Kwangu mimi, Regia Mtema ndio mbunge/mwanasiasa mahiri mwanamke mwaka 2011...

Ni moja ya sifa ambazo Mungu alimpa sasa mimi nifanyaje?

Uzuri upo kwa mtazamaji, wewe utaona mzuri wengine watasema anahitaji kwenda gym.

Isitoshe, uzuri unahusiana vipi na umahiri wa mbunge? Kwani ubunge ni beauty contest?
 
Huyu hapa kashaona ukiwa critical kuhusu mbunge wa CHADEMA lazima we ni clique ya CCM. Kazi kweli kweli, check my record hapa.

Nimesema hizo sifa za energetic, patriotic, confident etc zilizotajwa hazijawekewa specifics.

Mna kitu gani hususan cha kutuambia umahiri huu ukubalike, tusione mnampigia debe rafiki yenu tu?

Beauty si criteria ya umahiri wa kisiasa kwa sababu siasa si beauty contest, kwa hiyo mleta mada kwa kuweka criteria ambayo haihusiki katuonyesha hayuko makini, na pengine ameweka hapa sifa za kilemba cha ukoka kutokana na matamanio yake ya kimwili tu.

Mpaka sasa umahiri sijauona, sanasana wengine wamekuja na kumuonyesha kwamba hana discipline hata kwa wakubwa wa chama chake. Sasa huyu asiyeweza kunyenyekea hata wakubwa wa chama chake anaweza kuwanyenyekea wananchi?

Unapaswa kufatilia records za Regia na sio kudandia gari kwa mbele utasagwa mkuu,kwa hakika Regia ametumia muda wake mwingi kuimarisha chama kati ya wabunge wanawake wa CDM...tatizo umfahamu vyema na kwa hiyo unakuja na hoja za kupinga tu kienyeji bila kuwa na vigezo......
 
Uzuri upo kwa mtazamaji, wewe utaona mzuri wengine watasema anahitaji kwenda gym.

Isitoshe, uzuri unahusiana vipi na umahiri wa mbunge? Kwani ubunge ni beauty contest?

Narudia tena uzuri sio sifa ya kuwa mbunge,kwangu mimi ni sifa ya nje ya!!!! ila kwa hakika ni kati ya jembe la kike kwa sasa kwenye siasa za Bongo...fatilia habari zake.
 
ni kweli amepewa sifa zote hizo ni zake, ila akumbuke nidhamu yake iko chini kwani nikikumbuka Igunga aliwahi kumjibu majibu ya kunya Dr Slaa kwamba gari ni la ubunge wake na aliupata kwa jasho lake na kama ubunge ni rahisi hata dr angekuwa mbunge hivyo asione mtu akimfuatafuata kimsingi niliumia sana kwani Dr aliondoka kimya bila kutia neno. je hiyo ndiyo sababu iliyomfanya awe mwanamke mahiri kwanini Sii HALIMA MDEE aliyepambana kiume na tumekomaa nae kule igunga porini mwanzo mwisho hakuwahi kukimbilia mjini kama huyo mtema na kina Heche?
Migomo ya vyuo, unaonyesha wewe ni insider wa Chadema, kwa vile lengo la muanzisha thread ni kumfagilia Mhe. Regia Mtema ambaye ni mbunge wa chama chako, hivyo ni kiongozi wako, wewe kama mwanachama mtiifu, hukupaswa kuyaleta hayo mambo yake ya ndani humu!. Maadam lengo la thread ni fagilia, wewe kama hufagilii unajinyamazia tuu maana mbunge wenu akifagiliwa chama chenu pia kinazidi kupaa!.
 
Haya mambo ya "she is beautiful" si ndiyo haya haya CHADEMA mnawabonda kila siku watu waliomchagua Kikwete kwa msingi wa kwamba eti ni "handsome"?. Sasa hiki chama ambacho kinatakiwa kuwa mbadala, kinatuletea habari hizi hizi?

Kama unaona "she is beautiful/ handsome" kanywe naye chai, hilo linahusiana nini na uongozi?

Muanishaji wa hii thread kwa kuweka upupu kama huu katika vitu alivyoangalia kumpa umahiri kashatuonyesha kwamba standards zake ziko chini kweli kweli.

Wewe acha kutia aibu hapa,kwani haya ni mawazo ya CDM au ya kwangu? una uhakika CDM walimchagua kwasababu ya uzuri wake? Haya ni mawazo yangu binafsi na yasihusihwe na chama changu hata kidogo...kama una la kuchangia nenda kafanya kazi zingine...
 
Angetakiwa kuwa number ya pili kwenye
Ile list ya most influential woman in Tanzanian.

I like her ..
we need people with strong personality.
She has my vote . Keep up Regina. .....
 

Wewe acha kutia aibu hapa,kwani haya ni mawazo ya CDM au ya kwangu? una uhakika CDM walimchagua kwasababu ya uzuri wake? Haya ni mawazo yangu binafsi na yasihusihwe na chama changu hata kidogo...kama una la kuchangia nenda kafanya kazi zingine...

Angalia huyu hata hajui kwamba chama ni watu, na kama wanachama wenyewe ndio hawa sioni ajabu CCM inakuwa vigumu kuitoa. Huwezi kutoa uozo kwa kuonyesha wananchi uozo mwingine, tuonyesheni mna chama mbadala kweli.

Nimeuliza Regia kafanya nini cha maana kupewa umahiri sijapata kitu chochote concrete. Is this the best you guys can do?

Kubali kwamba kuweka uzuri kama moja ya sifa ya umahiri wa mbunge umechemsha.
 
Kakemea wageni waondoke morogoro warudi kwao!!

Hiyo si distinction, sanasana ni xenophobia na kutoelewa dynamics za globalization.

Umasikini wetu hauwezi kuletwa na wageni. Na hatutatui kitu kwa kufukuza wageni kama hatuwezi kufanya kazi wenyewe.Tunatafuta mchawi.

Kuweka kumbukumbu sawa

Alisema hivi bungeni 'wasio wazawa wa Morogoro waondoke' akirejelea Watanzania wa kawaida.

Siku ya pili, alifuta kauli yake hiyo bungeni na kuomba Hansad irekebishwe

Kwa hiyo hakuwa akizungumzia wageni kutoka nje ya nchi, alikuwa anazungumzia Watanzania wengine msiruhusiwe kumiliki ardhi Morogoro kama hamkuzaliwa huko.
 
Migomo ya vyuo, unaonyesha wewe ni insider wa Chadema, kwa vile lengo la muanzisha thread ni kumfagilia Mhe. Regia Mtema ambaye ni mbunge wa chama chako, hivyo ni kiongozi wako, wewe kama mwanachama mtiifu, hukupaswa kuyaleta hayo mambo yake ya ndani humu!. Maadam lengo la thread ni fagilia, wewe kama hufagilii unajinyamazia tuu maana mbunge wenu akifagiliwa chama chenu pia kinazidi kupaa!.

Haya ni mawazo mgando.

Kama mtu ni mchemfu ni mchemfu tu, na akisifiwa sifiwa isivyotakiwa, kama mtu ana data za kutuonyesha vingine, anatakiwa kutupa tu, ili mradi ziwe za kweli.

Hizi habari za kulindana kichamachama si ndio tunazikataa CCM?

Sasa kwa nini zikubalike CHADEMA?

Kwa nini tunataka double standards?
 
Kuweka kumbukumbu sawa

Alisema hivi bungeni 'wasio wazawa wa Morogoro waondoke' akirejelea Watanzania wa kawaida.

Siku ya pili, alifuta kauli yake hiyo bungeni.

Kwa hiyo hakuwa akizungumzia wageni kutoka nje ya nchi, alikuwa anazungumzia Watanzania wengine msiruhusiwe kumiliki ardhi Morogoro kama hamkuzaliwa huko.

Ahsante,

Sasa mtu mchemfu kama huyu anaropokaropoka tu na kulazimika kufuta kauli yake bungeni. Mtu ambaye hata haelewi kwamba kwa mujibu wa katiba ya Tanzania hakuna Mtanzania atakayekuwa mgeni nchini mwake (nimeona upumbavu huu hata Professor Mwandosya anaongea, ina more tioned down disguise, hii nchi hii), kwani nchi ni moja na mtu anaruhusiwa kwenda popote ilimradi asivunje sheria, mpuuzi kama huyu ndio mmemuona mbunge "mahiri".

I mean I am not against CHADEMA, najua pia nobody is perfect, lakini huyu mediocre aliyeshindwa ubunge na kwenda kuupata mezani, kisha akasema ubunge unamboa hata bila ya kumaliza mwaka, huyu mpuuzi aliyekuja kuitukana constituency yake hapa JF kwamba ni "wabeba box" ndiye mnamuona mtu mahiri?

Is this the best you can come up with?
 
To me Regia Mtema is another shouter in the political arena.She is poor in discipline and also ''limbukeni'' in politics, so i don't wonder any of her misbehavior to any body apart from her part Secretary General (slaa).

Mwanafalsafa mmoja aliwahi kuniambia kuwa Mungu anasababu zake katika kuumba watu wa aina hii.In most cases, most of them (disabled) ni wakorofi basing on their inferiority.
:A S thumbs_down:
 
Mm nimependa anavyo vaa nguo za heshima nywele ajaweka dawa(natural) upo juu dada
 
Nimeambiwa mbunge mahiri, umahiri hauji bila kazi inayoonekana, ndio maana nikataka kujua sababu za umahiri huu ni zipi ili tujue umahiri unaendana na kazi yake au la.
Mkuu Kiranga, with due respect, the motive behind hii thread ni consolation kwa Mhe. Regia Mtema kufuatia ile thread nyingine ya Wanawake 10 wa shoka Tanzania, kwa vile kule Mhe. Regia hayupo na kwa mujibu wa muanzisha mada kwake Mhe. Regia ndiye angestahili kuwa number 1 na vigezo vyake ndio hivyo kaviweka pia vikijumuisha gender yake, visibility yake, body mophology na ability etc.

Kwa vile huu ndio mtazamo wake, na hizo ndizo sifa zake, lengo likiwa ni kufagilia, nashauri kwa vile tuko kwenye festival season ungeacha tuu hii fagilia iendelee bila wewe kuingiza neno lolote!.

Kitendo tuu cha mwanamke kujaza form kugombea jimbo kwa kuzingatia hali aliyonayo dada huyu ni ushujaa tosha wa kustahili pongezi kwa sababu huko Chadema kuna wanawake wengi wamebwetekea viti maalum tuu. This means she is a dare devil with a darring heart!.

Tukija michango yake bungeni, kwa Mhe. Regia japo sio outspoken lady lakini she speak, she ask, hata kama anachoongea ni cha kawaida tuu au maswali yake ni mepesi lakini aneongea, anachangia na anauliza tena mpaka kwenye maswali kwa PM. Kitendo hicho kwa fans wake ni ushujaa maana kuna wabunge wangapi wako kimya kabisa!.

Wajameni hebu waacheni fans wawasifu watu wao this is festival season!.
 
Labda kwa kauli yake hii

"Makinda is a good Speaker ever. I admire her. Tatizo lenu ni mfumo dume unawasumbua. She is Democratic."

Kwa msingi wa wanachama kama hawa safari yetu si fupi hata kidogo.
 
....the motive behind hii thread ni consolation kwa Mhe. Regia Mtema kufuatia ile thread nyingine ya Wanawake 10 wa shoka Tanzania, kwa vile kule Mhe. Regia hayupo na kwa mujibu wa muanzisha mada kwake Mhe. Regia ndiye angestahili kuwa number 1 na vigezo vyake ndio hivyo kaviweka pia vikijumuisha gender yake, visibility yake, body mophology na ability etc.

Wajameni hebu waacheni fans wawasifu watu wao this is festival season!.

Sasa mbona kwenye thread ile Mkuu hukuja kusema watu wasiponde? Ukamuacha Pindi Chana afananishwe na Chakula cha Kihindi? Au kuna privileges maalum kwa watu maalum? Kama kule hakukuwa na haki ya festive season, lipi linalofanya hapa kuwe na haki hiyo?

Besides, mtu mwengine atakuuliza festive season kwa nani?


Kitendo tuu cha mwanamke kujaza form kugombea jimbo kwa kuzingatia hali aliyonayo dada huyu ni ushujaa tosha wa kustahili pongezi kwa sababu huko Chadema kuna wanawake wengi wamebwetekea viti maalum tuu. This means she is a dare devil with a darring heart!.

Hapa bila ya kujijua umeleta dharau kwake. Kuwa yeye ni dhaifu sana, na kwa kuwa amejaribu kugombea basi apongezwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom