinganisha na kwingineko ili kuleta uwiano wa wasomi nchini. Hivyo walijikuta wamechagua kuingia katika biashara, na kujenga shule nyigi zaidi za binafsi ili watoto wao wasome. Biashara, Elimu, na ardhi vimewafanya watawanyike duniani
ila hawajasahau kurudi kuendeleza kwao. Hili ni jambo zuri sana. HONGERENI SANA WACHAGA POPOTE MLIPO DUNIANI.
 
Binafsi si mchaga, ila nawapongeza sana wachaga kwa kwenda kwao Krismas na kukusanyika kusheherekea pamoja, ni mila na desturi nzuri sana zienziwe na kundelezwa
 
kwa hiyo moshi ni peponi?

Moshi ni peponi ya bongo. Hakuna vishida vidogo vidogo kama hizo zinazowasumbua huko kwenu. Na unajua ni kwa nini? ni kwa sababu hakuna migalula. Watu wanasakanya eleri na wanazipata na ndo tunazispend hapa na ndugu, jamaa na marafiki.
 
Mwenzenu nimeuliza tu halafu nyinyi mnanishambulia. Kwanini msijibu hoja kwa utuo na maarifa badala ya matusi na hasira. Kama wanafanya hivyo wakulaumiwa siyo muulizaji.

Kwani umeuliza swali gani? umeuliza upupu na lazima ujbiwe upupu. Vinginivyo kaliframe swali lako ili liakisi kile ambacho ulikusudia kuuliza bob
 
Back
Top Bottom